Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH
Showing posts with label MY WISDOM. Show all posts
Showing posts with label MY WISDOM. Show all posts

Friday, August 2

MUNGU KATI YETU

MUNGU KATI YETU


Hekima ipo katika kutambua tofauti iliyopo miongoni mwetu wanadamu.

“Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani,  alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.Yakafumbuliwa macho yao,wakamtambua,Kisha akatoweka mbele yao.
Wakaambiana,Je mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?Luka 24:30-32


Nahitaji mwalimu!!
Nahitaji msaidizi!!!
Nahitaji mwombezi!!

"Kama nikipata mwalimu ama yeyote atakayeniongoza,Maisha yangu yatakuwa mazuri!!

Inawezekana haya ni baadhi ya maoni yako ambayo unahisi yanaweza kubadili maisha yako,pasipo kutambua kwamba mwalimu,msaidizi , yupo kati yetu.
Wakati Fulani unaweza kutoka Singida, kukitafuta kitu Dar es salaam, kumbe umekiacha Singida kikipatikana kwa wingi na bure.

Natoa mfano huu kuonesha kwamba zipo nyakati unaweza ukatafuta kitu Fulani na kukifuata mbali,kumbe kinapatikana katika mazingira unayoishi.

Utashangaa nitakaposema kwamba,kuna watu ambao wanakuzunguka na unaishi nao, ambao Mungu amewaweka makusudi katika kuifanya safari yako ya maisha kuwa rahisi,lakini upofu ulio ndani yako,unakufanya usitambue kabisa.

Nyakati zote unawatazama kama ni wa kawaida tu, hawana umuhimu kwako,na hivyo badala ya safari yako ya mafanikio kuwa  ni siku 40, inakuwa  ni miaka 40.

Wapo watu ambao wakati mwingi nawafuatilia.Na huwa najiuliza ni kwa nini sikupata kuwatambua mapema.Matendo yao,mienendo yao, maneno yao, mitazamo yao huweza kuamsha nguvu ndani yangu.

Tabia yangu hii ya kudadisi imenifanya nianze kuwatazama kila nnayekutana nae kwa jicho la kipekee,kwa sababu naamini,kila ninayekutana nae katika kazi,sala,mijadala,daladala,hawajatokea kwa bahati mbaya, bali Mungu ana makusudi.

Mara nyingi nafanya hivi pasipo hata wao kutambua kwamba nathamini kukutana nao.

Mungu yupo miongoni mwetu,na wakati mwingi hatutambui hilo.

Mara nyingi tunadhani Mungu yupo kanisani ama msikitini.

Tukiwaona wachungaji,mapadre na viongozi wa kiimani,tunadhani ndipo tunapoweza kumwona Mungu.

Mungu yupo miongoni mwetu.Kwa wadogo,wadhaifu, warefu,wafupi,weusi,wembamba. Mungu yupo miongoni mwetu.

Binadamu wengi hawapendi kutazama zaidi ya mwonekano wa mtu.Ukijifunza kutazama zaidi ya mwonekano wa nje,unaweza kuona kilicho ndani na thamani ya kisichoonekana kwa macho ya nyama.

Kwa wale wanaoishi na wenzi wenu,Mungu anaweza kuwa ndni ya mwenzi wakounayelala nae kwenye kitanda kimoja.Moyo wa kudhani/kutazama kwa kuhukumu unaweza kukufanya usitambue hilo.

Anaweza kukupa suluhisho juu ya jambo,lakini kwa sababu unamtazama kwa nje, na kwa mazoea basi huwezi ona kilicho ndani yake.

Lakini akisimama kiongozi wa kiimani, akiongea kwa sauti ya kukuvuta, akikupa ushaurinhata usiofaa, utapiga kelele na mwitikio mkubwa moyoni mwako.Ndio baba!!!

Hekima ipo katika uwezo wa kutambua kisichoonekana.

Mungu yupo kati yetu, picha uliyonayo kichwani mwako kuhusu Mungu inakufanya usimtambue.

Kitu unachokifuata maili nyingi,kipo kinakuzunguka katika mazingira yako

Naitwa Pongu Joseph



x

Monday, September 30

SIFA ZA BINADAMU ANAYEJITAMBUA

Katika makala hii tunajifunza juu ya binadamu anayejitambua.Makala hii inaweza kukukumbusha mambo mengi kwa kifupi na hivyo kukufanya uchunguze juu ya maisha yako na kuyatumia vyema kwa wakati huu ulipo hapa duniani.


Kutambua ndani yako hakuhitaji uende shule na kusoma sana,na hakutokani na maamuzi ya mtu mwingine bali ni maamuzi yatokayo ndani mwako
Ni mguso unaotaka ndani mwako, ufahamu unaokua toka ndani mwako. Ni uchimbuzi wa chemchem zitokazo ndani mwako, Ni kumtambua Mungu kupitia mguso ndani ya moyo wako, kisha kuanza kutumia kipawa ulichonacho kwa ajili ya utukufu  wa Mungu . Ni hisia za ndani zitakazofanya umfahamu Mungu na si kufikiria tu.Upya ndani ya binadamu hutokea wakati wote  kwa kuunganisha moyo wako na ulimwengu wa hisia na kuendelea kujifunza kila wakati na kukuza nafasi ya moyo wako kuwa mpya.
 na
Je ni kwa namna gani unamtambua binadamu anayejitambua?

Mtu anayejitambua hubadili mtazamo wake kutoka kwenye mtazamo wa jamii unaofuata mila na desturi/kawaida kuelekea kwenye fikra za kuijenga dunia mpya na yenye fursa mpya.Hujenga dunia ambayo wanaomzunguka ni wanadamu wanaotambua utu na nafasi ya kila nafsi.Akiwa na misingi ya ujamaa na usawa, hufanya majukumu yake kutoka kujitazama yeye binafsi na kuanza kuwatazama wengine.Uchaguzi wake na matendo yake husukumwa na  maono na mtazamo wa mbali kwa ajili ya binadamu wote na viumbe vyote.Hutazama sio kila kiumbe kwa ajili yake,bali kila kiumbe kwa ajili ya wote.

Anayejitambua habagui jinsia bali hutambua jinsia kuwa ni matokeo ya fikra za Mungu yaliyokusuduia kutoa fursa.Huheshimu, hutambua wengine na kuthamini nafsi zao na uchaguzi wao.Hutengeneza dunia dunia ambayo jinsia zote huwa na uhuru wa  kutumia vipawa vyao, kutambua sauti zo,nuru ndani mwao na kutumia kwa ajili ya viumbe wote. 

Mtu anayejitambua hasukumwi kutenda na maamuzi ama fikra za wengine. Anatazama ndani yake.Hajifananishi na nafsi zingine na hivyo hatumii nafasi yeyote kuwakandamiza wengine.Husimama kwa miguu yake mwenyewe. Anawasikiliza wengine isipokuwa hatoi nafasi kwa wengine kumuamulia maisha atakayoishi. Anayaona mambo yajayo na hivyo huanza kuijenga kesho yake katika wakati tunaouita sasa. Ni alama ya uwezo wa Mungu uliopo ndani ya binadamu. Na alama ya maisha yake huishi enzi na enzi.

Mtu anayejitambua huchukua hatua juu ya hisia zitokazo ndani mwake na hivyo kutambua matokeo ya matendo yake.Hutenda kwa msukumo wa moyo. Hutambua mambo ambayo hayamletei faida na kutoyafanya na pia hutambua yale yanayomletea faida ..akitambua kuwa anapotenda kwa wengine anajitendea mwenyewe. Husikiliza hisia za ndani mwake na kujifunza lugha ya moyo wake.

Huishi maisha yenye sababu. Husikia muito alioitiwa na kuuuishi. Haridhishwi tu na maisha ya tokanayo na matukio kama kuamka,kutembea,kulala,kula bali hutambua kuwa yupo hapa duniani kwa sababu maalum,hivyo huchimba ndani mwake kuijua sababu na kuiiishi. Kila wakati anasukumwa na sababu hiyo  ya yeye kuishi ,kuendelea kuishi kwa dhati akitengeneza na  kuifuata njia inayomfikisha huko.

Hakimbii majukumu yake . Hajitoi katika kutafuta suluhu ya changamoto na wala halaumu wengine. Hutambua makosa yake na kujifunza kupitia hayo. Husanifu maisha yake na kuyafanya mapya kila wakati.
Hujifunza toka ndani mwake na kutoka kwa wengine. Hutilia mkazo katika mafanikio ya ukuaji ndani mwake kuliko mafanikio ya nje., hutengeneza ndani mwake. Hutafiti na kuvumbua chemchem zinazojenga na kubomoa nafsi na kutumia chemchem hiyo kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi.Hivyo aliyejitambua ni picha tosha ya uwezo na uwepo wa Mungu ndani ya binadamu. Hutengeneza msawazo kati ya chemchem ndani mwake na matokeo yaonekanayo halisia.;
Binadamu anayejitambua hutazama kila jambo kama fursa


Anayejitambua hatafuti usahihi katika utendaji bali hutenda kwa kujitolea katika nguvu na uwezo wote.Hufanya kwa uwezo wake wote.
Anayejitambua hujikita katika kutenda kuliko kusema tu.Huweka bidii katika kazi . Huanzisha na kutenda mambo ambayo hufaidisha viumbe wote . Husema pale inapohitajika,huheshimu mawazo yake na huwa tayari kuchukua malipo ya maneno yake mwenyewe.Hakimbii kivuli chake. Hayupo tayari kuona wengine wakikosa uhuru  kupitia yeye. Anatambua kuwa wakati wote huvuna alichopanda..

Anayejitambua huweka mkazo katika uhusiano mwema na nafsi zingine. Huthamini mahusiano yenye thamani. Mahusiano kwake hutokea ndani, hujengwa ndani na hivyo hudumu. Upendo kwake ni lugha ya moyoni, huleta furaha, mshikamano na amani.Zitokeapo changamoto katika mahusiano,huwa tayari kuyatatua kwa ajili ya kuyakuza zaidi.

Anayejitambua hutambua kuwa hapa duniani hatupo katika kushindana,ushindani kwake haupo,hushirikiana na ushindi kwake ni furaha katika kutimiza wajibu wake. Huandaa silaha zake ndani na kuteketeza kila kisicho na manufaa kwa binadamu. Baada ya milima na mabonde katika maisha yake ushindi huzaliwa ndani mwake. Hutumia uwezo wake kwa ajili ya Wengine na si dhidi ya wengine..

Huishi katika hali ya kujitolea na bidii. Huwa ni zawadi ya aina yake hapa duniani. Haogopi kutenda. Huendeleza mambo yaliyojenga utu,ubinadamu na misingi bora ya kuishi yaliyojengwa na binadamu waliomtangulia. Maisha yake hufundisha wengine.  Hutambua juhudi za wengine na wote wanaompa msukumo wa kutenda zaidi hasa pale anapokutana na  changamoto. Hutambua kuwa hayuko peke yake,bali dunia imejengwa kwa muungano wa nafsi zinazotimiza majukumu kwa dhati.

Haogopi ukweli hata pale unapoumiza. Hutoa nafasi ya kusamehe kila wakati anapokosewa. Hujisamehe yeye pia anapofanya makosa. Hushiriki katika ujenzi wa maisha yake.
Hutambua kuwa kila jambo hutoa fursa,kila kiumbe ana fursa. Hakusanyi ama kujilimbikizia kwa ajili ya sifa. Hutazama wengine kama anavyofanya kwa nafsi yake. Inapostahili hujitolea alichonacho,hutoa kwa wale walioshiriki kwa yeye kupata. Hutengeneza maisha yake yawe ya kutoa fursa kwa wengine badala ya kuwanyang’anya wengine .

Anayejitambua haichukuliai dunia kama chanzo cha maumivu bali hugundua kuwa dunia humpa kila mmoja kadiri anavyohitaji.Dunia husikiliza kutoka kwenye uwezo  ulio ndani mwetu tuliopewa na Mungu.Hata mara moja hajichukulii kuwa ni bora kuliko binadamu wengine na wala si dfhaifu kuliko wengine. Hutambua kushabihiana na kutegemeana kati ya kiumbe kimoja na kingine.Hivyo anatambua kuwa kama ikiharibu mazingira ,ni sawia na kuharibu nafsi yake.
Binadamu anayejitambua huyajenga na kuyatunza mazingira yanayomzunguka


Anayejitambua hamlaumu Mungu hata mara moja. Uhusiana wake na Mungu ni wa heshima,urafiki na huwa na umoja naye . Mienendo yake yote humwelekea Mungu .Anawaheshimu wanaoamini sawia naye na wasio amini sawia naye. Hashiriki kutumia imani ama dini kama njia ya  utengano kati ya binadamu,ama binadamu na mazingira yake.

Ni mfano wa sifa njema ya binadamu. Huchukua majukumu yake. Ana faida kwa viumbe wote.Hulinda, hujenga, huheshimu, Huishi vyema duniani. Ni mfano wa aliyeletwa kuifanya nuru ya Mungu ing’ae. Ni halisi,haishi maisha bandia. Ni wa kutumainiwa, si mbinafsi. Wakati wake kuwepo duniani ukifikia tamati,huondoka kwa furaha ya kutimiza alichotumwa,na kuacha dunia ikimlilia.Ni wewe na mimi.

Monday, February 4

RAFIKI WA KWELI

Rafiki wa kweli ni yule ambaye unaweza kumwamini,ni yule ambaye unaweza kumshirikisha furaha,huzuni na kila tamanio la moyo wako,ni yule ambaye hakuhukumu kwa kufikiri tu,ama kusikia toka kwa wengine,ni yule anayekubali na kuheshimu maamuzi yako,uchaguzi wako na uhuru wako,ni yule ambaye yupo tayari kutumia alichonacho kwa ajili yako,ni yule anayeweza kukukosoa na kukufanya utambue njia bora na kukua ukiendelea mbele daima,hutambua umuhimu wako na kukupa moyo,kukuamsha uwe bora zaidi na kufikia mafanikio,Hukusikiliza na kukushauri pale panapostahili na unapohitaji...daima huwa kwa ajili yako..rafiki wa kweli hawezi kuwa na ajenda za siri,hawezi kukuzunguka n A KUKUSALITI...rafiki wa kweli hufurahi pale unapofanikiwa na si kuweka kinyongo na kuumia pale unapofanikiwa,daima huwa pamoja nawe......na ni furaha kubwa pale unapogundua kuwa rafiki yako mkuu ni wewe mwenyewe....furaha pia ni kumpata rafiki wa kweli ..ni wachache....daima nafurahi kupata marafiki ambao wanathamini uwepo wangu,ambao hufurahi wakiona nasonga mbele.Ambao wako tayari kujitolea kwa ajili ya wengine,hasa kupitia blog hii .nitakuwa sina fadhila kama sitasema ahsante itokayo katika furaha ya moyo wangu

Friday, December 7

Kumbuka wimbo wako




Katika dunia hii ni vema kuyaishi maisha yako pasipo kuigiza,yawe yako halisi..Ukiyaishi kwa juhudi zako,hutapata kuwa na wasiwasi juu ya kifo na matokeo yake...Waheshimu wengine wote,heshimu imani zao,fikra zao na mitazamo yao.Yapende maisha yako,furahia maisha yako,heshimu maamuzi yako katika maisha,sikiliza hisia za moyo wako...Fikiri kuishi maisha marefu yenye thamani kwa wengine.Kila ukutanapo na watu,wafanye watambuae nuru ya Mungu iliyo ndani mwako...ing'ae kwao,nao wajifunze kutoka katika nuru hiyo,na kuwafanya nao pia waishi maisha yao halisi yenye thamani kwa wengine....Wathamini wote,wageni kwa wenyeji...Kila uamkapo tafakari thamani yako na nafasi uliyonayo kutenda makubwa zaidi..shukuru kwa siku mpya,Kama hutaona sababu ya kushukuru,basi ndani yako hujautambua mwanga,na utaidanganya nafsi yako mwenyewe..: Na pale wakati wako wa kuyaendea maisha mengine mapya hutapatwa na woga,wala wasiwasi juu ya yajayo.....usiogope kama wale ambao kifo kikiwajia hujaa hofu na kuomba muda kidogo wa kutekeleza yale ambayo hawakuyatilia maanani pale waliposukumwa na mioyo yao kutenda...Kumbuka wimbo wako...wa kumkaribisha rafiki yako,atakayekupokea katika maisha mapya,kifo...kisha aga dunia kwa furaha,kwa sababu uliishi vema..kishujaa.

Thursday, September 6

ujumbe 2

Ipo siku ambayo hutahesabu tena ni nini unamiliki ama umepoteza.......
chuki,hasira na majaribu yote hayatakuwepo
Haitajalisha kuwa ulikuwa na sura nzuri ya mvuto ama ulionekana wa sura mbaya
wala ngozi,wala jina halitahesabika
Ni NINI KITAHESABIKA....
KiTAHESAbika ulichotoa kwa wengine na si ulichopokea
Kitahesabika ulichojenga ukiwa duniani,kilichowainua wengine,,,na si kile cha kifahari ulichonunua
Ni kila upole,usawa,utu, na kuwanyanyua wote walio wahitaji,
nI vile ulivyo,wewe halisi,ulivyoyaishi maisha yako kwa ajili ya wengine
Si watu wangapi wanakufhamu,ama umaarufu wako bali ni kiasi gani wengine wataumia pale wanapokukosa
Ni ule umuhimu wako kwa wengine
Si kumbukumbu tu kwamba ulikwepo,bali ni kumbukumbu ya maisha ya wengine uliowabadilisha na kuwasaidia kufikia furaha.
Kitakachohesabika si ni muda gani utakmbukwa,bali ni nani na kwa nini unakumbukwa,ni kwa wema uliotenda
Katika maisha tuishio,ni muhimu kuishi maisha yenye faida kwa wengine....
jiulize ni nini kimekuleta duniani...ishi kilichokuleta

Sunday, September 2

UJUMBE

Wakati mwingine huhisi kuwa niandikayo hapotea tuu,hutazamwa tuu,na hata kutotiliwa maanani...hii hainikatishi tamaa...siuzi ujumbe...hutolewa bure...wakati mwingine nafikiri kurudia na kurudia
Wakati mwingine nasoma kwa kurudia na kurudia,nami hupata faraja.Siandiki tu kujifurahisha....naandika nikilenga kubadili maisha ya wale walio katika huzuni,kuanguka na wote wanaohitaji maneno tu kusimama na kuanza tena maisha yenye mafanikio...naweza nikawa sijaridhisha wengi,lakini ukweli ni kwamba nitaweza kuinua wachache...kwa yule ambaye huguswa na hata machache ,huu ni upendo wangu uende0 kwa wote....naamini siku moja nitakuwa sababu ya furaha kwa wengi...Ni tamaa yangu kuona ujumbe unafika mbali...kuwaamsha wengi....naamini ipo siku mlango mkubwa utafunguka...kwa ajili ya wengi..nami nitajitolea daima,kusimama pale Mungu atakaponituma.

Saturday, September 1

YALIYOPITA YAMEPITA...SONGA MBELE

Wapo wanaotazama mambo ya jana,juzi na yote waliyoyapitia na kukata tamaa,Wakisikia jinsi marafiki wao wanavyowanenea mabaya,wakitazama kila pande na kuhisi hakuna anayewajali,wakiangalia pande zote wasione tumaini,hukata tamaa lakini ukijitambua hutakata tamaa kamwe,kwani utatambua kuwa ni Mungu na wewe ndiye uliyetumaini juu ya yote...Hutaweka matumaini kwa wengine tu,bali utajifunza kuwa wewe ndiye unayepaswa kuchukua hatua juu ya maisha yako.
Maumivu tuliyopitia hutupatia juhudi mpya na uwezo mpya.Yote wanayokunenea wengine hayatakufanya uwe vile wanavyotaka ama kudhani kuwa utakuwa hivyo,bali uamuzi wako utayainua ama kudidimiza maisha yako mwenyewe.Utaacha aibu na woga wa kufanya jambo kwa kuogopa kuwa wengine watakucheka ama kusema vibaya juu yako.Jibu kwao ni mafanikio utakayoyapata,ambayo yatawafunza wao pia.Hutajiona kuwa hustahili kuwa unavyopenda,bali sasa utaamua na kujipenda,ukiishi kwa ajili ya wengine pia
Kila jambo huwa na sababu ya kutokea,ukitazama yaliyopita kwa moyo mweupe,utafurahi kupita huko,kwani ndiko kunliko kuinua na kukufanya uwe imara zaidi..Ndipo sasa utakapoanza kujitazama upya na kujipenda jinsi ulivyo,jinsi ulivyoumbwa,na si jinsi wengine wanavyotaka uonekane....usiwaache wengine wakuchagulie maisha yako...usiache yaliyopita yakakuchagulia jinsi utakavyokua.
Tazama ulivoshinda vikwazo,kisha chukua nguvu ya ushindi wako na songa mbele.Unaweza na maisha yanaendelea.Amka...songa mbele

AHSANTE WOTE


Rafiki wa kweli ni yule ambaye unaweza kumwamini,ni yule ambaye unaweza kumshirikisha furaha,huzuni na kila tamanio la moyo wako,ni yule ambaye hakuhukumu kwa kufikiri tu,ama kusikia toka kwa wengine,ni yule anayekubali na kuheshimu maamuzi yako,uchaguzi wako na uhuru wako,ni yule ambaye yupo tayari kutumia alichonacho kwa ajili yako,ni yule anayeweza kukukosoa na kukufanya utambue njia bora na kukua ukiendelea mbele daima,hutambua umuhimu wako na kukupa moyo,kukuamsha uwe bora zaidi na kufikia mafanikio,Hukusikiliza na kukushauri pale panapostahili na unapohitaji...daima huwa kwa ajili yako..rafiki wa kweli hawezi kuwa na ajenda za siri,hawezi kukuzunguka n A KUKUSALITI...rafiki wa kweli hufurahi pale unapofanikiwa na si kuweka kinyongo na kuumia pale unapofanikiwa,daima huwa pamoja nawe......na ni furaha kubwa pale unapogundua kuwa rafiki yako mkuu ni wewe mwenyewe....furaha pia ni kumpata rafiki wa kweli ..ni wachache....daima nafurahi kupata marafiki wa namna hii..nitakuwa sina fadhila kama sitasema ahsante itokayo katika furaha ya moyo wangu

Tuesday, August 28

TUNAENDELEA MBELE

KATIKA MAISHA TUNAPITIA MAGUMU.....tunapitia kuanguka mara nyingi...tunapitia kukatishwa tamaa,kusengenywa,kutengwa na hata kudaharauliwa.....tunapitiwa kuumizwa katika mahusiano,kuachwa,kudhulumiwa nk...haya yote hayana budi kutokea,jambo la muhimu ni kuwa tunavumilia yote na licha yakuwa tumeanguka mara nyingi,lakini pia tumesimama mara nyingi zaidi...na ndio maana tunaendelea na maisha kama ili

vyo kawaida,tunaendelea kuandika,kuwaelimisha wengine,kuwaburudisha wengine na kuwafariji wengi....tunayafahamu maisha,tunajua kuwa kama tutakata tamaa tutakuwa tumejidharau wenyewe,tumejiangusha wenyewe,tumejisengenya wenyewe na tumejidhulumu wenyewe.....
Hatukati tamaa kamwe
“Tunasikiliza mioyo yetu,kwa sababu hutupatia mwongozo wa maisha kila kukicha,hutukumbusha kuwa haklisi...hutukumbusha kuwa tupo kwa ajili ya wengine....hutukumbusha kuwa dunia inatuhitaji....hutukumbusha kuwa sisi ni zaidi ya tujifikiriavyo...sisi ni bora kama tulivyoumbwa

Tuesday, August 7

MWALIMU BORA

Wale waliopitia ugumu ,milima na mabonde katika maisha yao ni walimu bora,kwa sababu wanajua maana ya kila jambo walilolipitia,wanajua jinsi gani ya kubomoa ukuta wa mipaka ya kufikiri,wanajua kuumizwa,wanajua faraja,wanajua chuki,wanajua amani,wanajua upendo,wanajua kila jambo walilolipitioa si kwa kusoma nukuu tu,bali kwa kuishi na kupambana na vikwazo...wanatambua kuwa hakuna njia ya kupambana na woga zaidi ya kuamua kutenda unachokiogopa,wanatambua jinsi ya kufungua minyororo inayotuzuia kuyafikia mafanikio,hawa maisha yamewapa changamoto,maisha pia yamewapatia baraka tele...wamepata majaribu,wakayapita,wamepata maumivu,wakaendelea kusimama imara ,watu waliwakejeli,waliwaumiza na wengine waliwapa faraja...waliamua kuacha yaliyopita na kusimama tena kwa ushindi,wakachagua kuwa washindi,wakaishi maisha yao kwa ajili ya wengine pia,woga wao ni kuogopa kutenda wanapotakiwa kutenda..wamekuwa mifano bora katika jamii,wanatambua kujitolea ,hawa ni mashujaa ambao nuru ya maisha yao itaishi milele.Ni wakati sasa wa sisis kutoogopa kushindwa na kuamua kudiriki kutenda.

Tuesday, July 31

UPENDO,NDOA NA SHERIA

Mwisho wa makala hii utapata kujifunza mambo yafuatayo
  1. ni nini na jinsi gani upendo wa dhati
  2. HOFU-ADUI MKUBWA WA UPENDO
  3. ndoa,furaha,na huzuni katika ndoa-sababu
  4. sheria katika upendo na kushindwa kwa sheria kulinda ndoa
  5. jinsi gani utaishi maisha ya furaha katika ndoa
  6. nafasi yako katika upendo,ndoa.
  7. jinsi ya kuifanya ndoa yako idumu na kuwa na mafanikio kila kukicha
  8. jinsi ya kutazama kila jambo katika mfumo chanya na kubadili maisha yako

                                  UPENDO
 


     Upendo ni mvuto wa asili(nguvu ya asili) usio na shuruti kati ya mtu mmoja na mwingine.Ni lugha ya pekeee ambayo kiziwi,kipofu,mtoto,mzee, na kila kabila huisikia.Ni lugha ya moyoni..Ni NGUVU PEKEE INAYOTIBU,INAYOWEZA KUAMSHA WASIO NA TUMAINI,INAYOONDOA CHUKI,(UPENDO HUSHINDA YOTE).Upendo ndio ishara kuu ya Mungu(MUUMBA-ASILI YA VIUMBE VYOTE),,ni faraja,amani,ni tumaini...Ndio maana katika maandiko toka katika biblia tunaelezwa ya kuwa Mungu ni upendo
       Mara nyingi tumekuwa tukigawa aina mbalimbali kutokana na mazingira yetu na fikra zetu na kupata upendo wa dhati,upendo wa kawaida,lakini ukweli ni kwamba upendo unabaki kuwa ni upendo(unapopungua huo si upendo) na kinyume chake (chuki) inabaki kuwa chuki.Huwezi kusema kuwa unao upendo pasipo kuuishi/kutenda mambo yanayodhihirisha upendo.Upendo ni kutazama kwa huruma,upendo ni kuinua walkio chini,upendo ni kujitolea pasipo kuhitaji malipo,upendo hushinda yote.  
       Kama tulivyyoona hapo juu,upendo ni msukumo wa kiasili kabisa.Hutokana na mvuto wa asili utokao moyoni kwa mtu,na ndio maana nikauita upendo kuwa ni lugha ya moyoni.Kwa sababu ni mvuto wa kiasili,upendo haujengwi wala kulindwa na vitu visivyo vya asili.Fikra zetu zimejengwa kuutazama upendo katika mtazamo wa vitu ama mali.Mvuto huu wa asili huwa haujali rangi,dini,tofauti ya kimawazo ama mtazamo,haujali tofauti za taifa,ukanda ama lugha,kabila,haujali mali wala hali.Ni ukweli usiopingika kuwa kila mtu huweza kumpenda ama kuvutiwa na mwingine si kwa sababu ya dini,ama rangi,ama kabila,ama utaifa fulani,ama mali.....fikra za dini,mali,kabila,taifa huja kwa msukumo wa fikra(zenye athari ya kimazingira) na tamaa.
      Kwa maana hiyo,sitakuwa nakosea nikisema kuwa,upendo (mvuto wa asili) kwa sababu ni asili ya moyo,basi ukitazamwa kwa mtazamo wa vitu visivyo asili(vitokanavyo na fikra za kimazingira) basi huwa si upendo tena bali huwa ni tamaa na udanganyifu.Upendo hauwezi kulindwa kwa sheria,hakuna sheria itakayotungwa kuulinda upendo kati ya watu wawili,na sheria hiyo ikashinda isipokuwa tu,upendo wa dhati hutoka moyoni mwa kila mmoja,nao hudumu na kutukuka toka moyoni mwa wawili hao na ndio maana,tutaona hapo mbele ya kuwa sheria imeshindwa kulinda ndoa na badala yake baada ya sheria kuwa ndio mlinzi wa upendo,ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika(zipo sababu nyingine ndogo)
  Tumezaliwa tukiwa na upendo,lakini mitazamo yetu ya kifikra imefanya tuweke matabaka katika upendo,na hivyo hofu imetawala upendo,na kufanya hofu kuwa adui mkubwa wa upendo.
                                                Hofu,adui wa upendo(picha kwa hisani ya mtanzdao)
    Ni hofu ndiyo inayoleta chuki,hofu humfanya mtu kutojiamini na kuhisi wanaomzunguka ni maadui...Ni hofu ndiyo iliyosababisha viongozi wang'ang'anie madaraka,kufanya mauaji,kubagua..Ni hofu ndiyo  inayojenga uhasama.
                              
               NDOA
        Kila unapofikiri kuhusu mwenzi wako,umefikiri kuhusu wewe,unapomtendea mwenzi wako unajitendea wewe,unapomjali mwenzi wako umejipenda mwenyewe,unapomfanya mwenzi wako afurahi umejitendea wewe,upendo hutoka ndani ya moyo wako mwenyewe...pale unapovutiwa na mwingine...pasipo shinikizo litokalo nje ya moyo wako...ukamchagua na kuonesha nguvu hii ya asili kwake,ukishirikiana nae kukua na kuyafikia matarajio ya kila mmoja wenu,hii huitwa ndoa.Ndoa si kupata mwenza ambaye atakufanya uwe kamili(kwa kuwa kila mmoja amekamilika vile alivyo), ni urafiki na upendo uendao mbele ya maumbile.Ndoa ni muumngano wa wawili kila mmoja kwa ukamilifu wake,kwa ajili ya kufanya nuru ya Mungu ambayo ipo kwa kila mmoja,ing'ae kwa kila mmoja ili kuwafanya wawili hao na wale wanaowazunguka waujue utukufu wa Mungu
 Nimetazama ndani yangu na kuuona ukamilifu wangu,nami naungana nawe ili mimi nawe tushirikiane ukamilifu wetu(tafakari kwa kina)
            muhimu:wengi hufikiri kuwa hawajakamilika,wamekosa kitu fulani,na hivyo huingia kwenye ndoa wakitazamia kukipata kitu fulani toka kwa wenzi wao,baadae hugundua kuwa wanachokitafuta hakipo kwa wenzi wao,hapo ndipo matatizo huanza kutokea kwenye ndoa....baada ya changamoto nyingi ,wengine huomba Mungu awabadili wenzi wao,hawatambui kuwa ni fikra zao ndio adui wa ndoa yao(fikra huleta hofu)-(kama wangetambua wangemuomba Mungu abadili fikra zao.-hata ndoa kuvunjika,hutambua kuwa kumbe furaha,amani,upendo,kujali..kunaanza ndani mwao.
               Ndoa ni mungano ambao kila mmoja katika wenza huhakikisha anatumia kila alichonacho kuhakikisha kuwa mwenzi wake anakua na kutimiza yale aliyoyakusudia katka maisha yake.Ni mahali ambapo chemchem ya amani ilipo,ndoa si kifungo...ndoa ni chimbuko la uhuru ,ndoa si hofu,bali ni chemchem ya upendo,umoja na amani,ni mbegu iletayo matunda bora,ndoa ni ishara ya kukubali majukumu,ni chimbuko la kuifanya dunia kuwa sehemu bora
              Kinyume chake katika dunia ya sasa,ndo imekuwa ni sehemu ya watu kukimbia majukumu,ni sehemu ya watu kukwepa kufikiri,kuamua na kutenda...ndoa imekuwa ni sehemu ya mmoja kuweka matarajio dhidi ya mwenzi wake......tamaa ya kupata mali,kupata sifa ndio imekuwa msukumo wa watu kuingia kwenye ndoa...na kwa sababu ya hofu ya kukosa matamanio ama matarajio haya......mwanadamu akabuni sheria mabyo inamuhakikishia kuwa\ anatimiza matamanio yake......na kutengeneza sheria.....ya kwamba kila anayeingia katika ndoa basi huweka kiapo cha lazima(na kuifanya ndoa kuwa shuruti ya kisheria).Swali ni je,upendo (usio na shuruti) unaweza kulindwa kwa shuruti(sheria)?
               Kuingizwa kwa sheria(kiapo_katika ndoa ni dalili tosha ya kuwepo kwa hofu kati ya wawili waliopendana.Ni dalili ya kutoamini mioyo yao .Ni matokeo ya kutazama ndoa katikamisukumo ya hali na mali...gari,fedha,nyumba,ardhi,umaarufu...Matokeo yake ni kwamba mmoja kati yawenzi hawa huwa mtumwa na mwingine huwa mtwana...Hofu ndio msingi wa ndoa ya kisheria.....upendo hushinda yote..Mpendwa msomaji,jiulize ni kwa nini,watu wawili waliokutana wao wawili,wakathaminina na kupendana,huweka kiapo na kuandikishana kisheria.....je kiapo hiki huwasaidia kukua na kupendana pamoja? 
               Hivi majuzi nimesoma ripoti moja kuhusu ndoa duniani,ikionesha kuwa kuvunjika ndoa kumeongezeka sana toka katika karne ya kumi na tisa na sasa kasi ni kubwa sana..Sababu si ugumu wa maisha,sababu si utandawazi...sababu nimekwisha ieleza,ni fikra zetu na msukumo wa kuingia katka ndo kwa msukumo wa mali na hali,kwa matazamio ya kupata kuliko kutoa,sheria ikiwa ndio chimbuko lake
               KWA mtazamo wangu mimi upendo ,ni mvuto asilia...huvumilia,hujali,huthamini..na ndoa iliyojengwa katika upendo,hukua,tena pasipo kiapo kanisani ,msikitini,ama kwa mkuu wa wilaya,kila mmoja huishi kwa furaha ndani ya ndoa hii,kila mmoja huona fahari kuona mwenzi wake akikua nakutimiza ndoto zake....lakini ndoa itokanayo na msukumo wa kisheria...hujengwa katika tamaa,majivuno,hofu,kisasi...na kila mmoja hujitazama yeye anapata nini,mmoja huwa mtumwa na mwingine huwa mfalme.Hawa kinachowaunganisha ni sheria,(hofu) bali waliopendana kwa dhati upendo huwaunganisha.
 sisi twapendana kwa dhati.....kwetu thamani si magari,fedha,ufahari,umaarufu....sisi huvumilia,upendo hushinda yote
          Hivyo ,ni wazi kuwa ili uishi maisha ya furaha katika ndoa, unapaswa kufanya mabo yafuatayo
  1. Kubadili fikra zako,ya kuweka mategemeo ya kupata kitu fulani toka kwa mwenzi wako,kisha anza kutazama kwa mtazamo chanya,jitolee,timiza jukumu lako,daima kumbuka kuwa wewe una jukumu la kumfanya mwenzi wako akue na kutimiza malengo yake maishani,hivyo ni wakati wa kuacha kuomba tu Mungu ambadili mwenzi wako,bali muombe abadili fikra zako.
  2. Ondoa hofu,toa hofu juu ya mwenzi wako kuwa atakusaliti,atakuumiza,..anza kumtazama kwa wema,mfanye aamke na kutambua wajibu wake,hofu hupelekea kujaa wasiwasi na kufanya maamuzi yasiyo na manufaa.
  3. Zipo nyakati mbalimbali katika maisha,kuna wakati wa shida,raha......uvumilivu utokanao na upendo hurejesha matumaini..hivyo jipende wewe,kisha jifunze kumpenda mwenzi wako kama unavyojipenda wewe
  4. Tumezungukwa na jamii yenye maoni tofauti,sikiliza sauti ya moyo wako.....kama unaingia katika mahusiano kwa kusikiliza ushauri ama maoni tu ya wenginme pasipo kuchunguza na kusikia moyo wako,unatengeneza njia ya maangamizi yako mwenyewe,kama utambagua mytu kwa sura,umbo,rangi,kabila ama hali,basi umejibagua mwenyewe toka moyoni mwako
  5.  
       
      unapomsikiliza,kumthamini na kumjali mwenzi wako licha ya mapungufu ya kimaamuzi,hujenga ndoa imara na yenye furaha
     upendo hautazami nini mimi ninapata,bali mwenzangu anafanikiwa vipi kwa uwepo wangu



  Kuna rafiki  yangu alikataliwa kuoa kwa sababu ya kabila lake,akiambiwa kuwa 'mtoto wetu hawezi kuolewa na kakabila hako,labda ungekuwa umesoma sana maana sisi kabila letu ni wasomi,yupo ambaye aliwekewa pingamizi eti kwa sababu ya tofauti ya dini,....waliofanya hivi husukumwa na mali na hali.....upendo haujali dini,kabila wala hali........Kama hatujajitambua,basi migogoro katika ndoa haitakwisha kabisa....tafakari njema
 
     
   
      

Wednesday, July 25

HEKIMA.

Upo wakati ambao tunawalaumu wengine kwa matatizo yetu wenyewe ,lakini hakika,ukijitambua utajua ya kuwa wewe ni kiongozi wa maisha yako, utatambua kuwa wewe ni chemchem ya kila jambo,utaweza kuchanganua lipi la kushika,lipi la kuachia,utakwenda sambamba na mdundo wa maisha yako. utasimama na daima utakuwa na furaha maishani......

Wakati mwingi maishani,tunatengeneza maadui.tunawachukia wengine kwa kudhani kuwa wao ni sababu ya matatizo yetu,tunadhani ya kuwa wapo watu ambao ni wateule katika kutatua matatizo yetu wenyewe,na wakati mwingine tukiwaogopa na kuwafanya kuwa wakuu,ukweli ni kuwa  fikra zetu ndiye adui mkuu,utambuzi tu humfanya adui huyo mkuu kuwa rafiki mkuu katika kutatua matatizo yetu,kusonga mbele na kuyatawala mazingira yetu,na ndipo tutavitazama vitui katika uhalisia wake..

 Kila jambo lina kinyume chake,kuna upendo na chuki,kuna kishinda na kushindwa,kupanda na kuvuna.....utakapoanza kutazama kila jambo kwa mtazamo mpya,mtazamo chanya,utagundua kuwa kila jambo linapotokea huwa si mwisho,bali huwa ni mwanzo wa jambo lingine......kifo si mwisho wa maisha,ni mwanzo wa maisha mapya,kushindwa ni mwanzo wa ushindi.,dhihaka ni mwanzo wa heshima,chuki ni mwanzo wa upendo,udhalimu ni mwanzo wa ubinadamu......na hivi vyote hutoka ndani yetu wenyewe

 Tunafikiri k uwa nafsi zetu na Muumba wetu ni utengano...kwamba Muumba wetu yupo mbali nasi,kumbe yupo ndani mwetu,ni mawazo yetu tu ndio yanayotutenganisha na asili yetu..

  Shujaa si yule aliye na nguvu nyingi,wala hasira nyingi,wala simwenye umbo la kutisha,ama anayeweza  kuwapiga watu kwa hesabu yake....shujaa wa kweli ni yule ambaye huamini katika ushindi,huamini kuwa anaweza,na akawa tayari kupita magumu yote hata anapofika pale anapopachagua kufika,shujaa wa kweli hutazama kila jambo kama nafasi yakwenda mbele.
  
 Anayekata tamaa hana tofauti na yule ambaye anapoteleza ama kujikwaa na kuanguka hanyanyuki tena akiamini kuwa hawezi tena.
  Kila jambo huwa na mwanzo,anayeanza vibaya na kumaliza vibaya ni yule tu anayeamini kuwa kuna nguvu nje yake ya kubadili kile alichokichagua na kukiishi,naye mwanzo wake na mwisho wake,vyote husababishwa na nguvu hiyo iliyo nje yake,lakini ,yule anayejitambua....husimama na kuanza upya pale anapotambua kuwa nguvu zote za ushindi zipo ndani mwake.

Aibu,hasira,woga,chuki,ubinafsi na kulipiza kisasi(visasi) ni sifa za mtu asiyejitambua,asiyetambua kuwa anapotenda yote hayo kwa wengine anajitendea mwenyewe....anayefikiri kuwa ana akili na uwezo kuliko wengine hushusha uwezo wake wa kutenda na kujenga mambo mapya,anapofika ukomo wa fikra zake....husema kuwa haitawezekana tena na hakuna atakayeweza tena
  
  Anayelitambua jambo  pasipo kulitekeleza ni sawa na chumvi ama sukari isiyofaa...kama unajua kuwa wengine wananyonywa,ukanyamaza,kama unafahamu  hakuna linaloshindikana ,kisha ukaogopa kuchukua hatua,utajilaumu sana wakati wa kuiaga dunia hii,utajilaumu kwa kutokuwa chanzo cha mabadiliko,kuwa chanzo cha upendo,kuwa chanzo cha kuwaamsha wengine..lakini ukitenda lile unaloliamini,unapokuja muda wa wewe kuiaga dunia,utaiaga kwa furaha,nawe utakumbukwa kama ishara ya ushindi na nuru ya Mungu iliyo ndani mwako,,itang,aa daima,naamini,dunia itakulilia utakapoondoka
.

Monday, July 23

KWANGU MAFANIKIO NI.........

   UPENDO HUSHINDA YOTE

PICHA KWA HISANI YA MTANDAO

sihesabu  mafanikio katika maisha yangu kwa  kuhesabu idadi ya  namba za wale wanaonipigia simu,ama wale nliopata kuwa nao,nisiokuwa nao na nilio nao,sihesabu ni fedha kiasi gani nlichonacho,ama mimi ni wa daraja lipi,sihesabu nguo nlizonazo,ama ni vyuo gani na vingapi nimesoma....sihesabu ni marafiki wangapi ninao,ama kama nipo pekee,,,,,,,.nahesabu mimi ninawapenda wengine kiasi gani,na ni kiasi gani nawaumiza wengine,na mimi mwenyewe kwa chuki....nnahesabu,mimi ni nani na najitambua kiasi gani,,nahesabu heshima,usawa ,furaha,ubinadamu,amani..nahesabu ni namna gani nimeleta upendo palipo na chuki,,najifunza kutojisifu wala kutafuta sifa...nahesabu kutazama mbele na kuwa na imani na hakika ya ushindi,nahesabu ni maneno gani ninayasema na yana maana gani,yanawajenga vipi wengine.Kwangu maisha ya mafanikio ni kuwakubali wengine jinsi walivyo na si kwa kutazama mali wanazomiliki,Zaidi ya yote,kwangu maisha ni kuishi kwa kusikiliza moyo wangu,kwa dhati,na kuifanya nuru ya maisha yangu iwaguse wengine ,ili nao  wanapochagua  kuishi maisha yao kwa dhati-Pongu Joseph-0717903089

SIKILIZA SAUTI YA MOYO WAKO

Kabla ya kuanza kusoma makala hii,nakusihi uifanye huru fikra yako,fungua fikra zako,usifungwe na imani na mafundisho fulani ili usiathiri uelewa wa makala hii(your mind may become your great enemy,so empty it) ......Pili uwe huru kutafakari ndani ya moyo wako na kuuliza.

 Simaanishi unachoamini wewe ni uongo nami nnaandika ukweli.Jambo haliwi kweli eti  tu kwa sababu limeandikwa ama limesemwa..ama kwa sababu wengi wanaliamini,bali ukweli kuhusu jambo hutoka kwa mtu mwenyewe,kwa kuliishi jambo na kulifahamu.Mfano,hakuna anayeujua ukweli kuhusu wewe,isipokuwa wewe,hakuna anayeweza kujua ukweli kuhusu upendo,isipokuwa ameuishi upendo na kuifahamu chuki.

  Moyoni mwako,pana siri kubwa......ambayo ukiitambua,utakuwa umefungua njia ya ushindi katika kila jambo unalolitaka.


moyo wako ni chemchem ya uwezo wa ki Mungu
moyo wako ni chemchem ya uwezo wa ki Mungu ,ni hekalu la mawasiliano kati yako na asili yako(Muumba wako,Mungu,Mwenye uwezo wote)

   Moyo wako ndipo chimbuko kuu la mawasiliano kati yako na ASILI YAKO(MUNGU).Mungu hawasilIani nawe kwa kutumia vitabu,ama kwa kutumia maneno,bali huwasiliana nawe kupitia moyo wako.

Yeye huweza kutumia njia zingine endapo tu mhusika hasikilizi sauti ya moyo wake.Kwake matumizi ya lugha si ya lazima kwa sababu lugha huweza kuchanganya na wakati mwingine tafsiri huchangia kudhoofisha ujumbe uliokusudiwa.Hivyo  basi,kumbe Mungu huweza kutumia njia mbalimbali kufikisha ujumbe kwa watu,lakini njia iliyo kuu isiyoweza kupotea ama kuchanganya ni kupitia moyo wa mtu husika..

  Kwa wale wakristo,watakumbuka ya kuwa,miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu....
   Pia ikumbukwe kuwa Yesu alipata kuwaambia wanafunzi wake ya kuwa,hawaisikilizi sauti ya Mungu kwa sababu wameifanya migumu mioyo yako.
  Kuna wakati ambapo mtume Mohamed (S.A.W) alipata kuwaambia wafuasi wake ya kuwa yeye alikuwa akisikia sauti ya Mungu ikimtuma kutenda......wakashangaa,wakataka kujua ni kwa nini wao hawakusikia,sababu ni moja....waliifanya migumu mioyo yao.

  Hivyo ni  wakati sasa wa kutambua kuwa ule uzima tunaoutafuta kila siku,ile chemchem ya ushindi katika maisha,haipo mbali nawe,usiitafute juu kwenye nyota,usiitafute ndani ya sinagogi,usiitafute tu msikitini,na wale haijajitenga nawe,bali ipo ndani mwako.
SAUTI KUU IKUONGOZAYE KWENYE USHINDI IPO NDANI MWAKO
SAUTI KUU IKUONGOZAYE KWENYE USHINDI IPO NDANI MWAKO
 
    UTAITAMBUAJE?
    Mungu hukutuma kutenda kupitia moyo wako...pale unapopata hisia  na msukumo wa kutenda uletao faraja na furaha,usio na chemchem ya tamaa ya kupata sifa,wala fedha wala utajiri wa aina yeyote,bali kila unapoisikiliza sauti hii na kutenda kadiri inavyokutuma,hufungua milango ya ushindi(UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU ,KISHA YOTE MTAZIDISHIWA)

    Sauti hii hutuongoza kutenda kwa upendo,na sauti hii humjuza muhusika mwisho wa jambo alitendalo,naye aisikiaye hutambua matokeo yake,na hivyo kila aisikiaye sauti hii,haklati tamaa,hasikilizi maneno yanayomvunja ari,bali huyafanya yote kwa bidii.
  KUMBUKA..
  Kwa kuwa moyo wako huwasiliana na asili yako(mungu),basi,kila aliye tayari kuisikiliza sauti ya moyo wake,huwasiliana moja kwa moja na asili yake(mungu),wakati wowote ule pasipo vikwazo.Wapo wanoamini kwamba kuna wateule tu ambao huweza kuzungumza na Mungu,jibu ni laah,kila mtu ana uhuru na usawa mbele za Muumba,naye Muumba huwasiliana na kila mtu pale mtu huyo anaposikiliza moyo wake...
  Kwa udadisi huu,ni wazi kuwa moja ya sababu kwa nini wakati fulani unaomba.,haupati majibu,ama haufanikiwi ni kwa sababu,wewe huchagua jambo kwa kutazama tu faida,na wala si lile ambalo moyo wako unakusukuma kutenda(litokalo kwa Muumba) ama  unaomba usichokipenda toka moyoni mwako(kwa tamaa eitha ya kuona toka kwa wengine,eengi tunatafuta kufanya jambo tuwe kama watu fulani,tupate pesa ama mali,ama umaarufu,-vijana wengi siku hizi wanatafuta kazi ambayo wanasikia wanalipwa vizuri,wengi wanasomea kozi mbalimbali kwa msukumo wa malipo,si kwa msukumo toka moyoni-mfano udaktari kwa sababu wanalipwa fedha nyingi,ama uhasibu,ama kompyuta nk,lakini wale wanaosoma kwa msukumo wa moyo,wanaosukumwa na kujitolea na kutoa huduma kwa kujali utu na ubinadamu,hao hufunguliwa milango ya mafanikio......nao hutenda kwa bidii)
 Jifunze kutambua hisia za moyo wako.....jifunze kuingia ndani ya moyo wako na kujitazama kwa kina,tazama muungano kati yako na asili yako.....sikiliza moyo wako,sikiliza sauti ya moyo wako
                       
     

SHUKRANI

    SHUKRANI KWA KUJALI NA KUTHAMINI


Kila binadamu huhitaji kutambulika na kila mmoja wet u hufurahi kuona ya kuwa wengine wanamjali na kuthamini mchango wake.....kile anachokifanya,ama kukisema.......kwa kutambua hili,nachukua  nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote ambao wamekuwa wakitembelea blog hii.
  Shukrani yangu ya kwanza iende kwa Muumba wa vyote,ambaye ndiye aliye asili na chemchem ya elimu yote,kwa kuniweka salama na kunifanya mimi nijitambue ni nani,kisha kushiks kalam na karatasi na kuandika.......yale ambayo yanawaamsha wengi,na kuwafanya si tu wajitambue...bali wasimame na kuchukua hatua ya kuishi maisha wanayoyakusudia,wakijitolea kwa ajili ya wengine.
  Pili kwenu ninyi mnaoingia katika blog hii na kushiriki katika kusoma,na hata kuwaeklimisha wengine.Mnapoonesha kujali na kutaka tufike mbali zaidi na kuwaamsha wengi.Shukrani yangu kwangu ni kuendelea kujitolea zaidi,kuandika kwa sababu najua kila wakati yatupasa kutazama ni jninsi gani tutashinda.Si kwamba mimi ni mwalimu,bali ninyi mnaoingia na kushiriki kutoa maoni...mmekuwa walimu wangu...najifunza mengi kupitia wote wanaotuma maoni na wengine wengi.Rai yangu kwenu ni kwamba waalikeni wengine wengi tujifunze.....kama unao uwezo print pasipo kuathiri umiliki,wape wengine wasioweza kufikia huduma hii .....kuwa nuru kwa vitendo...amsha walio wahitaji..jitolee kwa dhati.
                                        

   chagua kuwa chemchem ya wengine kuamka

    Haikuwa  rahisi kuanza kufanya kazi hii ya uandishi....auonae mwisho husukumwa na upendo ,kutenda pasipo kukata tamaa,kuna furaha katika kutoa kuliko kupokea,na ndio maana tunaendelea mbele........Zipo blog nyingi sana,zinazofahamika sana na zenye kutembelewa na maelfu wa watu.......sisi tumeanza ....tutafika huko.Kwa ushirikiano wetu tutafika,lengo likiwa kuwafanya wengi wajitambue,na kuamsha upya matumaini ya wengi......tutafika,kwani katika mapambano(ushindani),wapo wenye kasi,wapo walio nanguvu...lakini anayeshinda ni yule anayeamini katiaka ushindi.....Tutashinda kuwafanya watu wajitambue,tutashinda kuamsha matumaini,tutashinda na kufundisha upendo....
    Natambua ya kuwa  mimi na wewe tunayo sababu ya kuwepo hapa duniani,nikitambua hilo,nitaishi kwa upendo,nitafundisha upendo na kuufundisha  kwawengine si kwa kuusema tu bali kwa kuuishi.Nitajiamini na kutenda kwa upendo..nikijitolea kwa ajili ya wengine pasipo kujali malipo ,ama dharau na kejeli.,kwa sababu hivi havitabadili ukweli ya kuwa mimi ni nani ....nitajitolea na kushiriki kuwaamsha waale wote walio wahitaji..nimejifunza kuwa mimi si chochote pasipo wengine,hivyo matendo yangu na majitoleo yangu yatatazama furaha ya wengine,nikiwapenda na kuwajali kama ninavyoitendea nafsi yangu....nina imani ya kuwa nitakua na kufikia mafanikio hata pale panapoonekana kuwa hapawezekani...kwa pamoja tutaweza
    Shukrani ziende kwa familia yangu,kwa wote waliokuwa tayari kujitolea ili blog hii ifanikishe lengo lake..Ahsante Mtaki R Muyenjwa Gamba kwa ushauri wa kiufundi  nilipohitaji,Lazaro Mafie,Faith Kassano,na wote walioshiriki kwa kila namna.

Wednesday, July 4

upendo ni lugha ya moyoni,ni lugha ambayo kila kabila,kila taifa na kila kiumbe huitambua,imepita maneno na maandishi,juu ya ubaguzi,juu ya dini juu ya siasa....na kila atoaye hupendo,hulipwa upendo