Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH
Showing posts with label UPLIFT YOURSELF. Show all posts
Showing posts with label UPLIFT YOURSELF. Show all posts

Friday, August 30

KWA SABABU HATUVIONI HIVI NDANI MWETU,HATUWEZI KUWAPA WENGINE



Tuanze kwa kutafakari nyakati  hizi ambazo hutokea katika maisha yetu  mara kadhaa.
kuna nyakati za magumu na upweke ambazo hutufunza

Ni zile nyakati ambazo  unajihisi ukiwa mpweke na kutengwa.Ukihisi ya kuwa hakuna hata mmoja anayekusikilizane. Unapata hisia kuwa upo peke yakojapokuwa wapo watu wengine unaoishi nao na licha ya kuwa unatambua kuwa dunia imejaa watu wengi na viumbe wengi wanaokuzunguka.

Ni kweli kuwa licha ya kuwa dunia imezunguka,ni wewe ndiye uijazayo na unayeisanifu.Wewe kama nafsi watosha.Na unabaki wakati ambao aliyebaki kwako ni Mungu.

Nyakati hizi  hutokea pale unapokuwa unajihisi kuwa umekosa kitu(vitu) ulivyovihitaji maishani,na hata wakati kunapohisi kuwa una kila kitu ulichokihitaji maishani mwako.Pia huja katika nyakati ambazo karibu kila kitu ulichokuwa nacho umekipoteza ama umepewa kila kitu ambacho ulikipoteza.

Nyakati hizi zinapofika , ni nyakati za kupona  na kuachia majeraha  mengi ambayo yalikuwa yakikurudisha nyuma kwa muda mrefu maishani mwako.Na ni nyakati za uvumbuzi wa chemchem ndani mwako.Ni kipindi cha giza kiletacho mwanga.
Na katika nyakati hizi bado kuna kitu muhimu ambacho moyo wako unakihitaji sana na ambacho wengi hukitafuta kwa muda mrefu maishani-Ni kupendwa kwa dhati na kuthaminiwa..
 Je kuna yeyote anayenipenda na kunidhamini kwa dhati jinsi nilivyo?.Ni maswali ambayo utajiuliza sana katika nyakati hizi za ugunduzi.

Tumekuwa tukidhani kwamba tunaweza kupata upendo wa dhati na thamani ya kweli toka kwa wengine.Tumetafuta kwa muda sana upendo toka kwa ndugu,marafiki na majirani.Tumetafuta kwa wale tuliowaamini kwa dhati na mara nyingi kuishia kwenye kuumia.

Tukaingia kuutafuta upendo na thamani ndani yetu lakini mara nyingi tumeshindwa kuupata.Hivyo kushindwa kuutambua ndani mwetu kumetupelekea kushindwa kutoa kwa wengine. Na kwa vile tumeshindwa kuupata kwetu tumeitafuta tunapodhani upo ,tunaokosa na kuishia kuogopa kuweka matumaini yetu huko tulipodhani upo.

Na hivyo ndivyo itokeavyo,
Tunatafuta pale ambapo hatukuhifadhi.Na kama hatukuuweka upendo popote vivyo hivyo hatuwezi kuupata.Kile ambacho hatukitoa maishani hatuwezi kukipata kwa sababu hapa duniani sisi ndie wasanifu na wabomoaji.

Kama tunakosa kusamehewa ,ni kwa sababu hatukupata kusamehe.Kama hatuthaminiwi ni kwa sababu hatukupata kuijenga thamani sisi wenyewe.Kama hatuvumiliwi, ni kwa sababu hatukujenga uvumilivu  sisi wenyewe.Kama hatupati haki na usawa ni kwa sababu hatukuanza kuijenga ndani mwetu.Kama hatuupati upendo ,basi ni kwa sababu hatukupata kuujenga upendo ndani mwetu. Na kama hakuna ambaye anapata thamani toka kwa wengine,ni kwa sababu hatukuanza sisi kuijenga ndani mwetu.

Mambo yote haya ni lazima yaanze ndani kwetu sisi kisha yaende kwenye maisha ya wengine.
Kwa wengi wetu, tumekosa kujipa thamani yetu sisi na kujipenda , ni havyo ni vigume kutoa kwa wengine.Wengine wengi wanahisi hawana stahili ya mambo yote hayo .Tunajitazama sisi kama dhaifu kuliko wengine ama bora kuliko wengine.

Hatuuoni uzuri uliopo ndani mwetu uliojazwa na uzuri wa Muumba.Hatuoni uaminifu ndani mwetu.Hatuoni usafi ndani mwetu.
Kwa sababu hatuvioni hivi vyote ndani mwetu,hatuwezi kuwapa wengine.
Lakini  PIA kwa sababu si kwamba sisi ni vipofu mioyoni mwetu,tunaviona kwa wengine na kuvihitaji tusitambue kuwa tunavyo.Ni mara nyingi tunaona upendo kwa wengine,tunaona huruma kwa wengine,tunauona usafi wa moyo kwa wengine,tunayaona matumaini kwa wengine. Hivyo kwa kuviona kwa wengine, tunajaribu kutenda kwa baadhi yao lakini si ndani mwetu
mara nyingi tunaona upendo,huruma kwa wengine

Je tunaweza kujitendea nafsii zetu?

Mara nyingi tunashindwa kwa sababu ya vidonda tulivyonavyo.
Kwa sababu ya vidonda tulivyonavyo,tunashindwa pia kutibu majeraha ya wengine.Hivyo hatuthamini jinsi dunia inavyotuhitaji kila mmoja kwa nafsi yetu.
Tunashindwa kutambua kuwa dunia inahitaji kile kitokacho ndani mwetu ikiwemo upendo,usawa,haki,thamani kwa wengine,uvumilivu na kujitolea.Tunaishia kuilamu dunia tusijue kuwa ni sisi ndio tulioanza kuisanifu.Na hivyo tunaweka picha ndani mwetu kuwa dunia ni mbaya na onevu tena sehemu ya kupita kwa machungu.

Hatuwezi kupata kutoka katika dunia vile ambavyo hatukuvipanda. Na sasa tunapaswa kukumbuka hapa kuwa : Chochote ambacho hatukukipanda duniani,hatuwezi kukipata katika dunia hiyohiyo.Tunavuna tulichopanda
Hapa ndipo unapokuja wakati tunapogundua kuwa sisi ndio wasanifu wa dunia na kila kilichomo.Ni wasanifu wa maisha ya leo na ya kizazi kijacho.Hakuna atakaye tupatia chochote kile ambacho hatukuanza sisi kukipanda na kukitoa kwa dunia hii tuishimo.Na mara nyingi tunamuomba Mungu na wakati mwingine kumlaumu kwa kutotupatia kileambacho hatukuanza sisi kukitengeneza na hata kukitoa kwa wengine pale tulipostahili kufanya hivyo
Nadhani ni wakati kwa viongozi wetu wa dini kuanza kufundisha hili.

Tunaweza kuanza kuona mifano katika kati mahusiano yetu.Kama huwezi kumsamehe unayeishi nae,unashindwa kumpenda,kuishi nae kwa amani na uhuru na hata kumvumilia,ni vigumu kutarajia kupata kutoka kwa huyohuyo unayeishi nae na kulala upendo,thamani,uvumilivu,uhuru,amani na thamani ya kweli.Tutapata kadiri tulivyotoa

Huwa tunafikiri kuwa  ndani ya mahusiano,mwenzi atakupatia vitu ambavyo unajihisi huna.Tunadhani tutapata upendo ambao sisis hatuutoi,msamaha ambao sisi wenyewe hatuutoi.Ni huu ni moja ya uongo mkubwa tunaoajidanganya ndani ya nafsi zetu.

Tunapotamani kupatiwa pasipo kutoa,mwisho wake kila kitu hufifia,kasha chuki huingia na kasha mahusiano hufa.Kisha tunagundua kuwa ni sisi wenyewe tulijidanganya.Sasa tiunatambua kuwa hakuna pa kukimbilia zaidi ya Mungu. Tunarudi kwa Mungu na kumwambia…"Tafadhali Mungu wangu naomba unisamehe.Naomba unijalie amani na upendo,nijalie uvumilivu na moyo wa kujitolea.Nakuomba baba unijalie hivi nami niwagawie wenzangu."

Kwa sasa dunia ipo kwenye machafuko na chuki. Majivuno,visasi na dharau vimetawala.Tumejenga wenyewe tena toka ndani mwetu.Na muda si mrefu baada ya mambo haya kukithiri,Binadamu watatambua kuwa sasa tutavipata kwa Mungu,naye ni Muweza na chemchem ya kila kitu.

Na wakati huo binadamu watatambua kuwa hakuna utengano kati ya Muumba,chemchem ya kila jambo na Nafsi ya kila binadamu.Binadamu watatambua kuwa miili yetu imebeba nafsi ndani,ambapo ndiko hekalu la chemchem ya kila jambo huishi. Kila mmoja atatambua umuhimu wa nafsi yake na jinsi anavyohusika katika ujenzi wa dunia.Kila mmoja ataanza kuchukua hatua katika kutambua matokeo ya kila jambo analotenda.

Kila nafsi itajifunza kupanda na kutaraji mavuno.Kila nafsi itathamini nafsi nyingine na kila nafsi itatambua kuwa inahusika kujenga dunia mpya na  haitakuwa tayari kulaumu dunia na kudai dunia kile ambacho haikukipanda wala kukitoa.Kisha dunia itakuwa sehemu bora ya kuishi

Ndani mwako kuna pumziko la kweli,furaha,amani,nuru ya kweli na chemchem ya uumbaji wa Mungu ambayo Mungu amekupa na kukuleta hapa duniani.Ukisikiliza moyo wako unaweza kutambua mengi yaliyo ndani mwako....Kazi yako ukiwa hapa duniani ni kutoa ulichonacho,kilicho ndani mwako kwa ajili ya wengine

Mpaka sasa wachache wanalitambua hili.Na wasiotambua huilamu dunia kila kukicha.Na hivyo wasio tayari kutambua hili watasubiri mpaka ule wakati watakapolia na kugundua hakuna zaidi ya Mungu na kasha kugundua hekalu la chemchem yake ndani mwao . Hii itakuja bada ya kubomoa mengi…ndoa,familia,amani,upendo na kIsha nafsi NA baadae kufanya juhudi kujijenga upya

Kila mmoja akiwa kama nafsi huru anapaswa kuchukua hatua,hasa kutambua kuwa hakuna mwingine zaidi ya Mungu, na kasha kuchimba ndani kutambua kuwa sisi ni hekalu iishipo nuru na chemchem ya kila tunachokihitaji

Unapoanza kumuona Mungu katika kila kiumbe kinachokuzunguka unatambua kuwa sasa umezaliwa upya.Sauti yake inakuwa ikiongea nawe ndani mwako toka ndani yako.Unatambua kuwa Mungu hayupo mbali nawe bali yupo ndani mwako wakati wote.Unaruhusu nguvu na chemchem ya kila ushindi kufanya kazi ndani yako na kukupa nafasi ya kugundua nguvu hii iliyo ndani mwako na kuitumia kuifanya dunia kuwa sehemu bora kwa viumbe wote
.Mungu ametupatia uwezo mkubwa wa kuyafanya maisha yetu kuwa yenye faida kwa wengine,na husubiri maamuzi yetu ili kutuonesha njia.Tunapokuwa tayari anatufundisha maana ya kuwa hapa na thamani ya maisha yetu . Ndipo unapomjua tena si kama kiumbe cha kutisha ama kisichoonekana lakini kama sehemu muhimu ndani mwako.Kisichoonekana ndani mwetu kinazaliwa upya na kuonekana kwa kila anayekuzunguka.Kisha hutupatia kila uwezo na kuingia ndani ya kila kilicho mwilini mwetu kwa maelfu,tayari kwa kumtumikia kwa njia mbalimbali. Tunajenga dunia mpya yenye matumaini na furaha


Saturday, January 5

HATUTAMUACHA HATA MMOJA 2013


Tumejifunza mambo mengi kwa mwaka 2012,ambayo yametufanya tutambue sisi ni akina nani na kwa nini tupo hapa duniani.Tumetambua kuwa sisi ndio wasanifu wa maisha yetu wenyewe.Tumejifunza kuwa kila jambo ni jema likitazamwa kwa mfumo chanya na kuwa mambo yote yatokeayo maishani mwetu ni matokeo ya fikra zetu na vitendo vyetu wenyewe...Tumejifunza kuwa upendo ndio silaha ya mafanikio ya kila jambo,upendo ni nuru.tumejifunza pia matokeo yake ambayo ni pamoja na furaha,amani,umoja,uvumilivu na ni mafanikio.Tukajifunza pia kuwa kinyume cha upendo ambayo ni chuki ndiyo matokeo ya maumivu,wivu,visasi,chuki,masengenyo na ndio matokeo ya kila jambo liletalo hasara katika maisha yetu
SISI NI WASANIFU WA MAISHA YETU WENYEWE
 

Leo hii tutajikumbusha kuhusu majukumu yetu …Mwaka mpya ulioanza tuuutazame kwa uchanya wake.Tuanze sasa kutimiza malengo yetu kila mmoja ya kuwepo hapa duniani.Kila mmoja wetu anayo majukumu yake.Kila mmoja ana wito unaomuita ndani mwake,ana sauti ya Mungu ndani yake inayomuita kutenda kwa ajili ya wengine na kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi

Hakuna hata mmoja wetu ambaye hatayapitia magumu,kwa sababu bila magumu kutokea hatuwezi kuendelea.Mwaka huu ni mwaka wa kusonga mbele ...tutasonga mbele,hatutamuacha hata mmoja nyuma
Ni mwaka ambao mwalimu anayeishi katika mazingira magumu yenye milima mingi,ataamka kila siku na kufundisha kwa bidii na kuwanyanyua wengine wengi.Anahitajika huyo ambaye hatalalamika na kusubiri serikali(kwani serikali ni kila mmoja wetu) bali atakuwa ni mfano wa kuigwa wa mbinu bora za kutatua matatizo.Mwalimu popote ulipo amka na kutenda kwa ajili ya wengine.Amka mwalimu.

Sauti ya upendo husikika kwa viumbe vyote.Huu ni mwaka wa kuwa nuru kwa wengine(picha toka helped by animals kwa msaada wa mtandao)


Ni mwaka ambao daktari ataamka mapema na kukumbuka jukumu lake ,ya kuwa hayupo tu kwa ajili ya kutazama idadi ya wagonjwa na kiasi cha fedha,bali yupo kwa ajili ya upendo,akijali utu wa wengine pasipo kubagua hali,kabila,rangi ama hali yeyote na daima atahesabu mafanikio yake kwa kuokoa wengine,kuwainua walio kata tamaa.....na hata akitokea mtoto akaulizwa upendo ni nini,basi amtazame daktari kwa ujasiri akisema......huu ndio upendo.

Ni mwaka ambao kila anayetoa huduma kwa wengine,atatoa akisukumwa na upendo.Kila atazamapo wengine,atambue kuwa anajitazama yeye,na kuwa thamani yake ni thamani ya wengine wote.Anapowatendea wengine akumbuke kuwa anaitendea nafsi yake.Ni mwaka ambao sisi tulio binadamu tutaonesha upendo uliotukuka,utakaofanya nuru ya Mungu iliyo ndani mwetu iwaangaze binadamu engine wasiotambua upendo,ili nao waishi maisha ya upendo.
Sisi ni wamoja,sisi wote ni wana wa Mungu,tofauti zetu zimejengwa na woga ,fikra zetu


Huu ni mwaka ambao tunapaswa kuifanya dunia kuwa sehemu bora,ili nasi tuwe malaika wa dunia hii.

Binafsi jiulize utamtendea nini yule Mungiu ambaye yupo ndani mwako?Je ukiwa katika nyakati za faragha na Muumba wako,utajivunia lipi ulilomtendea?Kumbuka kuwa kama huna malengo ya kutenda jambo lolote huwezi kutimiza lolote.Ni sawa na kusafiri safari isiyojulikana,mahali na hata uelekeo!Tukiweka malengo na kuamini katika kuyatekeleza,hakika yatatimia.

Mimi binafsi najisikia faraja sana kuhamasisha wengine na kuwasaidia wengine waweze kufikia mafanikio HASA PALE WANAPOKUWA NA MSUKUMO UTOKAO NDANI MWAO.Nimejitolea kwa ajiliya wengine na wakati wote najisikia faraja.Ninapokutana na magumu,ninayashinda kwa sababu naamini katika ushindi.Sisi  tumeumbwa kushinda.,na ushindi ni matokeo ya usanifu katika fikra za kila mmoja.

Ninapata faraja ninapoona kuwa yupo nesi ambaye licha ya kwamba anaumwa,anaamka na kwenda kazini kwa ajili ya wengine.Ninafarijika ninapoona kuwa yupo mtu ambaye licha ya kuwa na magumu mengi,anatenda ka ajili ya wengine pasipo kutegemea malipo.Nilikwenda kijijini nilipozaliwa,nikakutana na mama ambaye kipato chake ni kidogo,anaumwa kwa miaka mingi lakini anajitolea chakula na malazi kwa ajili ya wengine....anawafariji wengine,hata anapokuwa katika ugumu sana,hakati tamaa.Maisha yake ni nuru kwa wengi.Daima hamuachi jirani akiwa katika huzuni,nuru yake inaishi.Ni mwanga kwa waliokosa nuru.

Nafarijika kuona wengi ambao wanakwenda mbali na familia zao,mbali na wapendwa wao kwa ajili ya wengine. 
Nafarijika pia kuona wengi ambao wanajinyima kwa ajili ya wengine.Wengi wao wanaishi maisha ya kawaida,(kwa maana ya kipato) lakini wanatambua maana ya thamani yao kwa wengine,wapo tayari kujitolea pasipo kutambuliwa na wengine.Hii inanipa faraja ya kusonga mbele.Hwa wanatambua kuwa sisi binadamu wote ni wamoja ,tofauti zetu ni juu ya fikra zetu wenyewe.

Daima umoja ni nguvu.Usisubiri wengine wachukue hatua.Anza wewe.Mimi nimepata nafasi hii kwa kuandika.Wewe pekeyako pia watosha,unaweza kubadili wengine kwa kusamehe,kuimba,kufundisha,kutoa nakala nyingi za mafunzo kwa wengine,kwa kuwahurumia wengine,kutembelea wagonjwa,yatima,wafungwa na matendo yote yenye kuleta thamani kwa wanaotuzungua.Mwaka 2013 hatutamuacha mtu hata mmoja katika umasikini,chuki,uvivu,visasi,magonjwa huzuni...nk.Mwaka huu hatutamuacha yeyote kwenye giza.Tunao uwezo wa kuyatenda haya yote.Chukua hatua,mabadiliko yanaanza ndani yako.
Wathamini wengine,hata usiowafahamu....

Tujenge mwili mmoja,moyo mmoja na kupambana mpaka mwisho kwa ajili ya dunia iliyo bora na mafanikio kwa ajili yetu na wengine.

kila mmoja wetu anapochukua hatua licha ya vikwazo,tutayafika mafanikio(picha kwa msaada wa mtandao)




Tuishi maisha yetu kwa dhati bila uoga,tuchimbe ndani ya mioyo yetu ambapochemchem ya kila ushindi ipo,Tujifunze thamani yetu ,tuwathamini wengine kwa kuwa wao ni wa thamani kama tulivyo,tusamehe na kutazama mbele,tujali mawazo ya wenginena imani zao tuziheshimu.


Kila mmoja apende nafsi yake,ayapende maisha yake,asanifu vyema vyote vinavyomzunguka,KILA MMOJA AYAFANYE MAISHA YAKE YA THAMANI KWA WENGINE.Tutimize malengo yetu,yanayotokana na sauti iliyopo ndani mwetu,ili ule muda wa kuishi katika dunia hii unapokwisha ,na kifo kukuita,uitike kwa furaha,kwamba uliyaishi vyema,usipate hata sababu ya kuomba upewe tena muda,bali nuru ya maisha yako iwe mfano wa kuigwa milele.Uiage dunia na kuondoka kishujaa,kuelekea katika maisha mengine mapya yenye majukumu mapya.


Tutapita katika magumu mengi lakini daima tutasonga mbele,hatutamuacha yeyote nyuma,tutainuana sisi kwa sisi,hatutatazama nyuma,wala kuogopa kusonga kwa woga wetu,hatutaogopa lolote kwani sisi ni wa thamani,tutakumbuka daima kuwa dunia si sehemu ya ushindani bali ni sehemu ya ushirikiano na umoja na hivyo daima tutafikia tuendako,kwa sababu Mungu yu ndani mwetu.
Ahsanteni sana

Tuesday, December 4

IAMBIE NAFSI YAKO

 Tumeumbwa na kupewa mamlaka juu ya maisha yetu na juu ya kila kilicho juu ya nchi,Hivyo tunapaswa kukumbuka kuwa kila kitu tunachokihitaji maishani mwetu kipo katika uwezo wetu tuliopewa na Muumba...mradi tu ulihitaji jambo hilo kwa dhati kabisa toka moyoni mwako....
Kwa kutambua hilo huna sababu ya kuwa na wasiwasi juu ya maisha na juu ya kesho....iambie nafsi yako kwa dhati kabisa toka moyoni yakuwa Unaweza.
Unaweza kuwa imara kuliko hofu uliyonayo,
Unaweza kabisa kuwa na afya bora,furaha na amani,
Unaweza pia kuwa sababu ya vyote hivyo kwa wengine,
Unaweza kuwafanya wengine watambue kuwa wao ni nuru,nao wanapaswa kuifanya nuru hiyo iangaze wengine
Kuafanya wayatazame maisha katika upande wa mwangaza

Iambie nafsi yako kuwa,
Unaweza kubadili maisha yako na kuyafanya kuwa nuru,
Unaweza kufikiri chanya na kutenda kwa uwezo wako wote
Kuwa chachu ya mabadiliko chanya duniani,na kuwa mfano wa kuigwa

Iambie nafsi yako yakuwa unaweza kusahau yaliyopita,
ambayo yalikusababishia maumivu,na kuishi maisha yenye furaha na matumaini,ukianza upya bila woga,
Unaweza kuwapenda na kuwajali wengine pasipo kutazama maumivu ama mabaya waliyokutendea
Unaweza kusimama imara hata katika nyakati za magumu mengi
        furaha ni pale unapotumia maisha yako kuwa furaha kwa wengine-unaweza kuwa chachu ya upendo na anani


Sema kwa nafsi yako kuwa unaweza
Kuishi bila kusengenya na kuwanenea wengine kwa ubaya,bali unaweza kuwa faraja kwa watu wote,
Iambie nafsi yako kuwa wewe ,ukiwa kama nafsi huru,
Una jukumu la kutenda hapa duniani,
Iambie nafsi yako itazame kwa kina,
Ichunguze umuhimu wa maisha yako hapa duniani
Na kisha kuamua kufanya dunia kuwa sehemu ya upendo

Tuesday, August 7

MWALIMU BORA

Wale waliopitia ugumu ,milima na mabonde katika maisha yao ni walimu bora,kwa sababu wanajua maana ya kila jambo walilolipitia,wanajua jinsi gani ya kubomoa ukuta wa mipaka ya kufikiri,wanajua kuumizwa,wanajua faraja,wanajua chuki,wanajua amani,wanajua upendo,wanajua kila jambo walilolipitioa si kwa kusoma nukuu tu,bali kwa kuishi na kupambana na vikwazo...wanatambua kuwa hakuna njia ya kupambana na woga zaidi ya kuamua kutenda unachokiogopa,wanatambua jinsi ya kufungua minyororo inayotuzuia kuyafikia mafanikio,hawa maisha yamewapa changamoto,maisha pia yamewapatia baraka tele...wamepata majaribu,wakayapita,wamepata maumivu,wakaendelea kusimama imara ,watu waliwakejeli,waliwaumiza na wengine waliwapa faraja...waliamua kuacha yaliyopita na kusimama tena kwa ushindi,wakachagua kuwa washindi,wakaishi maisha yao kwa ajili ya wengine pia,woga wao ni kuogopa kutenda wanapotakiwa kutenda..wamekuwa mifano bora katika jamii,wanatambua kujitolea ,hawa ni mashujaa ambao nuru ya maisha yao itaishi milele.Ni wakati sasa wa sisis kutoogopa kushindwa na kuamua kudiriki kutenda.

Thursday, July 12

DINI NA UUMBAJI WA WAAMINIO.

tazama Mungu umtafutae yupo ndani mwako
TAZAMA MUNGU UMTAFUTAE,YU NDANI MWAKO

Waimbaji huiwakilisha nuru ya Mungu kwa nyimbo.Waandishi pia hutufundisha yatokayo ndani mwao kwa kutumia maneno na kuyaandika.Wahubiri huifundisha nuru ya Mungu kupitia vipawa vya kuzungumza na kwa mifano mbalimbali hukumbusha uwezo wa Mungu ulio ndani mwetu.Mjasiriamali vivyohivyo hutenda kwa kutumia maneno yao ya kibiashara na bidhaa zenye kumjali mnunuzi.

Je wewe binafsi unaufundisha vipi utukufu wa Mungu?

Hakuna aliye hapa kwa bahati mbaya.Tuna sababu ya kuwepo duniani.
Nayo ni kufurahia uumbaji wa Mungu na kuitengeneza dunia bora.
Je,ni jinsi gani dini na imani ndani yake inatujenga kutambua sababu ya sisi kuwepo?

Nianze kwa kukusihi usome kuanzia mwanzo mpaka mwisho,ili uweze kuelewa ni nini nimekusudia kukifikisha kwako.....SI KAWAIDA KWANGU KUTAZAMA JAMBO KATIKA UPANDE HASI,lakini nitajadili upande hasi wa dini kwani ndicho kilichonisukuma kuandika kwa sasa,ninakusihi uchukulie hii kama elimu chanya ili ikusaidie kujadili na kujitambua.

 Dini inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji-hii ndiyo maana ya kimtazamo kuhusu dini...Japo kimantiki hii si maana halisi.

Kila anayeingia katika imani hii,ama dini,matazamio yake huwa ni kwamba,dini itakuwa ni suluhisho la kila jambo kwa binadamu.....dini inatazamiwa kuwa ndio amani,ndiyo furaha,ndio umoja,ndio huruma,ndio usawa,ndio kila chimbuko la ubinadamu,na kikubwa kumfanya binadamu ajitambue yeye ni nani,anatoka wapi na anakwenda wapi......

Lakini kwa sasa imekuwa ikiwafanya binadamu kuwa tegemezi,wasio huru katika kila nyanja ikiwemo uhuru wa kufikiri usio na mipaka,uhuru wa kuchagua(simaanishi uchaguzi mbaya). Dini imekuwa kifungo cha kuwafanya wengi wasitumie vipawa walivyonavyo na hata wasisikilize sauti ya Mungu inayowatuma kutenda kwa ajili ya utukufu wake.(Unaweza kuuliza kivipi,jibu ni fupi...imani nyingi katika dini zimeweka mipaka ,inayomfanya muamini asifikiri juu ya hapo)NA KUWAFANYA wawe na maisha yasiyo na mwelekeo wa ushindi na hivyo kuamini kinyume na matarajio ya imani yenyewe.

1.KUMWOGOPA MUNGU
  Dini nyingi zimewafanya waumini wake wamwogope sana Mungu na kumuona kuwa ni adui.Wengi wamekuwa wakimuona Mungu ya kuwa yu mbali sana nao,asiye rahisi kufikika,asiye rahisi kuongea nae.

Wanasahau ya kuwa Mungu wamtafutao na kumwogopa yupo ndani mwao..Nae ni sauti iliyo kubwa kuliko utashi wa mtu mwenyewe,kuliko awazaye mtu,.Wanasahaulika ya kuwa yeye huzungumza na yeyote yule ,kwa wakati wowote pale kila mmoja awaye tayari kumsikiliza.

NAYE NI RAFIKI MKUBWA WA NAFSI YA KILA MMOJA WETU, Mungu ni mpole,mwenye huruma,asiyetazama tutazamavyo sisi,bali hutazama mawazo ya mioyo yetu,naye hujibu maombi ya mioyo yetu,na si maneno yatokayo kwa mtu..

 Hivyo kwa matokeo hayo dini hujenga jamii ya watu wenye kujiogopa wenyewe,wakimwogopa Mungu aliye rafiki mkuu,wakiishi maisha bandia ya kujionesha kwa wengine hasa wale wanaowaongoza,wawaone ya kuwa wamejaa nguvu za Mungu na matendo yaliyotukuka,huku wakifanya kinyume kwa siri(siri kwa binadamu wenzao,lakini Mungu ambaye tupo nae nafsini mwetu anatutazama kwa ubandia wetu)

2.KUISHI MAISHA YA WENGINE 
Dini zimekuwa zikiwafundisha na kuwafanya watu waishi maisha ya wengine na kuchagua maisha ya wengine waliopita na kuyaacha yetu yale tuliyoitiwa ili nuru yetu ing'ae kwa wengine....Hapa naomba nieleweke vizuri kuwa viongozi wengi wa dini wamekuwa wakiwafundisha watu kuishi kama fulani aliyepita(wapo wanaowaita watakatifu,wengine viongozi wao waliopita....)wakijitesa,wakijinyima pasipo sababu ya msingi,(SABABU ISIYO MSUKUMO WA MHUSIKA BALI MSUKUMO WA NJE}na matokeo yake kuishi maisha yasiyo ya furaha kwani mwisho hugundua ya kuwa furaha huja pale unapoishi maisha uliyoitiwa wewe mwenyewe,
Ukiyaishi kwa kujitolea si kwa ajili ya kuneemeka,bali ili wengine waitambue nuru ya Mungu aliyo ndani ya kila mmoja,na wale wasioamini ,wajitambue na kuiishi.

Dini zitakufundisha kuishi maisha ya wengine na matokeo ya wengine lakini ROHO WA MUNGU aliye ndani mwetu hutufundisha kuishi maisha yetu halisi ili tufikie katika matokeo mapya,yamtangazaye Mungu na utukufu wake.
Wengi wameingia kwenye mkumbo kwa kufuata tu imani ,kwa sababu ni za wazazi wao

3.DINI NA WATEULE

Dini hutoa picha ya matabaka,ya walio wakuu kuliko wengine,na wale wanyonge(watawaliwa) wanaosubiri pia kupewa ukuu na Mungu.inatokeaje? Viongozi wengi wa dini wamekuwa wakijipa ukuu na kuwaaminisha wengine kuwa ukuu huo umetoka kwa Mungu.Viongozi hawa wamejitangazia utawala,wakichuma kutoka kwa wengine ambao daima huwaogopa na kuhisi labda,Mungu kateua baadhi,na kwamba wao si wateule.

UKWELI NI KWAMBA,KILA MMOJA YU SAWIA KWA 
MUNGU,Yu bora akiwa na uwezo na nguvu za kuponya,kuamsha upya ari ya kila kitu,kulea,kuwanyanyua wanyonge badala ya kuwakandamiza,na ukweli ni kwamba,kwa sababu tuu mfano wa Mungu(tukifanana katika nguvu )tunauwezo wa kufanya chochote kile,kuyafikia mafanikio makubwa,kuvumbua vitu vipya,mradi tu tumetambua uwezo huu na kuchagua kuutumia  

aliye mkuu yu ndani mwetu,sote tu bora
kila mmoja akitumia kipawa chake vyema,basi huwa mkuu..tukumbuke aliye mkuu ni yule atendaye yote kwa ajili ya wengine pasipo kutegemea malipo,aliye tayari kuona wengine wakinyanyuka na kuendelea mbele,asiyetengeneza matabaka,ambaye kwake kila mmoja ni sawa,na katika yote,upendo humsukuma kutenda

Tunaweza kuyaona matokeo ya dini,ni jinsi gani inaumba mustakabali wa waamini wake dini zimekuwa ni chanzo kikuu cha matabaka na ubaguzi duniani hasa kutoka kwenye imani na mafundisho ya msingi ya imani husika,dini moja hujiona ni bora kuliko nyingine...tena zinawafanya baadhi kujiona wao ni wateule na kutengeneza tabaka la wanyonge tofautti kabisa na makusudio ya MUngu.mf. mkatoliki anajiona ni bora na ni mteule ukijilinganisha ma mlutheri,mkristo anajitazama kama ni mteule akijilinganisha na mwislamu.mlokole anajipa sifa ya kuwa mteule pekee wa mungu akijilinganisha na wengine...hili ni kinyume kabisa na malengo ya Muumba ya kumuumba kila binadamu na kumfanya kuwa sawa na mwingine..dini zimeleta imani iliyopelekea matabaka..choyo,majivuno,utengano na hata kutowasaidia wengine kwa kuwaona si wa darajasawia... tukirejea vita na vurugu nyingi ni zile ziletwazo na dini...rejea ireland,nigeria,sudan,uturuki zamani.....tena hizi ni vita kati ya dini kubwa zinazofundisha usawa na upendo lkn zikishindwa kuonesha matokeo bora... dini pia zimekuwa ni chanzo cha kumfanya binadamu kuwa mtumwa wa mawazo yake naa mazingira yake...zinafundisha kinyume cha makusudio ya MUumba ya kumfanya binadamu kuwa huru na kuyatawala mazingira yake...zinafundisha utegemezi huku viongozi wakuu wakiwatumia waumini wao kama daraja la kujipatia utajiri na utawala...

Mbele za Mungu hakuna aliye mkuu na wala mtawala...kila mmoja amepewa nguvu na uwezo na anapaswa kuzitumia kama nuru ya utukufu wake MUNGU hapa duniani... Ni WAKATI SASA KUTAMBUA YA KUWA DINI ya kweli ya kila mmoja,ipo ndani mwake...na kuwa ukitambua hilo,utakuwa huru,mawazo huru yasiyo na mipaka,kila jambo litawezekana na li ndani ya uwezo wako kwani Mungu aliye suluhisho la yoote,yu ndani mwako.

Lengo langu si kupinga uwepo wa dini,lengo langu ni kukufanya ujitambue na unyanyuke,uwe na hofu ya kweli,hofu ya kuona unamaliza uwepo wako hapa duniani pasipo kuifanya nuru ya Mungu iliyo ndani mako,ing'ae......hofu ambayo itakufanya utumie maisha yako yote kuwainua wengine.....walio wahitaji,walio wanyonge,walio wafungwa na kila mmoja ambaye upendo tu,huwaamsha

Thursday, July 5

FURAHIA MAISHA,FURAHIA JINSI ULIVYO

furahia maisha,furahia jinsi ulivyo
MAISHA HUTUMA CHANGAMOTO,MAISHA PIA HUTUPA MATUNDA NA NEEMA TELE,UTAPATA MAJARIBU,NA PIA MAISHA YATAKUPA MATOKEO MEMA,TUNAPATA MACHUNGU,LAKINI TUNAPATA MATOKEO YA FARAJA NA FURAHA,WENGI WATAKUJA NA KUWA FARAJA,WENGINE KUWA MWIBA,WENGINE WATAKUONESHA CHUKI,LAKINI YOTE YAKUPA WAKATI KUJIFUNZA NA KUKUA KUTOKANA NA CHANGAMOTO HIZO,MUDA UTAKWENDA...YALIYOPITA YANAKUWA FUNZO KWAKO....KUNA SABABU YA KILA JAMBO KUTOKEA...NA JINSI UNAVYOCHUKULIA KILA JAMBO,NALO HUKUPA MATOKEO YALEYALE...HIVYO NI VEMA TUKALICHUKUA KILA JAMBO KATIKA MFUMO CHANYA,YAANI KILA CHANGAMOTO IWE NI NJIA YA WEWE KUKUA NA KWENDA MBELE ZAIDI,,MAISHA YATAKUFUNZA KUCHAGUA...WAWEZA KUCHAGUA KWENDA MBELE KWA FARAJA AMA KUTAZAMA KILA JAMBO KWA WOGA NA KUANGUKA BILA KUSIMAMA...KILA MMOJA ANA UCHAGUZI...NI VEMA KUCHAGUA KWENDA MBELE NA MAISHA....TUNAWEZA KUYAISHI VYEMA MAISHA KWA KUCHAGUA KUWA BORA ZAIDI NA KUWA MIFANO BORA...KUFURAHIA MAISHA NA KUYAISHI BILKA KUOGOPA AMA KUTAZAMA KWA HUZUNI NA WOGA...HAYA YOTE TUTAYASHINDA KWA KUFANYA BIDII NA KWA KUJITOLEA KWA MOYO WOTE...KUWA MMOJA WA MJENZI WA DUNIA BORA...JUHUDI NA KUTOKATA TAMAA(UVUMILIVU)YATATUPATIA MATOKEO BORA...PALE TUNAPOCHAGUA KUWA MWONGOZO WETU....JIAMINI,...FUNGUA MOYO WAKO..SIKILIZA SAUTI YA MOYO WAKO....TIMIZA NDOTO YAKO.........ISHI NA KUYAFURAHIA MAISHA