Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Monday, July 23

SIKILIZA SAUTI YA MOYO WAKO

Kabla ya kuanza kusoma makala hii,nakusihi uifanye huru fikra yako,fungua fikra zako,usifungwe na imani na mafundisho fulani ili usiathiri uelewa wa makala hii(your mind may become your great enemy,so empty it) ......Pili uwe huru kutafakari ndani ya moyo wako na kuuliza.

 Simaanishi unachoamini wewe ni uongo nami nnaandika ukweli.Jambo haliwi kweli eti  tu kwa sababu limeandikwa ama limesemwa..ama kwa sababu wengi wanaliamini,bali ukweli kuhusu jambo hutoka kwa mtu mwenyewe,kwa kuliishi jambo na kulifahamu.Mfano,hakuna anayeujua ukweli kuhusu wewe,isipokuwa wewe,hakuna anayeweza kujua ukweli kuhusu upendo,isipokuwa ameuishi upendo na kuifahamu chuki.

  Moyoni mwako,pana siri kubwa......ambayo ukiitambua,utakuwa umefungua njia ya ushindi katika kila jambo unalolitaka.


moyo wako ni chemchem ya uwezo wa ki Mungu
moyo wako ni chemchem ya uwezo wa ki Mungu ,ni hekalu la mawasiliano kati yako na asili yako(Muumba wako,Mungu,Mwenye uwezo wote)

   Moyo wako ndipo chimbuko kuu la mawasiliano kati yako na ASILI YAKO(MUNGU).Mungu hawasilIani nawe kwa kutumia vitabu,ama kwa kutumia maneno,bali huwasiliana nawe kupitia moyo wako.

Yeye huweza kutumia njia zingine endapo tu mhusika hasikilizi sauti ya moyo wake.Kwake matumizi ya lugha si ya lazima kwa sababu lugha huweza kuchanganya na wakati mwingine tafsiri huchangia kudhoofisha ujumbe uliokusudiwa.Hivyo  basi,kumbe Mungu huweza kutumia njia mbalimbali kufikisha ujumbe kwa watu,lakini njia iliyo kuu isiyoweza kupotea ama kuchanganya ni kupitia moyo wa mtu husika..

  Kwa wale wakristo,watakumbuka ya kuwa,miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu....
   Pia ikumbukwe kuwa Yesu alipata kuwaambia wanafunzi wake ya kuwa,hawaisikilizi sauti ya Mungu kwa sababu wameifanya migumu mioyo yako.
  Kuna wakati ambapo mtume Mohamed (S.A.W) alipata kuwaambia wafuasi wake ya kuwa yeye alikuwa akisikia sauti ya Mungu ikimtuma kutenda......wakashangaa,wakataka kujua ni kwa nini wao hawakusikia,sababu ni moja....waliifanya migumu mioyo yao.

  Hivyo ni  wakati sasa wa kutambua kuwa ule uzima tunaoutafuta kila siku,ile chemchem ya ushindi katika maisha,haipo mbali nawe,usiitafute juu kwenye nyota,usiitafute ndani ya sinagogi,usiitafute tu msikitini,na wale haijajitenga nawe,bali ipo ndani mwako.
SAUTI KUU IKUONGOZAYE KWENYE USHINDI IPO NDANI MWAKO
SAUTI KUU IKUONGOZAYE KWENYE USHINDI IPO NDANI MWAKO
 
    UTAITAMBUAJE?
    Mungu hukutuma kutenda kupitia moyo wako...pale unapopata hisia  na msukumo wa kutenda uletao faraja na furaha,usio na chemchem ya tamaa ya kupata sifa,wala fedha wala utajiri wa aina yeyote,bali kila unapoisikiliza sauti hii na kutenda kadiri inavyokutuma,hufungua milango ya ushindi(UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU ,KISHA YOTE MTAZIDISHIWA)

    Sauti hii hutuongoza kutenda kwa upendo,na sauti hii humjuza muhusika mwisho wa jambo alitendalo,naye aisikiaye hutambua matokeo yake,na hivyo kila aisikiaye sauti hii,haklati tamaa,hasikilizi maneno yanayomvunja ari,bali huyafanya yote kwa bidii.
  KUMBUKA..
  Kwa kuwa moyo wako huwasiliana na asili yako(mungu),basi,kila aliye tayari kuisikiliza sauti ya moyo wake,huwasiliana moja kwa moja na asili yake(mungu),wakati wowote ule pasipo vikwazo.Wapo wanoamini kwamba kuna wateule tu ambao huweza kuzungumza na Mungu,jibu ni laah,kila mtu ana uhuru na usawa mbele za Muumba,naye Muumba huwasiliana na kila mtu pale mtu huyo anaposikiliza moyo wake...
  Kwa udadisi huu,ni wazi kuwa moja ya sababu kwa nini wakati fulani unaomba.,haupati majibu,ama haufanikiwi ni kwa sababu,wewe huchagua jambo kwa kutazama tu faida,na wala si lile ambalo moyo wako unakusukuma kutenda(litokalo kwa Muumba) ama  unaomba usichokipenda toka moyoni mwako(kwa tamaa eitha ya kuona toka kwa wengine,eengi tunatafuta kufanya jambo tuwe kama watu fulani,tupate pesa ama mali,ama umaarufu,-vijana wengi siku hizi wanatafuta kazi ambayo wanasikia wanalipwa vizuri,wengi wanasomea kozi mbalimbali kwa msukumo wa malipo,si kwa msukumo toka moyoni-mfano udaktari kwa sababu wanalipwa fedha nyingi,ama uhasibu,ama kompyuta nk,lakini wale wanaosoma kwa msukumo wa moyo,wanaosukumwa na kujitolea na kutoa huduma kwa kujali utu na ubinadamu,hao hufunguliwa milango ya mafanikio......nao hutenda kwa bidii)
 Jifunze kutambua hisia za moyo wako.....jifunze kuingia ndani ya moyo wako na kujitazama kwa kina,tazama muungano kati yako na asili yako.....sikiliza moyo wako,sikiliza sauti ya moyo wako
                       
     

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com