Ni kweli kwamba kila changamoto itupatayo huwa na sababu...na huwa ni wakati wetu kujifunza mbinu mpya za kufikia pale tunapohitaji kufika...wakati mwingine tunajifunza kutoshikilia sana mambo ambayo yanatuchelewesha kufika tuendako....wakati mwingine tunakumbushwa kuwa kila mlango mmoja ufungwapo,basi hutoa nafasi kwa milango mingine mingi na madirisha kufunguliwa ,na hivyo,waweza kukata tamaa,kwa kutokewa na changamoto,kumbe changamoto hiyo ndiyo inayokupa njia mpya
Si lengo langu kuandika mambo yanayonihusu mimi,ama watu fulani...kama ilivyo ada,blog hii ni mahali pa kukufanya ujitambue wewe ni nani,uweze kufungua minyororo ambayo inakuzuia kuyafikia mafanikio
Wikiendi nilikutana na rafiki yangu ambaye ameumizwa sana katika masuala ya mahusiano...kuumizwa huko kumemfanya ajihisi kuwa hana thamani,ana matatizo.....hajiamini tena na daima anashuka moyo,amekata tamaa na kuapa kuwa hatapenda tena...baada ya kuongea naye sana,alitokea kukubali kuwa hayo yalitokea,yamebaki historia.....anasimama tena na kusamehe,akianza maisha mapya.Amekubali kuwa aliumizwa,lakini yote hayo hayatamfanya ashindwe kuishi maisha mapya,amaetambua kuwa yeye ana jukumu juu ya maisha yake,hakuna anayeweza kumpangia maisha yake yajayo,bali ni yeye,yaliyopita yamempa nguvu ya kusimama na kukimbia kwa kasi zaidi
CHANGAMOTO ZINATUKUMBUSHA KUWA NI VEMA KUTAZAMA KILA JAMBO KUWA NI KUFUNZI
Lipo somo kubwa tunajifunza hapa......nakusihi usome kwa makini maneno haya chini,ambayo rafiki yangu huyo,aliyaandika baada ya kujitambua,toa pia maoni
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa