fikra ni mbegu ya kile unachotarajinayo hutoa sawia na kilichopandwa |
Nimeamua kuandika makala hii kujadili jambo muhimu sana,na
endapo utachukua nafasi kujifunza na kusoma mara kwa mara utatambua mambo mengi
Mwisho wa makala hii utatambua mambo yafuatayo
I. (a)
Wewe ni mjenzi na mbomoaji wa maisha yako
II. (b)
Mazingira yanayokuzunguka ni matokeo ya fikra
zitokazo ndani mwako
III. (c)
Jinsi gani unaweza kubadili maisha yako.
IV. (d)
Dunia mpya.
Mara nyingi tunapomuona mtu
akifanikiwa katika biashara tunasema ana bahati’ama kismati’.Tunapomuona mwenzetu
akifanya vizuri katika elimu tunasema Mungu amembariki na kumpa akili
nyingi,TUKIONA WENGINE WAKIFANYA UGUNDUZI tunasema ‘ana akili nyingi’.Hatutakumbuki
jambo moja,ya kuwa kuna magumu wanayoyapitia watu hawa mpaka kufikia mafanikio
lakini kubwa zaidi ni kwamba kabla ya matokeo hayo,walianza kufikiri,kisha
wakaweka nia ili kutimiza malengo hayo ambayo sasa yanaonekana wazi.
Ukiona simu,kumbuka kuwa aliyetengeneza
alianza na fikra juu ya mawasilano,akafanya juhudi mpaka kufika hapo.Ukiitazama
TELEVISHENI,Kumbuka kuwa haikugunduliwa kwa bahati mbaya bali ilianza na mtu
kufikiri.Ukiona kuna uoto mzuri nyumbani kwa mtu,si kwamba ulitokea kwa bahati
mbaya,ulianza na wazo ndani ya muhusika,kisha akafanya juhudi kutekeleza.
Kila unachokiona ,unachokitumia ni matokeo
ya fikra za watu na wewe ukiwa mmoja wao.Marimba,Kinanda,kijiko,sahani,gari,baiskeli
na vingine vingi vijavyo ni matokeo ya fikra za wanadamu.
Hakuna jambo hata moja ama ugunduzi wowote
uliojitokeza katika mazingira rahisi,fikra ilianza kufanya kazi,ikasukuma hamu
ya kufikia ndoto hizo,na mwisho wa siku..jambo lililokusudiwa linatimia
Kujenga maisha yako kunaanza na fikra
zako.Unapata kadiri unavyofikiri.Unapoweka fikra juu ya jambo,unapata matokeo
yake kadiri unavyofikiri.
Huwezi kutenganisha kile kilichopo ndani ya
fikra za mtu na kile akitendacho ama ambacho kinaonekana.Kinachoonekana ,ni matokeo ya fikra za mtendaji.Vivyo hivyo huwezi kutenganisha kati
ya ulimwengu wa kiroho na ulimwengu
unaoonekana kwa macho..Uonekanao kwa macho ni matokeo ya ule wa kiroho (usioonekama kwa macho).Katika
elimu ya Saikolojia unaweza kupima fikra
na tabia kwa kutazama matokeo ya mambo yanayotendwa na mtu .
Mazingira bora ya kuishi hayatokei kwa
bahati mbaya,yanajengwa na fikra (mtazamo).Mtazamo chanya huyajenga,nao mtazamo
hasi huyabomoa.Hivyo ni wazi kuwa unapotaka kupata mafanikio katika jambo
lolote,unaanza na fikra chanya juu ya jambo hilo,Jifunza kutazama kila jambo
katika mtazamo chanya. Kila mmoja wetu ana ndoto ( matarajio ) ya kufnya jambo Fulani
maishani,na kuwa mtu Fulani maishani…Unachokiwaza ndicho kitakachotokea katika
uhalisia.Fikra ni mbegu ya kuelekea mafanikio.Ukipanda mbegu ya fikra
chanya,utavuna kama ulivyopanda,vivyo hivyo ukipanda hasi,utavuna
ulivyopanda.Ukiona vyaelea ,vimeundwa.
Kwa maelezo hayo ,unaweza kubadili maisha
yako kwa kubadili fikra zako.Unaweza ukawa katika mazingira magumu sana,lakn
kamwe hutabaki hivyo kama utaanza kuwaza vyema,fikra za mafanikio,upendo,amani
zinakupelekea kwenye matokeo chanya
Mawazo uwazayo juu yako ni kipimo
unachojipimia katika mwenendo na matokeo ya maisha yako.Matokeo yake kamwe
hayajifichi.Hatuchagui mojakwa moja juu ya mtiririko wa maisha yetu,lakini
kupitia fikra,tunachagua matokeo ya maisha yetu na kuujenga mtiririko wa maisha
yetu.
Fikra huonekana matokeo yake haraka kwenye
tabia,na tabia huleta matokeo ya maumivu ama furaha (majuto ama furaha).Kwa
kifupi tabia uliyonayo,iletayo matokeo yake ya majuto ama furaha ndiyo inayotoa
picha ya fikra iliyotoa msukumo wa matokeo hayo..
Fikra yenye woga,wasiwasi,na kutowajibika
huonesha tabia ya unyonge , kutojiamini na kutochukua hatua,matokeoa yake ni
kukata tamaa, kushindwa na kuwa tegemezi kwa kila jambo.
Nazo fikra
yenye uvivu hupelekea tabia za udhaifu/unyonge, udanganyifu(usanii
sanii) na matokeo yake ni kuwa ombaomba,masikini na uzembe.(ukiona nchi ina
kila rasilimali,na inakuwa masikini,basi ujue watu wake wote ni wavivu kufikiri
na wasipobadili fikra hizo watabaki kuwa ombaomba hata kama matrilioni ya pesa
yatatolewa kama msaada)
Fikra za chuki na kutojiamini huleta tabia
za visasi na uonevu,matokeo yake ni vurugu,kutoweka kwa amani,mauaji ya kutumia
nguvu.Unaweza kujifunza matokeo ya viongozi wasiojiamini na wenye chuki.
Fikra za ubinafsi (umimi) huleta tabia ya
ushindani,unyang’anyi,(roho mbaya tunaita waswahili).Na matokeo yake kila mmoja
anayajua.
Kwa upande mwingine fikra zote njema huleta matokeo mema kwa watu wote.
Fikra za kutia moyo,kujiamini na kuchukua hatua
huonekana katika tabia za utu wema na kuwajibika,matokeo yake ni
amani,mafanikio na uhuru wa kweli.
Huwezi kuwa huru mpaka utakapokuwa na fikra
huru.Ukifahamu jinsi unavyoweza kubadili maisha yako kwa kubadili fikra
zako…umeyafikia mafanikio
Mkononi mwako ni matokeo halisi ya kile
ukiwazacho….maisha yako unayoyaishi sasa ni matokeo halisi ya fikra zako,kwa
kutambua ama kutotambua.Unavuna ulichopanda.Hakizidishwi wala kupunguzwa.Ukiachilia
mbali hali uliyonayo sasa,unao uwezo wa kubadili maisha yako…ama kubaki
ulivyo.Hii ni kwa kupitia mawazo yako mwenyewe. Utarudi nyuma kama mawazo yako
yanavyotaka,ama utasonga mbele kama mawazo yako yanavyotaka.Mawazo hutoa
msukumo moyoni.Msukumo huo huleta matokeo sawia.
Kama utasubiri mazingira ya mafanikio yako
yajengwe na mtu mwingine(wengine) basi utasubiri mpaka mwisho..Ni wewe na wala
si mwingine wa kuchukua hatua.Juhudi
huleta matokeo.Kiwango cha juhudi unayoiweka,kinatanabaisha juu ya
matokeo yake. Fikra unazozijaza katika mawazo yako,msukumo unaouweka moyoni
mwako ndio ujengao maisha yako,na ndivyo utakavyokuwa.
DUNIA MPYA
Dunia
mpya ni matokeo ya fikra zako mpya.Dunia mpya ni ile inayojengwa na wale
wanaoamini katika uwezo walionao.Dunia tunayoishi sasa,mazingira yake,hali yake
ni matokeo ya fikra zetu wanadamu.Kuongezeka kwa joto,kutoweka kwa amani na
upendo,uchoyo,wivu ni matokeo ya binadamu yaliyoanza muda mrefu.Dunia mpya
yenye amani,furaha,upendo,usawa,hali bora inajengw na sisi ,kila mmoja
akichukua hatua juu ya fikra zake na maamuzi yake.Mimi binafsi naiona dunia
mpya,yenye amani na furaha,upendo na maelewano,dunia hii itajengwa na watu
wenye fikra za usawa,upendo,umoja baada ya dunia inayojengwa na wenye chuki na
matabaka kushindwa.Love never fail