Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Tuesday, July 3

TAMBUA HILI

TAMBUA HILI.Hakuna mwenye jukumu la kukufanya uwe na furaha,amani,...hakuna ataKaye kuletea wewe maendeleo..hakuna nguvu nje yako.....hakuna uchawi wala kiini macho....Wewe ni kila kitu..wewe nijibu la kila ukitakacho katika maisha yako ,MAISHA YAMEJAA vipindi vingi,vya furaha,vya amani na changamoto mbalimbali......mtazamo wako daima huleta maatokeo ya maisha yako....... ukitegemea rafiki akuletee furaha............. ukitegemea rafiki ndugu yako akuletee maendeleo........ ukitegemea serikali ikuletee kila unalolitaka....... daima utavunjika moyo........utavunjika moyo kwa sababu utapata tofauti na mategemeo yako......utapata kuumia na kuvunjika moyo......... tambua ya kuwa wewe binafsi umeubwa ukiwa kamili....ukapewa uwezo wa kuifanya dunia kuwa sehemu bora....hivyo furaha,amani,maendeleo,chuki,ghasia umasikini huanza na wewe....fikra zako ndizo daima zitakazo kubomoa ama kukujenga.....ukihisi huwezi hutaweza...ukifikiri kuwa wewe utakuwa masikini vivyo hivyo ndivyo matokeo yake tambua ya kuwa kila unachofikiri hubadilishwa kuwa halisi.......uombapo na kunena....hutokea tambua pia pale unapoweka imani ......hutokea kadiri imani yako inavyokutuma daima tazama moyoni mwako...jiulize ni nani aliye rafiki yako bora...nani mwenye jukumu la furaha yako..je ni mwenzi wako,ni mzazi wako...ni rafiki yako?jibu ni hapana....kila unachokihitaji kinaanza na wewe.......jifunze kuyakubali maisha,uyaishi....kubali changamoto na kuzifanya kuwa ni ngazi yako ya mafanikio.....nawe tazama utaanza kusimama mwenyewe,kuwa mwenye furaha na daima hutavunjika moyo......daima jifunze kusababisha furaha,upendo na amani kwa wengine....kwani maisha huwa ya furaha pale unapotoa kuliko pale unapopokea
kumbuka,hakuna uchawi kuyafgikia mafanikio,ni kuamua sasa kuchukua hatua na kuishi maisha yako.....ukijitoleas kufanya kila jambo kwa ajili ya wengine mpaka pumzi yako ya mwisho

ISHI MAISHA YAKO HALISI

Kwa nini unasikitika kuwa vile ulivyo,kwa nini unatamani kuwa na mwonekano kama WA MTU FULANI...kwa nini unatamani kuiga fulani ili uwe maarufu ama ufanane nae?hii ni dalili ya kutotambua wewe ni nani..... wewe ni wa pekee,hakuna aliye kama wewe,hakuna mwenye kipawa kama ulichonacho,hakuna mwenye mfano wako....wewe ni wa kipekee toka kuumbwa kwako.....ni zaidi ya sura unayoitazama na kulaani ni kwa nini upo vile ulivyo.....tambua kuwa ndani mwako wewe ni zaidi ya hivyo ulivyo...ndani yako kuna uwezo mkubwa sana wa kutimiza kila jambo unalolihitaji...... vivyo hivyo ndivyo mungu kakuumba ukiwa wa kipekee...kakupa uwezo wa kila jambo ulitakalo...kakupa na uhuru wa kuchagua jtambue sasa na uyaishi misha uliyokusudia....amua leo ya kuwa utajikubali ulivyo na kusimama wewe ,kuishi maisha yako yaliyo halisi,kwa upendo huku ukitimia yote kwa nguvu zako zote,moyo wako wote ....hakikisha unasimama katika dira uliyojiwekea..pambana hata mwisho..na hakika utapata furaha ya kweli..katika maisha hakuna vita kubwa utakayokutana nayo kama ile utakayopigana kuwa wewe na kuishi maisha yako,kwani kila wanaokuzunguka wanataka uchague maisha wanayoyataka wao....tambua ya kuwa wao wanao pia uhuru wa kuchagua....wana uhuru wa kuishi maisha yao........ kuwa wewe,kuwa halisi,kuwa mdadisi na mvumbuzi ,kuwa wa pekee ilio pale utakapo maliza safari yako hapa duniani,dunia ikulilie nao wakaao ndani yake wakulilie,si kwa sababu ya kufa kwako,bali kwa alama yako iliyotukuka,iliyojaa upendo na thamani kwa bina damu wote....iliyojaa somo ya kuwa...hakuna kisichowezekan kwa binadamu na kwamba mafanikio huja tu pale mtu anapoamua kutembea ktk njia yake ambayo wengine walisema haiwezekani KUWA HALISI..ISHI MAISHA YAKO HALISI

WITO/NDOTO

Wito hutokana na sauti itokayo ndani kwa mtu..wito si shinikizo.Ni sauti ya pekee imuitaye mtu kutekeleza jambo fulani. kila mmoja wetu huitwa kutekeleza jukumu lake hapa duniani...na kila mmoja anaitwa kwa wakati wake...ni vema kila mmoja akatambua.lakini je,tunatambua kama tumeitwa,je tunaisikiaje sauti hii? kuna jambo ambalo moyo wako hukutuma mara nyingi kulifanya.....wakati mwingine unakuwa hulitilii maanani lakini hurudi na kukukumbusha....tofautisha na tamaa ya mwili ambayo mara nyingi huchagua vitu rahisi na vinavyotuletea umaarufu,wito hutuma kulifanya jambo hilo wakatio wote...na moyo husikia faraja kulitenda jambo hilo...japo wakati mwingine fikra hutuma mtu kutochukulia maanani,kwani wito ni kujitolea zaidi....wito ni kujitoa na kujitolea kuliko kupewa/kupokea. kama nlivyoeleza hapo awali,wito ni msukumo wa moyo,ni sauti ya Mungu inayotutuma kutenda kwa upendo,unyenyekevu na kujitolea vkuhakikisha nuru yako (Mungu aliye ndani mwako)inaonekana kwa wengine kwa vitendo...wito si nukuu tu ya maneno....wito ni kuishi maisha halisi,na kushirikisha kipawa/vipawa ulivyonavyo kwa wengine na kuhakikisha kuwa kila binadamu anafaidika na matunda ya kipawa chako......kama ni kuimba..imba kwa moyo wako wote na kuwafunza wengine.......kama ni kucheza,cheza kwa moyo wako wote......kama ni kufundisha...fundisha kwa moyo wako wote....kama ni kuandika...andika kwa moyo wako wote...kama ni kutibu.....tibu kwa moyo wako wote.......kama ni kulea lea kwa moyo wako wote. Unahitaji kujiuliza,wewe ni nani na je Kw A nini upo hapa duniani?...kisha tambua ya kuwa MUNGU ambaye wakatiwote tunamtafuta...yupo ndani mwako......kisha mpe ruhusa ya kuwa mueklekezi wako kwa kufungua moyo wako....na kusikiliza sauti yake....epuka kujichagulia jambo kwa sababu litskupstis tu fedha ama ukwasi....usichagua kuwa daktari ili upate ukwasi,usichaguia kuwa muhubiri ili upate ukwasi...usichagua kuwa injinia,mwanamuziki,muigizaji ili tu upate fedha....bali sikiliza sauti ya moyo wako ambayo daima hukutuma kuyatenda yote kwa upendo,unyenyekevu na huku ukijitoa kila ulichonacho kutimiza ndoto....naye Mungu aliye ndani mwako atakupa vyote..... furaha yangu si katika kupata umaarufu,ama utajiri...bali ni kuona kila mmoja anajitambua na kuifanya dunia kuwa sehemu bora