Tangu tumboni kwa mama umepewa uwezo wa kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi.Umepewa vipawa mbalimbali ili kusudi la Muumba litimie…Unatambua kuwa licha ya changamoto nyingi unapaswa kufurahia uwepo wako duniani na kutolaumu dunia, viumbe na nyakati zake bali kupitia hivyo unayafanya maisha yako kuwa ni ya faida kwa dunia hii na viumbe vilivyopo…Kumbuka umezaliwa na upo duniani kwa sababu muhimu ya kipekee.hivyo ishi maisha yenye makusudi na matazamio
Unapaswa kukumbuka sasa kuwa upo duniani si kwa bahati tu bali kwa sababu maalum,kisha amsha moyo wako na nuru iliyo ndani mwako.Kumbuka kuwa sisi tu wamoja, kila mmoja akiwa na thamani sawa na mwenzake.Thamini kilicho ndani mwako kisha utatambua thamani ya wengine
Tupo kuangaza viumbe wote kwa kuwapenda,kuwajali,kuwathamini na kushirikiana nao thamani ya ubinadamu.Walishe wenye njaa,wafariji yatima na wajane,visha wasio na mavazi..yote ni kuangaza nuru iliyo ndani mwetu hasa tunapofanya pasipo kutaka sifa wala malipo...Hupati kuwa na maisha ya thamani kama hutatenda kila jambo kwa msukumo wa moyo.
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa