Mwalimu wa kweli wa kiroho hana maneno ya
kukufundisha jambo jipya usilolifahamu, habari mpya taarifa mpya,sheria mpya
ama imani mpya.
Kazi pekee ya mwalimu wa kiroho ni kukusaidia na
kukuongoza kuondoa giza linalokutenganisha wewe kutoka kwenye ukweli wa kwa
nini Mungu alikuumba na undani wa sababu ya kwa nini upo hapa duniani.
Kazi
yake ni kukufunulia ujue ukweli unaokuunganisha kwa kina wewe na Muumba wako.
Tumemaliza mfululizo wa siku 40 katika kuweka tafakari
ya kina juu ya sababu ya sisi kuwepo hapa duniani kwa njia ya mfungo wa siku 40.
Kwa nini upo duniani? Nimevutiwa kutumia ujuzi
nilioupata kushirikiana nawe kwa mfululizo wa siku 40 kutafakari upya kwa
pamoja. Ni katika mfululizo wa makala kujikumbusha kwa nini tupo hapa katika dunia
hii.
Bila shaka mfululizo huu utakuwa ni njia ya kukufumbua
kuhusu swali hili ambalo wengi hujiuliza
‘’Kwa
nini nipo duniani? Nina jukumu gani katika dunia hii’’?
Ni imani yangu kwamba mwisho wa mfululizo hu utakuwa
na picha kubwa ya namna ulivyokuwa ukijitazama,na upya baada ya mfululizo huu.
SIKU
40 ZIJAZO
Takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa umri wa mwanadamu
kuishi unafikia wastani wa miaka 70.Unaonaje kama utafanya maamuzi ya kutumia
siku 40 tu kutafakari ni kwa nini Mungu alituleta hapa duniani?
Kwa wale wakristu mtakumbuka jinsi biblia
inavyoeleza umuhimu wa siku 40. Mungu alipotaka kumwandaa mtu kwa makusudi
Fulani,alitumia siku 40.
· Maisha
ya Nuhu yalibadilishwa kwa siku 40 zaa kunyesha mvua
· Musa
alibadilishwa kwa siku 40 katika mlima wa Sinai
· Daudi
akipambana na Goliath katika siku 40 alishinda na kubadilishwa katika imani.
· Eliya
alibadilishwa pale Mungu alipompa nguvu ya kuishi kwa siku 40 kwa mlo mmoja tu
· Mji
wote wa Ninawi ulibadilika baada ya Mungu kuwapa siku 40 za mabadiliko
· Yesu
aliinuliwa baada ya kufunga na kuomba kwa siku 40 nyikani
· Mitume
wa Yesu walibadilishwa kwa siku 40 baada ya ufufuko.
Bila
shaka siku 40 zijazo zitabadili maisha yako
Tutakuwa na mada zilizogawanywa kwa siku 40. Ruhusu
mabadiliko katika maisha yako kwa kubadili mtazamo wako katika tafakari ya siku
40. Ni muhimu kushiriki kwa kina katika kusoma makala hizi kwa siku 40 zijazo,
ukitafakari na kujadiliana kwa kina.Usikimbilie kusoma tu,tafakari, hata katika
mafunzo ya mwalimu mbovu, lipo la kujifunza.
Muombe Mungu akujalie tafakari ya kina, kudadisi na
kupata faida inayokusudiwa katika mfululizo huu. Washirikishe na
wengine,na shirikiana nao katika kujadili mada kwa kila siku .Ushirikiano wa
wawili ni bora kuliko mmoja.Mmoja atashika hili na mwingine lile,kushirikiana
kunajenga zaidi.
Nakutakia ushiriki mwema