Nimefanya utafiti na kupata matokeo kwamba katika Jamii nyingi za waafrika,wengi huwa hawapendi kuona wenzao wakifanikiwa..Mtu huchukia kuona mwenzake kaanzisha biashara,kapata ajira,kagundua kitu kipya,yaani kwa kifupi wengi huingiwa na chuki kuona wengine wakinyanyuka.Mfano,mpogoro yupo radhi kumfanyia fitina mpogoro mwenzake asiendelee,Mbena atamfanyia fitina mbena mwenzake asiendelee....msukuma atafanya kila awezalo kumrudisha nyuma msukuma mwenzake.
Katika utafiti huu,nilipata maoni tofauti pamoja na mifano lukuki ya jinsi jamii ya kiafrika tunavyofanyiana fitina sisi kwa sisi(roho mbaya).Mzee Mkiki ,anasema ameshuhudia chuki na visa vingi alipoanza kujenga nyumba ya kisasa (ya bati),wapo ambao waliapa kuwa watahakikisha kabla hajahamia katika nyumba ile basi atakuwa amedondoka....kwa hofu yake aliamua kusitisha ujenzi.....Rafiki yangu mmoja niliyesoma nae shule Mazengo,alinisimulia jinsi ambavyo wale aliokuwa akidhani ni marafiki wake wakubwa ,walipooneshwa kutofurahi pale alipofanikiwa kusimama mwenyewe katika biashana na hata kuanza kujenga....anasimulia kisa hiki ambacho kiliambatana na marafiki wake kumsengenya na hata kushirikiana na wahalifu kumuibia,ili mradi tu arudi nyuma....bila shaka hata wewe unao ushuhuda
Sababu kubwa ya roho mbaya hii ni elimu duni...hasa ya kutojitambua..Hatutambui kuwa kila mmoja wetu analo jukumu la kutimiza hapa duniani...Na kila tukifanyacho huwa eitha kinaweza kubomoa ama kuwajenga wengine,kulingana na uchaguzi wetu,......Tupo kwa ajili ya wengine....kila mmoja anamtegemea mwingine katika kuifanya dunia hii kuwa sehemu bora...
Sisi hatuwatazami wengine,tunatazama tu nafsi zetu,.Hatujui kuwa maendeleo ya wale wanaokuzungiuka ni maendeleo yako,hatutambui kuwa chuki hufunga milango ya mafanikio yetu wenyewe.
Hatupo tayari kujua wala kujifunza ushirikiano,hatupo tayari kujifunza wengine wamefanikiwaje!hatupo tayari kubadili maisha yetu....tumekuwa tukiendeleza chuki badala ya upendo,tukiendekeza majivuno,visasi na choyo..hatuwathamini wanaogusa maisha yetu..hatuwathamini wanaotuzunguka,hatuthamini michango ya wale waliothubutu kusimama licha ya vikwazo,hatuthamini mawazo mapya,hatuthamini chemichemi za fikra,hatuthamini wazalendo wa dunia hii....hatuthamini wanaojitolea kwa ajili yetu
Tujiulize,unapoteza nini pale mwenzako anapoushinda umasikini...unapoteza nini pale unapowainua wengine....unapoteza nini unaposimama kwa ajili ya wanyonge.....ni wakati sasa wa kujifunza kuwa mafanikio ya mwenzako ni mafanikio yako......kwangu mimi ninapata faraja ninapoona kuwa ninagusa maisha ya wengine....ninawathamini kila anayenizunguka
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa