Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Sunday, February 24

HADITHI YA TAI NA KUKU,NA FUNZO JUU YA KUSIKILIZA SAUTI ILIYO NDANI MWETU




Siku moja,pasipo kujua mkulima aliokota yai la tai.Kwa kuwa hakutambua kuwa ni la tai,alilichukua  na kupeleka kwa kuku ambaye alikuwa ameanza kuatamia akalichanganya na mengine ambayo tayari yalishaanza kuatamiwa.Kuku naye hakuweza kutambua utofauti wa yai hilo na mengine,akaliatamia.

Bada ya kuatamiwa kwa muda wa kutosha ,yai la tai likatotolewa tai kati ya kuku .Tai huyo wakati akikua,alibeba tabia za kuku,ya kukwaruza,kucharura na kudonoadonoa Akawa akiruka umbali mfupi tu sawa na kuku , akila nafaka na wadudu,na hata akawa akiamini kabisa kuwa yeye ni kuku na sio tai.

Siku moja tai huyo akataza juu akaona kiumbe akiruka juu sana angani na kuzunguka juu sana.Akashangaa na kuuliza ni kiumbe gani anayeweza kuruka juu kiasi kile na kuzunguka kwa mwendo kasi namna ile.Akamuuliza kuku aliyekuwa jirani yake,yule ni kiumbe gani anayeweza kuruka juu kiasi kile?Kuku akamjibu."Ni tai.,ndege mwenye uwezo kuliko ndege wote.Tai akasema,Nataka kuwa kama ndege huyo.” 

Kuku akacheka kwa mshangao,Huwezi kuwa tai",wewe ni kuku.Tai akaendelea kudonoa wadudu na kusema,"Ni kweli,mimi kuku sitaweza kuwa tai ,upo sahihi." na kuridhika na maelezo ya kuku ambaye aliamini kuwa hawezi kuwa bora kama tai.
Kwa miaka yote  tai huyo akiendelea kuishi maisha sawia na ya kuku akiamini yeye ni kuku,asijue ya kuwa yeye ana uwezo mkubwa ndani mwake.Hakujaribu wala kuthubutu hata mara moja kula chakula cha aina tofauti na kile anachoona kuku wenzake wakila.Aliaminishwa kuwa jambo jingine lolote zaidi ya wafanyalo kuku,haliwezekani.Alipokufa alikufa akiwa ni kuku.


Kabla hujazaliwa walikwepo waliotutanguli,kwa maana ya babu zetu na wengine wengi waliopita.Hawa walitengeneza mfumo yao ya maisha  ambayo tunaweza kuuita mfumo wa jamii,ambao ulijenga matarajio mengi ya watu mmojammoja  na jamii nzima.Mfumo huu ni pamoja na kanuni,mila ,desturi,imani,dini,serikali,sherehe.Mfumo huu umejengwa na sheria na kanuni nyingi ambazo unapozaliwa tu,unakuwa umefungwa moja kwa moja na mfumo huo pasipo kupenda ukiamini ndio mfumo sahihi.Sheria na kanuni zilizopo katika mfumo huu ulioukuta zinapokuwa kawaida kwako,zinaufanya mfumo wako wa tafakari uwe na uelekeo na fikra zilizo ndani ya mfumo huo.
Fikra zenye mipaka huleta matokeo yasiyo huru (picha kwa hisani ya www.rfidgeneral.com)


Mfumo huu unakulazimu kujifunza na kufuata mengi kama ni nini unapaswa kufuata,kuamini,ni nini kinakubalika na nini hakikubaliki,kipi ni chema na kipi ni kibaya.MFUMO HUU WOTE UNAKUPELEKA KUFUATILIA KILA JAMBO KADIRI YA TARATIBU NA MAWAZO YA MFUMO. Unapokuwa unakuwa na fikra za kimfumo kuwa jambo fulani lipo hivi tu,na hivyo mara nyingi hujenga mpaka wa kufikiri na kuamua.Unakuwa huwezi kufanya jambo mpaka usikilize waanaokuzunguka wanasemaje.Tai aliamini kila jambo aliloambiwa na tai kwa sababu tu ni desturi.


Mwisho kabisa tunaanza kuitazama  dunia kama sehemu ya ushindani.Tunajifunza uchoyo,ubinafsi,usiri na visasi kwa sababu ya mfumo licha ya kuwa yapo mengi mazuri.

Ushindani huo unatufanye tufikiri na kutenda kwa kuangalia mitazamo ya jamii.Unakuwa huna fikra za kutafakari jambo nje ya mipaka ya jamii.HIVYO unakuwa si huru katika maamuzi juu ya maisha yako mwenyewe.Kwa kifupi unakuwa mtumwa wa mfumo huu wa jamii.,ukifikiri na kutenda katika uwanja wa fikra za jamii.Ukweli ni kwamba usipotoka katika mpaka huu na kuuvuka,kuwa huru,hutaishi kamwe maisha yako halisi.
Maisha yetu ni matokeo ya fikrazetu (picha kwa hisani ya mtandao)


Ninachotaka kukisema hapa ni kuwa ukitaka kuishi maisha unayoyachagua wewe ,na kufikia mafanikio ni lazima uchukue uamuzi wa kufikiri nje ya mipaka ya mawazo ya jamii.Ni lazima uvunje mipaka ya mazoea na ile ya sheria na kanuni za imani ya jamii.Ni lazima ujifunze kuwa huru.Naomba nieleweke vizuri hapa si kwamba nahamasisha watu wavunje sheria za nchi ama mahalia,laaah,kuvunja mazoea ni kufikiri kwa mapana bila kufungwa na mawazo yanayoaminika tu na jamii.


Imani ya jamii ina nguvu sana,na hujenga upotofu ya kuwa tunapaswa kufikiri hivi na si vile,fulani yupo hivi na vile na inamsukuma mtu kutenda kadiri ya fikra za jamii husika.Tunalazimika kuishi maisha ya bandia ili tuonekane kwa wengine(Amini nakwambia utakuwa mtumwa katika mawazo mpaka pale utakapopanua wigo /uwanja wako wa fikra).

Unakuta jamii inaamini juu ya ushirikina na uchawi katika kutafuta mafanikio,hivyo kunakuwa na imani kuwa huwezi kufanikiwa mpaka uende kwa mganga.Watoto wakiugua magonjwa mabayo ni matokeo ya maisha anayoishi basdi inaaminika amechezewa(amelogwa).Tukumbuke kuwa mtu hawezi kukutendea ubaya  kama wewe si kisababishi cha fikra za mtu huyo kukufanyia ubaya.Nakumbuka kuna rafiki yangu ambaye nilisoma pamoja nae,alikuwa namsukumo sana kwa wengine,akiwaaminisha kuwa ili uwe bora na rafiki yake ni lazima uwe unakunywa pombe ama kuzisifia.Hii yote ni matokeo ya imani na fikra za kimfumo.

Hivyo tukumbuke kuwa kama tunaishi tukifikiri na kutenda kwa mipaka ya imani za wengine,basi sisi ni watumwa wa imani hizo mpaka pale tutakapotoka nje ya mipaka hiyo katika kufikiri na kutenda.Tunatafuta kukubaliwa na mawazo na mitazamo ya vikundi fulani.Tukumbuke kuwa picha halisi juu ya kinyago huwa sahihi kwa mchongaji,ambaye anachonga akiwa na picha yake katika fikra kuwa nataka awe hivi.Ukiwauliza wateja wanaonunua kinyago,kila mmoja atatafsiri kadiri ya fikra zake pia.
Mabadiliko katika fikra na maendeleo yako yanaanza pale unapoanza kufikiri nje ya mipaka ya wengine(picha kwa hisani ya mtandao)


Kwa nini uishi kwa mawazo ya wengine?Kwa nini uumie unapoambiwa una sura mbaya wakati hayo ni maoni ya msemaji tu.Ukitaka kupata majibu juu ya maisha yako,chimba ndani yako..Tafuta ndani yako.Ninaamini kila jambo huanza na wewe(mimi),Utajiri na mafanikio yote yanatoka ndani mwa muhusika.Zawadi kubwa juu ya maisha yako ni kuithamini nafsi yako  na kuisikiliza sauti kubwa itokayo moyoni mwako,ikuongozae juu ya kutenda,hii ni sauti ya Mungu iletayo mafanikio,furaha na kila lililo jema.Sauti hii inakupa nguvu ya kutenda miujiza kila wakati,ndiyo inayofanya nuru ya maisha yako ing'ae.

Jamii inakufanya ulazimike kuenenda kimawazo na fikra kadiri ya imani yake.Kwa nini usikuballi jinsi ulivyo na kuanza kuchimbandani yako palipo na siri kuu ya maisha yako?Mimi binafsi natambua jinsi ninavoonekana.Najikubali kwa kuwa mimi ni zaidi ya nilivyo.Ukiachilia mbali mazingira ninayoishi na sura yangu,mimi ni wa thamani,kama wengine.Wewe ni wa thamani jinsi ulivyo,na thamani yako ni sawa na binadamu wote.Unao uwezo wa kuwa na kuishi maisha ya furaha na mafanikio.Unastahili,wewe ni Matokeo ya kazi kubwa ya Mungu. 



Sasa anza kujikubali na kuepuka misukumo ya wale wanaokuzunguka.Anza kutazama uwezo ulio nao,tazama chemchem ya mafanikio iliyopo ndani mwako.Sisi sote ni bora .Sisi wote ni wamoja.
Huu ni wakati wa kujifunza kuwa wewe,kujikubali,kukua na kubadilika.Anzakujitambua wewe kisha utatambulika kwa wengine.


Vumbua uwezo ulionao.Tumia uwezo ulionao kupaa  juu ya mipaka unayofikiri ipo.Fanya yale unayoyakusudia maishani na uwe vile unavyotaraji kuwa.Umezaliwa kuwa kiongozi wa maisha yako na kuyatawala mazingira yako.Unaweza kupaa juu zaidi na zaidi pasipo kudondoka.Mipaka ulionayo ni ya kifikra tu.Usiruhusu fikra za wanaokuzunguka zikufanye uwe na mawazo mgando ama yenye mipaka.Huwezi kuruka juu kama utabaki na fikra kama za kuku na kuendelea kukwaruza na kudonoa tu.Amua sasa kuruka.
Karibu tujadiliane
Pongu Joseph F-0717903089,0765046644

Monday, February 18

WANAWAKE AMKENI


MWANAMKE-FURAHA ITOKAYO MOYONI-CHIMBUKO LA UPENDO
                                 
Ni miaka mingi imepita toka palipoingia mfumo wa kundamizi kwa  wanawake.Mfumo huu umemfanya mwanamke kudharaulika ,matokeo yake wanawake wenyewe wamekubaliana na mfumo huo bila kutambua.Nilipata kueleza jinsi mazingira tunayoyaishi yanavyoweza kupelekea kubadili fikra za mtu,hasa pale akiwa hatambui kuwa yeye ndiye anayepaswa kuyatawala mazingira.Wanawake wamekumbwa na mfumo huo.Mtu binafsi anapoukubali mfumo Fulani,huuona ni wa kawaida na hata kuuishi na kuusifia,asijue athari zake katika ujenzi wa maisha yake.

Mfumo huu kandamizi,umeonekana kuwa ni usahihi.Dini pia zimeingia katika kuuchagiza mfumo huu.Mara kadhaa zikifundisha ama kuwajengea waamini wake fikra kuwa  kuwa mwanaume yupo juu ya mwanamke.Wanaume wanaamini kuwa kuwa  na nguvu ni kumtawala mwingine badala ya kuyatawala mazingira na hivyo maisha ,wanafikiri kuwatawala wanawake.Wanaume wamekuwa wakijisifia kwa kuzaliwa jinsia ya kiume.Wamekuwa wakitoa maneno ya kejeli na dhalili dhidi ya jinsia ya pili(mwanamke).Mfumo huu ukakua na ndipo jinsia ya kike ilipoanza kutazamwa kuwa si bora.Ukweli ni kwamba hakuna jinsia iliyo bora kuliko nyingine.Kila jinsia ni bora jinsi ilivyo pasipo  kusahau kuwa  kila jambo huwa lina upekee wake.

Miaka ya hivi karibuni umeingia mfumo wa utandawazi.Mfumo ambao mifumo ya ,mawazo,uchumi,utamaduni inalengwa kufanywa kuwa sawia.Ni mfumo shindani ambao wanaoweza kuyatawala mazingira yao,wanafaidika kuliko wale wasiojitambua.Mfumo huu umewaathiri pia wanawake.Tumeshihudia wanawake wakivaa mavazi yanayoonesha sehemu zao nyeti,wakicheza picha za ngono na kudhalilishwa.Wanawake wanaonekana kuwa ni chombo cha starehe na dhalili.Kwenu ninyi wanawake,mnapaswa kuchukua hatua,kujitazama upya,mnawaza nini kila mmoja dhidi yenu wenyewe? Je mpo tayari kutumika kama msio na thamani kwenye matangazo,sinema na kwenye mawazo ya wanadamu wote? Je mpo tayari kujenga dunia duni yenye dhiki,chuki na isiyo na uelekeo?Mpo tayari kuendelea kutazamwa kuwa hamuwezi?

Leo ningependa wanawake waamke na kuvumbua siri kubwa ndani mwao.Hakuna wa kuchukua hatua ni ninyi wanawake,kila mmoja kwa nafsi yake. Ninyi ni wa thamani.Ni zaidi ya sura zenu,zaidi ya maumbile yenu.Ni zaidi ya mavazi mnayovaa.Uzuri wa mwanamke ni nuru iliyopo ndani mwake inayoangaza dunia kwa upendo.Ni nuru anayosubiria itumike kuimulika dunia,kuifanya kuwa sehemu bora ya kuishi. 

Ni nuru hiyo iliyo ndani mwenu ambayo ikiruhusiwa kutolewa huzaa upendo,amani,usawa,haki na chemchem zote za upendo.Anayetambua ni yule aliye tayari kuchimba ndani mwake na kugundua kuwa kama mwanamke, anaijenga na kuibomoa dunia kadiri ya matumizi ya uwezo aliopewa.Uwezo wenu upo ndani yenu.uzuri wenu upo ndani mwenu na si kwenye mavazi na maumbile tu.Uzuri huo ulio ndani mwenu,unapotumika hutoa matokea yanayotoa picha ya uzuri wenu,yaani Upendo.Kichwani mwenu na moyoni mwenu mmebeba hazina kubwa.Ninyi ni bora,zaidi ya mwili unaoonekana,zaidi ya idadi ya namba,idadi ya nyota..
                             

Wanawake ni viumbe muhimu katika dunia hii.Ndio wazazi wa kila jambo katika dunia hii.  Ni chumbuko la wema na upendo hapa duniani.Kupitia mwanamke binadamu wanazaliwa.Wakombozi wa fikra,wapigania haki,wahimiza upendo,wapigania amani wote wametoka kwa mwanamke.

Mungu alimuumba mwanamke na kumuwekea uzuri wa kila namna ndani mwake,ali kila apitiaye tumboni mwa mwanamke aubebe uzuri huo na kuuishi  hapa duniani.Katika kipindi chote aishipo akikua tumboni mwa mwanamke,kiumbe anayetarajiwa kuzaliwa  hubewa chemchem ya kila kitokacho kwa mama.Hivyo mwanamke anahusika katika kuijenga dunia iliyo bora.Ule usemi wa kuwa ukimuelimisha mwanamke,umeielimisha jamii,ni sahihi..kinyume chake pia ni sahihi.

Dunia tuliyonayo sasa,mwonekano wake,matukio na kila tukipatacho,ni matokeo ya usanifu wetu wenyewe.Ni matokeo ya mwanamke na mwanamume,mwanamke akihusika kwa kiasi kikubwa.Chuki zilizopo,matabaka yaliyopo,visasi,mauaji ni matokeo ambayo yameanza katika dunia isiyoonekana iliyopo ndani mwetu,na kisha tumeijenga katika mwonekano uliopo.

Ukandamizaji wa wanawake ,na udhalilishaji unatoa matokeo ya jamii kandamizi na dhalili.
Wanawake mnayo nafasi ya kujenga dunia mpya.Inayoanza ndani mwenu.Ubikira wenu (ukamilifu ndani mwenu) utumike kuimulika dunia,kuwa sehemu bora.Mwanamke akiutambua ubikira ndani mwake,maajabu makubwa ya mabadiliko ya maisha yake huanza,Maisha mapya,bora hutokea.Wanawake amkeni.
Kila mmoja wenu akiamka,mtaamsha dunia mpya.Tuanze kuwafunza watoto wetu juu ya thamani yao.Waanze kuthamini hazina walio nayo ndani mwao.Washeni mishumaa iliyo ndani mwenu,iimulike dunia kwa upendo.Mulikeni muondoe mtazamo mbaya wa jamii juu ya mwanamke.Jukumu ni lenu.Nguvu mlionayo haijapotea,kinachohitajika ni kuiamsha.Licha ya magumu mtafika.

Monday, February 4

RAFIKI WA KWELI

Rafiki wa kweli ni yule ambaye unaweza kumwamini,ni yule ambaye unaweza kumshirikisha furaha,huzuni na kila tamanio la moyo wako,ni yule ambaye hakuhukumu kwa kufikiri tu,ama kusikia toka kwa wengine,ni yule anayekubali na kuheshimu maamuzi yako,uchaguzi wako na uhuru wako,ni yule ambaye yupo tayari kutumia alichonacho kwa ajili yako,ni yule anayeweza kukukosoa na kukufanya utambue njia bora na kukua ukiendelea mbele daima,hutambua umuhimu wako na kukupa moyo,kukuamsha uwe bora zaidi na kufikia mafanikio,Hukusikiliza na kukushauri pale panapostahili na unapohitaji...daima huwa kwa ajili yako..rafiki wa kweli hawezi kuwa na ajenda za siri,hawezi kukuzunguka n A KUKUSALITI...rafiki wa kweli hufurahi pale unapofanikiwa na si kuweka kinyongo na kuumia pale unapofanikiwa,daima huwa pamoja nawe......na ni furaha kubwa pale unapogundua kuwa rafiki yako mkuu ni wewe mwenyewe....furaha pia ni kumpata rafiki wa kweli ..ni wachache....daima nafurahi kupata marafiki ambao wanathamini uwepo wangu,ambao hufurahi wakiona nasonga mbele.Ambao wako tayari kujitolea kwa ajili ya wengine,hasa kupitia blog hii .nitakuwa sina fadhila kama sitasema ahsante itokayo katika furaha ya moyo wangu

Saturday, February 2

CHUKUA HATUA

Mafanikio huanza pale unapoacha kuogopa na kuanza kuchukua hatua,yanaanza pale unapoacha kulaumu wengine juu ya matatizo yanayokukabili wewe, ambayo ukweli ni kwamba wewe ndiye msanifu mkuu.Yanaanza pale unapoacha kuogopa mazingira na kutafuta visingizio,na kuanza kuyatazama mazingira kama nafasi ya kwenda mbele na kuyatumia vema.Ni pale unapotafuta kuzigundua mbegu na nguvu zinazoendesha maisha yako na kugundua kuwa zipo ndani yako,na kuzitumia,ukichukua hatua juu ya kila mipango na malengo uliyoyaweka maishani mwako