Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Thursday, January 31

BINADAMU NA USANIFU WA MAISHA YAKE


fikra ni mbegu ya kile unachotarajinayo hutoa sawia na kilichopandwa
                                   
Nimeamua kuandika makala hii kujadili jambo muhimu sana,na endapo utachukua nafasi kujifunza na kusoma mara kwa mara utatambua mambo mengi
Mwisho wa makala hii utatambua mambo yafuatayo
        I.           (a)  Wewe ni mjenzi na mbomoaji wa maisha yako
      II.           (b)  Mazingira yanayokuzunguka ni matokeo ya fikra zitokazo ndani mwako
    III.            (c) Jinsi gani unaweza kubadili maisha yako.
    IV.             (d)  Dunia mpya.
Mara nyingi tunapomuona mtu akifanikiwa katika biashara tunasema ana bahati’ama kismati’.Tunapomuona mwenzetu akifanya vizuri katika elimu tunasema Mungu amembariki na kumpa akili nyingi,TUKIONA WENGINE WAKIFANYA UGUNDUZI tunasema ‘ana akili nyingi’.Hatutakumbuki jambo moja,ya kuwa kuna magumu wanayoyapitia watu hawa mpaka kufikia mafanikio lakini kubwa zaidi ni kwamba kabla ya matokeo hayo,walianza kufikiri,kisha wakaweka nia ili kutimiza malengo hayo ambayo sasa yanaonekana wazi.
Ukiona simu,kumbuka kuwa aliyetengeneza alianza na fikra juu ya mawasilano,akafanya juhudi mpaka kufika hapo.Ukiitazama TELEVISHENI,Kumbuka kuwa haikugunduliwa kwa bahati mbaya bali ilianza na mtu kufikiri.Ukiona kuna uoto mzuri nyumbani kwa mtu,si kwamba ulitokea kwa bahati mbaya,ulianza na wazo ndani ya muhusika,kisha akafanya juhudi kutekeleza.
Kila unachokiona ,unachokitumia ni matokeo ya fikra za watu na wewe ukiwa mmoja wao.Marimba,Kinanda,kijiko,sahani,gari,baiskeli na vingine vingi vijavyo ni matokeo ya fikra za wanadamu.

Hakuna jambo hata moja ama ugunduzi wowote uliojitokeza katika mazingira rahisi,fikra ilianza kufanya kazi,ikasukuma hamu ya kufikia ndoto hizo,na mwisho wa siku..jambo lililokusudiwa linatimia

Kujenga maisha yako kunaanza na fikra zako.Unapata kadiri unavyofikiri.Unapoweka fikra juu ya jambo,unapata matokeo yake kadiri unavyofikiri.

Huwezi kutenganisha kile kilichopo ndani ya fikra za mtu na kile akitendacho ama ambacho kinaonekana.Kinachoonekana ,ni matokeo ya fikra za mtendaji.Vivyo hivyo huwezi kutenganisha kati ya ulimwengu wa kiroho na  ulimwengu unaoonekana kwa macho..Uonekanao kwa macho ni matokeo ya ule wa kiroho (usioonekama kwa macho).Katika elimu ya Saikolojia unaweza kupima  fikra na tabia kwa kutazama matokeo ya mambo yanayotendwa na mtu .

Mazingira bora ya kuishi hayatokei kwa bahati mbaya,yanajengwa na fikra (mtazamo).Mtazamo chanya huyajenga,nao mtazamo hasi huyabomoa.Hivyo ni wazi kuwa unapotaka kupata mafanikio katika jambo lolote,unaanza na fikra chanya juu ya jambo hilo,Jifunza kutazama kila jambo katika mtazamo chanya. Kila mmoja wetu ana ndoto ( matarajio ) ya kufnya jambo Fulani maishani,na kuwa mtu Fulani maishani…Unachokiwaza ndicho kitakachotokea katika uhalisia.Fikra ni mbegu ya kuelekea mafanikio.Ukipanda mbegu ya fikra chanya,utavuna kama ulivyopanda,vivyo hivyo ukipanda hasi,utavuna ulivyopanda.Ukiona vyaelea ,vimeundwa.
                                  UNAWEZA KUBADILI MAISHA YAKO
ni wewe ndio uliye msanifu wa maisha yako
                                
                                        
Kwa maelezo hayo ,unaweza kubadili maisha yako kwa kubadili fikra zako.Unaweza ukawa katika mazingira magumu sana,lakn kamwe hutabaki hivyo kama utaanza kuwaza vyema,fikra za mafanikio,upendo,amani zinakupelekea kwenye matokeo chanya
Mawazo uwazayo juu yako ni kipimo unachojipimia katika mwenendo na matokeo ya maisha yako.Matokeo yake kamwe hayajifichi.Hatuchagui mojakwa moja juu ya mtiririko wa maisha yetu,lakini kupitia fikra,tunachagua matokeo ya maisha yetu na kuujenga mtiririko wa maisha yetu.
Fikra huonekana matokeo yake haraka kwenye tabia,na tabia huleta matokeo ya maumivu ama furaha (majuto ama furaha).Kwa kifupi tabia uliyonayo,iletayo matokeo yake ya majuto ama furaha ndiyo inayotoa picha ya fikra iliyotoa msukumo wa matokeo hayo..

Fikra yenye woga,wasiwasi,na kutowajibika huonesha tabia ya unyonge , kutojiamini na kutochukua hatua,matokeoa yake ni kukata tamaa, kushindwa na kuwa tegemezi kwa kila jambo.

Nazo fikra  yenye uvivu hupelekea tabia za udhaifu/unyonge, udanganyifu(usanii sanii) na matokeo yake ni kuwa ombaomba,masikini na uzembe.(ukiona nchi ina kila rasilimali,na inakuwa masikini,basi ujue watu wake wote ni wavivu kufikiri na wasipobadili fikra hizo watabaki kuwa ombaomba hata kama matrilioni ya pesa yatatolewa kama msaada)

Fikra za chuki na kutojiamini huleta tabia za visasi na uonevu,matokeo yake ni vurugu,kutoweka kwa amani,mauaji ya kutumia nguvu.Unaweza kujifunza matokeo ya viongozi wasiojiamini na wenye chuki.

Fikra za ubinafsi (umimi) huleta tabia ya ushindani,unyang’anyi,(roho mbaya tunaita waswahili).Na matokeo yake kila mmoja anayajua.
Kwa upande mwingine fikra zote njema  huleta matokeo mema kwa watu wote.
Fikra za kutia moyo,kujiamini na kuchukua hatua huonekana katika tabia za utu wema na kuwajibika,matokeo yake ni amani,mafanikio na uhuru wa kweli.
Huwezi kuwa huru mpaka utakapokuwa na fikra huru.Ukifahamu jinsi unavyoweza kubadili maisha yako kwa kubadili fikra zako…umeyafikia mafanikio
Mkononi mwako ni matokeo halisi ya kile ukiwazacho….maisha yako unayoyaishi sasa ni matokeo halisi ya fikra zako,kwa kutambua ama kutotambua.Unavuna ulichopanda.Hakizidishwi wala kupunguzwa.Ukiachilia mbali hali uliyonayo sasa,unao uwezo wa kubadili maisha yako…ama kubaki ulivyo.Hii ni kwa kupitia mawazo yako mwenyewe. Utarudi nyuma kama mawazo yako yanavyotaka,ama utasonga mbele kama mawazo yako yanavyotaka.Mawazo hutoa msukumo moyoni.Msukumo huo huleta matokeo sawia.
Kama utasubiri mazingira ya mafanikio yako yajengwe na mtu mwingine(wengine) basi utasubiri mpaka mwisho..Ni wewe na wala si mwingine wa kuchukua hatua.Juhudi  huleta matokeo.Kiwango cha juhudi unayoiweka,kinatanabaisha juu ya matokeo yake. Fikra unazozijaza katika mawazo yako,msukumo unaouweka moyoni mwako ndio ujengao maisha yako,na ndivyo utakavyokuwa.

                                                    DUNIA MPYA
                Dunia mpya ni matokeo ya fikra zako mpya.Dunia mpya ni ile inayojengwa na wale wanaoamini katika uwezo walionao.Dunia tunayoishi sasa,mazingira yake,hali yake ni matokeo ya fikra zetu wanadamu.Kuongezeka kwa joto,kutoweka kwa amani na upendo,uchoyo,wivu ni matokeo ya binadamu yaliyoanza muda mrefu.Dunia mpya yenye amani,furaha,upendo,usawa,hali bora inajengw na sisi ,kila mmoja akichukua hatua juu ya fikra zake na maamuzi yake.Mimi binafsi naiona dunia mpya,yenye amani na furaha,upendo na maelewano,dunia hii itajengwa na watu wenye fikra za usawa,upendo,umoja baada ya dunia inayojengwa na wenye chuki na matabaka kushindwa.Love never fail

