Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Wednesday, July 11

MAFANIKIO HUANZA NA FUKUTO NDANI MWAKO

KIFARANGA KUTOKA NJE YA YAI(kutotolewa),HUTOKANA NA YEYE MWENYEWE KIFARANGA
KIFARANGA KUTOKA NJE YA YAI(kutotolewa),HUTOKANA NA YEYE MWENYEWE KIFARANGA, KUANZISHA KISHA KUPASUA KIWAMBO CHA NJE
MUASISI WA HATUA ZOTE ZA KUTOKA TUMBONI KWA MAMA HADI KUZALIWA HUANZA KWA MTOTO MWENYEWE

MUASISI WA HATUA ZOTE ZA KUTOKA TUMBONI KWA MAMA HADI KUZALIWA HUANZA KWA MTOTO MWENYEWE NA KISHA TAARIFA HUPELEKWA KWA MAMA NA NDIPO KICHOCHEO CHA UCHUNGU HUTOLEWA

Juu ni mifano inayokupa picha kuwa,tangu hatua ya kuzaliwa msukumo hutolewa na anayezaliwa mwenyewe na si anayezaa....hii ni sawa na kusema mtoto ndio aanzishaye hatua za yeye kuzaliwa.Kwa wale waliopata kujifunza zaidi somo la baiolojia,warejee na watakubaliana nami kwamba msukumo wa awali wa kiumbe kuzaliwa huanza kwa kiumbe anayezaliwa,,yaani,msukumo unaofanikisha hutoka ndani.....hivyo kwa kifupi ni kuwa ,msukumo utuleteayo matokeo yetu chanya ama hasi hutoka ndani mwetu wenyewe
 KUCHANUA KWA UA NI MATOKEO YA MSUKUMO UTOKAO NDANI YA UA LENYEWE
KUCHANUA KWA UA NI MATOKEO YA MSUKUMO UTOKAO NDANI YA UA LENYEWE
 Vivyo hivyo,msukumo unapotoka nje(external forces) matokeo yake huwa ni kuharibu,mfano msukumo utokao nje kwenda kwa mtoto husababisha mimba(kiumbe) kuharibika ama kufa,vivyo hivyo msukumo utokao nje kwenye yai hulipasua na kuliharibu....mfano huu huwa sawia pale ua linapopigwa sana na jua(msukumo wa nje) nalo hulazimishwa kuchanua na matokeo yake hunyauka
msukumo wa nje huharibu

Ukitaka mafanikio maishani,ukitaka furaha,ukitaka amani,nk hivi vyote haviletwi kwako na mtu mwingine,wala hakuna kitu nje yako kitakachokuletea,wala haitokei kama bahati..bali hutoka kutoka kwenye fukuto litokalo ndani ya chemchem isiyokauka,toka moyoni mwako .
 FURAHA YA KWELI HUTOKA NDANI MWAKO Wengi tumekuwa tukifikiri kwamba furaha yetu hutoka nje yetu, Mafanikio yetu yataletwa na wengine pasipo sisi kuyatamani kwa dhati,tumekuwa tukilaumu wengine kwa mambo yanayotuhusu sisi wenyewe,na kumbe sisi ndio tunaohusika na maisha yetu na uchaguzi wetu tunaoufanya...

Utakapotambua hili ya kuwa wewe ndio chemchem ya matokeo na matazamio yote maishani,utaanza kuchukua hatua ukitafakari kwa kina bila ukomo,ukichuja na kuchagua yenye manufaa na kuyasimamia kwa dhati .
furaha huanzia ndani
.



NDANI MWAKO NDIMO PALIPO NA CHEMCHEM YA KILA JAMBO
 Mifano hiyo yote juu inatufunza jambo moja la muhimu sana....ya kwamba kila jambo ambalo hufanyika pasipo manung;uniko na hatimae kufanikiwa ama kuleta matokeo yaliyokusudiwa,huanza ndani (hutoka ndani mwa alifanyaye...Aliyefanya ugunduzi wa ndege,roketi,bastola,komputa,simu...nk.wote hawa msukumo wa kufika walipofika ulitoka ndani mwao...


 NDANI MWAKO NDIMO PALIPO NA CHEMCHEM YA KILA JAMBO....ULIFIKIRIALO HUTOKEA..HIVYO UNAPASWA KUCHAGUA KIPI UKITOE,KIPI UKITUMIE,KIPI KIKUONGOZE..... TAZAMA,WEWE NI JINSI UWAZAVYO,WEWE NI FUKUTO LA KILA JAMBO


ULIFIKIRIALO HUTOKEA.
WEWE NI JINSI UWAZAVYO



 Hivyo,wewe ni fukuto la mafanikio unayoyatarajia,mafanikio katika kila nyanja hayaji kwa kusema tu,ama kwa kusoma tu,bali huja pale unapoweka nia,na kuhakikisha unasimamia wazo unaloliwaza pasipo ukomo mpaka pale unapofikia.....ukisema huwezi,umeshindwa,ukisema unaweza bila kuchukua hatua,wewe si shujaa,kwani daima shujaa anapotambua jukumu lake hulifanya na kuliishi..... Ahsante ,nategemea maoni,maswali na ushauri

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com