Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Friday, July 20

MAADUI WAKUU KUFIKIA MAFANIKIO

Mafanikio ni kutimiza jambo lolote lile ambalo umelipangilia na kuamua kulitenda kwa dhati.Kuyafikia mafanikio kunahitaji kujitolea,kutenda kwa moyo wote na kwa nguvu zote...ukitilia mkazo lengo(malengo) uliyoyaweka.

Ikiwa umekuwa ukifuatilia makala hizi,utakuwa umeanza kujitambua wewe ni nani na hata kuanza kuchukua hatua stahili kuyainua maisha unayoyapenda,ukichagua na kusikiliza moyo wako.Unaweza kuwa unajaribu tu kutenda na wala si kuamua kuchukua hatua na kuamka,kuishi maisha unayoyahitaji,ukitenda kwa bidii kuyafikia mafanikio,mimi pia nimechagua kusimama,kuacha yaliyopita ambayo hayakuwa msaada kwangu,kusimama na kufurahia maisha,nikitenda kwa upendo na msukumo wa kuona kuwa kupitia mimi,wengine wataiona nuru ya Mungu iliyo ndani mwao kama ilivyo kwangu,wakiishi maisha waliyoyachagua,wakitumia vipawa vyao vyema,na kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi. Yapo mambo ambayo,ni chanzo kikubwa cha kutofikia mafanikio tunayoyakusudia...hayo ni kama ilivyo hapa chini....nakusihi usome kwa makini,ili uweze kuelewa vyema.

 1.KUTOCHUKUA HATUA

KUTOCHUKUA HATUA KUNACHELEWESHA MAENDELEO

USISUBIRI,KESHO AMA MWAKANI KUAMUA KUTENDA,WAKATI NI SASA USIUDHARAU AMA KUUSHUSHA UWEZO ULIO NDANI MWAKO....CHUKUA HATUA
USISUBIRI,KESHO AMA MWAKANI KUAMUA KUTENDA,WAKATI NI SASA .
 USIUDHARAU AMA KUUSHUSHA UWEZO ULIO NDANI MWAKO....CHUKUA HATUA

Wengi wetu tumekuwa tukifikiri kwamba upo wakati fulani wa kuamua kuchukua hatua na kuchagua kutenda kile ambacho sauti ya moyo wako inakutuma kufanya.Tumekuwa tunasubiri kesho,ama tukimaliza shule,ama mwanzoni mwa mwaka unaofuata,ama nikiruhusiwa....Tambua kuwa hakuna wakati mwingine wa kuweka mpango wako wa maisha yako yajayo zaidi ya sasa.

Wakati ni sasa,amua sasa kutenda,usiogope kushindwa,tazama kila jambo katika mtazamo chanya,kushindwa huleta mwanga utakaotuonesha ni njia ipi itakayotufanya kugundua njia mpya ya ushindi,mafanikio yahaji pasipo kukwama,kuangua na kunyanyuka,amini nakwambia kushindwa ndio njia pekee ya kuuendea ushindi.....kama unafanya jambo lisilo na changamoto,tambua kuwa njia hiyo si sahihi kwako...tambua pia kuwa hakuna aliye na jukumu la kuyaandaa maisha yako,Hakuna mwenye jukumu la kukuchagulia maisha,hakuna wa kukusukuma,bali fukuto la ushindi hutoka ndani mwako
HAKUNA WA KUCHUKUA HATUA JUU YA MAISHA YAKO,NI WEWE,HATUA MOJA TU YA MWANZO ITAKUPELEKA KWENYE HATUA NYINGINE YA MAFANIKIO
(REJEA MAKALA- USHINDI HUANZA NA FUKUTO NDANI YAKO Soma hapa)

 2.KUKATA TAMAA
Nikupe siri moja,kama unaamini kwenye dhambi.....hakuna dhambi iliyo kubwa kama kukata tamaa.Kama unaamini katika usaliti...hakuna usaliti ulio mkubwa kama kukata tamaa.
Kukata tamaa ni kutoamini katika uwezo ulio nao,kukata tamaa ni kutotambua uwezo ulio nao,kutoitambua nuru iliyo ndani mwako,kutomjua Mungu aliye ndani mwako.....kukata tamaa ni kwa wale wasio tambua nini wanachokifanya.....anayekata tamaa ni yule asiyeona kinachokuja mbele yake...ni kwa yule asiye na maono ya ndani ya moyo wake.....ni usaliti wa sauti iliyo ndani mwako
ANAYEKATA TAMAA NI YULE ASIYEUJUA MWISHO,ASIYE SIKILIZA SAUTI YA MOYO WAKE...ASIYE NA TUMAINI YA MAMBO YAJAYO
LICHA YA VIKWAZO,WEWE  ATENDAYE KWA UPENDO HAKATI TAMAA,ANAYESIKILIZA SAUTI ya moyo wake
Aujuaye mwisho hakati tamaa
 3.WOGA
 Woga ni matokeo ya kutojitambua, kuogopa kutenda jambo kwa sababu ya kushindwa ama sababu ambazo si halisi,zitokazo katika fikra ya mtu binafsi.
Katika maisha yetu kila mahali tumefundishwa kuogopa.Tumefundishwa kuogopa wazazi,kuogopa walimu,kuogopa viongozi,kuogopa vitu visivyoonekan,tumefundishwa kumuogopa Mungu.....na ndio maana kila wakati tunaogopa kutenda pale moyo unapotutaka kutenda kwa sababu ya woga...woga umetuletea aibu...hatutendi kwa kuogopa macho ya wengine.......(mfano mhitimu wa chuo kikuu anaogopa kupita nyumba hadi nyumba kuuza bidhaa yake..kwa woga wa kuonekana kwa wengine kuwa labda hajasoma...kwa kifupi anaogopa mafanikio yake mwenyewe).

Kumbe woga unatokana na kutoamini uwezo wetu wenyewe...woga ni kukataa kufikia mafanikio yako mwenyewe..chagua kuondoa uoga,chagua umakini,chagua kuwa rafiki wa vyote unavyoviogopa,chagua kuwa rafiki wa Mungu wako

 4.KUTOAMINI KUWA TUNASTAHILI TUNACHOKITAKA
Hiki pia ni kikwazo kikubwa na adui mkubwa wa maendeleo.Wengi  hawaamini kuwa wanastahili kuishi maisha bora,hawastahili elimu bora,hawastahili hata kutenda mambo makubwa..
Mfano ni rafiki yangu mmoja,alipata kuniambia kuwa yeye eti kwa sababu aliishia darasa la saba,haoni kwamba anaweza na wala anastahili kuwa kiongozi,haoni kama anastahili kuishi maisha bora yenye furaha....anaona mbele yake kuwa kuna ukuta mkubwa kati yake na maisha bora ama mafanikio yeyote....anaona hastahili furaha,anajiona kuwa hastahili hata kuitwa katika kazi,hajiamini,haamini kama anastahili kila jambo analolipenda....kwa hivyo huyu hawezi kuijua sauti ya moyo wake. Wakati mwingi maishani tunakosa kufanikiwa kwa sababu tunaamini hatustahili.....rejea makala..(NI JINSI GANI TUNAPATA TUWAZACHO)

Ukiamini huwezi umeshindwa tayari...ukiamini unaweza lakini huchukui hatua,umeshindwa......ushindi ni kwa yule amabaye anaamini ya kuwa mwisho wa pambano atashinda.

 5.KUSHIKILIA MAMBO(JAMBO)AMBAYO YANARUDISHA NYUMA(CHELEWESHA)
Upo wakati tunashikilia mambo ambayo yanatuchelewesha ama yanatuzuia kusonga mbele...mfano kung'ang'ania kukaa katika mahusiano ambayo ni ya maumivu kila wakati....kufanya jambo ambalo (biashara)ama huduma yeyote ambayo moyo wako haupati furaha na wala haukusukumi kufanya....achia songa mbele...kumbuka kwisha kwa jambo moja hufungua milango kwa mambo mengine mengi.....tazama kila jambo kama nafasi ya wewe kwenda mbele......kuumizwa kwenye mahusiano,hakufungi milango ya wewe kwenda mbele....inapobidi,pima,anza upya...utaipata furaha

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com