Hekima ipo katika kutambua tofauti iliyopo miongoni mwetu
wanadamu.
“Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega,
akawapa.Yakafumbuliwa macho yao,wakamtambua,Kisha akatoweka mbele
yao.
Wakaambiana,Je mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi
njiani, na kutufunulia maandiko?Luka 24:30-32
Nahitaji mwalimu!!
Nahitaji msaidizi!!!
Nahitaji mwombezi!!
"Kama nikipata mwalimu ama yeyote atakayeniongoza,Maisha
yangu yatakuwa mazuri!!
Inawezekana haya ni baadhi ya maoni yako ambayo unahisi yanaweza kubadili maisha yako,pasipo kutambua kwamba mwalimu,msaidizi , yupo kati yetu.
Wakati Fulani unaweza kutoka Singida, kukitafuta kitu Dar es
salaam, kumbe umekiacha Singida kikipatikana kwa wingi na bure.
Natoa mfano huu kuonesha kwamba zipo nyakati unaweza
ukatafuta kitu Fulani na kukifuata mbali,kumbe kinapatikana katika mazingira
unayoishi.
Utashangaa nitakaposema kwamba,kuna watu ambao wanakuzunguka
na unaishi nao, ambao Mungu amewaweka makusudi katika kuifanya safari yako ya
maisha kuwa rahisi,lakini upofu ulio ndani yako,unakufanya usitambue kabisa.
Nyakati zote unawatazama kama ni wa kawaida tu, hawana
umuhimu kwako,na hivyo badala ya safari yako ya mafanikio kuwa ni siku 40, inakuwa ni miaka 40.
Wapo watu ambao wakati mwingi nawafuatilia.Na huwa najiuliza
ni kwa nini sikupata kuwatambua mapema.Matendo yao,mienendo yao, maneno yao, mitazamo yao huweza kuamsha nguvu ndani yangu.
Tabia yangu hii ya kudadisi imenifanya nianze kuwatazama kila nnayekutana nae kwa jicho
la kipekee,kwa sababu naamini,kila ninayekutana nae katika
kazi,sala,mijadala,daladala,hawajatokea kwa bahati mbaya, bali Mungu ana
makusudi.
Mara nyingi nafanya hivi pasipo hata wao kutambua kwamba nathamini kukutana nao.
Mungu yupo miongoni mwetu,na wakati mwingi hatutambui hilo.
Mara nyingi tunadhani Mungu yupo kanisani ama msikitini.
Tukiwaona
wachungaji,mapadre na viongozi wa kiimani,tunadhani ndipo tunapoweza kumwona
Mungu.
Mungu yupo miongoni mwetu.Kwa wadogo,wadhaifu,
warefu,wafupi,weusi,wembamba. Mungu yupo miongoni mwetu.
Binadamu wengi hawapendi kutazama zaidi ya mwonekano wa
mtu.Ukijifunza kutazama zaidi ya mwonekano wa nje,unaweza kuona kilicho ndani
na thamani ya kisichoonekana kwa macho ya nyama.
Kwa wale wanaoishi na wenzi wenu,Mungu anaweza kuwa ndni ya
mwenzi wakounayelala nae kwenye kitanda kimoja.Moyo wa kudhani/kutazama kwa
kuhukumu unaweza kukufanya usitambue hilo.
Anaweza kukupa suluhisho juu ya jambo,lakini kwa sababu
unamtazama kwa nje, na kwa mazoea basi huwezi ona kilicho ndani yake.
Lakini akisimama kiongozi wa kiimani, akiongea kwa sauti ya
kukuvuta, akikupa ushaurinhata usiofaa, utapiga kelele na mwitikio mkubwa
moyoni mwako.Ndio baba!!!
Hekima ipo katika uwezo wa kutambua kisichoonekana.
Mungu yupo kati yetu, picha uliyonayo kichwani mwako kuhusu
Mungu inakufanya usimtambue.
Kitu unachokifuata maili nyingi,kipo kinakuzunguka katika
mazingira yako
Naitwa Pongu Joseph
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa