Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Sunday, April 27

Waraka kwa vijana wote

Barua Ya Wazi Kwa
Kijana Wa Kitanzania
-na Makirita Amani

Hakuna kipindi kigumu kwenye
maisha ya mwanadamu kama
muongo wa tatu wa maisha
yaani kati ya miaka 20 mpaka
30. Huu ni wakati ambao una
changamoto nyingi sana za
maisha na ni wakati ambao
unaweza kujenga au kubomoa
maisha yako moja kwa moja.
Kama wewe upo katika kipindi
hiki endelea kusoma hapa ili
uweze kupata mwanga pale
mambo yanapokwenda
usivyotarajia. Kama umri wako
umezidi hapo unaweza kusoma
pia na ukawashauri wadogo
zako au watoto wako. Na hata
kama umri wako uko chini ya
hapa sio vibaya ukajifunza na
kujua ni nini unakwenda
kukutana nacho mbele.
Huu ni wakati mgumu sana
kwako.
Kwa maisha yetu ya kitanzania,
kijana wa miaka kati ya 20-30
anakuwa anaingia elimu ya
chuo, yuko chuoni, amemaliza
chuo, anatafuta kazi au ndio
ameanza kazi. Pia ni wakati
ambao kijana huyu anakuwa
kwenye mahusiano ya mapenzi,
uchumba na hata kuingia
kwenye ndoa. Pia ni wakati
ambao wengi wanaondoka
kwenye mikono ya wazazi au
walezi na kwenda kujitegemea
wenyewe. Mambo yote haya
yameleta changamoto kubwa
sana kwa kijana na kwa
changamoto hizi kijana
anaweza kujijenga au
kujibomoa.
Changamoto kubwa
anazokutana nazo kijana katika
wakati huu ni;
1. Kumaliza elimu ya sekondari
na kwenda kuanza maisha ya
tofauti kabisa vyuoni. Kuna
tofauti kubwa sana ya elimu ya
sekondari na elimu ya chuo,
wakati sekondari unasimamiwa
sana, chuoni unakuwa na
uhuru zaidi. Kwa uhuru huu
vijana wengi wamejikuta
wanafanya mambo ambayo
yanasababisha washindwe
kufatilia masomo yao vizuri.
2. Kuingia kwenye mahusiano
ya kimapenzi na kuvunjika kwa
baadhi ya mahusiano.
Mahusiano sio rahisi katika
umri huu, kijana anakutana na
mwenzake ambaye anafikiri
wanapendana sana na siku
moja watakuwa mume na mke
baada ya muda anagundua
mtu aliyeingia nae kwenye
mapenzi hakumjua vizuri. Hii
inapelekea mapenzi kuvunjika
na kuumizwa sana.
3. Kukabiliana na maisha ya
masomo vyuoni na maisha
mengine ya kijamii. Licha ya
masomo kuna shughuli nyingi
za kijamii na binafsi pia. Kuna
vijana wanajikuta wakiendekeza
starehe sana na kusahau
masomo, wengine wanajikuta
wakikazana na masomo sana
na kusahau nini kinaendelea
kwenye jamii.
4. Kupata ajira baada ya
kumaliza chuo. Hii ndio
changamoto kubwa sana hasa
nyakati hizi. Vijana wanatoka
vyuoni wakiwa na habari nzuri
walizodanganywa kwamba
ukisoma na kufaulu vizuri
utapata kazi nzuri na kuwa na
maisha mazuri. Ni pale
wanapojikuta mtaani mwaka
mzima wakizunguka na
bahasha bila ya kupata kazi
ndio wanagundua maisha sio
rahisi kama walivyodanganywa.
5. Kuanza kazi na kukabiliana
na changamoto za kazi. Kupata
kazi ni kitu kimoja, kufanya kazi
na kuridhishwa nayo au
kuifurahia ni kitu kingine. Kuna
changamoto nyingi sana
kwenye kazi hasa kwa
wafanyakazi wageni, pia jinsi ya
kuchangamana na watu wenye
haiba tofauti ni kazi kubwa
sana kwa kijana.
5. Kuanza maisha ya
kujitegemea mwenyewe na
kuweza kufanya maamuzi
sahihi. Katika wakati huu kijana
anaweza kuona ana uhuru
mkubwa sana wa kufanya yale
aliyokuwa anashindwa kufanya
wakati yuko kwenye mikono ya
wazazi au walezi. Ni katika
wakati huu wengi wanafanya
starehe kupitiliza na kujikuta
wanapotelea katika ulevi.
6. Kuingia kwenye ndoa na
kuanza maisha ya kifamilia.
Katika wakati huu kijana
anaingia kwenye ndoa na
kuanza maisha ya familia.
Maisha ya ndoa ni tofauti sana
na maisha ya mapenzi na
uchumba, hapa ndipo kijana
anamfahamu vizuri mwenzake
na kwa kushindwa kupambana
na changamoto za ndoa, ndoa
nyingi zinaishia kuvunjika
mapema sana.
Kutokana na ukosefu wa elimu
ya kupambana na changamoto
hizi za maisha vijana wengi
sana maisha yao yamepotelea
kwenye kipindi hiki na kuja
kushtuka baadae wakati umri
umekwenda na kujiuliza ni
wapi mambo yalikwenda
hovyo.
Kijana ufanye nini
kukabiliana na changamoto
hizi?
Hapa nitazungumzia mambo
matano muhimu ambayo kijana
anatakiwa kufanya au kujua ili
kuweza kuvuka salama kipindi
hiki kigumu.
1. Kuna wakati hutajua
unafanya nini.
Katika kipindi hiki cha maisha
kuna wakati hutajua ni nini
unafanya kwenye maisha yako
au ni wapi maisha yako
yanaelekea. Usikatishwe tamaa
na hali hii bali weka mipango
na malengo ya maisha yako na
ujitahidi kutekeleza.
2. Maisha hayatakuwa vile
unavyopanga au kufikiri
yatakuwa.
Mambo yanabadilika tena kwa
kasi sana, pamoja na kuwa na
mipango mizuri bado hutoweza
kuitimiza yote hasa ndani ya
kipindi hiki. Utajitahidi sana
lakini kuna ambavyo
vitakushinda. Usife moyo,
endelea na maisha yako
mwisho wa siku maisha lazima
yataenda. Kingine cha muhimu
zaidi jua unahitaji muda ili
kufikia mafanikio yoyote
unayofikiria, hakuna kitu
kinachokuja haraka na kwa
urahisi.
3. Sio kila mtu anayekuja
kwenye maisha yako atakaa.
Hili nalisema hasa kwenye
mahusiano ya kimapenzi.
Usifikiri mpenzi uliyempata ni
lazima uje uishi naye, kuna
uwezekano mkashindwa
kuendana na kila mtu
akachukua hamsini zake.
Badala ya kulaumu na kuharibu
maisha yako furahia kwamba
huyo ni mmoja wa watu ambao
walikuwa wakupita tu kwenye
maisha yako. Umekuwa na
marafiki wengi kwanzia utoto
mpaka sasa, wengi kwa sasa
hujui hata wako wapi, ndivyo
maisha yalivyo. Kuna
watakaokuja na kukaa, kuna
wengine watapita tu.
4. Uhuru una mipaka yake.
Kwa kuwa umefika wakati wa
wewe kujitegemea na kuwa
huru na maisha yako,
haimaanishi unaweza kufanya
chochote unachotaka na
maisha yako. Ni lazima uwe na
busara ya kujua ni kipi kizuri
kwenye maisha yako na kipi
kibaya. Kama unaenda disko na
kulewa kila mwisho wa wiki kwa
sababu ulikosa haya ulipokuwa
nyumbani, fikiria maisha yako
ya mbele unataka yaweje kisha
punguza mambo ambayo
yatakuzuia kufika kule.
5. Jaribu mambo mengi sana
katika wakati huu.
Jaribu kufanya vitu vingi sana
kwenye kipindi hiki, usiridhike
na kazi moja unayotafuta au
uliyopata. Huenda mpaka sasa
hujajua ni nini unafurahia
kufanya au hujajua vipaji
vyako. Katika wakati huu
ambao bado hujawa na
majukumu makubwa unaweza
kujaribu kufanya vitu vya
tofauti kwenye maisha yako ili
kujua ni nini unafurahia
kufanya. Muhimu zaidi
tengeneza vyanzo mbadala vya
kipato katika wakati huu.
6. Jifunze, jifunze, jifunze
Vijana wengi wanaomaliza
elimu zao huona kujifunza ndio
kumefika mwisho. Au
watajifunza tena wakienda
kuongeza masomo. Hili ni kosa
kubwa sana, jifunze kila siku
kutoka kwa watu na kwa
kujisomea vitabu vya
kukuendeleza. Kama unakosa
kabisa cha kujifunza tembelea
AMKA MTANZANIA na
utajifunze mengi sana. Kama
hujifunzi unarudi nyuma na
kama unarudi nyuma hutoweza
kupambana na changamoto za
maisha hivyo maisha yako
yatakuwa magumu sana.
7. Dunia haiko sawa.
Kuna wakati kijana unafikiri
dunia ingetakiwa kuwa sawa na
kuona kama unaonewa. Ukweli
ni kwamba dunia haijawahi
kuwa sawa na haitokuja kuwa
sawa. Unaweza kufanya kazi
kwa bidii na maarifa halafu
mwenzako akaja kuchukua
pongezi zako, unaweza kufanya
haki na bado ukaingizwa
kwenye uhalifu, unaweza kuwa
na elimu kubwa na ufaulu
mzuri ila ambaye hana elimu
ndio akawa bosi wako kazini,
unaweza kuwa na roho nzuri
na ukazulumiwa, haya yote ni
maisha.
8. Chocote kitakachotokea
jua huo sio mwisho wa dunia.
Hata litokee jambo baya kiasi
gani kwenye maisha yako kama
bado upo hai basi jua unaweza
kuyafanya maisha yako kuwa
bora zaidi. Usikubali
changamoto yoyote iharibu
maisha yako, jua itapita na
maisha yataendelea. Kila kitu
kinapita, hata hayo magumu
unayopitia yatapita, hakikisha
maisha yako yanakuwa imara
baada ya mapito hayo.
9. Safiri.
Jitahidi sana katika kipindi hiki
jitahidi sana usafiri sehemu
mbalimbali ndani na nje ya
nchi. Kusafiri na kwenda
sehemu ngeni kunakufanya
ufikiri tofauti na uwe na
mtizamo mpana sana kwenye
maisha yako. Kama umezaliwa
moshi ukasoma na kukulia
moshi, ukafanya kazi na kuishi
moshi utakuwa na mawazo
mgando sana kwa sababu
unaona mambo na
changamoto zile zile kila siku.
Ila unaposafiri na kuishi na
watu wenye maisha na
mitizamo tofauti na ya kwako
hapo ndipo unapoweza
kujifunza zaidi.
10. Furahia kila hatua ya
maisha yako.
Kama unatamani nyakati
ngumu zifutike kwenye maisha
yako hujajua umuhimu wake.
Kila changamoto unayokutana
nayo inakujenga uwe mtu bora
zaidi. Furahia kila hatua
unayopitia kwenye maisha
yako, iwe ni ya kufurahisha au
ya kuumiza. Kuna somo
muhimu la kujifunza kwenye
kila jambo na kila mtu
unayekutana naye.
Kijana haya maisha ni ya
kwako, yapangilie maisha yako
na uyaishi. Usiogope
changamoto unazokutana nazo
hizi ndizo zinazokusaidia ukue
zaidi. Usilalamike wala
usilaumu yeyote, chukua hatua
juu ya maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika
wakati huu mgumu sana
kwenye maisha yako, nina
imani utavuka wakati huu
ukiwa salama na ukiwa na
malengo makubwa.
Kumbuka , TUKO PAMOJA.
Mshirikishe kijana mwenzako
mafunzo haya ili naye ajifunze,
bonyeza kitufe cha facebook