MWANAMKE-FURAHA ITOKAYO MOYONI-CHIMBUKO LA UPENDO |
Ni miaka mingi imepita toka palipoingia mfumo wa kundamizi kwa wanawake.Mfumo huu umemfanya mwanamke kudharaulika ,matokeo yake wanawake wenyewe wamekubaliana na mfumo huo bila kutambua.Nilipata kueleza jinsi mazingira tunayoyaishi yanavyoweza kupelekea kubadili fikra za mtu,hasa pale akiwa hatambui kuwa yeye ndiye anayepaswa kuyatawala mazingira.Wanawake wamekumbwa na mfumo huo.Mtu binafsi anapoukubali mfumo Fulani,huuona ni wa kawaida na hata kuuishi na kuusifia,asijue athari zake katika ujenzi wa maisha yake.
Mfumo huu kandamizi,umeonekana kuwa ni usahihi.Dini pia
zimeingia katika kuuchagiza mfumo huu.Mara kadhaa zikifundisha ama kuwajengea waamini wake fikra kuwa kuwa mwanaume yupo juu ya
mwanamke.Wanaume wanaamini kuwa kuwa na nguvu ni kumtawala mwingine badala ya kuyatawala
mazingira na hivyo maisha ,wanafikiri kuwatawala wanawake.Wanaume wamekuwa
wakijisifia kwa kuzaliwa jinsia ya kiume.Wamekuwa wakitoa maneno ya kejeli na
dhalili dhidi ya jinsia ya pili(mwanamke).Mfumo huu ukakua na ndipo jinsia ya
kike ilipoanza kutazamwa kuwa si bora.Ukweli ni kwamba hakuna jinsia iliyo bora
kuliko nyingine.Kila jinsia ni bora jinsi ilivyo pasipo kusahau kuwa kila jambo
huwa lina upekee wake.
Miaka ya hivi karibuni umeingia mfumo wa utandawazi.Mfumo
ambao mifumo ya ,mawazo,uchumi,utamaduni inalengwa kufanywa kuwa sawia.Ni mfumo shindani ambao wanaoweza kuyatawala mazingira yao,wanafaidika
kuliko wale wasiojitambua.Mfumo huu umewaathiri pia wanawake.Tumeshihudia
wanawake wakivaa mavazi yanayoonesha sehemu zao nyeti,wakicheza picha za ngono
na kudhalilishwa.Wanawake wanaonekana kuwa ni chombo cha starehe na dhalili.Kwenu
ninyi wanawake,mnapaswa kuchukua hatua,kujitazama upya,mnawaza nini kila mmoja
dhidi yenu wenyewe? Je mpo tayari kutumika kama msio na thamani kwenye
matangazo,sinema na kwenye mawazo ya wanadamu wote? Je mpo tayari kujenga dunia
duni yenye dhiki,chuki na isiyo na uelekeo?Mpo tayari kuendelea kutazamwa kuwa hamuwezi?
Leo ningependa wanawake waamke na kuvumbua siri kubwa ndani
mwao.Hakuna wa kuchukua hatua ni ninyi wanawake,kila mmoja kwa nafsi yake.
Ninyi ni wa thamani.Ni zaidi ya sura zenu,zaidi ya maumbile yenu.Ni zaidi ya
mavazi mnayovaa.Uzuri wa mwanamke ni nuru iliyopo ndani mwake inayoangaza dunia
kwa upendo.Ni nuru anayosubiria itumike kuimulika dunia,kuifanya kuwa sehemu
bora ya kuishi.
Ni nuru hiyo iliyo ndani mwenu ambayo ikiruhusiwa kutolewa
huzaa upendo,amani,usawa,haki na chemchem zote za upendo.Anayetambua ni yule
aliye tayari kuchimba ndani mwake na kugundua kuwa kama mwanamke, anaijenga na
kuibomoa dunia kadiri ya matumizi ya uwezo aliopewa.Uwezo wenu upo ndani
yenu.uzuri wenu upo ndani mwenu na si kwenye mavazi na maumbile tu.Uzuri huo
ulio ndani mwenu,unapotumika hutoa matokea yanayotoa picha ya uzuri wenu,yaani
Upendo.Kichwani mwenu na moyoni mwenu mmebeba hazina kubwa.Ninyi ni bora,zaidi
ya mwili unaoonekana,zaidi ya idadi ya namba,idadi ya nyota..
Wanawake ni viumbe muhimu katika dunia hii.Ndio wazazi wa
kila jambo katika dunia hii. Ni chumbuko
la wema na upendo hapa duniani.Kupitia mwanamke binadamu wanazaliwa.Wakombozi
wa fikra,wapigania haki,wahimiza upendo,wapigania amani wote wametoka kwa
mwanamke.
Mungu alimuumba mwanamke na kumuwekea uzuri wa kila namna ndani mwake,ali kila apitiaye tumboni mwa mwanamke aubebe uzuri huo na kuuishi hapa duniani.Katika kipindi chote aishipo akikua tumboni mwa mwanamke,kiumbe anayetarajiwa kuzaliwa hubewa chemchem ya kila kitokacho kwa mama.Hivyo mwanamke anahusika katika kuijenga dunia iliyo bora.Ule usemi wa kuwa ukimuelimisha mwanamke,umeielimisha jamii,ni sahihi..kinyume chake pia ni sahihi.
Mungu alimuumba mwanamke na kumuwekea uzuri wa kila namna ndani mwake,ali kila apitiaye tumboni mwa mwanamke aubebe uzuri huo na kuuishi hapa duniani.Katika kipindi chote aishipo akikua tumboni mwa mwanamke,kiumbe anayetarajiwa kuzaliwa hubewa chemchem ya kila kitokacho kwa mama.Hivyo mwanamke anahusika katika kuijenga dunia iliyo bora.Ule usemi wa kuwa ukimuelimisha mwanamke,umeielimisha jamii,ni sahihi..kinyume chake pia ni sahihi.
Dunia tuliyonayo sasa,mwonekano wake,matukio na kila
tukipatacho,ni matokeo ya usanifu wetu wenyewe.Ni matokeo ya mwanamke na
mwanamume,mwanamke akihusika kwa kiasi kikubwa.Chuki zilizopo,matabaka
yaliyopo,visasi,mauaji ni matokeo ambayo yameanza katika dunia isiyoonekana
iliyopo ndani mwetu,na kisha tumeijenga katika mwonekano uliopo.
Ukandamizaji wa wanawake ,na udhalilishaji unatoa matokeo ya
jamii kandamizi na dhalili.
Wanawake mnayo nafasi ya kujenga dunia mpya.Inayoanza ndani
mwenu.Ubikira wenu (ukamilifu ndani mwenu) utumike kuimulika dunia,kuwa sehemu
bora.Mwanamke akiutambua ubikira ndani mwake,maajabu makubwa ya mabadiliko ya
maisha yake huanza,Maisha mapya,bora hutokea.Wanawake amkeni.
Kila mmoja wenu akiamka,mtaamsha dunia mpya.Tuanze kuwafunza
watoto wetu juu ya thamani yao.Waanze kuthamini hazina walio nayo ndani
mwao.Washeni mishumaa iliyo ndani mwenu,iimulike dunia kwa upendo.Mulikeni muondoe
mtazamo mbaya wa jamii juu ya mwanamke.Jukumu ni lenu.Nguvu mlionayo
haijapotea,kinachohitajika ni kuiamsha.Licha ya magumu mtafika.
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa