Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH
Showing posts with label MOTIVATION STORIES AND QUOTES. Show all posts
Showing posts with label MOTIVATION STORIES AND QUOTES. Show all posts

Monday, September 30

SIFA ZA BINADAMU ANAYEJITAMBUA

Katika makala hii tunajifunza juu ya binadamu anayejitambua.Makala hii inaweza kukukumbusha mambo mengi kwa kifupi na hivyo kukufanya uchunguze juu ya maisha yako na kuyatumia vyema kwa wakati huu ulipo hapa duniani.


Kutambua ndani yako hakuhitaji uende shule na kusoma sana,na hakutokani na maamuzi ya mtu mwingine bali ni maamuzi yatokayo ndani mwako
Ni mguso unaotaka ndani mwako, ufahamu unaokua toka ndani mwako. Ni uchimbuzi wa chemchem zitokazo ndani mwako, Ni kumtambua Mungu kupitia mguso ndani ya moyo wako, kisha kuanza kutumia kipawa ulichonacho kwa ajili ya utukufu  wa Mungu . Ni hisia za ndani zitakazofanya umfahamu Mungu na si kufikiria tu.Upya ndani ya binadamu hutokea wakati wote  kwa kuunganisha moyo wako na ulimwengu wa hisia na kuendelea kujifunza kila wakati na kukuza nafasi ya moyo wako kuwa mpya.
 na
Je ni kwa namna gani unamtambua binadamu anayejitambua?

Mtu anayejitambua hubadili mtazamo wake kutoka kwenye mtazamo wa jamii unaofuata mila na desturi/kawaida kuelekea kwenye fikra za kuijenga dunia mpya na yenye fursa mpya.Hujenga dunia ambayo wanaomzunguka ni wanadamu wanaotambua utu na nafasi ya kila nafsi.Akiwa na misingi ya ujamaa na usawa, hufanya majukumu yake kutoka kujitazama yeye binafsi na kuanza kuwatazama wengine.Uchaguzi wake na matendo yake husukumwa na  maono na mtazamo wa mbali kwa ajili ya binadamu wote na viumbe vyote.Hutazama sio kila kiumbe kwa ajili yake,bali kila kiumbe kwa ajili ya wote.

Anayejitambua habagui jinsia bali hutambua jinsia kuwa ni matokeo ya fikra za Mungu yaliyokusuduia kutoa fursa.Huheshimu, hutambua wengine na kuthamini nafsi zao na uchaguzi wao.Hutengeneza dunia dunia ambayo jinsia zote huwa na uhuru wa  kutumia vipawa vyao, kutambua sauti zo,nuru ndani mwao na kutumia kwa ajili ya viumbe wote. 

Mtu anayejitambua hasukumwi kutenda na maamuzi ama fikra za wengine. Anatazama ndani yake.Hajifananishi na nafsi zingine na hivyo hatumii nafasi yeyote kuwakandamiza wengine.Husimama kwa miguu yake mwenyewe. Anawasikiliza wengine isipokuwa hatoi nafasi kwa wengine kumuamulia maisha atakayoishi. Anayaona mambo yajayo na hivyo huanza kuijenga kesho yake katika wakati tunaouita sasa. Ni alama ya uwezo wa Mungu uliopo ndani ya binadamu. Na alama ya maisha yake huishi enzi na enzi.

Mtu anayejitambua huchukua hatua juu ya hisia zitokazo ndani mwake na hivyo kutambua matokeo ya matendo yake.Hutenda kwa msukumo wa moyo. Hutambua mambo ambayo hayamletei faida na kutoyafanya na pia hutambua yale yanayomletea faida ..akitambua kuwa anapotenda kwa wengine anajitendea mwenyewe. Husikiliza hisia za ndani mwake na kujifunza lugha ya moyo wake.

Huishi maisha yenye sababu. Husikia muito alioitiwa na kuuuishi. Haridhishwi tu na maisha ya tokanayo na matukio kama kuamka,kutembea,kulala,kula bali hutambua kuwa yupo hapa duniani kwa sababu maalum,hivyo huchimba ndani mwake kuijua sababu na kuiiishi. Kila wakati anasukumwa na sababu hiyo  ya yeye kuishi ,kuendelea kuishi kwa dhati akitengeneza na  kuifuata njia inayomfikisha huko.

