Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Wednesday, April 4

SAFARI YA KUTAMBUA KWA NINI UPO DUNIANI.


Mwalimu wa kweli wa kiroho hana maneno ya kukufundisha jambo jipya usilolifahamu, habari mpya taarifa mpya,sheria mpya ama imani mpya.
Kazi pekee ya mwalimu wa kiroho ni kukusaidia na kukuongoza kuondoa giza linalokutenganisha wewe kutoka kwenye ukweli wa kwa nini Mungu alikuumba na undani wa sababu ya kwa nini upo hapa duniani.
Kazi yake ni kukufunulia ujue ukweli unaokuunganisha kwa kina wewe na Muumba wako.
Tumemaliza mfululizo wa siku 40 katika kuweka tafakari ya kina juu ya sababu ya sisi kuwepo hapa duniani kwa njia ya mfungo wa siku 40.
Kwa nini upo duniani? Nimevutiwa kutumia ujuzi nilioupata kushirikiana nawe kwa mfululizo wa siku 40 kutafakari upya kwa pamoja. Ni katika mfululizo wa makala kujikumbusha kwa nini tupo hapa katika dunia hii.
Bila shaka mfululizo huu utakuwa ni njia ya kukufumbua  kuhusu swali hili ambalo wengi hujiuliza ‘’Kwa nini nipo duniani? Nina jukumu gani katika dunia hii’’?
Ni imani yangu kwamba mwisho wa mfululizo hu utakuwa na picha kubwa ya namna ulivyokuwa ukijitazama,na upya baada ya mfululizo huu.
SIKU 40 ZIJAZO
Takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa umri wa mwanadamu kuishi unafikia wastani wa miaka 70.Unaonaje kama utafanya maamuzi ya kutumia siku 40 tu kutafakari ni kwa nini Mungu alituleta hapa duniani?
Kwa wale wakristu mtakumbuka jinsi biblia inavyoeleza umuhimu wa siku 40. Mungu alipotaka kumwandaa mtu kwa makusudi Fulani,alitumia siku 40.
·       Maisha ya Nuhu yalibadilishwa kwa siku 40 zaa kunyesha mvua
·       Musa alibadilishwa kwa siku 40 katika mlima wa Sinai
·       Daudi akipambana na Goliath katika siku 40 alishinda na kubadilishwa katika imani.
·       Eliya alibadilishwa pale Mungu alipompa nguvu ya kuishi kwa siku 40 kwa mlo mmoja tu
·       Mji wote wa Ninawi ulibadilika baada ya Mungu kuwapa siku 40 za mabadiliko
·       Yesu aliinuliwa baada ya kufunga na kuomba kwa siku 40 nyikani
·       Mitume wa Yesu walibadilishwa kwa siku 40 baada ya ufufuko.
Bila shaka siku 40 zijazo zitabadili maisha yako
Tutakuwa na mada zilizogawanywa kwa siku 40. Ruhusu mabadiliko katika maisha yako kwa kubadili mtazamo wako katika tafakari ya siku 40. Ni muhimu kushiriki kwa kina katika kusoma makala hizi kwa siku 40 zijazo, ukitafakari na kujadiliana kwa kina.Usikimbilie kusoma tu,tafakari, hata katika mafunzo ya mwalimu mbovu, lipo la kujifunza.
Muombe Mungu akujalie tafakari ya kina, kudadisi na kupata faida inayokusudiwa katika mfululizo huu. Washirikishe na wengine,na shirikiana nao katika kujadili mada kwa kila siku .Ushirikiano wa wawili ni bora kuliko mmoja.Mmoja atashika hili na mwingine lile,kushirikiana kunajenga zaidi.
Nakutakia ushiriki mwema

Saturday, February 17

MAISHA YAKO YANA THAMANI GANI KWA WENGINE?>

Maisha yako yamechangia nini katika dunia hii?Maisha yako yameleta faida gani kwa wengine?Umekuwa zawadi kiasi gani kwa wengine?
Kipawa ulichopewa, uwezo wa ubunifu uliopewa,ujuzi uliopewa,umeutumia namna gani kwa ajili ya wengine,kama utukufu kwa aliyekuumba?
Wakati mwingi tumekuwa tukitazama tunapata nini,tunaongeza nini kwa ajili yetu pasipo kutazama ni kwa namna gani umekuwa mwenye manufaa kwa dunia na viumbe wote.

Hii ndiyo sababu inayonisukuma kuendelea kuandika,ili niwe sababu ya faraja,mabadiliko ,changamoto na hata chemchem ya wengine kujitambua.

Tuesday, December 20

KITABU KITAKACHOKUWEZESHA KUWEKA KUMBUKUMBU YA MAPATO NA NMATUMIZI YAKO

JE WAJUA?: Watanzania wengi hatuweki rekodi ya Mapato na matumizi tunayoyafanya kwa siku,juma ,mwezi na hata mwaka?Je unajua kwamba wengi wetu tunatamani kuwa na kumbukumbu na mwisho wa mwaka kujua tulipata kiasi gani na tulikitumia vipi?Sasa umerahisishiwa.Unaweza kuweka kumbukumbu ya mapato yako kila siku na matumizi.
Nimeandaa kitabu kitakachokurahisishia kuweka kumbukumbu juu ya ulichozalisha(wapi,lini,namna gani,kiasi gani) na hivyo kujua unakitumiaje.
Ni kitabu kidogo chenye kurasa 32 (karatasi 8) kiitwacho BAJETI YAKO MIKONONI MWAKO /YOUR BUDGET ON YOUR HAND.Kipo kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza,Ni wewe utachagua unapenda cha lugha gani.

Hauhitaji kuwa na elimu ya uhasibu ama biashara ili kuweza kukitumia,kila kitu kimerahisishwa. Unachohitaji ni kuweka kumbukumbu kwa usahihi kama utakavyokuta kwenye maelezo.Kwa nini unapaswa kuwa na kitabu hiki kabla ya kuanza mwaka
1.Utaweza kujua mapato yako yanatokana vema na nini na namna gani uweke bidi
2.Kitakurahisishia kujua matumizi yasiyokuwa na tija na kuyaepuka.
3.Kitakuwezesha kujua vyanzo vyako vya mapato halisi na vyanzo vya matumizi makubwa
4.Ni rahisi kukitumia,kidogo na rahisi kukibeba.
5.Kitakurahisishia kuweka mikakati ya kimaendeleo na kuweka vipaumbele
6.Kitakurahisishia kujua ulipata kiasi gani kwa wiki,juma,mwezi na hata mwaka na hivyo kujua napopaswa kuongeza bidi na kupunguza /kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima
7.Kitakurahisishia kupanga mipango ijayo kwani utajua mapato yako na matumizi halisi nay ale yanayojitokeza.
8.Ni kizuri kwa watu wote wenye nia ya kupanga mipango ya kiuchumi na kuitekeleza.
9.Unajenga tabia ya kuthamini kidogo ulichonacho
UNAKIPATAJE?
Kitabu kinapatikana kwa bei ya tshs 5,000/= .Wasiliana nami kwa namba 0765046644 ama 0717903089 utaletewa popote ulipo.

Sunday, April 27

Waraka kwa vijana wote

Barua Ya Wazi Kwa
Kijana Wa Kitanzania
-na Makirita Amani

Hakuna kipindi kigumu kwenye
maisha ya mwanadamu kama
muongo wa tatu wa maisha
yaani kati ya miaka 20 mpaka
30. Huu ni wakati ambao una
changamoto nyingi sana za
maisha na ni wakati ambao
unaweza kujenga au kubomoa
maisha yako moja kwa moja.
Kama wewe upo katika kipindi
hiki endelea kusoma hapa ili
uweze kupata mwanga pale
mambo yanapokwenda
usivyotarajia. Kama umri wako
umezidi hapo unaweza kusoma
pia na ukawashauri wadogo
zako au watoto wako. Na hata
kama umri wako uko chini ya
hapa sio vibaya ukajifunza na
kujua ni nini unakwenda
kukutana nacho mbele.
Huu ni wakati mgumu sana
kwako.
Kwa maisha yetu ya kitanzania,
kijana wa miaka kati ya 20-30
anakuwa anaingia elimu ya
chuo, yuko chuoni, amemaliza
chuo, anatafuta kazi au ndio
ameanza kazi. Pia ni wakati
ambao kijana huyu anakuwa
kwenye mahusiano ya mapenzi,
uchumba na hata kuingia
kwenye ndoa. Pia ni wakati
ambao wengi wanaondoka
kwenye mikono ya wazazi au
walezi na kwenda kujitegemea
wenyewe. Mambo yote haya
yameleta changamoto kubwa
sana kwa kijana na kwa
changamoto hizi kijana
anaweza kujijenga au
kujibomoa.
Changamoto kubwa
anazokutana nazo kijana katika
wakati huu ni;
1. Kumaliza elimu ya sekondari
na kwenda kuanza maisha ya
tofauti kabisa vyuoni. Kuna
tofauti kubwa sana ya elimu ya
sekondari na elimu ya chuo,
wakati sekondari unasimamiwa
sana, chuoni unakuwa na
uhuru zaidi. Kwa uhuru huu
vijana wengi wamejikuta
wanafanya mambo ambayo
yanasababisha washindwe
kufatilia masomo yao vizuri.
2. Kuingia kwenye mahusiano
ya kimapenzi na kuvunjika kwa
baadhi ya mahusiano.
Mahusiano sio rahisi katika
umri huu, kijana anakutana na
mwenzake ambaye anafikiri
wanapendana sana na siku
moja watakuwa mume na mke
baada ya muda anagundua
mtu aliyeingia nae kwenye
mapenzi hakumjua vizuri. Hii
inapelekea mapenzi kuvunjika
na kuumizwa sana.
3. Kukabiliana na maisha ya
masomo vyuoni na maisha
mengine ya kijamii. Licha ya
masomo kuna shughuli nyingi
za kijamii na binafsi pia. Kuna
vijana wanajikuta wakiendekeza
starehe sana na kusahau
masomo, wengine wanajikuta
wakikazana na masomo sana
na kusahau nini kinaendelea
kwenye jamii.
4. Kupata ajira baada ya
kumaliza chuo. Hii ndio
changamoto kubwa sana hasa
nyakati hizi. Vijana wanatoka
vyuoni wakiwa na habari nzuri
walizodanganywa kwamba
ukisoma na kufaulu vizuri
utapata kazi nzuri na kuwa na
maisha mazuri. Ni pale
wanapojikuta mtaani mwaka
mzima wakizunguka na
bahasha bila ya kupata kazi
ndio wanagundua maisha sio
rahisi kama walivyodanganywa.
5. Kuanza kazi na kukabiliana
na changamoto za kazi. Kupata
kazi ni kitu kimoja, kufanya kazi
na kuridhishwa nayo au
kuifurahia ni kitu kingine. Kuna
changamoto nyingi sana
kwenye kazi hasa kwa
wafanyakazi wageni, pia jinsi ya
kuchangamana na watu wenye
haiba tofauti ni kazi kubwa
sana kwa kijana.
5. Kuanza maisha ya
