Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Wednesday, August 7

Itendee haki nafsi yako

Wewe upo hapa duniani ukiwa ni nafsi huru kabisa.Ni nafsi ya pekee ambayo hakuna mwingine anayoweza kuwa mbadala yake isipokuwa wewe tu.
Nafsi ya mtu inabeba ujumbe wa pekee ndani mwake,inabeba nuru ya Mungu ili kuwamulika wengine.Inatamisha thamani ya.maisha na umuhimu wa kuyaishi maisha ya kila nafsi kwa dhati.
Ni wachache wanaotambua kuwa wao si nyama tu zionekanazo,bali wanabeba nafsi yenye umuhimu mkubwa kwa kila kiumbe hapa duniani.Wasiotambua husaliti nafsi zao kwa kipindi chote wanapoishi hapa duniani.Huishi maisha yasiyo na sababu yeyote hapa duniani.Hawana mipango wala malengo maishani mwao.Wao huendeshwa na matukio yatikeayo pamoja na fikra na mawazo ya watu wanaowazunguka.
Ni wakati sasa kila nafsi kutambua thamani iliyo ndani yakw na kuiishi.Kila mtu aanze kujifunza yeye ni nani na kwa nini yupo duniani.Unaweza ukajikumbusha kama ufuatavyo.
chunguza thamani ya maisha yako.-vumbua uwezo uliopo ndani.mwako.
-jifunze na kugundua uwezo wa fikra zako.
-anza kuchukua hatua juu ya fijra zako,msukumo wa moyo wako na juu ya uchaguzi unaoufanta ukiambatana na matokeo ya uchaguzi wako.
-tafuta furaha ndani mwako na iishi.
- Anza kufanya mabadiliko katika maisha yako kwanza ndipo utakapo badili kila kitu kinachokuzunguka
-chagua marafiki watakaokujenga
- Epuka kuogopa kutenda kile unachokiamini.
-tazama kila jambo kama nafasi,zifurahie changamoto unazokutana nazo,shirikiana na wanaokuzunguka

Anza kuishi ukiwa nafsi huru yenye ushiriki na nafsi zingine.Fanya maamuzi.Pangilia majsha yako.Hutasubiri kikundi cha watu ama watu wengine kuchukua hatua ya kujenga maisha yako bali utaanza kuishi sbbu ya wewe kuwepo hapa duniani kama nafsi huru yenye thamani

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 Comments:

Post a Comment

maoni yako hapa