Hakimbii majukumu yake . Hajitoi katika kutafuta suluhu ya changamoto na wala halaumu wengine. Hutambua makosa yake na kujifunza kupitia hayo. Husanifu maisha yake na kuyafanya mapya kila wakati.
Hujifunza toka ndani mwake na kutoka kwa wengine. Hutilia mkazo katika mafanikio ya ukuaji ndani mwake kuliko mafanikio ya nje., hutengeneza ndani mwake. Hutafiti na kuvumbua chemchem zinazojenga na kubomoa nafsi na kutumia chemchem hiyo kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi.Hivyo aliyejitambua ni picha tosha ya uwezo na uwepo wa Mungu ndani ya binadamu. Hutengeneza msawazo kati ya chemchem ndani mwake na matokeo yaonekanayo halisia.;
Binadamu anayejitambua hutazama kila jambo kama fursa


Anayejitambua hatafuti usahihi katika utendaji bali hutenda kwa kujitolea katika nguvu na uwezo wote.Hufanya kwa uwezo wake wote.
Anayejitambua hujikita katika kutenda kuliko kusema tu.Huweka bidii katika kazi . Huanzisha na kutenda mambo ambayo hufaidisha viumbe wote . Husema pale inapohitajika,huheshimu mawazo yake na huwa tayari kuchukua malipo ya maneno yake mwenyewe.Hakimbii kivuli chake. Hayupo tayari kuona wengine wakikosa uhuru  kupitia yeye. Anatambua kuwa wakati wote huvuna alichopanda..

Anayejitambua huweka mkazo katika uhusiano mwema na nafsi zingine. Huthamini mahusiano yenye thamani. Mahusiano kwake hutokea ndani, hujengwa ndani na hivyo hudumu. Upendo kwake ni lugha ya moyoni, huleta furaha, mshikamano na amani.Zitokeapo changamoto katika mahusiano,huwa tayari kuyatatua kwa ajili ya kuyakuza zaidi.

Anayejitambua hutambua kuwa hapa duniani hatupo katika kushindana,ushindani kwake haupo,hushirikiana na ushindi kwake ni furaha katika kutimiza wajibu wake. Huandaa silaha zake ndani na kuteketeza kila kisicho na manufaa kwa binadamu. Baada ya milima na mabonde katika maisha yake ushindi huzaliwa ndani mwake. Hutumia uwezo wake kwa ajili ya Wengine na si dhidi ya wengine..

Huishi katika hali ya kujitolea na bidii. Huwa ni zawadi ya aina yake hapa duniani. Haogopi kutenda. Huendeleza mambo yaliyojenga utu,ubinadamu na misingi bora ya kuishi yaliyojengwa na binadamu waliomtangulia. Maisha yake hufundisha wengine.  Hutambua juhudi za wengine na wote wanaompa msukumo wa kutenda zaidi hasa pale anapokutana na  changamoto. Hutambua kuwa hayuko peke yake,bali dunia imejengwa kwa muungano wa nafsi zinazotimiza majukumu kwa dhati.

Haogopi ukweli hata pale unapoumiza. Hutoa nafasi ya kusamehe kila wakati anapokosewa. Hujisamehe yeye pia anapofanya makosa. Hushiriki katika ujenzi wa maisha yake.
Hutambua kuwa kila jambo hutoa fursa,kila kiumbe ana fursa. Hakusanyi ama kujilimbikizia kwa ajili ya sifa. Hutazama wengine kama anavyofanya kwa nafsi yake. Inapostahili hujitolea alichonacho,hutoa kwa wale walioshiriki kwa yeye kupata. Hutengeneza maisha yake yawe ya kutoa fursa kwa wengine badala ya kuwanyang’anya wengine .

Anayejitambua haichukuliai dunia kama chanzo cha maumivu bali hugundua kuwa dunia humpa kila mmoja kadiri anavyohitaji.Dunia husikiliza kutoka kwenye uwezo  ulio ndani mwetu tuliopewa na Mungu.Hata mara moja hajichukulii kuwa ni bora kuliko binadamu wengine na wala si dfhaifu kuliko wengine. Hutambua kushabihiana na kutegemeana kati ya kiumbe kimoja na kingine.Hivyo anatambua kuwa kama ikiharibu mazingira ,ni sawia na kuharibu nafsi yake.
Binadamu anayejitambua huyajenga na kuyatunza mazingira yanayomzunguka


Anayejitambua hamlaumu Mungu hata mara moja. Uhusiana wake na Mungu ni wa heshima,urafiki na huwa na umoja naye . Mienendo yake yote humwelekea Mungu .Anawaheshimu wanaoamini sawia naye na wasio amini sawia naye. Hashiriki kutumia imani ama dini kama njia ya  utengano kati ya binadamu,ama binadamu na mazingira yake.

Ni mfano wa sifa njema ya binadamu. Huchukua majukumu yake. Ana faida kwa viumbe wote.Hulinda, hujenga, huheshimu, Huishi vyema duniani. Ni mfano wa aliyeletwa kuifanya nuru ya Mungu ing’ae. Ni halisi,haishi maisha bandia. Ni wa kutumainiwa, si mbinafsi. Wakati wake kuwepo duniani ukifikia tamati,huondoka kwa furaha ya kutimiza alichotumwa,na kuacha dunia ikimlilia.Ni wewe na mimi.

Sunday, September 8

JINSI YA KUPIGIA KURA BLOG YAKO KATIKA SHINDANO LA TANZANIA BLOG AWARDS

Napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu kwenu kwa kupendekeza blog hii kushiriki katika shindano la Tanzania blog awards. Blog hii imependekezwa katika vipengele viwili ambavyo ni

1. Best Inspirational Blog
2. Best Creative Writing Blog

 Nakuomba kwa nafasi yako uchukue muda kuipigia kura blogu yako katika vipengele tajwa hapo juu kabla ya tarehe 15/09/2013 kwa njia zifuatazo
(a)Bonyeza hapa  kisha chagua pongujoseph.blogspot.com
(b)-(i) Kwa kupigia kura Best Inspirational Blog bonyeza hapa
      (ii) Kwa kupigia kura Best Creative writing Blog Bonyeza hapa
Hakikisha unachagua pongujoseph.blogspot.com

Ahsante sana kwa ushirikiano

Kwa maoni,maswali ama ushauri usisite kuniandikia +255765046644, Whatsapp namba +255765046644

Saturday, January 5

HATUTAMUACHA HATA MMOJA 2013


Tumejifunza mambo mengi kwa mwaka 2012,ambayo yametufanya tutambue sisi ni akina nani na kwa nini tupo hapa duniani.Tumetambua kuwa sisi ndio wasanifu wa maisha yetu wenyewe.Tumejifunza kuwa kila jambo ni jema likitazamwa kwa mfumo chanya na kuwa mambo yote yatokeayo maishani mwetu ni matokeo ya fikra zetu na vitendo vyetu wenyewe...Tumejifunza kuwa upendo ndio silaha ya mafanikio ya kila jambo,upendo ni nuru.tumejifunza pia matokeo yake ambayo ni pamoja na furaha,amani,umoja,uvumilivu na ni mafanikio.Tukajifunza pia kuwa kinyume cha upendo ambayo ni chuki ndiyo matokeo ya maumivu,wivu,visasi,chuki,masengenyo na ndio matokeo ya kila jambo liletalo hasara katika maisha yetu
SISI NI WASANIFU WA MAISHA YETU WENYEWE
 

Leo hii tutajikumbusha kuhusu majukumu yetu …Mwaka mpya ulioanza tuuutazame kwa uchanya wake.Tuanze sasa kutimiza malengo yetu kila mmoja ya kuwepo hapa duniani.Kila mmoja wetu anayo majukumu yake.Kila mmoja ana wito unaomuita ndani mwake,ana sauti ya Mungu ndani yake inayomuita kutenda kwa ajili ya wengine na kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi

Hakuna hata mmoja wetu ambaye hatayapitia magumu,kwa sababu bila magumu kutokea hatuwezi kuendelea.Mwaka huu ni mwaka wa kusonga mbele ...tutasonga mbele,hatutamuacha hata mmoja nyuma
Ni mwaka ambao mwalimu anayeishi katika mazingira magumu yenye milima mingi,ataamka kila siku na kufundisha kwa bidii na kuwanyanyua wengine wengi.Anahitajika huyo ambaye hatalalamika na kusubiri serikali(kwani serikali ni kila mmoja wetu) bali atakuwa ni mfano wa kuigwa wa mbinu bora za kutatua matatizo.Mwalimu popote ulipo amka na kutenda kwa ajili ya wengine.Amka mwalimu.

Sauti ya upendo husikika kwa viumbe vyote.Huu ni mwaka wa kuwa nuru kwa wengine(picha toka helped by animals kwa msaada wa mtandao)


Ni mwaka ambao daktari ataamka mapema na kukumbuka jukumu lake ,ya kuwa hayupo tu kwa ajili ya kutazama idadi ya wagonjwa na kiasi cha fedha,bali yupo kwa ajili ya upendo,akijali utu wa wengine pasipo kubagua hali,kabila,rangi ama hali yeyote na daima atahesabu mafanikio yake kwa kuokoa wengine,kuwainua walio kata tamaa.....na hata akitokea mtoto akaulizwa upendo ni nini,basi amtazame daktari kwa ujasiri akisema......huu ndio upendo.

Ni mwaka ambao kila anayetoa huduma kwa wengine,atatoa akisukumwa na upendo.Kila atazamapo wengine,atambue kuwa anajitazama yeye,na kuwa thamani yake ni thamani ya wengine wote.Anapowatendea wengine akumbuke kuwa anaitendea nafsi yake.Ni mwaka ambao sisi tulio binadamu tutaonesha upendo uliotukuka,utakaofanya nuru ya Mungu iliyo ndani mwetu iwaangaze binadamu engine wasiotambua upendo,ili nao waishi maisha ya upendo.
Sisi ni wamoja,sisi wote ni wana wa Mungu,tofauti zetu zimejengwa na woga ,fikra zetu


Huu ni mwaka ambao tunapaswa kuifanya dunia kuwa sehemu bora,ili nasi tuwe malaika wa dunia hii.

Binafsi jiulize utamtendea nini yule Mungiu ambaye yupo ndani mwako?Je ukiwa katika nyakati za faragha na Muumba wako,utajivunia lipi ulilomtendea?Kumbuka kuwa kama huna malengo ya kutenda jambo lolote huwezi kutimiza lolote.Ni sawa na kusafiri safari isiyojulikana,mahali na hata uelekeo!Tukiweka malengo na kuamini katika kuyatekeleza,hakika yatatimia.

Mimi binafsi najisikia faraja sana kuhamasisha wengine na kuwasaidia wengine waweze kufikia mafanikio HASA PALE WANAPOKUWA NA MSUKUMO UTOKAO NDANI MWAO.Nimejitolea kwa ajiliya wengine na wakati wote najisikia faraja.Ninapokutana na magumu,ninayashinda kwa sababu naamini katika ushindi.Sisi  tumeumbwa kushinda.,na ushindi ni matokeo ya usanifu katika fikra za kila mmoja.

Ninapata faraja ninapoona kuwa yupo nesi ambaye licha ya kwamba anaumwa,anaamka na kwenda kazini kwa ajili ya wengine.Ninafarijika ninapoona kuwa yupo mtu ambaye licha ya kuwa na magumu mengi,anatenda ka ajili ya wengine pasipo kutegemea malipo.Nilikwenda kijijini nilipozaliwa,nikakutana na mama ambaye kipato chake ni kidogo,anaumwa kwa miaka mingi lakini anajitolea chakula na malazi kwa ajili ya wengine....anawafariji wengine,hata anapokuwa katika ugumu sana,hakati tamaa.Maisha yake ni nuru kwa wengi.Daima hamuachi jirani akiwa katika huzuni,nuru yake inaishi.Ni mwanga kwa waliokosa nuru.

Nafarijika kuona wengi ambao wanakwenda mbali na familia zao,mbali na wapendwa wao kwa ajili ya wengine. 
Nafarijika pia kuona wengi ambao wanajinyima kwa ajili ya wengine.Wengi wao wanaishi maisha ya kawaida,(kwa maana ya kipato) lakini wanatambua maana ya thamani yao kwa wengine,wapo tayari kujitolea pasipo kutambuliwa na wengine.Hii inanipa faraja ya kusonga mbele.Hwa wanatambua kuwa sisi binadamu wote ni wamoja ,tofauti zetu ni juu ya fikra zetu wenyewe.

Daima umoja ni nguvu.Usisubiri wengine wachukue hatua.Anza wewe.Mimi nimepata nafasi hii kwa kuandika.Wewe pekeyako pia watosha,unaweza kubadili wengine kwa kusamehe,kuimba,kufundisha,kutoa nakala nyingi za mafunzo kwa wengine,kwa kuwahurumia wengine,kutembelea wagonjwa,yatima,wafungwa na matendo yote yenye kuleta thamani kwa wanaotuzungua.Mwaka 2013 hatutamuacha mtu hata mmoja katika umasikini,chuki,uvivu,visasi,magonjwa huzuni...nk.Mwaka huu hatutamuacha yeyote kwenye giza.Tunao uwezo wa kuyatenda haya yote.Chukua hatua,mabadiliko yanaanza ndani yako.
Wathamini wengine,hata usiowafahamu....

