Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Monday, December 31

UKWELI KUHUSU WEWE

Wewe ndiye mjenzi na mbomoaji wa maisha yako katika nyanja zote kwa fikra zako kwani fikra ndiyo mbegu ndani yako itoayo matokeo kadiri ya sababisho litokanalo na msukumo wa kimazingira. Hivyo mafanikio yako huja kwa kupanda fikra za mafanikio na kutofanikiwa huja kwa kupanda fikra za kushindwa,uma kwa kujua na kutojua.
Wewe ni msanifu na mjenzi wa maisha yako(picha na cognitivesocialweb.com)




Wewe ndiye unayebomoa na kuangamiza maisha yako kwa fikra zako,kwa kujua ama pasipo kutambua(picha na hot100tips.com)

Kamwe huwezi kufanikiwa kama hujui unachokitaka,huwezi kuona mbele pasipoonekana kama hufahamu uendapo,ni mpaka pale utakapojua unataka kuwa nani,ndipo utakapokuwa.....ni sawa na kwenda safari isiyojulikana hata uelekeo.

Mungu alipokuuumba alikupa nguvu na uwezo,akaifanya dunia na vyote vinavyokuzunguka vitii maagizo yako,hasa yale yanayotokana na msukumo wa moyo wako..hivyo wewe ni kiumbe bora jinsi ulivyoumbwa,wewe ni aidi ya ulivyo,wewe ni upendo,amani,faraja,chuki,visasi,wewe ni mwerevu,na msanifu wa maisha yako mwenyewe,hivyo hupaswi kumlaumu yeyote kuhusiana na jambo lolote linalohusu maisha yako,chukua hatua juu ya maisha yako mwenyewe.

Ndani yako ni chemchemi ya kila hali iletayo matokeo hasi ama chanya,ukifikiri kuhusu upendo utafute ndani yako,ukitaka kujua kuhusu uwezo ulio nao,utafute ndani yako,ukitaka kujua kuhusu mafanikio yako,tafuta ndani mwako...chemchemi yako haileti faida kama hujachukua maamuzi

Huna tofauti na binadamu mwingine kwa maana ya uwezo......anza kwanza kuuchunguza ubora wako uujue,ukiutambua,utambue kuwa wengine ni bora kama wewe,hivyo matendo yako yazingatie matokeo yake,fikra zako ziwe fikra njema juu yako na kwa wengine kwani kila utendalo kwa wengine,umejitendea mwenyewe.Maisha ni uchaguzi wako,na matokeo ya kila unachochagua ni juu yako.

Fikra zitokazo kwako ni sewa na bustani ama shamba,inaitaji kutazamwa na kupaliliwa...kuhakikisha kuwa unapanda mbegu bora,ukipanda mbegu isiyo bora (fikra mbaya dhidi yako na maisha yako) huleta matokeo sawia na mbegu uliyoipanda.

Maisha unayoyaishi hayatokei kwa kiitwacho bahati(nzuri ama mbaya) bali ni matokeo ya uchaguzi wako mwenyewe ama kwa kutambua na kutotambua.Umasikini,utajiri,furaha,huzuni,amani,chuki,upendo vyote ni matokeo ya uchaguzi wa maisha yako.Nguvu na uwezo wa kubadili matokeo hayo hutoka ndani mwako....Ni msukumo utokao ndani mwako pekee ndio utakaobadili maisha yako.

Kamwe wewe huvuti maishani vile vitu unavyovitamani ama maisha unayoyatamani,bali unavuta jinsi ya fikra zako.Fikra a ushindi huleta ushindi,fikra za kushindwa huleta kushindwa.

Mara nyingi unajaribu kubadili hali ama mazingira yanayokuzunguka pasipo kubadili fikra zako juu ya mambo hayo....Jinsi uvitazamavyo vitu huwa...ukilitazama jambo kwa uchanya wake,basi kila hali huwa ni nafasi,kama ni mtazamo hasi,basi matokeo yake huwa hasi na kwako huwa ni maumivu.

NURU NA GIZA

Bila shaka kila mmoja yu na furaha siku ya leo.Karibu tena katika somo jipya leo hii.Somo hili litakufanya utambue jinsi wewe ulivyo muendeshaji wa maisha yko,ni somo litakalokufanya ujue kuwa wewe ndiye mjenzi na ndiye unayebomoa maisha yako mwenyewe,iwe kwa kutambua ama kutotambua.Karibu tujifunze pamoja

Ni mara nyingi tumekuwa tukikumbushana kuwa Mungu ametuumba kwa mfano wake,kwa kutupatia uwezo wa kutenda kama yeye.Naye hujidhihirisha kuwepo kwetu kwa njia ya upendo,ni sawa na kusema upendo ni Mungu ndani yetu.Upendo ni nuru ya Mungu iliyopo ndani yetu.Hivyo kila jambo litendwalo kwa msukumo wa upendo hufanya nuru ya Mungu iliyopo ndani yetu hung'aa.
Upendo ni nuru,kama nilivyoeleza hapo juu.Kinyume chake ni chuki,ama giza. Kila tutendapo jambo kwa chuki,basi nuru huzimika ndani yetu  na linabaki giza


Upendo ni nuru iliyo ndani ya mioyo yetu,kila tutendapo kwa upendo maisha yetu huwa nuru kwa wengine (picha kwa msaada wa mtandao)


 Giza ndani ya mioyo yetu hutokana na kutoweka kwa mwanga,yaani kutenda pasipo upendo.Inamaanisha visasi,migogoro,ugomvi....yote hii huipoteza nuru iliyopo kwako.Ama kwa kutambua na kutotambua,unayajenga maisha yako kwa uchaguzi wako mwenyewe,ambao hutokana na kutenda kwa upendo ama kinyume chake (giza).Ni sawa na kusema tunayafanya maisha yetu kung'ara ama kufifia kwa maamuzi yetu wenyewe.
Atandaye kwa upendo hulipwa upendo.Moyo wake hujawa furaha na hivyo hufungua njia ya mafanikio katika kila jambo alipendalo.Huamsha mwili wenye uchangamfu na uso uliojawa bna furaha na amani.Nuru yake hung'aa daima.Hata siku zake za kuishi hapa duniani zinapokwisha,huenda kwa amani.Nuru yake huendelea kung'aa vizazi hata vizazi.Mifano ipo mingi
Mfano wa kwanza ni ule wa Yesu,Kristu (mnazareti).Huyu alifanya kila jambo kwa kusukumwa na upendo.Alitoa maisha yake kwa ajili ya wengine.Alifundisha upendo kwa kutenda na kuuishi.Akawa faraja kwa wote ambao walikuwa hawathaminiki katika jamii.Hata alipoondoka,wengi wa wafuasi wake na wasio wafuasi wamezidi kumkumbuka,na hata sasa wanaozaliwa baada yake hukumbuka na kumtambua kwa kupitia matokeo ya upendo .Wengine ni wengi ambao tumekuwa tukiwasikia ama kupata kuwaona katika jamii yetu.
Kutenda kwa upendo humaanisha kujali,kuthamini wengine.
Sisi ni wa thamani kwa sababu Mungu yupo ndani yetu.Hivyo kila unapojitazama na kujikumbusha thamani yako,kumbuka ya kuwa kila anayekuzunguka ana thamani sawia na ile uliyonayo,hivyo kila utendalo kwa wengine,umejitendea wewe.Unapotenda kwa upendo kwa wengine,umejitendea wewe,vivyo hivyo,unapotenda kwa wenako kwa chuki,basi umejitendea mwenyewe.
Upendo ndio lugha ya pekee inayounganisha viumbe wote duniani(picha kwa msaada wa mtandao)
 

Hivyo kwa maelezo hayo juu,tunajifunza kuwa sisi tunajenga ama kubomoa maisha wetu wenyewe kwa uchaguzi tunaoufanya wenyewe.Katika kila huduma unayoitoa,iwe ni elimu,biashara..ukitenda kwa upendo unafanikiwa.Ukitoa huduma kwa chuki unadidimiza mafanikio yako mwenyewe,iwe kwa kutambua hilo ama kutotambua.Chukua mfano unafanya biashara;wanapokuja wateja unawachangamkia kwa furaha na upendo..ukiwahudumia vema na kuwapa ushauri mzuri na ukatenda kinyume chake,ni lipi kati ya matendo hayo juu itakuletea mafanikio?

Nuru ya Mungu iliyopo ndani mwetu haifichiki kamwe,viumbe vyote duniani huvutiwa na nuru hiyo
Tunapokianza kipindi kipya katika mpangili wa miaka,tukumbuke kuwa tutahesabu mafanikio ama kutofanikiwa katika malengo yetu kwa  kuchagua wenyewe,nuru ama giza

Kuna furaha kubwa kwa wale wanaouchagua upendo,furaha huwa daima maishani mwao,na daima nuru ya Mungu iliyo ndani mwao hung'aa daima na kuwafanya wengine wajifunze toka kwao.Heri ya maandalizi ya kipindi kipya cha mwaka 2013.


Friday, December 7

Kumbuka wimbo wako




Katika dunia hii ni vema kuyaishi maisha yako pasipo kuigiza,yawe yako halisi..Ukiyaishi kwa juhudi zako,hutapata kuwa na wasiwasi juu ya kifo na matokeo yake...Waheshimu wengine wote,heshimu imani zao,fikra zao na mitazamo yao.Yapende maisha yako,furahia maisha yako,heshimu maamuzi yako katika maisha,sikiliza hisia za moyo wako...Fikiri kuishi maisha marefu yenye thamani kwa wengine.Kila ukutanapo na watu,wafanye watambuae nuru ya Mungu iliyo ndani mwako...ing'ae kwao,nao wajifunze kutoka katika nuru hiyo,na kuwafanya nao pia waishi maisha yao halisi yenye thamani kwa wengine....Wathamini wote,wageni kwa wenyeji...Kila uamkapo tafakari thamani yako na nafasi uliyonayo kutenda makubwa zaidi..shukuru kwa siku mpya,Kama hutaona sababu ya kushukuru,basi ndani yako hujautambua mwanga,na utaidanganya nafsi yako mwenyewe..: Na pale wakati wako wa kuyaendea maisha mengine mapya hutapatwa na woga,wala wasiwasi juu ya yajayo.....usiogope kama wale ambao kifo kikiwajia hujaa hofu na kuomba muda kidogo wa kutekeleza yale ambayo hawakuyatilia maanani pale waliposukumwa na mioyo yao kutenda...Kumbuka wimbo wako...wa kumkaribisha rafiki yako,atakayekupokea katika maisha mapya,kifo...kisha aga dunia kwa furaha,kwa sababu uliishi vema..kishujaa.

Tuesday, December 4

IAMBIE NAFSI YAKO

 Tumeumbwa na kupewa mamlaka juu ya maisha yetu na juu ya kila kilicho juu ya nchi,Hivyo tunapaswa kukumbuka kuwa kila kitu tunachokihitaji maishani mwetu kipo katika uwezo wetu tuliopewa na Muumba...mradi tu ulihitaji jambo hilo kwa dhati kabisa toka moyoni mwako....
Kwa kutambua hilo huna sababu ya kuwa na wasiwasi juu ya maisha na juu ya kesho....iambie nafsi yako kwa dhati kabisa toka moyoni yakuwa Unaweza.
Unaweza kuwa imara kuliko hofu uliyonayo,
Unaweza kabisa kuwa na afya bora,furaha na amani,
Unaweza pia kuwa sababu ya vyote hivyo kwa wengine,
Unaweza kuwafanya wengine watambue kuwa wao ni nuru,nao wanapaswa kuifanya nuru hiyo iangaze wengine
Kuafanya wayatazame maisha katika upande wa mwangaza

Iambie nafsi yako kuwa,
Unaweza kubadili maisha yako na kuyafanya kuwa nuru,
Unaweza kufikiri chanya na kutenda kwa uwezo wako wote
Kuwa chachu ya mabadiliko chanya duniani,na kuwa mfano wa kuigwa

Iambie nafsi yako yakuwa unaweza kusahau yaliyopita,
ambayo yalikusababishia maumivu,na kuishi maisha yenye furaha na matumaini,ukianza upya bila woga,
Unaweza kuwapenda na kuwajali wengine pasipo kutazama maumivu ama mabaya waliyokutendea
Unaweza kusimama imara hata katika nyakati za magumu mengi
        furaha ni pale unapotumia maisha yako kuwa furaha kwa wengine-unaweza kuwa chachu ya upendo na anani


Sema kwa nafsi yako kuwa unaweza
Kuishi bila kusengenya na kuwanenea wengine kwa ubaya,bali unaweza kuwa faraja kwa watu wote,
Iambie nafsi yako kuwa wewe ,ukiwa kama nafsi huru,
Una jukumu la kutenda hapa duniani,
Iambie nafsi yako itazame kwa kina,
Ichunguze umuhimu wa maisha yako hapa duniani
Na kisha kuamua kufanya dunia kuwa sehemu ya upendo