Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Tuesday, August 28

TUNAENDELEA MBELE

KATIKA MAISHA TUNAPITIA MAGUMU.....tunapitia kuanguka mara nyingi...tunapitia kukatishwa tamaa,kusengenywa,kutengwa na hata kudaharauliwa.....tunapitiwa kuumizwa katika mahusiano,kuachwa,kudhulumiwa nk...haya yote hayana budi kutokea,jambo la muhimu ni kuwa tunavumilia yote na licha yakuwa tumeanguka mara nyingi,lakini pia tumesimama mara nyingi zaidi...na ndio maana tunaendelea na maisha kama ili

vyo kawaida,tunaendelea kuandika,kuwaelimisha wengine,kuwaburudisha wengine na kuwafariji wengi....tunayafahamu maisha,tunajua kuwa kama tutakata tamaa tutakuwa tumejidharau wenyewe,tumejiangusha wenyewe,tumejisengenya wenyewe na tumejidhulumu wenyewe.....
Hatukati tamaa kamwe
“Tunasikiliza mioyo yetu,kwa sababu hutupatia mwongozo wa maisha kila kukicha,hutukumbusha kuwa haklisi...hutukumbusha kuwa tupo kwa ajili ya wengine....hutukumbusha kuwa dunia inatuhitaji....hutukumbusha kuwa sisi ni zaidi ya tujifikiriavyo...sisi ni bora kama tulivyoumbwa

Monday, August 27

NAFASI YAKO HAPA DUNIANI NI YA MUHIMU SANA

Kwa sababu kila mmoja wetu anahitaji kuthaminiwa,kuheshimiwa na kila mmoja anahitaji kuona wengine wanamjali....mioyo yetu haiwezi kuwa na furaha ya kweli kama hatutakuwa sauti kwa wale ambao wanataka kusema lkn hawapati japo nafasi....kuwa faraja kwa wale wenye machozi,kuwa mwangaza kwa wale wanaohitaji nuru ya kuamsha mioyo yao na ari ya kuyaishi maisha yao....tutakapokuwa nguvu kwa wanyonge,na zaidi..kuishi kwa ajili ya wengine

Haujatokea duniani kama bahati mbaya,ama pasipo lengo,lipo lengo....nalo ni kuishi lengo hilo ili nuru ya Mungu iliyopo ndani mwako ionekane ,Bila wewe kuwepo na kuishi maisha yako,lipo jambo ambalo halitakuwa vile linatakiwa liwe,upo kwa ajili ya kuiangaza dunia...wewe ni mwanga...wewe ni chachu ya maendeleo ya dunia hii....si nyota,wala jua,wala miti,wala majani ,wanyama kila uoto ambao unakukosa pale unapokuwa upo duniani pasipo kutenda jambo lililokuleta.....nafasi yako wewe haijazwi na mtu yeyote mwingine,ndio maana umeletwa hapa duniani....amua kutimiza lengo lililo kuleta,viumbe wote wanakuhitaji....ishi kwa ajili ya wengine,wauone upendo,waione amani,waijue faraja,wafahamu kujitolea...na haya yote yanatoka kwako wewe..wewe ni wa pekee


 

Saturday, August 25

WEKA JUHUDI KUJITAMBUA WEWE KWANZA

Wapo watu wanaofikiri kwamba yupo mtu ambaye anahusika juu ya uchaguzi wa wanataka kuwa nani,na kuishi maisha ya namna gani...Wapo wanaofikiri kuwa wenzao ni bora kuliko wao...Wapo wanaofikiri kuwa upo wakati utafika watabadilika tu katika kufikiri,kutafakari na kufanya maamuzi pasipo kuweka juhudi binafsi.Nikupe siri moja katika kutafuta mafanikio,jiulize unataka maisha ya namna gani,uishi vipi maishani....jiulize kila mara kabla ya kulala,na baada ya kuamka,jikumbushe ....kila siku mpaka pale moyo wako na nafsi yako itakapofanya kuwa kanuni ya msingi,kisha chukua hatua pasipo kutazama pembeni ama wanaokutazama....Acha uiga wengine...wewe ni wa pekee na nafsi yako...maisha ni mwanga,fuata mwanga wako..acha uoga...chagua ujasiri ....amka ,chimba ndani ya moyo wako,chimba ujitambue wewe ni nani.

Wednesday, August 22

TUNAPATA KILE TUTOACHO

Nakusihi usome kwa makini makala yenye kichwa cha habari.JINSI GANI TUNAPATA TUWAZACHO hapa http://pongujoseph.blogspot.com/2012/07/ni-jinsi-gani-tunapata-tuwazacho.html   kabla ya kusoma makala hii..
   Kabla ya kueleza kanuni hii...nitoe mifano miwili

          Kwanza kabisa...tafakari pale unapokuwa na rafiki yako...unapomtendea jambo la kumuudhi....hukasirika,akasirikapo huchukia ,na chuki aliyonayo huweza kumfanya akakutendea pia jambo mfano neno baya ,na kisasi.....kifuatacho ni kwamba wote huwa mnakuwa katika hali ya kutokuwa na furaha,.Hata kama yule umtendeaye ubaya atanyamaza pasipo kukutenda lolote....wewe utabaki na wasiwasi na huzuni
         Pili,upo na mwenzako,katika hali ya kawaida....ukamchekesha....kitendo cha kumchekesha husababisha atabasamu ,kutabasamu huamsha furaha katika moyo wake.....nawe uliyechekesha utacheka na kuamsha furaha moyoni mwako.....
   Ni sawa na pale mtu anapopiga miayo....unapomtazama nawe pasipo shuruti unapiga miayo

unapotoa upendo,unapata upendo uleule ulioutoa
                   

                  Mifano hiyo hapo juu inatueleza jinsi gani pale tunaposababisha jambo fulani kwa wengine,basi jambo hilo huturudia sisi wenyewe.Sisi ni matokeo ya nguvu,sisi ni nguvu..kila tunachokitoa ndani mwetu ni nguvu...upendo ni nguvu,chuki ni nguvu,mawazo ni nguvu ,furaha ni nguvu....Ipo kanuni ambayo ilitolewa na mwanasayansi mkongwe,Isaack Newton,inayosema..kwa kiingereza, to every action there is equal and opposite reaction---kwa tafsiri isiyo rasmi ,kwa kila tendo /jambo litokealo/lisababishwalo...basi huwa na kinyume chake kilicho sawia na jambo /tukio/tendo hilo.
                       Hivyo kila tunachokiwaza,tunachokitenda dhidi ya wengine...basi hutokea kwetu wenyewe...ukiwafanyia wanaokuzunguka kwa upendo,nawe upendo utakurudia,ukitoa pasipo vikwazo nawe pia utapata pasipo vikwazo...ukifurahi na kutamani wengine wafanikiwe kupitia wewe basi,mafanikio unayoyatoa kwa wengine huja kwako.......
                Hivyo basi,hapa tunapatas kanuni ya pekee ambayo inatusaidia kufanikiwa katika maisha tunayoyaishi,ya kwamba...mafanikio huja pale unapokuwa sababu ya wengine kufanikiwa,unapofanya juhudi maishani mwako kuwainua wengine,ndivyo nawe unapoinuliwa,ndivyo unavyofungua milango ya mafanikio kwako.Ukifanya chuki,chuki hukurudia siku moja......majuto huwa ni sehemu ya maisha yako

   

Saturday, August 18

simama kwa ajili ya wengine

Kila mmoja anacho kipaji chake...haijalishi mzee ama kijana...simama kwa ajili ya wengine..wapo wahitaji,wanyonge,walioshuka moyo..wapo waliokata tamaa,simama kwa ajili yao...unaweza kuhisi kuwa wewe si lolote ..lakini ukisimama kwa ajili ya wahitaji.....utapata furaha isiyo kifani.....natamani sana kuona maisha ya wengi ya kibadilika...ninaweza kuwa sina fedha lakini daima nitakuwa chanzo cha wengine kuamka na kusimama...wewe unajisikiaje?

 Ninaishi maisha yangu,lakini nikiwatazama walionizunguka,moyo wangu unapata faraja kuwaona wakifanikiwa....nipo kama mimi,lakini nikisimama kwa ajili ya wengine.......nimesimama nikiwa peke yangu lakini kwa kujitolea kwa wengine nasimama kwa mamiolioni...tujitolee maisha yetu kwa ajili ya wengine

Friday, August 17

THAMINI WANAOKUZUNGUKA.

    Nimefanya utafiti na kupata matokeo kwamba katika Jamii nyingi za waafrika,wengi huwa hawapendi kuona wenzao wakifanikiwa..Mtu huchukia kuona mwenzake kaanzisha biashara,kapata ajira,kagundua kitu kipya,yaani kwa kifupi wengi huingiwa na chuki kuona wengine wakinyanyuka.Mfano,mpogoro yupo radhi kumfanyia fitina mpogoro mwenzake asiendelee,Mbena atamfanyia fitina mbena mwenzake asiendelee....msukuma atafanya kila awezalo kumrudisha nyuma msukuma mwenzake.
     Katika utafiti huu,nilipata maoni tofauti pamoja na mifano lukuki ya jinsi jamii ya kiafrika tunavyofanyiana fitina sisi kwa sisi(roho mbaya).Mzee  Mkiki ,anasema ameshuhudia chuki na visa vingi alipoanza kujenga nyumba ya kisasa (ya bati),wapo ambao waliapa kuwa watahakikisha kabla hajahamia katika nyumba ile basi atakuwa amedondoka....kwa hofu yake aliamua kusitisha ujenzi.....Rafiki yangu mmoja niliyesoma nae shule Mazengo,alinisimulia jinsi ambavyo wale aliokuwa akidhani ni marafiki wake wakubwa ,walipooneshwa kutofurahi pale alipofanikiwa kusimama mwenyewe katika biashana na hata kuanza kujenga....anasimulia kisa hiki ambacho kiliambatana na marafiki wake kumsengenya na hata kushirikiana na wahalifu kumuibia,ili mradi tu arudi nyuma....bila shaka hata wewe unao ushuhuda
     Sababu kubwa ya roho mbaya hii ni elimu duni...hasa ya kutojitambua..Hatutambui kuwa kila mmoja wetu analo jukumu la kutimiza hapa duniani...Na kila tukifanyacho huwa eitha kinaweza kubomoa ama kuwajenga wengine,kulingana na uchaguzi wetu,......Tupo kwa ajili ya wengine....kila mmoja anamtegemea mwingine katika kuifanya dunia hii kuwa sehemu bora...
      Sisi hatuwatazami wengine,tunatazama tu nafsi zetu,.Hatujui kuwa maendeleo ya wale wanaokuzungiuka ni maendeleo yako,hatutambui kuwa chuki hufunga milango ya mafanikio yetu wenyewe.
   Hatupo tayari kujua wala kujifunza ushirikiano,hatupo tayari kujifunza wengine wamefanikiwaje!hatupo tayari kubadili maisha yetu....tumekuwa tukiendeleza chuki badala ya upendo,tukiendekeza majivuno,visasi na choyo..hatuwathamini wanaogusa maisha yetu..hatuwathamini wanaotuzunguka,hatuthamini michango ya wale waliothubutu kusimama licha ya vikwazo,hatuthamini mawazo mapya,hatuthamini chemichemi za fikra,hatuthamini wazalendo wa dunia hii....hatuthamini wanaojitolea kwa ajili yetu
    Tujiulize,unapoteza nini pale mwenzako anapoushinda umasikini...unapoteza nini pale unapowainua wengine....unapoteza nini unaposimama kwa ajili ya wanyonge.....ni wakati sasa wa kujifunza kuwa mafanikio ya mwenzako ni mafanikio yako......kwangu mimi ninapata faraja ninapoona kuwa ninagusa maisha ya wengine....ninawathamini kila anayenizunguka

Monday, August 13

KUMRADHI

 Karibuni nyote mnaofuatilia blog hii.
 Kwa siku kadhaa nilipata shida kuweza kuandika katika blog hii kutokana na tatizo la kiufundi,akaunti yangu ilipata hitilafu na kuingiliwa,nikapata changamoto katika kuandika......nilikuwa nikiumia kwa kuwa furaha yangu ni kuona kuwa kila mara tunajifunza jambo jipya,ni kuona waliokuwa wanakata tamaa wanaamka upya..ni kuona kuwa wewe na mimi tunakua na kuyafikia mafanikio...
 Changamoto zilizotokea zimenifanya niongeze bidii,bila shaka tutafika pale tunapokusudia kufika

Tuesday, August 7

MWALIMU BORA

Wale waliopitia ugumu ,milima na mabonde katika maisha yao ni walimu bora,kwa sababu wanajua maana ya kila jambo walilolipitia,wanajua jinsi gani ya kubomoa ukuta wa mipaka ya kufikiri,wanajua kuumizwa,wanajua faraja,wanajua chuki,wanajua amani,wanajua upendo,wanajua kila jambo walilolipitioa si kwa kusoma nukuu tu,bali kwa kuishi na kupambana na vikwazo...wanatambua kuwa hakuna njia ya kupambana na woga zaidi ya kuamua kutenda unachokiogopa,wanatambua jinsi ya kufungua minyororo inayotuzuia kuyafikia mafanikio,hawa maisha yamewapa changamoto,maisha pia yamewapatia baraka tele...wamepata majaribu,wakayapita,wamepata maumivu,wakaendelea kusimama imara ,watu waliwakejeli,waliwaumiza na wengine waliwapa faraja...waliamua kuacha yaliyopita na kusimama tena kwa ushindi,wakachagua kuwa washindi,wakaishi maisha yao kwa ajili ya wengine pia,woga wao ni kuogopa kutenda wanapotakiwa kutenda..wamekuwa mifano bora katika jamii,wanatambua kujitolea ,hawa ni mashujaa ambao nuru ya maisha yao itaishi milele.Ni wakati sasa wa sisis kutoogopa kushindwa na kuamua kudiriki kutenda.

Sunday, August 5

KILA JAMBO LITOKEALO LINA SABABU, KILA JAMBO HUTUFUNZA

     Ni  kweli kwamba kila changamoto itupatayo huwa na sababu...na huwa ni wakati wetu kujifunza mbinu mpya za kufikia pale tunapohitaji kufika...wakati mwingine tunajifunza kutoshikilia sana mambo ambayo yanatuchelewesha kufika tuendako....wakati mwingine tunakumbushwa kuwa kila mlango mmoja ufungwapo,basi hutoa nafasi kwa milango mingine mingi na madirisha kufunguliwa ,na hivyo,waweza kukata tamaa,kwa kutokewa na changamoto,kumbe changamoto hiyo ndiyo inayokupa njia mpya
    Si lengo langu kuandika mambo yanayonihusu mimi,ama watu fulani...kama ilivyo ada,blog hii ni mahali pa kukufanya ujitambue wewe ni nani,uweze kufungua minyororo ambayo inakuzuia kuyafikia mafanikio
    Wikiendi nilikutana na rafiki yangu ambaye ameumizwa sana katika masuala ya mahusiano...kuumizwa huko kumemfanya ajihisi kuwa hana thamani,ana matatizo.....hajiamini tena na daima anashuka moyo,amekata tamaa na kuapa kuwa hatapenda tena...baada ya kuongea naye sana,alitokea kukubali kuwa hayo yalitokea,yamebaki historia.....anasimama tena na kusamehe,akianza maisha mapya.Amekubali kuwa aliumizwa,lakini yote hayo hayatamfanya ashindwe kuishi maisha mapya,amaetambua kuwa yeye ana jukumu juu ya maisha yake,hakuna anayeweza kumpangia maisha yake yajayo,bali ni yeye,yaliyopita yamempa nguvu ya kusimama na kukimbia kwa kasi zaidi




  CHANGAMOTO ZINATUKUMBUSHA KUWA NI VEMA KUTAZAMA KILA JAMBO  KUWA NI KUFUNZI
    Lipo somo kubwa tunajifunza hapa......nakusihi usome kwa makini maneno haya chini,ambayo rafiki yangu huyo,aliyaandika baada ya kujitambua,toa pia maoni


Kuachana nawe kumenifunza jinsi ya kuwathamini watu wengine,kuwapenda hata pale panapoonekana ni vigumu, kumenifanya nijifunze kuwa mimi sipo tu kwa ajili yang u,bali kwa ajili ya wengi,hivyo,maisha yangu yana sababu kubwa hapa duniani,nimejifunza kuwajibika na kujitolea kwa wale wote ambao jamii haiwathamini—wafungwa,yatima,wajane na wote ambao hawana tumaini la kusimama tena,nimetambua kuwa sisi sote ni wamoja,uadui huletwa na wale wasiojitambua,wanaofikiri kuwa dunia
hii ni sehemu ya ushindani badala ya ushirikiano,wanaodhani kuwa wao ni bora kuliko wengine...nimejifunza kuwa ni furaha katika kutoa kuliko kupokea,nimejifunza kuwa hata kama binadamu atakuwa amekosa viungo vya mwili,sura nzuri,mavazi,fedha ama umaarufu,lakini bado ni binadamu mwenye thamani kubwa,kwani thamani ya binadamu ni zaidi ya sura,umbo,mali,umaarufu,hivyo nitawatazama binadamu wote kwa usawa na kujitolea kwao kwa usawa,nimejifunza kuwa sipaswi kutazama changamoto kwa upande hasi,bali nitazame daima kwa mtazamo chanya,na mwisho,nimejifunza kusimama mwenyewe,na kumshukuru Mungu,nikimsihi anitumie daima kwa ajili ya  w engine…Amina (Pongu)

  

Saturday, August 4

TUJIKUMBUSHE SISI NI NANI.


     Kwa kipindi hiki cha mwisho wa wiki,ningependa tujikumbushe sisi ni nani,anza na wewe,
 Kaa sehemu tulivu,kisha funga macho,vuta pumzi taratibu ,sikiliza na kufuatilia mapigo ya moyo wako,kisha jiuliza maswali yafuatayo
  1.  mimi ni nani?
  2. kwa nini nipo hapa duniani
  3. je ni kwa kiasi gani nimetimiza jukumu langu la kuwepo hapa duniani?
  4. je ninajipenda na kujithamini kwa jinsi nilivyoumbwa?
  5. je,nitakapokuwa tayari kumaliza maisha yangua hapa duniani,ni jambo gani la msingi litakalo nipa furaha na kumbukumbu kwa wengne?
  6. je nimekuwa faida gani katika dunia hii?
  7. kama bado sijafanya chochote,ama siridhiki na maisha niyaishiyo,ntabadilika?lini?kama sio sasa,ni nini inanifanya nisiamue?
  8. je maisha ninayoyaishi si ya bandia?