Tujenge mwili mmoja,moyo mmoja na kupambana mpaka mwisho kwa ajili ya dunia iliyo bora na mafanikio kwa ajili yetu na wengine.

kila mmoja wetu anapochukua hatua licha ya vikwazo,tutayafika mafanikio(picha kwa msaada wa mtandao)




Tuishi maisha yetu kwa dhati bila uoga,tuchimbe ndani ya mioyo yetu ambapochemchem ya kila ushindi ipo,Tujifunze thamani yetu ,tuwathamini wengine kwa kuwa wao ni wa thamani kama tulivyo,tusamehe na kutazama mbele,tujali mawazo ya wenginena imani zao tuziheshimu.


Kila mmoja apende nafsi yake,ayapende maisha yake,asanifu vyema vyote vinavyomzunguka,KILA MMOJA AYAFANYE MAISHA YAKE YA THAMANI KWA WENGINE.Tutimize malengo yetu,yanayotokana na sauti iliyopo ndani mwetu,ili ule muda wa kuishi katika dunia hii unapokwisha ,na kifo kukuita,uitike kwa furaha,kwamba uliyaishi vyema,usipate hata sababu ya kuomba upewe tena muda,bali nuru ya maisha yako iwe mfano wa kuigwa milele.Uiage dunia na kuondoka kishujaa,kuelekea katika maisha mengine mapya yenye majukumu mapya.


Tutapita katika magumu mengi lakini daima tutasonga mbele,hatutamuacha yeyote nyuma,tutainuana sisi kwa sisi,hatutatazama nyuma,wala kuogopa kusonga kwa woga wetu,hatutaogopa lolote kwani sisi ni wa thamani,tutakumbuka daima kuwa dunia si sehemu ya ushindani bali ni sehemu ya ushirikiano na umoja na hivyo daima tutafikia tuendako,kwa sababu Mungu yu ndani mwetu.
Ahsanteni sana

Tuesday, July 31

DUNIA INAKUHITAJI

 dunia inakuhitaji uwatazame wenzako kwa huruma,ukijali mahitaji yao,ukiwainua na kuwafanya wajitambue na kujikwamua(picha kwa hisani ya www.viewtz.com)
DUNIA HAIITAJI WATU WENYE FEDHA NYINGI,MAGARI,NYUMBA,NGUO NYINGI AMA WENYE UMAARUFU MKUBWA..DUNIA INAHITAJI WATU WENYE KUJITOLEA KWA WENGINE,WENYE UTAJIRI WA UPENDO,WENYE KUUGUZA,KUPONYA,KUAMSHA MATUMAINI YA WALIOKATA TAMAA,WENYE KUSAMEHE NA KUTAZAMA UPYA KWA UPENDO,WENYE KUPIGANIA UHURU ,WENYE KUJALI NA KUTETEA WENGINE.,WENYE KUTENDA YALE YANAYOONEKANA HAYAWEZEKANI,..DUNIA INAKUHITAJI WEWE KWA YOTE HAYA.CHUKUA HATUA
 tunapaswa kuwapenda wengine ,kuthamini changamoto zao na kuthamini mawazo yao ,kuwa tayari kujitolea pasipo kujali rangi,kabila,dini,taifa.picha kwa hisani ya helped by animals
 

SONGA MBELE.







 KAMA HUWEZI KUPAA,USILALAMIKE,...KIMBIA,  KAMA HUWEZI KUKIMBIE USIKATE TAMAA,TEMBEA......KAMA HUWEZI KUTEMBEA USIBAKI TU UNALALAMA, TAMBAA,ILI MRADI TU KILA SIKU UNASONGA MBELE

Thursday, July 26

KUMBUKA YAFUATAYO UNAPOPATA HOFU NA KUVUNJIKA MOYO

 Upo wakati ambapo tumnapita katika magumu ,huwa tunafika wakati tunashindwa kujitambua,na wakati mwingine tunapatwa na msongo mkubwa wa mawazo hata tunakata tamaa.Kila wakati jitazame ndani mwako,usome uwezo wako ulio ndani mwako...utaondoa hofu,woga na kukata tamaa.Jikumbushe ya kuwa wewe u bora vile ulivyoumbwa.....wewe ni bora kwa sababu zifuatazo

   Wewe  ni wa pekee,unaipenda nafsi yako,hivyo unampenda Muumba wako na watu wote   pasipo kujali sura,rangi,kabila,dini , na hivyo upo katika uhuru na usalama pote ulipo

  • Unatambua kuwa furaha,amani havitoki nje yako na kwamba furaha ya kweli huanza ndani yako
  • Wakati wote katika maisha yako unaishi ukithamini wengine na kuhakikisha kuwa wewe ni sababu ya wengine kuamka na kufanikiwa,hivyo unapata marafiki na ndugu kwa maisha yako halisi,hivyo wote anaoutambua mchango wako,wanathamini maisha yako.
  • yote yaliyopita kwako,hayakufanyi uwe mnyonge bali yote hayo yalikuwa ni mwanzo wa wewe kuyaendea mafanikio,na hivyo daima utatazama sasa(wakati uliopo) na kuyaandaa maisha yako yajayo kwa kujali pia maisha ya wengine.
  • unatambua kuwa kuanguka(kushindwa) si mwisho wa maisha ,bali ni mwanzo wa kuuelekea ushindi na kadiri unavyoshindwa mara nyingi,ndivyo unavyokuwa mpya kupambana na huhesabu ni mara ngapi umeanguka,bali ni mara ngapi na namna gani umesimama na kushinda.
  • unatambua ya kuwa katika maisha hakuna jambo lililo baya kama kukata tamaa,hivyo magumu hayatakupoteza katika lengo uliloliweka,bali yatakupa mbinu mpya za kufika uendapo.
  • kwa kuwa kila jambo unalolitenda linasukumwa na upendo,na daima unafurahi kuona wengine wakifurahi,unajitolea,unatazama wengine kwa huruma,unawakumbuka wenye mahitaji,hivyo yote yaliyo mema unaowatendea wengine yatakuja kwako pasipo wewe kutegemea.
  • kwa sababu  unayo imani,unayo matumaini na upendo na daima unaepuka hasira,masengenyo,woga,choyo na visasi.
  • unatambua kuwa kutochukua hatua kwa kuogopa kufa ama kuumia ni usaliti wa nafsi yako mwenyewe.
  • moyo wako unawapenda wale ambao jamii imewasahau,unawatia moyo wale walioshuka moyo na wenye katika hali ya kukata tamaa,wwe ni rafiki wa waliotengwa,na  tumaini jipya kwa wasio na tumaini.
  • Daima upo tayari kusamehe,unatazama mbele kwa tumaini la maisha mapya,unaitika sauti ikuitayo kwa ajili ya yatima,wafungwa,wagonjwa,wajane na daima unasimama upya kuyafikia matazamio yako.
    • unapokuwa msaada kwa wanyonge,watima,wajane,wafungwa,matatizo yako yote hupata suluhisho(picha kwa msaada wa mtandao)
    • kwa kuwa unakiri na kutambua na kutumia nguvu na uwezo,akili na  uwezo usioonekana uliopewa na Muumba(Mungu)  kwa utukufu wa Muumba wako,na yote utayafanya kwa ajili ya binadamu wote,hivyo utaepuka kudhuru,kuumiza wengine.
    • kwa sababu unatambua tu kuwa,ili kuwa mkuu mbele ya wengine...ni lazima uwe mtumwa kwanza

Monday, July 9

NITAYASHINDA YOTE

nitapanda milima na mabonde,nikiyaishi vyema maisha niliyoyachagua,nitashinda
Nitapanda milima na mabonde,nikiyaishi vyema ambayo ni uchaguzi wa moyo wangu,nitashinda .
Sauti zote zinazonikatisha tamaa zitashindwa .
 Nitayashinda yote na kuvunja imani zote na kauli zote zinazoaminisha kushindwa,na kunifananisha mimi na wengine ambao wanaamini katika kushindwa, ama kushinda kwa kutazama mifano ya wachache na wengi walioshindwa.....Nitashinda kwa sababu katika kupambana kwangu....nautambua mwisho,ya kuwa  nitashinda licha ya changamoto zote,

Nitashinda....ninaongozwa na visheni ionayo mbali,isiyotazama tu hatua chache,bali itokanayo na uhuru usio na mipaka wa tafakari,na uhuru usio na mipaka wa kuchagua,,,,,Sitakuwa na chochote cha kupoteza hata nikipoteza maisha,kwani kuishi maisha yasiyo na mtazamo wala matokeo ya kuifanya dunia kuwa sehemu bora,kwangu ni hasara kubwa......sitajutia uamuzi wangu,kwani kwangu majuto ni kutofanya jambo kwa kuamini kuwa haliwezekani, Na kisha mwingine akalifanya... 

Sitasikiliza sauti zote ambazo zitanikatisha tamaa,zitokao kwa wale wanayoyatazama maisha katika mtazamo hasi,na wote watakao nifanya niishi maisha ya bandia,bali daima nitaisikiliza sauti iliyo moyoni mwangu,ile iliyo kubwa kuliko ile ya mawazo mengi,ile iletayo furaha..kwani natambua kuwa kila mmoja ana jukumu la kusikiliza muito wa moyo wake, .umuitaye kuifanya kazi ambayo hujengwa katika upendo na kuijtolea,ili Nuru ya MUNGU iliyo ndani mwetu ionekane...
natazama mbele daima nikiyafurahia maisha
Nitatumia nguvu zangu, akili zangu na uwezo wangu wote kuisikiliza sauti ya Mungu kutenda kadiri sauti huru ya Mungu initumapo,nikitekeleza kwa upendo,ili alama ya maisha yangu,iandikwe hapa duniani,na siku nitakapo yaanza maisha yangu baada ya maisha katika dunia hii,alama hii iwe ni nuru kwa wengine na kuwa ishara ya umoja,kujitolea,na ushindi dhidi ya wasioamini...

Nitafundisha upendo kwa kuuishi,nikitimiza malengo yangu na ndipo nitakapouvuta upendo wa wengine.
Nitafanya bila kumdhuru yeyote,nikisamehe na kuyakubali maisha na changamoto zake....na ndipo wengine watakapotambua sababu ya wao kuwepo duniani,waamke,wajitambue,watumie vipawa vyao ,wakiifanya dunia kuwa sehemu bora ... kwani kila mmoja anazo nguvu zisizoonekana..lakini zikiwe ni zaidi ya vile kila mmoja ajiwaziaye na kufikiri.....

Licha ya kuwa niendako ni mbali,nitashinda yote
 DUNIA INILILIE PALE NTAKAPOONDOKA NA KUYAENDEA MAISHA MAPYA,SIO TU KWA SABABU YA NILIKUWEPO,BALI KWA SABABU NILIYAISHE VYEMA MAISHA,PASIPO KUOGOPA MACHO YA WENGINE,BALI KWA KUTAMBUA KILE NIKIAMINICHO,AMBACHO HAKUNA AWEZAYE KUKIONA,ISIPOKUWA MWENYE MACHO YAONAYO MBALI,YALE YAUONAO MWISHO KABLA YA KUANZA KWA MWANZO EWE MUUMBA WA VYOTE NISAIDIE...AMINA.

Saturday, July 7

UTANG'AA,UTAPAA LICHA YA VIKWAZO

NITAPAA,NITANG'AA KUFIKA KULE AMBAKO WENGI WANASEMA SITAFIKA
NITAPAA,NITANG'AA KUFIKA KULE AMBAKO WENGI WANASEMA SITAFIKA WEWE NI WA KIPEKEE,HUNA TOFAUTI NA WALIO NA MALI NYINGI,HUNA TOFAUTI NA WENYE ELIMU YA JUU YA DIGRII....

UTANGAAA,UTAPAA -Kuwa tayari kutambua ya kuwa wewe una uwezo mkubwa ndani yako....utapaa,kuwa tayari kutambua kuwa vipo vikwazo,milima na mabonde...lakini siri ni moja.....weka visheni yako juu ya jambo unalotaka kutimiza.....UTANG'AA,UTAPAA...

SIKILIZA HISIA ZA MOYO WAKO....SIKILIZA MOYO WAKO...TIMIZA MOYO WAKO UNAPOKUTUMA..UTANG'AA,UTAPAA...

KUWA NA VISHENI MWANANGU......HUTAKATA TAMAA KAMWE KWANI UNAJUA MWISHO WA PALE UNAPOTAKA KUFIKA,HIVYO VIKWAZO ,MILIMA NA MABONDE,HAVITAKUDONDOSHA KAMWE KWANI WAIJUA NJIA,WAUONA MWISHO...

.UTANG'AA,UTAPAA....UMEPEWA UHURU USIO NA KIKOMO WA KUCHAGUA...UMEPEWA UHURU WA KUTUMIA FIKRA ZAKO PASIPO UKOMO...UTANG'AA,UTAPAA...UTAPAMBANA NA WENYE NGUVU,WENYE KASI YA KUTISHA ,LAKINI WEWE UTASHINDA NA SABABU NI MOJA,,,WEWE UNAAMINI KATIKA USHINDI...WEWE WATAZAMA MBALI,HATA ZAIDI YA MAWINGU...MBELE YA BAHARI,NDANI ZAIDI YA MIAMBA..

UTASHINDAWEWE UNA NURU...NURU NDANI YAKO...NURU IKUONGOZAE HATA KATIKA MWISHO WA UPEO WAKO......UTAPAA...WAO WANAVUTA OKSIJENI ...NAWE PIA...KWA NINI WEWE USISHINDE?HAUMTEGEMEI MGANGA,WALA MIUJIZA YA KUFIKIRIKA...BALI WAUTAMBUA UWEZO WAKO WA KIPEKEE ALIYEKUPA MUUMBA..... UTADONDOKA MARA NYINGI,UTAUMIA,UTACHOKA SANA LAKINI WAITAMBUA FARAJA YAKO...PALE UFIKIAPO MWISHO...HIVYO KWAKO HIVI NI VIGEZO MUHIMU KWENDA MBELE, KWENDA JUU ZAIDI.

NJIANI KATIKA MAGUMU UTAGUNDUA MBINU  MBINU MPYA NA DAIMA HUTAPOTEZA MWELEKEO-UTANG'AA,UTAPAA...

TAZAMA WATAKUCHEKA...WATASEMA HUNA LOLOTE,WENGI WALISHASHINDWA...LAKINI WAONA MBALI,NAWE WAUJUA MWISHO,NAO MOYO WAKO UMEJAA NGUVU,ISIYO KIFANI....WATAFIKIRI YA KUWA HUTATOKA ULIPO...LAKINI TAZAMA WANAPOKUJA WATAKUKUTA UKIWA JUU....JUUU...NAO WATAPEWA TAARIFA YA KUWA...HAYUPO...KATANGULIA .... MTAMKUTA....KAMA ALIVYOSEMA
simama mwanangu......usikumbuke maumivu...kumbuka faraja iliyobaki......allow your wing to fly to greater


ruhusu mabawa ya uwezo Uliopewa ,kuruka juu na kuyafikia mafanikio makubwa,,...
UMESHAJITAMBUA NAWE WAUONA MWISHO..........ruka kwa nguvu zote,usisikilize maneno ya wengine ya kukukatisha tamaa,fanya yote ukisukumwa na upendo...hutakatishwa tamaa na milima wala mabonde.....changamoto hazitakufanya utepoze mwelekeo...kuwa imara kwani M UNGU YU NDANI MWAKO.... simama mwanangu......usikumbuke maumivu...kumbuka faraja iliyobaki......allow your wing to fly to greater height
NITAPAA KUYAFIKIA MAFANIKIO LICHA YA KUWA WENGINE HAWAAMINI
NITAPAA KUYAFIKIA MAFANIKIO LICHA YA KUWA WENGINE HAWAAMINI MWANANGU,CHUKUA KILA KIKWAZO KATIKA MINAJILI CHANYA,IWE NDIO SABABU YA WEWE KUFIKIA MAFANIKIO,WAKATI WAO WANASEMA HAIFAI,HAITAWEZEKANA,HAITATOKEA KAMWE...WEWE UTAWEZA KWA SABABU TU UMEAMINI NA KUCHUKUA HATUA...KUTUMIA NGUVU ZOTE NA UWEZO WAKO WOTE..TAZAMA UTAFIKA-TAFAKARI

Tuesday, July 3

may motivate yu

The CREDIT belongs to the man who is actually in the ARENA, whose face is marred by DUST and sweat and blood, who STRIVES valiantly, who errs and comes up short again and again, because there is NO EFFORT WITHOUT ERROR or shortcoming, but who knows the great enthusiasms, the great devotions, who spends himself for a worthy cause; who, at the best, knows, in the end, the triumph of high achievement, and who, at the worst, if he fails, at least he fails while daring greatly, so that his place shall never be with those cold and timid souls who knew neither victory nor defeat."-- Theodore Roosevelt (26th President of the United States of America|September 14, 1901-March 3, 1909) in his speech titled "Citizenship in a Republic," at the Sorbonne, Paris-France on April 23, 1910 Any fool can criticize, it is one of the EASIEST thing to do. There is a difference between a FEEDBACK and mindless CRITICISM. Of more use is a CONSTRUCTIVE criticism.