Katika makala hii tunajifunza juu ya binadamu anayejitambua.Makala hii inaweza kukukumbusha mambo mengi kwa kifupi na hivyo kukufanya uchunguze juu ya maisha yako na kuyatumia vyema kwa wakati huu ulipo hapa duniani.
Kutambua ndani yako hakuhitaji uende shule na kusoma sana,na hakutokani na maamuzi ya mtu mwingine bali ni maamuzi yatokayo ndani mwako
Kutambua ndani yako hakuhitaji uende shule na kusoma sana,na hakutokani na maamuzi ya mtu mwingine bali ni maamuzi yatokayo ndani mwako
Ni mguso unaotaka ndani mwako, ufahamu unaokua toka ndani mwako. Ni uchimbuzi wa chemchem zitokazo ndani mwako, Ni kumtambua Mungu kupitia mguso ndani ya moyo wako, kisha kuanza kutumia kipawa ulichonacho kwa ajili ya utukufu wa Mungu . Ni hisia za ndani zitakazofanya umfahamu Mungu na si kufikiria
tu.Upya ndani ya binadamu hutokea wakati wote
kwa kuunganisha moyo wako na ulimwengu wa hisia na kuendelea kujifunza
kila wakati na kukuza nafasi ya moyo wako kuwa mpya.
na
Je ni kwa namna gani unamtambua binadamu anayejitambua?
Mtu anayejitambua hubadili mtazamo
wake kutoka kwenye mtazamo wa jamii unaofuata mila na desturi/kawaida kuelekea kwenye fikra za
kuijenga dunia mpya na yenye fursa mpya.Hujenga dunia ambayo wanaomzunguka ni
wanadamu wanaotambua utu na nafasi ya kila nafsi.Akiwa na misingi ya ujamaa na
usawa, hufanya majukumu yake kutoka kujitazama yeye binafsi na kuanza
kuwatazama wengine.Uchaguzi wake na matendo yake husukumwa na maono na mtazamo wa mbali kwa ajili ya
binadamu wote na viumbe vyote.Hutazama sio kila kiumbe kwa ajili yake,bali kila
kiumbe kwa ajili ya wote.
Anayejitambua habagui jinsia bali
hutambua jinsia kuwa ni matokeo ya fikra za Mungu yaliyokusuduia kutoa
fursa.Huheshimu, hutambua wengine na kuthamini nafsi zao na uchaguzi
wao.Hutengeneza dunia dunia ambayo jinsia zote huwa na uhuru wa kutumia vipawa vyao, kutambua sauti zo,nuru
ndani mwao na kutumia kwa ajili ya viumbe wote.
Mtu anayejitambua hasukumwi kutenda
na maamuzi ama fikra za wengine. Anatazama ndani yake.Hajifananishi na nafsi
zingine na hivyo hatumii nafasi yeyote kuwakandamiza wengine.Husimama kwa miguu
yake mwenyewe. Anawasikiliza wengine isipokuwa hatoi nafasi kwa wengine
kumuamulia maisha atakayoishi. Anayaona mambo yajayo na hivyo huanza kuijenga
kesho yake katika wakati tunaouita sasa. Ni alama ya uwezo wa Mungu uliopo
ndani ya binadamu. Na alama ya maisha yake huishi enzi na enzi.
Mtu anayejitambua huchukua hatua juu
ya hisia zitokazo ndani mwake na hivyo kutambua matokeo ya matendo
yake.Hutenda kwa msukumo wa moyo. Hutambua mambo ambayo hayamletei faida na
kutoyafanya na pia hutambua yale yanayomletea faida ..akitambua kuwa
anapotenda kwa wengine anajitendea mwenyewe. Husikiliza hisia za ndani mwake na
kujifunza lugha ya moyo wake.
Huishi maisha yenye sababu. Husikia
muito alioitiwa na kuuuishi. Haridhishwi tu na maisha ya tokanayo na matukio
kama kuamka,kutembea,kulala,kula bali hutambua kuwa yupo hapa duniani kwa
sababu maalum,hivyo huchimba ndani mwake kuijua sababu na kuiiishi. Kila wakati
anasukumwa na sababu hiyo ya yeye kuishi ,kuendelea kuishi kwa dhati akitengeneza na kuifuata njia
inayomfikisha huko.
Hakimbii majukumu yake . Hajitoi
katika kutafuta suluhu ya changamoto na wala halaumu wengine. Hutambua makosa
yake na kujifunza kupitia hayo. Husanifu maisha yake na kuyafanya mapya kila
wakati.
Hujifunza toka ndani mwake na kutoka
kwa wengine. Hutilia mkazo katika mafanikio ya ukuaji ndani mwake kuliko
mafanikio ya nje., hutengeneza ndani mwake. Hutafiti na kuvumbua chemchem
zinazojenga na kubomoa nafsi na kutumia chemchem hiyo kuifanya dunia kuwa
sehemu bora ya kuishi.Hivyo aliyejitambua ni picha tosha ya uwezo na uwepo wa Mungu ndani ya binadamu.
Hutengeneza msawazo kati ya chemchem ndani mwake na matokeo yaonekanayo
halisia.;
Binadamu anayejitambua hutazama kila jambo kama fursa |
Anayejitambua hatafuti usahihi
katika utendaji bali hutenda kwa kujitolea katika nguvu na uwezo wote.Hufanya
kwa uwezo wake wote.
Anayejitambua hujikita katika kutenda
kuliko kusema tu.Huweka bidii katika kazi . Huanzisha na kutenda mambo ambayo hufaidisha viumbe
wote . Husema pale inapohitajika,huheshimu mawazo yake na huwa tayari kuchukua
malipo ya maneno yake mwenyewe.Hakimbii kivuli chake. Hayupo tayari kuona
wengine wakikosa uhuru kupitia yeye.
Anatambua kuwa wakati wote huvuna alichopanda..
Anayejitambua huweka mkazo katika
uhusiano mwema na nafsi zingine. Huthamini mahusiano yenye thamani. Mahusiano
kwake hutokea ndani, hujengwa ndani na hivyo hudumu. Upendo kwake ni lugha ya
moyoni, huleta furaha, mshikamano na amani.Zitokeapo changamoto katika
mahusiano,huwa tayari kuyatatua kwa ajili ya kuyakuza zaidi.
Anayejitambua hutambua kuwa hapa
duniani hatupo katika kushindana,ushindani kwake haupo,hushirikiana na ushindi
kwake ni furaha katika kutimiza wajibu wake. Huandaa silaha zake ndani na
kuteketeza kila kisicho na manufaa kwa binadamu. Baada ya milima na mabonde
katika maisha yake ushindi huzaliwa ndani mwake. Hutumia uwezo wake kwa ajili
ya Wengine na si dhidi ya wengine..
Huishi katika hali ya kujitolea na
bidii. Huwa ni zawadi ya aina yake hapa duniani. Haogopi kutenda. Huendeleza
mambo yaliyojenga utu,ubinadamu na misingi bora ya kuishi yaliyojengwa na
binadamu waliomtangulia. Maisha yake hufundisha wengine. Hutambua juhudi za wengine na wote wanaompa
msukumo wa kutenda zaidi hasa pale anapokutana na changamoto. Hutambua kuwa hayuko peke
yake,bali dunia imejengwa kwa muungano wa nafsi zinazotimiza majukumu kwa dhati.
Haogopi ukweli hata pale unapoumiza.
Hutoa nafasi ya kusamehe kila wakati anapokosewa. Hujisamehe yeye pia anapofanya
makosa. Hushiriki katika ujenzi wa maisha yake.
Hutambua kuwa kila jambo hutoa
fursa,kila kiumbe ana fursa. Hakusanyi ama kujilimbikizia kwa ajili ya sifa.
Hutazama wengine kama anavyofanya kwa nafsi yake. Inapostahili hujitolea
alichonacho,hutoa kwa wale walioshiriki kwa yeye kupata. Hutengeneza maisha
yake yawe ya kutoa fursa kwa wengine badala ya kuwanyang’anya wengine .
Anayejitambua haichukuliai dunia
kama chanzo cha maumivu bali hugundua kuwa dunia humpa kila mmoja kadiri
anavyohitaji.Dunia husikiliza kutoka kwenye uwezo ulio ndani mwetu tuliopewa na Mungu.Hata mara
moja hajichukulii kuwa ni bora kuliko binadamu wengine na wala si dfhaifu
kuliko wengine. Hutambua kushabihiana na kutegemeana kati ya kiumbe kimoja na
kingine.Hivyo anatambua kuwa kama ikiharibu mazingira ,ni sawia na kuharibu
nafsi yake.
Binadamu anayejitambua huyajenga na kuyatunza mazingira yanayomzunguka |
Anayejitambua hamlaumu Mungu hata
mara moja. Uhusiana wake na Mungu ni wa heshima,urafiki na huwa na umoja naye
. Mienendo yake yote humwelekea Mungu .Anawaheshimu wanaoamini sawia naye na
wasio amini sawia naye. Hashiriki kutumia imani ama dini kama njia ya utengano kati ya binadamu,ama binadamu na
mazingira yake.
Ni mfano wa sifa njema ya binadamu.
Huchukua majukumu yake. Ana faida kwa viumbe wote.Hulinda, hujenga, huheshimu,
Huishi vyema duniani. Ni mfano wa aliyeletwa kuifanya nuru ya Mungu ing’ae. Ni
halisi,haishi maisha bandia. Ni wa kutumainiwa, si mbinafsi. Wakati wake kuwepo
duniani ukifikia tamati,huondoka kwa furaha ya kutimiza alichotumwa,na kuacha
dunia ikimlilia.Ni wewe na mimi.