Nakusihi usome kwa makini makala yenye kichwa cha habari.JINSI GANI TUNAPATA TUWAZACHO hapa http://pongujoseph.blogspot.com/2012/07/ni-jinsi-gani-tunapata-tuwazacho.html kabla ya kusoma makala hii..
Kabla ya kueleza kanuni hii...nitoe mifano miwili
Pili,upo na mwenzako,katika hali ya kawaida....ukamchekesha....kitendo cha kumchekesha husababisha atabasamu ,kutabasamu huamsha furaha katika moyo wake.....nawe uliyechekesha utacheka na kuamsha furaha moyoni mwako.....
Ni sawa na pale mtu anapopiga miayo....unapomtazama nawe pasipo shuruti unapiga miayo
unapotoa upendo,unapata upendo uleule ulioutoa |
Mifano hiyo hapo juu inatueleza jinsi gani pale tunaposababisha jambo fulani kwa wengine,basi jambo hilo huturudia sisi wenyewe.Sisi ni matokeo ya nguvu,sisi ni nguvu..kila tunachokitoa ndani mwetu ni nguvu...upendo ni nguvu,chuki ni nguvu,mawazo ni nguvu ,furaha ni nguvu....Ipo kanuni ambayo ilitolewa na mwanasayansi mkongwe,Isaack Newton,inayosema..kwa kiingereza, to every action there is equal and opposite reaction---kwa tafsiri isiyo rasmi ,kwa kila tendo /jambo litokealo/lisababishwalo...basi huwa na kinyume chake kilicho sawia na jambo /tukio/tendo hilo.
Hivyo kila tunachokiwaza,tunachokitenda dhidi ya wengine...basi hutokea kwetu wenyewe...ukiwafanyia wanaokuzunguka kwa upendo,nawe upendo utakurudia,ukitoa pasipo vikwazo nawe pia utapata pasipo vikwazo...ukifurahi na kutamani wengine wafanikiwe kupitia wewe basi,mafanikio unayoyatoa kwa wengine huja kwako.......
Hivyo basi,hapa tunapatas kanuni ya pekee ambayo inatusaidia kufanikiwa katika maisha tunayoyaishi,ya kwamba...mafanikio huja pale unapokuwa sababu ya wengine kufanikiwa,unapofanya juhudi maishani mwako kuwainua wengine,ndivyo nawe unapoinuliwa,ndivyo unavyofungua milango ya mafanikio kwako.Ukifanya chuki,chuki hukurudia siku moja......majuto huwa ni sehemu ya maisha yako