Sunday, January 20

KANUNI YA MAFANIKIO MAISHANI

Kutekeleza majukumu yote kwa uaminifu na bila shuruti..kujiamini katika Kila ukifanyacho binafsi na ktk maamuzi ya jumuia..
Kuwa na moyo wa imani kuwa unao uwezo wa kufanya kitu kipya chochote unachokidhamiria hata kama wapo wameamini ya kuwa haiwezekani...
Kuwa na tumaini moyoni mwako na kuwa kioo kwa wote wanaokuzunguka..
Uwe na moyo wa kujitolea kila wakati...kupenda na kuwajali wote na kwa maana hiyo kuufundisha upendo kwa wengine...
Jiamini na kupigania imani yako.
Kuwa tayari kutenda kwa wema kwa wengine,na kujifunza na kutoa kwa wale wenye mahitaji..
Jitolea kwao pasipo fikira na malengo ya kujipatia ama sifa ama zawadi yeyote.
Jiamini na kutenda na kufikiri kwa mfano wako wa kipekee bila kupotoshwa ama kutegemea fikra na njia za watu,kwani hizo zitakupeleka ktk matokeo yao,bali sikiliza sauti iliyo moyoni mwako ili maisha yako yawe ya mfano kwa watu wote,na kwa kufanya hivi utawaafundisha wengine kujitambua na kuishi maisha yao yasiyo ya bandia.. Waunge mkono wote wenye kuhitaji,fundisha kila jambo unalofahamu kuwa ni la manufaa ...Amina

Thursday, January 17

FIKRA ZAKO NA MATOKEO YAKE


fikra za kila mtu hazijifichi,matokeo yake huleta tabia,tabia huleta matokeo hasi ama chanya(picha ya Hayati  baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere)

Fikra ni sawa na mbegu ndani ya maisha yetu..Unapopanda mbegu kwenye udongo,matokeo yake huota kile ulichokipanda,kama umepanda mahindi,utavuna mahindi.Vivyohivyo ,jinsi unavyofikiri(unavyowaza),unapanda mbegu katika mitazamo na mienendo  ya maisha yako na matokeo yake huonekana sawia na fikra zako.

Ni wazi kuwa huwezi kupanda mahindi ukavuna machungwa,vivyo hivyo huwezi kupanda mbegu itokanayo na fikra za kushindwa,umasikini,huzuni,kisha ukapata matokeo ya  maisha mazuri,furaha na amani.Hivyo ni wazi kuwa ukitaka jambo jema litokee,anza kupanda kwanza fikra za wema(jambo hilo).Ukitaka kupata matokeo mazuri katika mahusiano anza kwanza kupanda mbegu ya mtazamo chanya juu ya mahusiano,upendo na furaha.Kama matarajio yako ni kuona dunia yenye mazingira mazuri na bora kwa viumbe wote,anza kwanza kupanda fikra ya wema na kujali viumbe wengine.Ukitaraji kuona mwenzi wako ana mwenendo mwema,anza kupanda mbegu ya ushirikiano,upendo,kujali badala ya kufikiri kuwa kuna jambo nje yako wewe,ama nguvu nje yako itakayoleta mabadiliko maishani mwako.Fikiri vema juu yako ubadili maisha yako.
Muonekao wa mazingira yanayotuzunguka ni matokeo ya fikra zetu wenyewe

Mawazo uwazayo juu yako ni kipimo unachojipimia katika mwenendo na matokeo ya maisha yako.Matokeo yake kamwe hayajifichi.Hatuchagui mojakwa moja juu ya mtiririko wa maisha yetu,lakini kupitia fikra,tunachagua matokeo ya maisha yetu na kuujenga mtiririko wa maisha yetu.

Mazingira huchangia sana binadamu kuwa na fikra Fulani juu(dhidi) yake.Mfano,mtu aishiye katika mazingira ambayo ni ya kipato cha juu,fikra zake huwa mara nyingi si za kushindwa jambo tofauti na aliye katika mazingira yenye vikwazo vingi.Anayepita kwenye magumu mengi,anapojitambua huweza kufanya mambo makubwa kuliko aliyeko kwenye mazingira yasiyo na vikwazo vingi kwa sababu huanza kuwa na fikra za ushindi.
Tunapofikiri hasi juu ya maisha yetu,tunapata matokeo hayohayo.Tunapofikiri chanya na kuchukulia kila jambo ama mazingira kama nafasi,matokeo yake ni kukua zaidi na kusonga mbele.Tunachokipata maishani ni matokeo yenye uasilia ndani mwetu na si nje yetu.Tabia za marafiki ulionao ni picha ya tabia ulionayo wewe.Matokeo ya mafanikio ama kutofanikiwa kwa wewe na unaowaongoza ni picha ya fikra ulizonazo pamoja na unaowaongoza.
Ukijitazama kwenye kioo,unaiona sura  yako.Kama una makovu,si tatizo la kioo,ni uhalisia wa jinsi ulivyo.Tabia unazoonesha nje,ni picha halisi ya fikra zako ndani mwako.
Unaweza kujifunza fikra,tabia na mienendo ya jamii kwa kuangalia matokeo yake.Jamii yenye umasikini,maradhi na ujinga ni picha halisi ya fikra zao,elimu yao na mitazamo yao.Ukiona katika jamii wapo watu wanaopenda kutembea wakiwa nusu uchi,ni picha kamili kuwa wengi wa wana jamii hiyo wanapenda tabia hiyo.Mbuzi hawezi kuzaa kondoo,na kinyume chake ni sawia.
Wapo wanaodhani  kuwa fikra alizonazo mtu huweza kuwa siri.Ukweli ni kwamba matokeo ya matendo yako,ni matokeo ya mawazo yako.Fikra zetu huonesha  matokeo sawasawa na msukumo wake.Anayefikiri dunia ni sehemu mbaya,huishi akiishutumu dunia siku zote.,Anayefikiri watu wanaomzunguka ni kikwazo kwake,huishi daima ikawaona kuwa ndio sababu ya matatizo yake.Fikra huonekana matokeo yake haraka kwenye tabia,na tabia huleta matokeo ya maumivu ama furaha (majuto ama furaha).Kwa kifupi tabia uliyonayo,iletayo matokeo yake ya majuto ama furaha ndiyo inayotoa picha ya fikra iliyotoa msukumo wa matokeo hayo..

Fikra yenye woga,wasiwasi,na kutowajibika huonesha tabia ya unyonge , kutojiamini na kutochukua hatua,matokeoa yake ni kukata tamaa, kushindwa na kuwa tegemezi kwa kila jambo.

Nazo fikra  yenye uvivu hupelekea tabia za udhaifu/unyonge, udanganyifu(usanii sanii) na matokeo yake ni kuwa ombaomba,masikini na uzembe.(ukiona nchi ina kila rasilimali,na inakuwa masikini,basi ujue watu wake wote ni wavivu kufikiri na wasipobadili fikra hizo watabaki kuwa ombaomba hata kama matrilioni ya pesa yatatolewa kama msaada)

Fikra za chuki na kutojiamini huleta tabia za visasi na uonevu,matokeo yake ni vurugu,kutoweka kwa amani,mauaji ya kutumia nguvu.Unaweza kujifunza matokeo ya viongozi wasiojiamini na wenye chuki.

Fikra za ubinafsi (umimi) huleta tabia ya ushindani,unyang’anyi,(roho mbaya tunaita waswahili).Na matokeo yake kila mmoja anayajua.
Kwa upande mwingine fikra zote njema  huleta matokeo mema kwa watu wote.
Fikra za kutia moyo,kujiamini na kuchukua hatua huonekana katika tabia za utu wema na kuwajibika,matokeo yake ni amani,mafanikio na uhuru wa kweli.
Huwezi kuwa huru mpaka utakapokuwa na fikra huru.Ukifahamu jinsi unavyoweza kubadili maisha yako kwa kubadili fikra zako…umeyafikia mafanikio…usikate tamaa.

Monday, January 7

WAKATI NI SASA


Ulishawahi kujiuliza ni lini unasubiri ,ama ni lini umeamua kuanza kutimiza yale ambayo umepangilia kuyafanya maishani?Umewahi pia kujiuliza  ni lini malengo yako yatatimia?
Kama unatambua kuna sababu ya wewe kuishi hapa duniani,unasubiri nini kutenda kadiri moyo wako unavyokutuma?Unasubiri kesho,kesho kutwa,mwisho wa mwezi ,ukihitimu masomo,ama unasubiri umri wako ufike miaka kadhaa?
Ipo siku hutakuwa na uwezo wa kutenda chochote,hutakuwa na nafasi ya kutenda kile ulichokuwa kutimiza,na wakati huo ndipo utakapokuwa na majuto ni kwa nini hukutenda pale ulipoweza.
Hakuna muda mwingine zaidi ya sasa.Matokeo ya mambo yote yajayo hufanywa na maamuzi ya wakati uliopo.AMUA sasa.Amua kuanza kuishi maisha uliyoyakusudia sasa.
Utatambua kila kitu juu ya maisha yako ukianza kuchimba ndani yako sasa.Anza kusikiliza sauti iliyopo ndani mwako sasa.Usisubiri mwisho,fanya kwa bidii sasa.Badili maisha yako na ndoto zako zote kuwa halisi sasa.Usisubiri hatari ya kusubiri kesho,baadae….Mavuno ya baadae ni matokeo ya kupanda sasa

Saturday, January 5

ATHARI ZA MSUKUMO WA WANAOKUZUNGUKA

Watu wanaotuzunguka hutusukuma kufikiri na kutenda kadiri ya kanuni  na imani zao na kutufanya kuwa watumwa wa fikra za kimitazamo(picha na www.nlm.nih.gov)

Nilikwisha kujadili ni namna gani mafanikio ya mtu yanaanza ndani mwako,   soma zaidi hapa
Katika makala hiyo,tunajifunza kuwa kila jambo huanza na wewe.Chochote kinachoanza na msukumo utokao ndani yako,ndilo linaloleta mafanikio.Kwa kifupi tu mafanikio ya mtu yanaanza na yeye mwenywe na si msukumo utokao nje yake yeye.

Leo tutajadili jinsi msukumo wa nje (toka kwa marafiki,ndugu na wote wanaokuzunguka unavyowezakuathiri upekee wako na maamuzi.

Tumejifunzapia kuwa kila mmoja ni wa kipekee kwa maana ya nafsi yake na atasimami katika maamuzi yake na ujenzi wa maisha yake.Lakini tunaishi katika jamii ambayo inatutia msukumo wa kuamua na kutenda kadiri ya mawazo na kawaida yao.
Kabla hujazaliwa walikwepo waliotutanguli,kwa maana ya babu zetu na wengine wengi waliopita.Hawa walitengeneza mfumo yao ya maisha  ambayo tunaweza kuuita mfumo wa jamii,ambao ulijenga matarajio mengi ya watu mmojammoja  na jamii nzima.Mfumo huu ni pamoja na kanuni,mila ,desturi,imani,dini,serikali,sherehe.Mfumo huu umejengwa na sheria na kanuni nyingi ambazo unapozaliwa tu,unakuwa umefungwa moja kwa moja na mfumo huo pasipo kupenda ukiamini ndio mfumo sahihi.Sheria na kanuni zilizopo katika mfumo huu ulioukuta zinapokuwa kawaida kwako,zinaufanya mfumo wako wa tafakari uwe na uelekeo na fikra zilizo ndani ya mfumo huo.
Fikra zenye mipaka huleta matokeo yasiyo huru (picha kwa hisani ya www.rfidgeneral.com)


Mfumo huu unakulazimu kujifunza na kufuata mengi kama ni nini unapaswa kufuata,kuamini,ni nini kinakubalika na nini hakikubaliki,kipi ni chema na kipi ni kibaya.MFUMO HUU WOTE UNAKUPELEKA KUFUATILIA KILA JAMBO KADIRI YA TARATIBU NA MAWAZO YA MFUMO.Maka unapokuwa unakuwa na fikra za kimfumo kuwa jambo fulani lipo hivi tu,na hivyo mara nyingi hujenga mpaka wa kufikiri na kuamua.Unakuwa huwezi kufanya jambo mpaka usikilize waanaokuzunguka wanasemaje.
Natoa mfano wa mjomba wanguambaye pale alipotakakuoa binti ambaye walikubaliana na kupendana,alibadilisha uamuzio baada ya kuambiwa tu eti dini anayoiamini binti huyo si nzuri.Hapo dini ikawa juu ya upendo.
Pia kuna rafiki yangu mmoja alikuwa akijadili na marafiki juu ya imani ya dini nyingine,akashawishiwa kuifuata imani mpya,akakiri kuridhika na imani hiyo lakini hofu yake ikwa je,wazazi watanionaje?,licha ya kuwa yeye ni mkubwa kiumri.

Hii ni baadhi tu ya mifano.Mwisho kbisa tunaanza kuitazama  dunia kama sehemu ya ushindani.Tunajifunza uchoyo,ubinafsi,usiri na visasi kwa sababu ya mfumo licha ya kuwa yapo mengi mazuri.

Ushindani huo unatufanye tufikiri na kutenda kwa kuangalia mitazamo ya jamii.Unakuwa huna fikra za kutafakari jambo nje ya mipaka ya jamii.HIVYO unakuwa si huru katika maamuzi juu ya maisha yako mwenyewe.Kwa kifupi unakuwa mtumwa wa mfumo huu wa jamii.,ukifikiri na kutenda katika uwanja wa fikra za jamii.Ukweli ni kwamba usipotoka katika mpaka huu na kuuvuka,kuwa huru,hutaishi kamwe maisha yako halisi.
Maisha yetu ni matokeo ya fikrazetu (picha kwa hisani ya mtandao)


Ninachotaka kukisema hapa ni kuwa ukitaka kuishi maisha unayoyachagua wewe ,na kufikia mafanikio ni lazima uchukue uamuzi wa kufikiri nje ya mipaka ya mawazo ya jamii.Ni lazima uvunje mipaka ya mazoea na ile ya sheria na kanuni za imani ya jamii.Ni lazima ujifunze kuwa huru.Naomba nieleweke vizuri hapa si kwamba nahamasisha watu wavunje sheria za nchi ama mahalia,laaah,kuvunja mazoea ni kufikiri kwa mapana bila kufungwa na mawazo yanayoaminika tu na jamii.


Imani ya jamii ina nguvu sana,na hujenga upotofu ya kuwa tunapaswa kufikiri hivi na si vile,fulani yupo hivi na vile na inamsukuma mtu kutenda kadiri ya fikra za jamii husika.Tunalazimika kuishi maisha ya bandia ili tuonekane kwa wengine(Amini nakwambia utakuwa mtumwa katika mawazo mpaka pale utakapopanua wigo /uwanja wako wa fikra).

Unakuta jamii inaamini juu ya ushirikina na uchawi katika kutafuta mafanikio,hivyo kunakuwa na imani kuwa huwezi kufanikiwa mpaka uende kwa mganga.Watoto wakiugua magonjwa mabayo ni matokeo ya maisha anayoishi basdi inaaminika amechezewa(amelogwa).Tukumbuke kuwa mtu hawezi kukutendea ubaya  kama wewe si kisababishi cha fikra za mtu huyo kukufanyia ubaya.Nakumbuka kuna rafiki yangu ambaye nilisoma pamoja nae,alikuwa namsukumo sana kwa wengine,akiwaaminisha kuwa ili uwe bora na rafiki yake ni lazima uwe unakunywa pombe ama kuzisifia.Hii yote ni matokeo ya imani na fikra za kimfumo.

Hivyo tukumbuke kuwa kama tunaishi tukifikiri na kutenda kwa mipaka ya imani za wengine,basi sisi ni watumwa wa imani hizo mpaka pale tutakapotoka nje ya mipaka hiyo katika kufikiri na kutenda.Tunatafuta kukubaliwa na mawazo na mitazamo ya vikundi fulani.Tukumbuke kuwa picha halisi juu ya kinyago huwa sahihi kwa mchongaji,ambaye anachonga akiwa na picha yake katika fikra kuwa nataka awe hivi.Ukiwauliza wateja wanaonunua kinyago,kila mmoja atatafsiri kadiri ya fikra zake pia.
Mabadiliko katika fikra na maendeleo yako yanaanza pale unapoanza kufikiri nje ya mipaka ya wengine(picha kwa hisani ya mtandao)


Kwa nini uishi kwa mawazo ya wengine?Kwa nini uumie unapoambiwa una sura mbaya wakati hayo ni maoni ya msemaji tu.Ukitaka kupata majibu juu ya maisha yako,chimba ndani yako..Tafuta ndani yako.Ninaamini kila jambo huanza na wewe(mimi),Utajiri na mafanikio yote yanatoka ndani mwa muhusika.Zawadi kubwa juu ya maisha yako ni kuithamini nafsi yako  na kuisikiliza sauti kubwa itokayo moyoni mwako,ikuongozae juu ya kutenda,hii ni sauti ya Mungu iletayo mafanikio,furaha na kila lililo jema.Sauti hii inakupa nguvu ya kutenda miujiza kila wakati,ndiyo inayofanya nuru ya maisha yako ing'ae.

Jamii inakufanya ulazimike kuenenda kimawazo na fikra kadiri ya imani yake.Kwa nini usikuballi jinsi ulivyo na kuanza kuchimbandani yako palipo na siri kuu ya maisha yako?Mimi binafsi natambua jinsi ninavoonekana.Najikubali kwa kuwa mimi ni zaidi ya nilivyo.Ukiachilia mbali mazingira ninayoishi na sura yangu,mimi ni wa thamani,kama wengine.Wewe ni wa thamani jinsi ulivyo,na thamani yako ni sawa na binadamu wote.Unao uwezo wa kuwa na kuishi maisha ya furaha na mafanikio.Unastahili,wewe ni Matokeo ya kazi kubwa ya Mungu. 



Sasa anza kujikubali na kuepuka misukumo ya wale wanaokuzunguka.Anza kutazama uwezo ulio nao,tazama chemchem ya mafanikio iliyopo ndani mwako.Sisi sote ni bora .Sisi wote ni wamoja.
Huu ni wakati wa kujifunza kuwa wewe,kujikubali,kukua na kubadilika.Anzakujitambua wewe kisha utatambulika kwa wengine.Hongera kwa kujitambua

Ahsante. Joseph Pongu-0717903089,0765046644.Karibu tujadiliane na kuinuana.

HATUTAMUACHA HATA MMOJA 2013


Tumejifunza mambo mengi kwa mwaka 2012,ambayo yametufanya tutambue sisi ni akina nani na kwa nini tupo hapa duniani.Tumetambua kuwa sisi ndio wasanifu wa maisha yetu wenyewe.Tumejifunza kuwa kila jambo ni jema likitazamwa kwa mfumo chanya na kuwa mambo yote yatokeayo maishani mwetu ni matokeo ya fikra zetu na vitendo vyetu wenyewe...Tumejifunza kuwa upendo ndio silaha ya mafanikio ya kila jambo,upendo ni nuru.tumejifunza pia matokeo yake ambayo ni pamoja na furaha,amani,umoja,uvumilivu na ni mafanikio.Tukajifunza pia kuwa kinyume cha upendo ambayo ni chuki ndiyo matokeo ya maumivu,wivu,visasi,chuki,masengenyo na ndio matokeo ya kila jambo liletalo hasara katika maisha yetu
SISI NI WASANIFU WA MAISHA YETU WENYEWE
 

Leo hii tutajikumbusha kuhusu majukumu yetu …Mwaka mpya ulioanza tuuutazame kwa uchanya wake.Tuanze sasa kutimiza malengo yetu kila mmoja ya kuwepo hapa duniani.Kila mmoja wetu anayo majukumu yake.Kila mmoja ana wito unaomuita ndani mwake,ana sauti ya Mungu ndani yake inayomuita kutenda kwa ajili ya wengine na kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi

Hakuna hata mmoja wetu ambaye hatayapitia magumu,kwa sababu bila magumu kutokea hatuwezi kuendelea.Mwaka huu ni mwaka wa kusonga mbele ...tutasonga mbele,hatutamuacha hata mmoja nyuma
Ni mwaka ambao mwalimu anayeishi katika mazingira magumu yenye milima mingi,ataamka kila siku na kufundisha kwa bidii na kuwanyanyua wengine wengi.Anahitajika huyo ambaye hatalalamika na kusubiri serikali(kwani serikali ni kila mmoja wetu) bali atakuwa ni mfano wa kuigwa wa mbinu bora za kutatua matatizo.Mwalimu popote ulipo amka na kutenda kwa ajili ya wengine.Amka mwalimu.

Sauti ya upendo husikika kwa viumbe vyote.Huu ni mwaka wa kuwa nuru kwa wengine(picha toka helped by animals kwa msaada wa mtandao)


Ni mwaka ambao daktari ataamka mapema na kukumbuka jukumu lake ,ya kuwa hayupo tu kwa ajili ya kutazama idadi ya wagonjwa na kiasi cha fedha,bali yupo kwa ajili ya upendo,akijali utu wa wengine pasipo kubagua hali,kabila,rangi ama hali yeyote na daima atahesabu mafanikio yake kwa kuokoa wengine,kuwainua walio kata tamaa.....na hata akitokea mtoto akaulizwa upendo ni nini,basi amtazame daktari kwa ujasiri akisema......huu ndio upendo.

Ni mwaka ambao kila anayetoa huduma kwa wengine,atatoa akisukumwa na upendo.Kila atazamapo wengine,atambue kuwa anajitazama yeye,na kuwa thamani yake ni thamani ya wengine wote.Anapowatendea wengine akumbuke kuwa anaitendea nafsi yake.Ni mwaka ambao sisi tulio binadamu tutaonesha upendo uliotukuka,utakaofanya nuru ya Mungu iliyo ndani mwetu iwaangaze binadamu engine wasiotambua upendo,ili nao waishi maisha ya upendo.
Sisi ni wamoja,sisi wote ni wana wa Mungu,tofauti zetu zimejengwa na woga ,fikra zetu


Huu ni mwaka ambao tunapaswa kuifanya dunia kuwa sehemu bora,ili nasi tuwe malaika wa dunia hii.

Binafsi jiulize utamtendea nini yule Mungiu ambaye yupo ndani mwako?Je ukiwa katika nyakati za faragha na Muumba wako,utajivunia lipi ulilomtendea?Kumbuka kuwa kama huna malengo ya kutenda jambo lolote huwezi kutimiza lolote.Ni sawa na kusafiri safari isiyojulikana,mahali na hata uelekeo!Tukiweka malengo na kuamini katika kuyatekeleza,hakika yatatimia.

Mimi binafsi najisikia faraja sana kuhamasisha wengine na kuwasaidia wengine waweze kufikia mafanikio HASA PALE WANAPOKUWA NA MSUKUMO UTOKAO NDANI MWAO.Nimejitolea kwa ajiliya wengine na wakati wote najisikia faraja.Ninapokutana na magumu,ninayashinda kwa sababu naamini katika ushindi.Sisi  tumeumbwa kushinda.,na ushindi ni matokeo ya usanifu katika fikra za kila mmoja.

Ninapata faraja ninapoona kuwa yupo nesi ambaye licha ya kwamba anaumwa,anaamka na kwenda kazini kwa ajili ya wengine.Ninafarijika ninapoona kuwa yupo mtu ambaye licha ya kuwa na magumu mengi,anatenda ka ajili ya wengine pasipo kutegemea malipo.Nilikwenda kijijini nilipozaliwa,nikakutana na mama ambaye kipato chake ni kidogo,anaumwa kwa miaka mingi lakini anajitolea chakula na malazi kwa ajili ya wengine....anawafariji wengine,hata anapokuwa katika ugumu sana,hakati tamaa.Maisha yake ni nuru kwa wengi.Daima hamuachi jirani akiwa katika huzuni,nuru yake inaishi.Ni mwanga kwa waliokosa nuru.

Nafarijika kuona wengi ambao wanakwenda mbali na familia zao,mbali na wapendwa wao kwa ajili ya wengine. 
Nafarijika pia kuona wengi ambao wanajinyima kwa ajili ya wengine.Wengi wao wanaishi maisha ya kawaida,(kwa maana ya kipato) lakini wanatambua maana ya thamani yao kwa wengine,wapo tayari kujitolea pasipo kutambuliwa na wengine.Hii inanipa faraja ya kusonga mbele.Hwa wanatambua kuwa sisi binadamu wote ni wamoja ,tofauti zetu ni juu ya fikra zetu wenyewe.

Daima umoja ni nguvu.Usisubiri wengine wachukue hatua.Anza wewe.Mimi nimepata nafasi hii kwa kuandika.Wewe pekeyako pia watosha,unaweza kubadili wengine kwa kusamehe,kuimba,kufundisha,kutoa nakala nyingi za mafunzo kwa wengine,kwa kuwahurumia wengine,kutembelea wagonjwa,yatima,wafungwa na matendo yote yenye kuleta thamani kwa wanaotuzungua.Mwaka 2013 hatutamuacha mtu hata mmoja katika umasikini,chuki,uvivu,visasi,magonjwa huzuni...nk.Mwaka huu hatutamuacha yeyote kwenye giza.Tunao uwezo wa kuyatenda haya yote.Chukua hatua,mabadiliko yanaanza ndani yako.
Wathamini wengine,hata usiowafahamu....

Tujenge mwili mmoja,moyo mmoja na kupambana mpaka mwisho kwa ajili ya dunia iliyo bora na mafanikio kwa ajili yetu na wengine.

kila mmoja wetu anapochukua hatua licha ya vikwazo,tutayafika mafanikio(picha kwa msaada wa mtandao)




Tuishi maisha yetu kwa dhati bila uoga,tuchimbe ndani ya mioyo yetu ambapochemchem ya kila ushindi ipo,Tujifunze thamani yetu ,tuwathamini wengine kwa kuwa wao ni wa thamani kama tulivyo,tusamehe na kutazama mbele,tujali mawazo ya wenginena imani zao tuziheshimu.


Kila mmoja apende nafsi yake,ayapende maisha yake,asanifu vyema vyote vinavyomzunguka,KILA MMOJA AYAFANYE MAISHA YAKE YA THAMANI KWA WENGINE.Tutimize malengo yetu,yanayotokana na sauti iliyopo ndani mwetu,ili ule muda wa kuishi katika dunia hii unapokwisha ,na kifo kukuita,uitike kwa furaha,kwamba uliyaishi vyema,usipate hata sababu ya kuomba upewe tena muda,bali nuru ya maisha yako iwe mfano wa kuigwa milele.Uiage dunia na kuondoka kishujaa,kuelekea katika maisha mengine mapya yenye majukumu mapya.


Tutapita katika magumu mengi lakini daima tutasonga mbele,hatutamuacha yeyote nyuma,tutainuana sisi kwa sisi,hatutatazama nyuma,wala kuogopa kusonga kwa woga wetu,hatutaogopa lolote kwani sisi ni wa thamani,tutakumbuka daima kuwa dunia si sehemu ya ushindani bali ni sehemu ya ushirikiano na umoja na hivyo daima tutafikia tuendako,kwa sababu Mungu yu ndani mwetu.
Ahsanteni sana