KARIBU SANA
HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH
Friday, August 2
Wednesday, April 4
SAFARI YA KUTAMBUA KWA NINI UPO DUNIANI.
Saturday, February 17
MAISHA YAKO YANA THAMANI GANI KWA WENGINE?>
Kipawa ulichopewa, uwezo wa ubunifu uliopewa,ujuzi uliopewa,umeutumia namna gani kwa ajili ya wengine,kama utukufu kwa aliyekuumba?
Wakati mwingi tumekuwa tukitazama tunapata nini,tunaongeza nini kwa ajili yetu pasipo kutazama ni kwa namna gani umekuwa mwenye manufaa kwa dunia na viumbe wote.
Hii ndiyo sababu inayonisukuma kuendelea kuandika,ili niwe sababu ya faraja,mabadiliko ,changamoto na hata chemchem ya wengine kujitambua.
Tuesday, December 20
KITABU KITAKACHOKUWEZESHA KUWEKA KUMBUKUMBU YA MAPATO NA NMATUMIZI YAKO
Nimeandaa kitabu kitakachokurahisishia kuweka kumbukumbu juu ya ulichozalisha(wapi,lini,namna gani,kiasi gani) na hivyo kujua unakitumiaje.
Ni kitabu kidogo chenye kurasa 32 (karatasi 8) kiitwacho BAJETI YAKO MIKONONI MWAKO /YOUR BUDGET ON YOUR HAND.Kipo kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza,Ni wewe utachagua unapenda cha lugha gani.
Hauhitaji kuwa na elimu ya uhasibu ama biashara ili kuweza kukitumia,kila kitu kimerahisishwa. Unachohitaji ni kuweka kumbukumbu kwa usahihi kama utakavyokuta kwenye maelezo.Kwa nini unapaswa kuwa na kitabu hiki kabla ya kuanza mwaka
1.Utaweza kujua mapato yako yanatokana vema na nini na namna gani uweke bidi
2.Kitakurahisishia kujua matumizi yasiyokuwa na tija na kuyaepuka.
3.Kitakuwezesha kujua vyanzo vyako vya mapato halisi na vyanzo vya matumizi makubwa
4.Ni rahisi kukitumia,kidogo na rahisi kukibeba.
5.Kitakurahisishia kuweka mikakati ya kimaendeleo na kuweka vipaumbele
6.Kitakurahisishia kujua ulipata kiasi gani kwa wiki,juma,mwezi na hata mwaka na hivyo kujua napopaswa kuongeza bidi na kupunguza /kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima
7.Kitakurahisishia kupanga mipango ijayo kwani utajua mapato yako na matumizi halisi nay ale yanayojitokeza.
8.Ni kizuri kwa watu wote wenye nia ya kupanga mipango ya kiuchumi na kuitekeleza.
9.Unajenga tabia ya kuthamini kidogo ulichonacho
UNAKIPATAJE?
Kitabu kinapatikana kwa bei ya tshs 5,000/= .Wasiliana nami kwa namba 0765046644 ama 0717903089 utaletewa popote ulipo.
Sunday, April 27
Waraka kwa vijana wote
Barua Ya Wazi Kwa
Kijana Wa Kitanzania
-na Makirita Amani
Hakuna kipindi kigumu kwenye
maisha ya mwanadamu kama
muongo wa tatu wa maisha
yaani kati ya miaka 20 mpaka
30. Huu ni wakati ambao una
changamoto nyingi sana za
maisha na ni wakati ambao
unaweza kujenga au kubomoa
maisha yako moja kwa moja.
Kama wewe upo katika kipindi
hiki endelea kusoma hapa ili
uweze kupata mwanga pale
mambo yanapokwenda
usivyotarajia. Kama umri wako
umezidi hapo unaweza kusoma
pia na ukawashauri wadogo
zako au watoto wako. Na hata
kama umri wako uko chini ya
hapa sio vibaya ukajifunza na
kujua ni nini unakwenda
kukutana nacho mbele.
Huu ni wakati mgumu sana
kwako.
Kwa maisha yetu ya kitanzania,
kijana wa miaka kati ya 20-30
anakuwa anaingia elimu ya
chuo, yuko chuoni, amemaliza
chuo, anatafuta kazi au ndio
ameanza kazi. Pia ni wakati
ambao kijana huyu anakuwa
kwenye mahusiano ya mapenzi,
uchumba na hata kuingia
kwenye ndoa. Pia ni wakati
ambao wengi wanaondoka
kwenye mikono ya wazazi au
walezi na kwenda kujitegemea
wenyewe. Mambo yote haya
yameleta changamoto kubwa
sana kwa kijana na kwa
changamoto hizi kijana
anaweza kujijenga au
kujibomoa.
Changamoto kubwa
anazokutana nazo kijana katika
wakati huu ni;
1. Kumaliza elimu ya sekondari
na kwenda kuanza maisha ya
tofauti kabisa vyuoni. Kuna
tofauti kubwa sana ya elimu ya
sekondari na elimu ya chuo,
wakati sekondari unasimamiwa
sana, chuoni unakuwa na
uhuru zaidi. Kwa uhuru huu
vijana wengi wamejikuta
wanafanya mambo ambayo
yanasababisha washindwe
kufatilia masomo yao vizuri.
2. Kuingia kwenye mahusiano
ya kimapenzi na kuvunjika kwa
baadhi ya mahusiano.
Mahusiano sio rahisi katika
umri huu, kijana anakutana na
mwenzake ambaye anafikiri
wanapendana sana na siku
moja watakuwa mume na mke
baada ya muda anagundua
mtu aliyeingia nae kwenye
mapenzi hakumjua vizuri. Hii
inapelekea mapenzi kuvunjika
na kuumizwa sana.
3. Kukabiliana na maisha ya
masomo vyuoni na maisha
mengine ya kijamii. Licha ya
masomo kuna shughuli nyingi
za kijamii na binafsi pia. Kuna
vijana wanajikuta wakiendekeza
starehe sana na kusahau
masomo, wengine wanajikuta
wakikazana na masomo sana
na kusahau nini kinaendelea
kwenye jamii.
4. Kupata ajira baada ya
kumaliza chuo. Hii ndio
changamoto kubwa sana hasa
nyakati hizi. Vijana wanatoka
vyuoni wakiwa na habari nzuri
walizodanganywa kwamba
ukisoma na kufaulu vizuri
utapata kazi nzuri na kuwa na
maisha mazuri. Ni pale
wanapojikuta mtaani mwaka
mzima wakizunguka na
bahasha bila ya kupata kazi
ndio wanagundua maisha sio
rahisi kama walivyodanganywa.
5. Kuanza kazi na kukabiliana
na changamoto za kazi. Kupata
kazi ni kitu kimoja, kufanya kazi
na kuridhishwa nayo au
kuifurahia ni kitu kingine. Kuna
changamoto nyingi sana
kwenye kazi hasa kwa
wafanyakazi wageni, pia jinsi ya
kuchangamana na watu wenye
haiba tofauti ni kazi kubwa
sana kwa kijana.
5. Kuanza maisha ya
kujitegemea mwenyewe na
kuweza kufanya maamuzi
sahihi. Katika wakati huu kijana
anaweza kuona ana uhuru
mkubwa sana wa kufanya yale
aliyokuwa anashindwa kufanya
wakati yuko kwenye mikono ya
wazazi au walezi. Ni katika
wakati huu wengi wanafanya
starehe kupitiliza na kujikuta
wanapotelea katika ulevi.
6. Kuingia kwenye ndoa na
kuanza maisha ya kifamilia.
Katika wakati huu kijana
anaingia kwenye ndoa na
kuanza maisha ya familia.
Maisha ya ndoa ni tofauti sana
na maisha ya mapenzi na
uchumba, hapa ndipo kijana
anamfahamu vizuri mwenzake
na kwa kushindwa kupambana
na changamoto za ndoa, ndoa
nyingi zinaishia kuvunjika
mapema sana.
Kutokana na ukosefu wa elimu
ya kupambana na changamoto
hizi za maisha vijana wengi
sana maisha yao yamepotelea
kwenye kipindi hiki na kuja
kushtuka baadae wakati umri
umekwenda na kujiuliza ni
wapi mambo yalikwenda
hovyo.
Kijana ufanye nini
kukabiliana na changamoto
hizi?
Hapa nitazungumzia mambo
matano muhimu ambayo kijana
anatakiwa kufanya au kujua ili
kuweza kuvuka salama kipindi
hiki kigumu.
1. Kuna wakati hutajua
unafanya nini.
Katika kipindi hiki cha maisha
kuna wakati hutajua ni nini
unafanya kwenye maisha yako
au ni wapi maisha yako
yanaelekea. Usikatishwe tamaa
na hali hii bali weka mipango
na malengo ya maisha yako na
ujitahidi kutekeleza.
2. Maisha hayatakuwa vile
unavyopanga au kufikiri
yatakuwa.
Mambo yanabadilika tena kwa
kasi sana, pamoja na kuwa na
mipango mizuri bado hutoweza
kuitimiza yote hasa ndani ya
kipindi hiki. Utajitahidi sana
lakini kuna ambavyo
vitakushinda. Usife moyo,
endelea na maisha yako
mwisho wa siku maisha lazima
yataenda. Kingine cha muhimu
zaidi jua unahitaji muda ili
kufikia mafanikio yoyote
unayofikiria, hakuna kitu
kinachokuja haraka na kwa
urahisi.
3. Sio kila mtu anayekuja
kwenye maisha yako atakaa.
Hili nalisema hasa kwenye
mahusiano ya kimapenzi.
Usifikiri mpenzi uliyempata ni
lazima uje uishi naye, kuna
uwezekano mkashindwa
kuendana na kila mtu
akachukua hamsini zake.
Badala ya kulaumu na kuharibu
maisha yako furahia kwamba
huyo ni mmoja wa watu ambao
walikuwa wakupita tu kwenye
maisha yako. Umekuwa na
marafiki wengi kwanzia utoto
mpaka sasa, wengi kwa sasa
hujui hata wako wapi, ndivyo
maisha yalivyo. Kuna
watakaokuja na kukaa, kuna
wengine watapita tu.
4. Uhuru una mipaka yake.
Kwa kuwa umefika wakati wa
wewe kujitegemea na kuwa
huru na maisha yako,
haimaanishi unaweza kufanya
chochote unachotaka na
maisha yako. Ni lazima uwe na
busara ya kujua ni kipi kizuri
kwenye maisha yako na kipi
kibaya. Kama unaenda disko na
kulewa kila mwisho wa wiki kwa
sababu ulikosa haya ulipokuwa
nyumbani, fikiria maisha yako
ya mbele unataka yaweje kisha
punguza mambo ambayo
yatakuzuia kufika kule.
5. Jaribu mambo mengi sana
katika wakati huu.
Jaribu kufanya vitu vingi sana
kwenye kipindi hiki, usiridhike
na kazi moja unayotafuta au
uliyopata. Huenda mpaka sasa
hujajua ni nini unafurahia
kufanya au hujajua vipaji
vyako. Katika wakati huu
ambao bado hujawa na
majukumu makubwa unaweza
kujaribu kufanya vitu vya
tofauti kwenye maisha yako ili
kujua ni nini unafurahia
kufanya. Muhimu zaidi
tengeneza vyanzo mbadala vya
kipato katika wakati huu.
6. Jifunze, jifunze, jifunze
Vijana wengi wanaomaliza
elimu zao huona kujifunza ndio
kumefika mwisho. Au
watajifunza tena wakienda
kuongeza masomo. Hili ni kosa
kubwa sana, jifunze kila siku
kutoka kwa watu na kwa
kujisomea vitabu vya
kukuendeleza. Kama unakosa
kabisa cha kujifunza tembelea
AMKA MTANZANIA na
utajifunze mengi sana. Kama
hujifunzi unarudi nyuma na
kama unarudi nyuma hutoweza
kupambana na changamoto za
maisha hivyo maisha yako
yatakuwa magumu sana.
7. Dunia haiko sawa.
Kuna wakati kijana unafikiri
dunia ingetakiwa kuwa sawa na
kuona kama unaonewa. Ukweli
ni kwamba dunia haijawahi
kuwa sawa na haitokuja kuwa
sawa. Unaweza kufanya kazi
kwa bidii na maarifa halafu
mwenzako akaja kuchukua
pongezi zako, unaweza kufanya
haki na bado ukaingizwa
kwenye uhalifu, unaweza kuwa
na elimu kubwa na ufaulu
mzuri ila ambaye hana elimu
ndio akawa bosi wako kazini,
unaweza kuwa na roho nzuri
na ukazulumiwa, haya yote ni
maisha.
8. Chocote kitakachotokea
jua huo sio mwisho wa dunia.
Hata litokee jambo baya kiasi
gani kwenye maisha yako kama
bado upo hai basi jua unaweza
kuyafanya maisha yako kuwa
bora zaidi. Usikubali
changamoto yoyote iharibu
maisha yako, jua itapita na
maisha yataendelea. Kila kitu
kinapita, hata hayo magumu
unayopitia yatapita, hakikisha
maisha yako yanakuwa imara
baada ya mapito hayo.
9. Safiri.
Jitahidi sana katika kipindi hiki
jitahidi sana usafiri sehemu
mbalimbali ndani na nje ya
nchi. Kusafiri na kwenda
sehemu ngeni kunakufanya
ufikiri tofauti na uwe na
mtizamo mpana sana kwenye
maisha yako. Kama umezaliwa
moshi ukasoma na kukulia
moshi, ukafanya kazi na kuishi
moshi utakuwa na mawazo
mgando sana kwa sababu
unaona mambo na
changamoto zile zile kila siku.
Ila unaposafiri na kuishi na
watu wenye maisha na
mitizamo tofauti na ya kwako
hapo ndipo unapoweza
kujifunza zaidi.
10. Furahia kila hatua ya
maisha yako.
Kama unatamani nyakati
ngumu zifutike kwenye maisha
yako hujajua umuhimu wake.
Kila changamoto unayokutana
nayo inakujenga uwe mtu bora
zaidi. Furahia kila hatua
unayopitia kwenye maisha
yako, iwe ni ya kufurahisha au
ya kuumiza. Kuna somo
muhimu la kujifunza kwenye
kila jambo na kila mtu
unayekutana naye.
Kijana haya maisha ni ya
kwako, yapangilie maisha yako
na uyaishi. Usiogope
changamoto unazokutana nazo
hizi ndizo zinazokusaidia ukue
zaidi. Usilalamike wala
usilaumu yeyote, chukua hatua
juu ya maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika
wakati huu mgumu sana
kwenye maisha yako, nina
imani utavuka wakati huu
ukiwa salama na ukiwa na
malengo makubwa.
Kumbuka , TUKO PAMOJA.
Mshirikishe kijana mwenzako
mafunzo haya ili naye ajifunze,
bonyeza kitufe cha facebook
Monday, September 30
SIFA ZA BINADAMU ANAYEJITAMBUA
Kutambua ndani yako hakuhitaji uende shule na kusoma sana,na hakutokani na maamuzi ya mtu mwingine bali ni maamuzi yatokayo ndani mwako
![]() |
| Binadamu anayejitambua hutazama kila jambo kama fursa |
![]() |
| Binadamu anayejitambua huyajenga na kuyatunza mazingira yanayomzunguka |
Sunday, September 8
JINSI YA KUPIGIA KURA BLOG YAKO KATIKA SHINDANO LA TANZANIA BLOG AWARDS
1. Best Inspirational Blog
2. Best Creative Writing Blog
Nakuomba kwa nafasi yako uchukue muda kuipigia kura blogu yako katika vipengele tajwa hapo juu kabla ya tarehe 15/09/2013 kwa njia zifuatazo
(a)Bonyeza hapa kisha chagua pongujoseph.blogspot.com
(b)-(i) Kwa kupigia kura Best Inspirational Blog bonyeza hapa
(ii) Kwa kupigia kura Best Creative writing Blog Bonyeza hapa
Hakikisha unachagua pongujoseph.blogspot.com
Ahsante sana kwa ushirikiano
Kwa maoni,maswali ama ushauri usisite kuniandikia +255765046644, Whatsapp namba +255765046644
UJUMBE WA LEO JUMAPILI
Tuesday, September 3
NINI THAMANI YAKO KWA WENGINE
chuki,hasira na majaribu yote hayatakuwepo
Haitajalisha kuwa ulikuwa na sura nzuri ya mvuto ama ulionekana wa sura mbaya
wala ngozi,wala jina halitahesabika
Ni NINI KITAHESABIKA....
KiTAHESAbika ulichotoa kwa wengine na si ulichopokea
Kitahesabika ulichojenga ukiwa duniani,kilichowainua wengine,,,na si kile cha kifahari ulichonunua
Ni kila upole,usawa,utu, na kuwanyanyua wote walio wahitaji,
nI vile ulivyo,wewe halisi,ulivyoyaishi maisha yako kwa ajili ya wengine
Si watu wangapi wanakufhamu,ama umaarufu wako bali ni kiasi gani wengine wataumia pale wanapokukosa
Ni ule umuhimu wako kwa wengine
Si kumbukumbu tu kwamba ulikwepo,bali ni kumbukumbu ya maisha ya wengine uliowabadilisha na kuwasaidia kufikia furaha.
Kitakachohesabika si ni muda gani utakmbukwa,bali ni nani na kwa nini unakumbukwa,ni kwa wema uliotenda
Katika maisha tuishio,ni muhimu kuishi maisha yenye faida kwa wengine....
jiulize ni nini kimekuleta duniani...ishi kilichokuleta - See more at: http://pongujoseph.blogspot.com/2012/09/ujumbe-2.html#sthash.nspMdMHf.dpuf

Nashukuru kupata ujumbe kutoka kwa wasomaji mbalimbali wakieleza jinsi walivyoguswa na kwa jinsi gani makala hizo zimekuwa zikiwasaidia.Nashukuru kuona nikiwa nuru kwa wengine,jambo ambalo nimekuwa nikilifikiria kwa muda mrefu na ndiyo sababu inayonifanya niandike.Siandiki kwa ajili ya kupata umaarufu ama fedha,bali nafanya hivi nikijua kuwa nina sababu kuwepo katika dunia hii.
Leo hii naandika tena kusisitiza kuyaishi maisha yetu kwa dhati na kuifanya dunia kuwa sehemu bora.
Kila kukicha upendo unapungua baina ya binadamu.Matokeo ya vita,visasi,dhuluma, majivuno,matabaka,umasikini yanazidi kuongezeka.Mambo haya hayatokei kwa bahati mbaya.Ni matokeo ya jamii ambayo imejengwa na sisi wenyewe (binadamu) kwa mlolongo wa miaka kwa ujumuisho wa uchaguzi wa kila mmoja kwa nafsi yake na msukumo wa jamii.
Tumechagua eitha kwa kujua ama kutokujua kuifanya dunia ilivyo sasa.Mfano mzuri ni jinsi tunavyochagua kutumia nguvu kumaliza vita ama mfarakano.Hutashangaa kusikia nchi inaivamia nchi nyingine kwa madai ya kusuluhisha wakati tukijua wazi kuwa amani hailetwi kwa vita bali kwa upendo.
Tumechagua kuwatoa elimu iletayo utegemezi na matabaka na kudai kuwa ni elimu bora.Yapo mambo mengi ambayo tunayafanya kinyume lakini tukitegemea matokeo chanya,yenye kuinua watu wote.
Baada ya matokeo ya uchaguzi wetu kuanza kuonekana,si jambo la kushangaza utakaposikia baadhi wakimsingizia shetani ama Mungu.Lakini wanamlaumu na kumsingizia shetani ama Mungu kwa matokeo ya maamuzi yao binafsi.Wanasahau kuwa yote hayo ni matokeo ya maamuzi yao.
![]() |
| binadamu wa kweli huishi kwa ajili ya wengine |
Leo hii lengo langu ni kuwaalika wale wanaotambua kuwa wana sababu ya msingi kuishi hapa duniani,kuiishi sababu hiyo.Nawaalika kufungua milango,japo kidogo na kuanza kuchimbua ,kuvumbua na kuuishi wito ulioitiwa hapa duniani.Kuchukua hatua na kuanza kuishi maisha yako halisi ni mwanzo tosha wa kuwamulika wengine.Huitaji utajiri wa mali ama nafasi,ulipo na hali uliyonayo inatosha kuanza kuishi ubinadamu.
Binadamu si tu mjumuiko wa nyama,mifupa na muonekano,.bali ni mjumuisho wa upendo,usawa,uhuru,hurun
ma,kujitolea na kuishi kwa ajili ya wengine.Ni pale unapoamua kuishi na kujitolea kwa ajili ya wengine ukitambua kuwa kila unachowatendea,unajitendea mwenyewe.
Nuru ya Mungu ipo ndani mwetu,nasi ni mawakala wake Mungu.Nuru ya Mungu huanza kung'aa pale unapoishi maisha yako kwa ajili ya wengine.Hakuna aliyekuja kushindana na mwenzake.Tupo kujenga pamoja.
Sisi ni wawakilishi wa Mungu hapa duniani
Wale ambao wapo tayari kujitolea kwa ajili ya wengine katika nyakati za shida na maumivu pasipo kujali malipo,ni mfano bora wa binadamu wa kweli .Hutokea kwa hali mbalimbali...wanyama,binadamu,ndege,wadudu...Malaika hapa duniani ni wale ambao hutenda na kufanya kazi na kuanzisha mambo kwa ajili ya wengine.Hawako tayari kudhuru,kudharau,kuumiza,kuchutenga,kunyang'anya na hata kubagua binadamuwengine kwa hali yeyote .Hawako tayari kutoa uhai wa yeyote,hata anayeonekana ni adui,kwani wanatambua thamani ya kila uhai wa nafsi iliyopo hapa duniani.Hivyo huwa tayari kutumia nuru na iliyo ndani mwao kuwamulika wengine na kuwakumbusha sababu ya wao kuwepo katika dunia hii na hatimae waiishi sababu hiyo.Ni mfano bora wa binadamu wa kwelu
Nakualika uchimbue ndani ya moyo wako na kufungua chemchem ya Mungu ndani mwako na kuiishi pasipo kuchoka
Ushiriki wako katika ujenzi wa dunia mpya(KATIKA FIKRA MPYA) unatokana na maamuzi na matendo yako ya kila sekunde.Ujenzi unaanza ndani mwako kwanza.Ubinadamu umetokana na maamuzi ya Muumba.Na matumizi yake yanaanza na uamuzi ndani mwako.Kila fikra yako kuhusu wewe,dunia unayoijenga na maisha ndani ya dunia mpya.Kila mmoja akifanya maamuzi sahihi,tunajenga dunia mpya yenye uhuru wa kweli,upendo na amani
Napenda kunukuu maneno niliyopata kuyaandika wakati fulani.
![]() |
| ishi kwa ajili ya wengine,tenda kwa ajili ya kila binadamu |
chuki,hasira na majaribu yote hayatakuwepo
Haitajalisha kuwa ulikuwa na sura nzuri ya mvuto ama ulionekana wa sura mbaya
wala ngozi,wala jina halitahesabika
Ni NINI KITAHESABIKA....
KiTAHESAbika ulichotoa kwa wengine na si ulichopokea
Kitahesabika ulichojenga ukiwa duniani,kilichowainua wengine,,,na si kile cha kifahari ulichonunua
Ni kila upole,usawa,utu, na kuwanyanyua wote walio wahitaji,
nI vile ulivyo,wewe halisi,ulivyoyaishi maisha yako kwa ajili ya wengine
Si watu wangapi wanakufhamu,ama umaarufu wako bali ni kiasi gani wengine wataumia pale wanapokukosa
Ni ule umuhimu wako kwa wengine
Si kumbukumbu tu kwamba ulikwepo,bali ni kumbukumbu ya maisha ya wengine uliowabadilisha na kuwasaidia kufikia furaha.
Kitakachohesabika si ni muda gani utakmbukwa,bali ni nani na kwa nini unakumbukwa,ni kwa wema uliotenda
Katika maisha tuishio,ni muhimu kuishi maisha yenye faida kwa wengine....
jiulize ni nini kimekuleta duniani...ishi kilichokuleta - See more at: http://pongujoseph.blogspot.com/2012/09/ujumbe-2.html#sthash.nspMdMHf.dpuf
chuki,hasira na majaribu yote hayatakuwepo
Haitajalisha kuwa ulikuwa na sura nzuri ya mvuto ama ulionekana wa sura mbaya
wala ngozi,wala jina halitahesabika
Ni NINI KITAHESABIKA....
KiTAHESAbika ulichotoa kwa wengine na si ulichopokea
Kitahesabika ulichojenga ukiwa duniani,kilichowainua wengine,,,na si kile cha kifahari ulichonunua
Ni kila upole,usawa,utu, na kuwanyanyua wote walio wahitaji,
nI vile ulivyo,wewe halisi,ulivyoyaishi maisha yako kwa ajili ya wengine
Si watu wangapi wanakufhamu,ama umaarufu wako bali ni kiasi gani wengine wataumia pale wanapokukosa
Ni ule umuhimu wako kwa wengine
Si kumbukumbu tu kwamba ulikwepo,bali ni kumbukumbu ya maisha ya wengine uliowabadilisha na kuwasaidia kufikia furaha.
Kitakachohesabika si ni muda gani utakmbukwa,bali ni nani na kwa nini unakumbukwa,ni kwa wema uliotenda
Katika maisha tuishio,ni muhimu kuishi maisha yenye faida kwa wengine....
jiulize ni nini kimekuleta duniani...ishi kilichokuleta - See more at: http://pongujoseph.blogspot.com/2012/09/ujumbe-2.html#sthash.97x7DSLn.dpuf

Si watu wangapi wanakufahamu,ama umaarufu wako bali ni kiasi gani wengine wataumia pale wanapokukosa
Ni ule umuhimu wako kwa wengine
Si kumbukumbu tu kwamba ulikwepo,bali ni kumbukumbu ya maisha ya wengine uliowabadilisha na kuwasaidia kufikia furaha.
Kitakachohesabika si ni muda gani utakumbukwa,bali ni nani na kwa nini unakumbukwa,ni kwa wema uliotenda
Katika maisha tuishio,ni muhimu kuishi maisha yenye faida kwa wengine....
jiulize ni nini kimekuleta duniani...ishi kilichokuleta -Pongu Joseph
chuki,hasira na majaribu yote hayatakuwepo
Haitajalisha kuwa ulikuwa na sura nzuri ya mvuto ama ulionekana wa sura mbaya
wala ngozi,wala jina halitahesabika
Ni NINI KITAHESABIKA....
KiTAHESAbika ulichotoa kwa wengine na si ulichopokea
Kitahesabika ulichojenga ukiwa duniani,kilichowainua wengine,,,na si kile cha kifahari ulichonunua
Ni kila upole,usawa,utu, na kuwanyanyua wote walio wahitaji,
nI vile ulivyo,wewe halisi,ulivyoyaishi maisha yako kwa ajili ya wengine
Si watu wangapi wanakufhamu,ama umaarufu wako bali ni kiasi gani wengine wataumia pale wanapokukosa
Ni ule umuhimu wako kwa wengine
Si kumbukumbu tu kwamba ulikwepo,bali ni kumbukumbu ya maisha ya wengine uliowabadilisha na kuwasaidia kufikia furaha.
Kitakachohesabika si ni muda gani utakmbukwa,bali ni nani na kwa nini unakumbukwa,ni kwa wema uliotenda
Katika maisha tuishio,ni muhimu kuishi maisha yenye faida kwa wengine....
jiulize ni nini kimekuleta duniani...ishi kilichokuleta - See more at: http://pongujoseph.blogspot.com/2012/09/ujumbe-2.html#sthash.97x7DSLn.dpuf
Friday, August 30
KWA SABABU HATUVIONI HIVI NDANI MWETU,HATUWEZI KUWAPA WENGINE
Tuanze kwa kutafakari nyakati hizi ambazo hutokea katika maisha yetu mara kadhaa.
| kuna nyakati za magumu na upweke ambazo hutufunza |
Ni zile nyakati ambazo unajihisi ukiwa mpweke na kutengwa.Ukihisi ya kuwa hakuna hata mmoja anayekusikilizane. Unapata hisia kuwa upo peke yakojapokuwa wapo watu wengine unaoishi nao na licha ya kuwa unatambua kuwa dunia imejaa watu wengi na viumbe wengi wanaokuzunguka.
Ni kweli kuwa licha ya kuwa dunia imezunguka,ni wewe ndiye uijazayo na unayeisanifu.Wewe kama nafsi watosha.Na unabaki wakati ambao aliyebaki kwako ni Mungu.
Nyakati hizi hutokea pale unapokuwa unajihisi kuwa umekosa kitu(vitu) ulivyovihitaji maishani,na hata wakati kunapohisi kuwa una kila kitu ulichokihitaji maishani mwako.Pia huja katika nyakati ambazo karibu kila kitu ulichokuwa nacho umekipoteza ama umepewa kila kitu ambacho ulikipoteza.
Nyakati hizi zinapofika , ni nyakati za kupona na kuachia majeraha mengi ambayo yalikuwa yakikurudisha nyuma kwa muda mrefu maishani mwako.Na ni nyakati za uvumbuzi wa chemchem ndani mwako.Ni kipindi cha giza kiletacho mwanga.
Na katika nyakati hizi bado kuna kitu muhimu ambacho moyo wako unakihitaji sana na ambacho wengi hukitafuta kwa muda mrefu maishani-Ni kupendwa kwa dhati na kuthaminiwa..
Je kuna yeyote anayenipenda na kunidhamini kwa dhati jinsi nilivyo?.Ni maswali ambayo utajiuliza sana katika nyakati hizi za ugunduzi.
Tumekuwa tukidhani kwamba tunaweza kupata upendo wa dhati na thamani ya kweli toka kwa wengine.Tumetafuta kwa muda sana upendo toka kwa ndugu,marafiki na majirani.Tumetafuta kwa wale tuliowaamini kwa dhati na mara nyingi kuishia kwenye kuumia.
Tukaingia kuutafuta upendo na thamani ndani yetu lakini mara nyingi tumeshindwa kuupata.Hivyo kushindwa kuutambua ndani mwetu kumetupelekea kushindwa kutoa kwa wengine. Na kwa vile tumeshindwa kuupata kwetu tumeitafuta tunapodhani upo ,tunaokosa na kuishia kuogopa kuweka matumaini yetu huko tulipodhani upo.
Na hivyo ndivyo itokeavyo,
Tunatafuta pale ambapo hatukuhifadhi.Na kama hatukuuweka upendo popote vivyo hivyo hatuwezi kuupata.Kile ambacho hatukitoa maishani hatuwezi kukipata kwa sababu hapa duniani sisi ndie wasanifu na wabomoaji.
Kama tunakosa kusamehewa ,ni kwa sababu hatukupata kusamehe.Kama hatuthaminiwi ni kwa sababu hatukupata kuijenga thamani sisi wenyewe.Kama hatuvumiliwi, ni kwa sababu hatukujenga uvumilivu sisi wenyewe.Kama hatupati haki na usawa ni kwa sababu hatukuanza kuijenga ndani mwetu.Kama hatuupati upendo ,basi ni kwa sababu hatukupata kuujenga upendo ndani mwetu. Na kama hakuna ambaye anapata thamani toka kwa wengine,ni kwa sababu hatukuanza sisi kuijenga ndani mwetu.
Mambo yote haya ni lazima yaanze ndani kwetu sisi kisha yaende kwenye maisha ya wengine.
Kwa wengi wetu, tumekosa kujipa thamani yetu sisi na kujipenda , ni havyo ni vigume kutoa kwa wengine.Wengine wengi wanahisi hawana stahili ya mambo yote hayo .Tunajitazama sisi kama dhaifu kuliko wengine ama bora kuliko wengine.
Hatuuoni uzuri uliopo ndani mwetu uliojazwa na uzuri wa Muumba.Hatuoni uaminifu ndani mwetu.Hatuoni usafi ndani mwetu.
Kwa sababu hatuvioni hivi vyote ndani mwetu,hatuwezi kuwapa wengine.
Lakini PIA kwa sababu si kwamba sisi ni vipofu mioyoni mwetu,tunaviona kwa wengine na kuvihitaji tusitambue kuwa tunavyo.Ni mara nyingi tunaona upendo kwa wengine,tunaona huruma kwa wengine,tunauona usafi wa moyo kwa wengine,tunayaona matumaini kwa wengine. Hivyo kwa kuviona kwa wengine, tunajaribu kutenda kwa baadhi yao lakini si ndani mwetu
![]() |
| mara nyingi tunaona upendo,huruma kwa wengine |
Je tunaweza kujitendea nafsii zetu?
Mara nyingi tunashindwa kwa sababu ya vidonda tulivyonavyo.
Kwa sababu ya vidonda tulivyonavyo,tunashindwa pia kutibu majeraha ya wengine.Hivyo hatuthamini jinsi dunia inavyotuhitaji kila mmoja kwa nafsi yetu.
Tunashindwa kutambua kuwa dunia inahitaji kile kitokacho ndani mwetu ikiwemo upendo,usawa,haki,thamani kwa wengine,uvumilivu na kujitolea.Tunaishia kuilamu dunia tusijue kuwa ni sisi ndio tulioanza kuisanifu.Na hivyo tunaweka picha ndani mwetu kuwa dunia ni mbaya na onevu tena sehemu ya kupita kwa machungu.
Hatuwezi kupata kutoka katika dunia vile ambavyo hatukuvipanda. Na sasa tunapaswa kukumbuka hapa kuwa : Chochote ambacho hatukukipanda duniani,hatuwezi kukipata katika dunia hiyohiyo.Tunavuna tulichopanda
Hapa ndipo unapokuja wakati tunapogundua kuwa sisi ndio wasanifu wa dunia na kila kilichomo.Ni wasanifu wa maisha ya leo na ya kizazi kijacho.Hakuna atakaye tupatia chochote kile ambacho hatukuanza sisi kukipanda na kukitoa kwa dunia hii tuishimo.Na mara nyingi tunamuomba Mungu na wakati mwingine kumlaumu kwa kutotupatia kileambacho hatukuanza sisi kukitengeneza na hata kukitoa kwa wengine pale tulipostahili kufanya hivyo
Nadhani ni wakati kwa viongozi wetu wa dini kuanza kufundisha hili.
Tunaweza kuanza kuona mifano katika kati mahusiano yetu.Kama huwezi kumsamehe unayeishi nae,unashindwa kumpenda,kuishi nae kwa amani na uhuru na hata kumvumilia,ni vigumu kutarajia kupata kutoka kwa huyohuyo unayeishi nae na kulala upendo,thamani,uvumilivu,uhuru,amani na thamani ya kweli.Tutapata kadiri tulivyotoa
Huwa tunafikiri kuwa ndani ya mahusiano,mwenzi atakupatia vitu ambavyo unajihisi huna.Tunadhani tutapata upendo ambao sisis hatuutoi,msamaha ambao sisi wenyewe hatuutoi.Ni huu ni moja ya uongo mkubwa tunaoajidanganya ndani ya nafsi zetu.
Tunapotamani kupatiwa pasipo kutoa,mwisho wake kila kitu hufifia,kasha chuki huingia na kasha mahusiano hufa.Kisha tunagundua kuwa ni sisi wenyewe tulijidanganya.Sasa tiunatambua kuwa hakuna pa kukimbilia zaidi ya Mungu. Tunarudi kwa Mungu na kumwambia…"Tafadhali Mungu wangu naomba unisamehe.Naomba unijalie amani na upendo,nijalie uvumilivu na moyo wa kujitolea.Nakuomba baba unijalie hivi nami niwagawie wenzangu."
Kwa sasa dunia ipo kwenye machafuko na chuki. Majivuno,visasi na dharau vimetawala.Tumejenga wenyewe tena toka ndani mwetu.Na muda si mrefu baada ya mambo haya kukithiri,Binadamu watatambua kuwa sasa tutavipata kwa Mungu,naye ni Muweza na chemchem ya kila kitu.
Na wakati huo binadamu watatambua kuwa hakuna utengano kati ya Muumba,chemchem ya kila jambo na Nafsi ya kila binadamu.Binadamu watatambua kuwa miili yetu imebeba nafsi ndani,ambapo ndiko hekalu la chemchem ya kila jambo huishi. Kila mmoja atatambua umuhimu wa nafsi yake na jinsi anavyohusika katika ujenzi wa dunia.Kila mmoja ataanza kuchukua hatua katika kutambua matokeo ya kila jambo analotenda.
Kila nafsi itajifunza kupanda na kutaraji mavuno.Kila nafsi itathamini nafsi nyingine na kila nafsi itatambua kuwa inahusika kujenga dunia mpya na haitakuwa tayari kulaumu dunia na kudai dunia kile ambacho haikukipanda wala kukitoa.Kisha dunia itakuwa sehemu bora ya kuishi
Ndani mwako kuna pumziko la kweli,furaha,amani,nuru ya kweli na chemchem ya uumbaji wa Mungu ambayo Mungu amekupa na kukuleta hapa duniani.Ukisikiliza moyo wako unaweza kutambua mengi yaliyo ndani mwako....Kazi yako ukiwa hapa duniani ni kutoa ulichonacho,kilicho ndani mwako kwa ajili ya wengine
Mpaka sasa wachache wanalitambua hili.Na wasiotambua huilamu dunia kila kukicha.Na hivyo wasio tayari kutambua hili watasubiri mpaka ule wakati watakapolia na kugundua hakuna zaidi ya Mungu na kasha kugundua hekalu la chemchem yake ndani mwao . Hii itakuja bada ya kubomoa mengi…ndoa,familia,amani,upendo na kIsha nafsi NA baadae kufanya juhudi kujijenga upya
Kila mmoja akiwa kama nafsi huru anapaswa kuchukua hatua,hasa kutambua kuwa hakuna mwingine zaidi ya Mungu, na kasha kuchimba ndani kutambua kuwa sisi ni hekalu iishipo nuru na chemchem ya kila tunachokihitaji
Unapoanza kumuona Mungu katika kila kiumbe kinachokuzunguka unatambua kuwa sasa umezaliwa upya.Sauti yake inakuwa ikiongea nawe ndani mwako toka ndani yako.Unatambua kuwa Mungu hayupo mbali nawe bali yupo ndani mwako wakati wote.Unaruhusu nguvu na chemchem ya kila ushindi kufanya kazi ndani yako na kukupa nafasi ya kugundua nguvu hii iliyo ndani mwako na kuitumia kuifanya dunia kuwa sehemu bora kwa viumbe wote
.Mungu ametupatia uwezo mkubwa wa kuyafanya maisha yetu kuwa yenye faida kwa wengine,na husubiri maamuzi yetu ili kutuonesha njia.Tunapokuwa tayari anatufundisha maana ya kuwa hapa na thamani ya maisha yetu . Ndipo unapomjua tena si kama kiumbe cha kutisha ama kisichoonekana lakini kama sehemu muhimu ndani mwako.Kisichoonekana ndani mwetu kinazaliwa upya na kuonekana kwa kila anayekuzunguka.Kisha hutupatia kila uwezo na kuingia ndani ya kila kilicho mwilini mwetu kwa maelfu,tayari kwa kumtumikia kwa njia mbalimbali. Tunajenga dunia mpya yenye matumaini na furaha