kujitegemea mwenyewe na
kuweza kufanya maamuzi
sahihi. Katika wakati huu kijana
anaweza kuona ana uhuru
mkubwa sana wa kufanya yale
aliyokuwa anashindwa kufanya
wakati yuko kwenye mikono ya
wazazi au walezi. Ni katika
wakati huu wengi wanafanya
starehe kupitiliza na kujikuta
wanapotelea katika ulevi.
6. Kuingia kwenye ndoa na
kuanza maisha ya kifamilia.
Katika wakati huu kijana
anaingia kwenye ndoa na
kuanza maisha ya familia.
Maisha ya ndoa ni tofauti sana
na maisha ya mapenzi na
uchumba, hapa ndipo kijana
anamfahamu vizuri mwenzake
na kwa kushindwa kupambana
na changamoto za ndoa, ndoa
nyingi zinaishia kuvunjika
mapema sana.
Kutokana na ukosefu wa elimu
ya kupambana na changamoto
hizi za maisha vijana wengi
sana maisha yao yamepotelea
kwenye kipindi hiki na kuja
kushtuka baadae wakati umri
umekwenda na kujiuliza ni
wapi mambo yalikwenda
hovyo.
Kijana ufanye nini
kukabiliana na changamoto
hizi?
Hapa nitazungumzia mambo
matano muhimu ambayo kijana
anatakiwa kufanya au kujua ili
kuweza kuvuka salama kipindi
hiki kigumu.
1. Kuna wakati hutajua
unafanya nini.
Katika kipindi hiki cha maisha
kuna wakati hutajua ni nini
unafanya kwenye maisha yako
au ni wapi maisha yako
yanaelekea. Usikatishwe tamaa
na hali hii bali weka mipango
na malengo ya maisha yako na
ujitahidi kutekeleza.
2. Maisha hayatakuwa vile
unavyopanga au kufikiri
yatakuwa.
Mambo yanabadilika tena kwa
kasi sana, pamoja na kuwa na
mipango mizuri bado hutoweza
kuitimiza yote hasa ndani ya
kipindi hiki. Utajitahidi sana
lakini kuna ambavyo
vitakushinda. Usife moyo,
endelea na maisha yako
mwisho wa siku maisha lazima
yataenda. Kingine cha muhimu
zaidi jua unahitaji muda ili
kufikia mafanikio yoyote
unayofikiria, hakuna kitu
kinachokuja haraka na kwa
urahisi.
3. Sio kila mtu anayekuja
kwenye maisha yako atakaa.
Hili nalisema hasa kwenye
mahusiano ya kimapenzi.
Usifikiri mpenzi uliyempata ni
lazima uje uishi naye, kuna
uwezekano mkashindwa
kuendana na kila mtu
akachukua hamsini zake.
Badala ya kulaumu na kuharibu
maisha yako furahia kwamba
huyo ni mmoja wa watu ambao
walikuwa wakupita tu kwenye
maisha yako. Umekuwa na
marafiki wengi kwanzia utoto
mpaka sasa, wengi kwa sasa
hujui hata wako wapi, ndivyo
maisha yalivyo. Kuna
watakaokuja na kukaa, kuna
wengine watapita tu.
4. Uhuru una mipaka yake.
Kwa kuwa umefika wakati wa
wewe kujitegemea na kuwa
huru na maisha yako,
haimaanishi unaweza kufanya
chochote unachotaka na
maisha yako. Ni lazima uwe na
busara ya kujua ni kipi kizuri
kwenye maisha yako na kipi
kibaya. Kama unaenda disko na
kulewa kila mwisho wa wiki kwa
sababu ulikosa haya ulipokuwa
nyumbani, fikiria maisha yako
ya mbele unataka yaweje kisha
punguza mambo ambayo
yatakuzuia kufika kule.
5. Jaribu mambo mengi sana
katika wakati huu.
Jaribu kufanya vitu vingi sana
kwenye kipindi hiki, usiridhike
na kazi moja unayotafuta au
uliyopata. Huenda mpaka sasa
hujajua ni nini unafurahia
kufanya au hujajua vipaji
vyako. Katika wakati huu
ambao bado hujawa na
majukumu makubwa unaweza
kujaribu kufanya vitu vya
tofauti kwenye maisha yako ili
kujua ni nini unafurahia
kufanya. Muhimu zaidi
tengeneza vyanzo mbadala vya
kipato katika wakati huu.
6. Jifunze, jifunze, jifunze
Vijana wengi wanaomaliza
elimu zao huona kujifunza ndio
kumefika mwisho. Au
watajifunza tena wakienda
kuongeza masomo. Hili ni kosa
kubwa sana, jifunze kila siku
kutoka kwa watu na kwa
kujisomea vitabu vya
kukuendeleza. Kama unakosa
kabisa cha kujifunza tembelea
AMKA MTANZANIA na
utajifunze mengi sana. Kama
hujifunzi unarudi nyuma na
kama unarudi nyuma hutoweza
kupambana na changamoto za
maisha hivyo maisha yako
yatakuwa magumu sana.
7. Dunia haiko sawa.
Kuna wakati kijana unafikiri
dunia ingetakiwa kuwa sawa na
kuona kama unaonewa. Ukweli
ni kwamba dunia haijawahi
kuwa sawa na haitokuja kuwa
sawa. Unaweza kufanya kazi
kwa bidii na maarifa halafu
mwenzako akaja kuchukua
pongezi zako, unaweza kufanya
haki na bado ukaingizwa
kwenye uhalifu, unaweza kuwa
na elimu kubwa na ufaulu
mzuri ila ambaye hana elimu
ndio akawa bosi wako kazini,
unaweza kuwa na roho nzuri
na ukazulumiwa, haya yote ni
maisha.
8. Chocote kitakachotokea
jua huo sio mwisho wa dunia.
Hata litokee jambo baya kiasi
gani kwenye maisha yako kama
bado upo hai basi jua unaweza
kuyafanya maisha yako kuwa
bora zaidi. Usikubali
changamoto yoyote iharibu
maisha yako, jua itapita na
maisha yataendelea. Kila kitu
kinapita, hata hayo magumu
unayopitia yatapita, hakikisha
maisha yako yanakuwa imara
baada ya mapito hayo.
9. Safiri.
Jitahidi sana katika kipindi hiki
jitahidi sana usafiri sehemu
mbalimbali ndani na nje ya
nchi. Kusafiri na kwenda
sehemu ngeni kunakufanya
ufikiri tofauti na uwe na
mtizamo mpana sana kwenye
maisha yako. Kama umezaliwa
moshi ukasoma na kukulia
moshi, ukafanya kazi na kuishi
moshi utakuwa na mawazo
mgando sana kwa sababu
unaona mambo na
changamoto zile zile kila siku.
Ila unaposafiri na kuishi na
watu wenye maisha na
mitizamo tofauti na ya kwako
hapo ndipo unapoweza
kujifunza zaidi.
10. Furahia kila hatua ya
maisha yako.
Kama unatamani nyakati
ngumu zifutike kwenye maisha
yako hujajua umuhimu wake.
Kila changamoto unayokutana
nayo inakujenga uwe mtu bora
zaidi. Furahia kila hatua
unayopitia kwenye maisha
yako, iwe ni ya kufurahisha au
ya kuumiza. Kuna somo
muhimu la kujifunza kwenye
kila jambo na kila mtu
unayekutana naye.
Kijana haya maisha ni ya
kwako, yapangilie maisha yako
na uyaishi. Usiogope
changamoto unazokutana nazo
hizi ndizo zinazokusaidia ukue
zaidi. Usilalamike wala
usilaumu yeyote, chukua hatua
juu ya maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika
wakati huu mgumu sana
kwenye maisha yako, nina
imani utavuka wakati huu
ukiwa salama na ukiwa na
malengo makubwa.
Kumbuka , TUKO PAMOJA.
Mshirikishe kijana mwenzako
mafunzo haya ili naye ajifunze,
bonyeza kitufe cha facebook

