sihesabu mafanikio katika maisha yangu kwa kuhesabu idadi ya namba za wale wanaonipigia simu,ama wale nliopata kuwa nao,nisiokuwa nao na nilio nao,sihesabu ni fedha kiasi gani nlichonacho,ama mimi ni wa daraja lipi,sihesabu nguo nlizonazo,ama ni vyuo gani na vingapi nimesoma....sihesabu ni marafiki wangapi ninao,ama kama nipo pekee,,,,,,,.nahesabu mimi ninawapenda wengine kiasi gani,na ni kiasi gani nawaumiza wengine,na mimi mwenyewe kwa chuki....nnahesabu,mimi ni nani na najitambua kiasi gani,,nahesabu heshima,usawa ,furaha,ubinadamu,amani..nahesabu ni namna gani nimeleta upendo palipo na chuki,,najifunza kutojisifu wala kutafuta sifa...nahesabu kutazama mbele na kuwa na imani na hakika ya ushindi,nahesabu ni maneno gani ninayasema na yana maana gani,yanawajenga vipi wengine.Kwangu maisha ya mafanikio ni kuwakubali wengine jinsi walivyo na si kwa kutazama mali wanazomiliki,Zaidi ya yote,kwangu maisha ni kuishi kwa kusikiliza moyo wangu,kwa dhati,na kuifanya nuru ya maisha yangu iwaguse wengine ,ili nao wanapochagua kuishi maisha yao kwa dhati-Pongu Joseph-0717903089
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa