Mafanikio huanza pale unapoacha kuogopa na kuanza kuchukua
hatua,yanaanza pale unapoacha kulaumu wengine juu ya matatizo yanayokukabili wewe,
ambayo ukweli ni kwamba wewe ndiye msanifu mkuu.Yanaanza pale unapoacha kuogopa
mazingira na kutafuta visingizio,na kuanza kuyatazama mazingira kama nafasi ya
kwenda mbele na kuyatumia vema.Ni pale unapotafuta kuzigundua mbegu na nguvu
zinazoendesha maisha yako na kugundua kuwa zipo ndani yako,na
kuzitumia,ukichukua hatua juu ya kila mipango na malengo uliyoyaweka maishani
mwako
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa