Bila shaka kila mmoja yu na furaha siku ya leo.Karibu tena katika somo jipya leo hii.Somo hili litakufanya utambue jinsi wewe ulivyo muendeshaji wa maisha yko,ni somo litakalokufanya ujue kuwa wewe ndiye mjenzi na ndiye unayebomoa maisha yako mwenyewe,iwe kwa kutambua ama kutotambua.Karibu tujifunze pamoja
Ni mara nyingi tumekuwa tukikumbushana kuwa Mungu ametuumba kwa mfano wake,kwa kutupatia uwezo wa kutenda kama yeye.Naye hujidhihirisha kuwepo kwetu kwa njia ya upendo,ni sawa na kusema upendo ni Mungu ndani yetu.Upendo ni nuru ya Mungu iliyopo ndani yetu.Hivyo kila jambo litendwalo kwa msukumo wa upendo hufanya nuru ya Mungu iliyopo ndani yetu hung'aa.
Upendo ni nuru,kama nilivyoeleza hapo juu.Kinyume chake ni chuki,ama
giza. Kila tutendapo jambo kwa chuki,basi nuru huzimika ndani yetu na
linabaki giza
|
Upendo ni nuru iliyo ndani ya mioyo yetu,kila tutendapo kwa upendo maisha yetu huwa nuru kwa wengine | (picha kwa msaada wa mtandao) |
Giza ndani ya mioyo yetu hutokana na kutoweka kwa mwanga,yaani kutenda pasipo upendo.Inamaanisha visasi,migogoro,ugomvi....yote hii huipoteza nuru iliyopo kwako.Ama kwa kutambua na kutotambua,unayajenga maisha yako kwa uchaguzi wako mwenyewe,ambao hutokana na kutenda kwa upendo ama kinyume chake (giza).Ni sawa na kusema tunayafanya maisha yetu kung'ara ama kufifia kwa maamuzi yetu wenyewe.
Atandaye kwa upendo hulipwa upendo.Moyo wake hujawa furaha na hivyo hufungua njia ya mafanikio katika kila jambo alipendalo.Huamsha mwili wenye uchangamfu na uso uliojawa bna furaha na amani.Nuru yake hung'aa daima.Hata siku zake za kuishi hapa duniani zinapokwisha,huenda kwa amani.Nuru yake huendelea kung'aa vizazi hata vizazi.Mifano ipo mingi
Mfano wa kwanza ni ule wa Yesu,Kristu (mnazareti).Huyu alifanya kila jambo kwa kusukumwa na upendo.Alitoa maisha yake kwa ajili ya wengine.Alifundisha upendo kwa kutenda na kuuishi.Akawa faraja kwa wote ambao walikuwa hawathaminiki katika jamii.Hata alipoondoka,wengi wa wafuasi wake na wasio wafuasi wamezidi kumkumbuka,na hata sasa wanaozaliwa baada yake hukumbuka na kumtambua kwa kupitia matokeo ya upendo .Wengine ni wengi ambao tumekuwa tukiwasikia ama kupata kuwaona katika jamii yetu.
Kutenda kwa upendo humaanisha kujali,kuthamini wengine.
Sisi ni wa thamani kwa sababu Mungu yupo ndani yetu.Hivyo kila unapojitazama na kujikumbusha thamani yako,kumbuka ya kuwa kila anayekuzunguka ana thamani sawia na ile uliyonayo,hivyo kila utendalo kwa wengine,umejitendea wewe.Unapotenda kwa upendo kwa wengine,umejitendea wewe,vivyo hivyo,unapotenda kwa wenako kwa chuki,basi umejitendea mwenyewe.
|
Upendo ndio lugha ya pekee inayounganisha viumbe wote duniani(picha kwa msaada wa mtandao) |
Hivyo kwa maelezo hayo juu,tunajifunza kuwa sisi tunajenga ama kubomoa maisha wetu wenyewe kwa uchaguzi tunaoufanya wenyewe.Katika kila huduma unayoitoa,iwe ni elimu,biashara..ukitenda kwa upendo unafanikiwa.Ukitoa huduma kwa chuki unadidimiza mafanikio yako mwenyewe,iwe kwa kutambua hilo ama kutotambua.Chukua mfano unafanya biashara;wanapokuja wateja unawachangamkia kwa furaha na upendo..ukiwahudumia vema na kuwapa ushauri mzuri na ukatenda kinyume chake,ni lipi kati ya matendo hayo juu itakuletea mafanikio?
|
Nuru ya Mungu iliyopo ndani mwetu haifichiki kamwe,viumbe vyote duniani huvutiwa na nuru hiyo |
Tunapokianza kipindi kipya katika mpangili wa miaka,tukumbuke kuwa tutahesabu mafanikio ama kutofanikiwa katika malengo yetu kwa kuchagua wenyewe,nuru ama giza
Kuna furaha kubwa kwa wale wanaouchagua upendo,furaha huwa daima maishani mwao,na daima nuru ya Mungu iliyo ndani mwao hung'aa daima na kuwafanya wengine wajifunze toka kwao.Heri ya maandalizi ya kipindi kipya cha mwaka 2013.
Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
Related Posts:
JITAMBUE