Monday, September 30

SIFA ZA BINADAMU ANAYEJITAMBUA

Katika makala hii tunajifunza juu ya binadamu anayejitambua.Makala hii inaweza kukukumbusha mambo mengi kwa kifupi na hivyo kukufanya uchunguze juu ya maisha yako na kuyatumia vyema kwa wakati huu ulipo hapa duniani.


Kutambua ndani yako hakuhitaji uende shule na kusoma sana,na hakutokani na maamuzi ya mtu mwingine bali ni maamuzi yatokayo ndani mwako
Ni mguso unaotaka ndani mwako, ufahamu unaokua toka ndani mwako. Ni uchimbuzi wa chemchem zitokazo ndani mwako, Ni kumtambua Mungu kupitia mguso ndani ya moyo wako, kisha kuanza kutumia kipawa ulichonacho kwa ajili ya utukufu  wa Mungu . Ni hisia za ndani zitakazofanya umfahamu Mungu na si kufikiria tu.Upya ndani ya binadamu hutokea wakati wote  kwa kuunganisha moyo wako na ulimwengu wa hisia na kuendelea kujifunza kila wakati na kukuza nafasi ya moyo wako kuwa mpya.
 na
Je ni kwa namna gani unamtambua binadamu anayejitambua?

Mtu anayejitambua hubadili mtazamo wake kutoka kwenye mtazamo wa jamii unaofuata mila na desturi/kawaida kuelekea kwenye fikra za kuijenga dunia mpya na yenye fursa mpya.Hujenga dunia ambayo wanaomzunguka ni wanadamu wanaotambua utu na nafasi ya kila nafsi.Akiwa na misingi ya ujamaa na usawa, hufanya majukumu yake kutoka kujitazama yeye binafsi na kuanza kuwatazama wengine.Uchaguzi wake na matendo yake husukumwa na  maono na mtazamo wa mbali kwa ajili ya binadamu wote na viumbe vyote.Hutazama sio kila kiumbe kwa ajili yake,bali kila kiumbe kwa ajili ya wote.

Anayejitambua habagui jinsia bali hutambua jinsia kuwa ni matokeo ya fikra za Mungu yaliyokusuduia kutoa fursa.Huheshimu, hutambua wengine na kuthamini nafsi zao na uchaguzi wao.Hutengeneza dunia dunia ambayo jinsia zote huwa na uhuru wa  kutumia vipawa vyao, kutambua sauti zo,nuru ndani mwao na kutumia kwa ajili ya viumbe wote. 

Mtu anayejitambua hasukumwi kutenda na maamuzi ama fikra za wengine. Anatazama ndani yake.Hajifananishi na nafsi zingine na hivyo hatumii nafasi yeyote kuwakandamiza wengine.Husimama kwa miguu yake mwenyewe. Anawasikiliza wengine isipokuwa hatoi nafasi kwa wengine kumuamulia maisha atakayoishi. Anayaona mambo yajayo na hivyo huanza kuijenga kesho yake katika wakati tunaouita sasa. Ni alama ya uwezo wa Mungu uliopo ndani ya binadamu. Na alama ya maisha yake huishi enzi na enzi.

Mtu anayejitambua huchukua hatua juu ya hisia zitokazo ndani mwake na hivyo kutambua matokeo ya matendo yake.Hutenda kwa msukumo wa moyo. Hutambua mambo ambayo hayamletei faida na kutoyafanya na pia hutambua yale yanayomletea faida ..akitambua kuwa anapotenda kwa wengine anajitendea mwenyewe. Husikiliza hisia za ndani mwake na kujifunza lugha ya moyo wake.

Huishi maisha yenye sababu. Husikia muito alioitiwa na kuuuishi. Haridhishwi tu na maisha ya tokanayo na matukio kama kuamka,kutembea,kulala,kula bali hutambua kuwa yupo hapa duniani kwa sababu maalum,hivyo huchimba ndani mwake kuijua sababu na kuiiishi. Kila wakati anasukumwa na sababu hiyo  ya yeye kuishi ,kuendelea kuishi kwa dhati akitengeneza na  kuifuata njia inayomfikisha huko.

Hakimbii majukumu yake . Hajitoi katika kutafuta suluhu ya changamoto na wala halaumu wengine. Hutambua makosa yake na kujifunza kupitia hayo. Husanifu maisha yake na kuyafanya mapya kila wakati.
Hujifunza toka ndani mwake na kutoka kwa wengine. Hutilia mkazo katika mafanikio ya ukuaji ndani mwake kuliko mafanikio ya nje., hutengeneza ndani mwake. Hutafiti na kuvumbua chemchem zinazojenga na kubomoa nafsi na kutumia chemchem hiyo kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi.Hivyo aliyejitambua ni picha tosha ya uwezo na uwepo wa Mungu ndani ya binadamu. Hutengeneza msawazo kati ya chemchem ndani mwake na matokeo yaonekanayo halisia.;
Binadamu anayejitambua hutazama kila jambo kama fursa


Anayejitambua hatafuti usahihi katika utendaji bali hutenda kwa kujitolea katika nguvu na uwezo wote.Hufanya kwa uwezo wake wote.
Anayejitambua hujikita katika kutenda kuliko kusema tu.Huweka bidii katika kazi . Huanzisha na kutenda mambo ambayo hufaidisha viumbe wote . Husema pale inapohitajika,huheshimu mawazo yake na huwa tayari kuchukua malipo ya maneno yake mwenyewe.Hakimbii kivuli chake. Hayupo tayari kuona wengine wakikosa uhuru  kupitia yeye. Anatambua kuwa wakati wote huvuna alichopanda..

Anayejitambua huweka mkazo katika uhusiano mwema na nafsi zingine. Huthamini mahusiano yenye thamani. Mahusiano kwake hutokea ndani, hujengwa ndani na hivyo hudumu. Upendo kwake ni lugha ya moyoni, huleta furaha, mshikamano na amani.Zitokeapo changamoto katika mahusiano,huwa tayari kuyatatua kwa ajili ya kuyakuza zaidi.

Anayejitambua hutambua kuwa hapa duniani hatupo katika kushindana,ushindani kwake haupo,hushirikiana na ushindi kwake ni furaha katika kutimiza wajibu wake. Huandaa silaha zake ndani na kuteketeza kila kisicho na manufaa kwa binadamu. Baada ya milima na mabonde katika maisha yake ushindi huzaliwa ndani mwake. Hutumia uwezo wake kwa ajili ya Wengine na si dhidi ya wengine..

Huishi katika hali ya kujitolea na bidii. Huwa ni zawadi ya aina yake hapa duniani. Haogopi kutenda. Huendeleza mambo yaliyojenga utu,ubinadamu na misingi bora ya kuishi yaliyojengwa na binadamu waliomtangulia. Maisha yake hufundisha wengine.  Hutambua juhudi za wengine na wote wanaompa msukumo wa kutenda zaidi hasa pale anapokutana na  changamoto. Hutambua kuwa hayuko peke yake,bali dunia imejengwa kwa muungano wa nafsi zinazotimiza majukumu kwa dhati.

Haogopi ukweli hata pale unapoumiza. Hutoa nafasi ya kusamehe kila wakati anapokosewa. Hujisamehe yeye pia anapofanya makosa. Hushiriki katika ujenzi wa maisha yake.
Hutambua kuwa kila jambo hutoa fursa,kila kiumbe ana fursa. Hakusanyi ama kujilimbikizia kwa ajili ya sifa. Hutazama wengine kama anavyofanya kwa nafsi yake. Inapostahili hujitolea alichonacho,hutoa kwa wale walioshiriki kwa yeye kupata. Hutengeneza maisha yake yawe ya kutoa fursa kwa wengine badala ya kuwanyang’anya wengine .

Anayejitambua haichukuliai dunia kama chanzo cha maumivu bali hugundua kuwa dunia humpa kila mmoja kadiri anavyohitaji.Dunia husikiliza kutoka kwenye uwezo  ulio ndani mwetu tuliopewa na Mungu.Hata mara moja hajichukulii kuwa ni bora kuliko binadamu wengine na wala si dfhaifu kuliko wengine. Hutambua kushabihiana na kutegemeana kati ya kiumbe kimoja na kingine.Hivyo anatambua kuwa kama ikiharibu mazingira ,ni sawia na kuharibu nafsi yake.
Binadamu anayejitambua huyajenga na kuyatunza mazingira yanayomzunguka


Anayejitambua hamlaumu Mungu hata mara moja. Uhusiana wake na Mungu ni wa heshima,urafiki na huwa na umoja naye . Mienendo yake yote humwelekea Mungu .Anawaheshimu wanaoamini sawia naye na wasio amini sawia naye. Hashiriki kutumia imani ama dini kama njia ya  utengano kati ya binadamu,ama binadamu na mazingira yake.

Ni mfano wa sifa njema ya binadamu. Huchukua majukumu yake. Ana faida kwa viumbe wote.Hulinda, hujenga, huheshimu, Huishi vyema duniani. Ni mfano wa aliyeletwa kuifanya nuru ya Mungu ing’ae. Ni halisi,haishi maisha bandia. Ni wa kutumainiwa, si mbinafsi. Wakati wake kuwepo duniani ukifikia tamati,huondoka kwa furaha ya kutimiza alichotumwa,na kuacha dunia ikimlilia.Ni wewe na mimi.

Sunday, September 8

JINSI YA KUPIGIA KURA BLOG YAKO KATIKA SHINDANO LA TANZANIA BLOG AWARDS

Napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu kwenu kwa kupendekeza blog hii kushiriki katika shindano la Tanzania blog awards. Blog hii imependekezwa katika vipengele viwili ambavyo ni

1. Best Inspirational Blog
2. Best Creative Writing Blog

 Nakuomba kwa nafasi yako uchukue muda kuipigia kura blogu yako katika vipengele tajwa hapo juu kabla ya tarehe 15/09/2013 kwa njia zifuatazo
(a)Bonyeza hapa  kisha chagua pongujoseph.blogspot.com
(b)-(i) Kwa kupigia kura Best Inspirational Blog bonyeza hapa
      (ii) Kwa kupigia kura Best Creative writing Blog Bonyeza hapa
Hakikisha unachagua pongujoseph.blogspot.com

Ahsante sana kwa ushirikiano

Kwa maoni,maswali ama ushauri usisite kuniandikia +255765046644, Whatsapp namba +255765046644

UJUMBE WA LEO JUMAPILI

Kwa kila hatua unayopiga katika kujitambua na kutumia nuru uliyonayo,inazidi kukufanya uvumbue uwezo wako katika kupenda wengine ,sababu ya kuwapenda na kutenda hivyo.Inakufanya ujue faida na sababu ya kujitolea ili nawe upokee na kuiishi,kujifunza na kufundisha wengine kupitia maisha yako. Safari ya kuvumbua uwezo ulio ndani mwako ndiyo safari muhimu katika maisha yako ya kila siku.Inaanza pale tu unapoamua kutafiti wewe ni nani na kwa nini upo hapa duniani.Na haiishi sawia na maisha yalivyo endelevu. Katika safari hii utajifunza kujisamehe na kuwasamehe wengine.Utajifunza pia kukubali kuishi kwa dhati katika dunia hii na kukubali maisha yako halisi.Utaacha kuwahukumu wengine na kukubali mawazo yao na maamuzi wanayoyachukua juu ya maisha yao Mwishoni utagundua nyumba ilipo furaha na amani,ndani mwako na kujenga maisha yako kadiri ya uchaguzi wako na kuiiunda dunia mpya ndani mwako.