Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Sunday, August 25

UJUMBE WA JUMAPILI

Unapoanza kumuona Mungu katika kila kiumbe kinachokuzunguka unatambua kuwa sasa umezaliwa upya.Sauti yake inakuwa ikiongea nawe ndani mwako toka ndani yako.Unatambua kuwa Mungu hayupo mbali nawe bali yupo ndani mwako wakati wote.
Unaruhusu nguvu na chemchem ya kila ushindi kufanya kazi ndani yako na kukupa nafasi ya kugundua nguvu hii iliyo ndani mwako na kuitumia kuifanya dunia kuwa sehemu bora kwa viumbe wote.

Mungu ametupatia uwezo mkubwa wa kuyafanya maisha yetu kuwa yenye faida kwa wengine,na husubiri maamuzi yetu ili kutuonesha njia.

Tunapokuwa tayari anatufundisha maana ya kuwa hapa na thamani ya maisha yetu . Ndipo unapomjua tena si kama kiumbe cha kutisha ama kisichoonekana lakini kama sehemu muhimu ndani mwako.Kisichoonekana ndani mwetu kinazaliwa upya na kuonekana kwa kila anayekuzunguka.

Kisha hutupatia kila uwezo na kuingia ndani ya kila kilicho mwilini mwetu kwa maelfu,tayari kwa kumtumikia kwa njia mbalimbali.Unitambua kuwa maisha yako ni ya thamani kwako na kwa wengine,unafungua ndani ya moyo wako kuishi kwa dhati.Sauti ndani mwako inaanza kusikika kwa viumbe wengine.Unapata thamani zaidi kupita vito vya thamani na zaidi ya fedha.

Maisha yako yanakuwa mwanga kwa viumbe wote.Unaanza kutumia kila kipawa na nafasi unayopewa na Muumba kwa ajili ya wote kwa utukufu wake yeye.Maisha yako yanaongea Tunajenga dunia mpya yenye matumaini na furaha-Jumapili njema

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 Comments:

Post a Comment

maoni yako hapa