Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Tuesday, July 31

UPENDO,NDOA NA SHERIA

Mwisho wa makala hii utapata kujifunza mambo yafuatayo
  1. ni nini na jinsi gani upendo wa dhati
  2. HOFU-ADUI MKUBWA WA UPENDO
  3. ndoa,furaha,na huzuni katika ndoa-sababu
  4. sheria katika upendo na kushindwa kwa sheria kulinda ndoa
  5. jinsi gani utaishi maisha ya furaha katika ndoa
  6. nafasi yako katika upendo,ndoa.
  7. jinsi ya kuifanya ndoa yako idumu na kuwa na mafanikio kila kukicha
  8. jinsi ya kutazama kila jambo katika mfumo chanya na kubadili maisha yako

                                  UPENDO
 


     Upendo ni mvuto wa asili(nguvu ya asili) usio na shuruti kati ya mtu mmoja na mwingine.Ni lugha ya pekeee ambayo kiziwi,kipofu,mtoto,mzee, na kila kabila huisikia.Ni lugha ya moyoni..Ni NGUVU PEKEE INAYOTIBU,INAYOWEZA KUAMSHA WASIO NA TUMAINI,INAYOONDOA CHUKI,(UPENDO HUSHINDA YOTE).Upendo ndio ishara kuu ya Mungu(MUUMBA-ASILI YA VIUMBE VYOTE),,ni faraja,amani,ni tumaini...Ndio maana katika maandiko toka katika biblia tunaelezwa ya kuwa Mungu ni upendo
       Mara nyingi tumekuwa tukigawa aina mbalimbali kutokana na mazingira yetu na fikra zetu na kupata upendo wa dhati,upendo wa kawaida,lakini ukweli ni kwamba upendo unabaki kuwa ni upendo(unapopungua huo si upendo) na kinyume chake (chuki) inabaki kuwa chuki.Huwezi kusema kuwa unao upendo pasipo kuuishi/kutenda mambo yanayodhihirisha upendo.Upendo ni kutazama kwa huruma,upendo ni kuinua walkio chini,upendo ni kujitolea pasipo kuhitaji malipo,upendo hushinda yote.  
       Kama tulivyyoona hapo juu,upendo ni msukumo wa kiasili kabisa.Hutokana na mvuto wa asili utokao moyoni kwa mtu,na ndio maana nikauita upendo kuwa ni lugha ya moyoni.Kwa sababu ni mvuto wa kiasili,upendo haujengwi wala kulindwa na vitu visivyo vya asili.Fikra zetu zimejengwa kuutazama upendo katika mtazamo wa vitu ama mali.Mvuto huu wa asili huwa haujali rangi,dini,tofauti ya kimawazo ama mtazamo,haujali tofauti za taifa,ukanda ama lugha,kabila,haujali mali wala hali.Ni ukweli usiopingika kuwa kila mtu huweza kumpenda ama kuvutiwa na mwingine si kwa sababu ya dini,ama rangi,ama kabila,ama utaifa fulani,ama mali.....fikra za dini,mali,kabila,taifa huja kwa msukumo wa fikra(zenye athari ya kimazingira) na tamaa.
      Kwa maana hiyo,sitakuwa nakosea nikisema kuwa,upendo (mvuto wa asili) kwa sababu ni asili ya moyo,basi ukitazamwa kwa mtazamo wa vitu visivyo asili(vitokanavyo na fikra za kimazingira) basi huwa si upendo tena bali huwa ni tamaa na udanganyifu.Upendo hauwezi kulindwa kwa sheria,hakuna sheria itakayotungwa kuulinda upendo kati ya watu wawili,na sheria hiyo ikashinda isipokuwa tu,upendo wa dhati hutoka moyoni mwa kila mmoja,nao hudumu na kutukuka toka moyoni mwa wawili hao na ndio maana,tutaona hapo mbele ya kuwa sheria imeshindwa kulinda ndoa na badala yake baada ya sheria kuwa ndio mlinzi wa upendo,ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika(zipo sababu nyingine ndogo)
  Tumezaliwa tukiwa na upendo,lakini mitazamo yetu ya kifikra imefanya tuweke matabaka katika upendo,na hivyo hofu imetawala upendo,na kufanya hofu kuwa adui mkubwa wa upendo.
                                                Hofu,adui wa upendo(picha kwa hisani ya mtanzdao)
    Ni hofu ndiyo inayoleta chuki,hofu humfanya mtu kutojiamini na kuhisi wanaomzunguka ni maadui...Ni hofu ndiyo iliyosababisha viongozi wang'ang'anie madaraka,kufanya mauaji,kubagua..Ni hofu ndiyo  inayojenga uhasama.
                              
               NDOA
        Kila unapofikiri kuhusu mwenzi wako,umefikiri kuhusu wewe,unapomtendea mwenzi wako unajitendea wewe,unapomjali mwenzi wako umejipenda mwenyewe,unapomfanya mwenzi wako afurahi umejitendea wewe,upendo hutoka ndani ya moyo wako mwenyewe...pale unapovutiwa na mwingine...pasipo shinikizo litokalo nje ya moyo wako...ukamchagua na kuonesha nguvu hii ya asili kwake,ukishirikiana nae kukua na kuyafikia matarajio ya kila mmoja wenu,hii huitwa ndoa.Ndoa si kupata mwenza ambaye atakufanya uwe kamili(kwa kuwa kila mmoja amekamilika vile alivyo), ni urafiki na upendo uendao mbele ya maumbile.Ndoa ni muumngano wa wawili kila mmoja kwa ukamilifu wake,kwa ajili ya kufanya nuru ya Mungu ambayo ipo kwa kila mmoja,ing'ae kwa kila mmoja ili kuwafanya wawili hao na wale wanaowazunguka waujue utukufu wa Mungu
 Nimetazama ndani yangu na kuuona ukamilifu wangu,nami naungana nawe ili mimi nawe tushirikiane ukamilifu wetu(tafakari kwa kina)
            muhimu:wengi hufikiri kuwa hawajakamilika,wamekosa kitu fulani,na hivyo huingia kwenye ndoa wakitazamia kukipata kitu fulani toka kwa wenzi wao,baadae hugundua kuwa wanachokitafuta hakipo kwa wenzi wao,hapo ndipo matatizo huanza kutokea kwenye ndoa....baada ya changamoto nyingi ,wengine huomba Mungu awabadili wenzi wao,hawatambui kuwa ni fikra zao ndio adui wa ndoa yao(fikra huleta hofu)-(kama wangetambua wangemuomba Mungu abadili fikra zao.-hata ndoa kuvunjika,hutambua kuwa kumbe furaha,amani,upendo,kujali..kunaanza ndani mwao.
               Ndoa ni mungano ambao kila mmoja katika wenza huhakikisha anatumia kila alichonacho kuhakikisha kuwa mwenzi wake anakua na kutimiza yale aliyoyakusudia katka maisha yake.Ni mahali ambapo chemchem ya amani ilipo,ndoa si kifungo...ndoa ni chimbuko la uhuru ,ndoa si hofu,bali ni chemchem ya upendo,umoja na amani,ni mbegu iletayo matunda bora,ndoa ni ishara ya kukubali majukumu,ni chimbuko la kuifanya dunia kuwa sehemu bora
              Kinyume chake katika dunia ya sasa,ndo imekuwa ni sehemu ya watu kukimbia majukumu,ni sehemu ya watu kukwepa kufikiri,kuamua na kutenda...ndoa imekuwa ni sehemu ya mmoja kuweka matarajio dhidi ya mwenzi wake......tamaa ya kupata mali,kupata sifa ndio imekuwa msukumo wa watu kuingia kwenye ndoa...na kwa sababu ya hofu ya kukosa matamanio ama matarajio haya......mwanadamu akabuni sheria mabyo inamuhakikishia kuwa\ anatimiza matamanio yake......na kutengeneza sheria.....ya kwamba kila anayeingia katika ndoa basi huweka kiapo cha lazima(na kuifanya ndoa kuwa shuruti ya kisheria).Swali ni je,upendo (usio na shuruti) unaweza kulindwa kwa shuruti(sheria)?
               Kuingizwa kwa sheria(kiapo_katika ndoa ni dalili tosha ya kuwepo kwa hofu kati ya wawili waliopendana.Ni dalili ya kutoamini mioyo yao .Ni matokeo ya kutazama ndoa katikamisukumo ya hali na mali...gari,fedha,nyumba,ardhi,umaarufu...Matokeo yake ni kwamba mmoja kati yawenzi hawa huwa mtumwa na mwingine huwa mtwana...Hofu ndio msingi wa ndoa ya kisheria.....upendo hushinda yote..Mpendwa msomaji,jiulize ni kwa nini,watu wawili waliokutana wao wawili,wakathaminina na kupendana,huweka kiapo na kuandikishana kisheria.....je kiapo hiki huwasaidia kukua na kupendana pamoja? 
               Hivi majuzi nimesoma ripoti moja kuhusu ndoa duniani,ikionesha kuwa kuvunjika ndoa kumeongezeka sana toka katika karne ya kumi na tisa na sasa kasi ni kubwa sana..Sababu si ugumu wa maisha,sababu si utandawazi...sababu nimekwisha ieleza,ni fikra zetu na msukumo wa kuingia katka ndo kwa msukumo wa mali na hali,kwa matazamio ya kupata kuliko kutoa,sheria ikiwa ndio chimbuko lake
               KWA mtazamo wangu mimi upendo ,ni mvuto asilia...huvumilia,hujali,huthamini..na ndoa iliyojengwa katika upendo,hukua,tena pasipo kiapo kanisani ,msikitini,ama kwa mkuu wa wilaya,kila mmoja huishi kwa furaha ndani ya ndoa hii,kila mmoja huona fahari kuona mwenzi wake akikua nakutimiza ndoto zake....lakini ndoa itokanayo na msukumo wa kisheria...hujengwa katika tamaa,majivuno,hofu,kisasi...na kila mmoja hujitazama yeye anapata nini,mmoja huwa mtumwa na mwingine huwa mfalme.Hawa kinachowaunganisha ni sheria,(hofu) bali waliopendana kwa dhati upendo huwaunganisha.
 sisi twapendana kwa dhati.....kwetu thamani si magari,fedha,ufahari,umaarufu....sisi huvumilia,upendo hushinda yote
          Hivyo ,ni wazi kuwa ili uishi maisha ya furaha katika ndoa, unapaswa kufanya mabo yafuatayo
  1. Kubadili fikra zako,ya kuweka mategemeo ya kupata kitu fulani toka kwa mwenzi wako,kisha anza kutazama kwa mtazamo chanya,jitolee,timiza jukumu lako,daima kumbuka kuwa wewe una jukumu la kumfanya mwenzi wako akue na kutimiza malengo yake maishani,hivyo ni wakati wa kuacha kuomba tu Mungu ambadili mwenzi wako,bali muombe abadili fikra zako.
  2. Ondoa hofu,toa hofu juu ya mwenzi wako kuwa atakusaliti,atakuumiza,..anza kumtazama kwa wema,mfanye aamke na kutambua wajibu wake,hofu hupelekea kujaa wasiwasi na kufanya maamuzi yasiyo na manufaa.
  3. Zipo nyakati mbalimbali katika maisha,kuna wakati wa shida,raha......uvumilivu utokanao na upendo hurejesha matumaini..hivyo jipende wewe,kisha jifunze kumpenda mwenzi wako kama unavyojipenda wewe
  4. Tumezungukwa na jamii yenye maoni tofauti,sikiliza sauti ya moyo wako.....kama unaingia katika mahusiano kwa kusikiliza ushauri ama maoni tu ya wenginme pasipo kuchunguza na kusikia moyo wako,unatengeneza njia ya maangamizi yako mwenyewe,kama utambagua mytu kwa sura,umbo,rangi,kabila ama hali,basi umejibagua mwenyewe toka moyoni mwako
  5.  
       
      unapomsikiliza,kumthamini na kumjali mwenzi wako licha ya mapungufu ya kimaamuzi,hujenga ndoa imara na yenye furaha
     upendo hautazami nini mimi ninapata,bali mwenzangu anafanikiwa vipi kwa uwepo wangu



  Kuna rafiki  yangu alikataliwa kuoa kwa sababu ya kabila lake,akiambiwa kuwa 'mtoto wetu hawezi kuolewa na kakabila hako,labda ungekuwa umesoma sana maana sisi kabila letu ni wasomi,yupo ambaye aliwekewa pingamizi eti kwa sababu ya tofauti ya dini,....waliofanya hivi husukumwa na mali na hali.....upendo haujali dini,kabila wala hali........Kama hatujajitambua,basi migogoro katika ndoa haitakwisha kabisa....tafakari njema
 
     
   
      

DUNIA INAKUHITAJI

 dunia inakuhitaji uwatazame wenzako kwa huruma,ukijali mahitaji yao,ukiwainua na kuwafanya wajitambue na kujikwamua(picha kwa hisani ya www.viewtz.com)
DUNIA HAIITAJI WATU WENYE FEDHA NYINGI,MAGARI,NYUMBA,NGUO NYINGI AMA WENYE UMAARUFU MKUBWA..DUNIA INAHITAJI WATU WENYE KUJITOLEA KWA WENGINE,WENYE UTAJIRI WA UPENDO,WENYE KUUGUZA,KUPONYA,KUAMSHA MATUMAINI YA WALIOKATA TAMAA,WENYE KUSAMEHE NA KUTAZAMA UPYA KWA UPENDO,WENYE KUPIGANIA UHURU ,WENYE KUJALI NA KUTETEA WENGINE.,WENYE KUTENDA YALE YANAYOONEKANA HAYAWEZEKANI,..DUNIA INAKUHITAJI WEWE KWA YOTE HAYA.CHUKUA HATUA
 tunapaswa kuwapenda wengine ,kuthamini changamoto zao na kuthamini mawazo yao ,kuwa tayari kujitolea pasipo kujali rangi,kabila,dini,taifa.picha kwa hisani ya helped by animals
 

SONGA MBELE.







 KAMA HUWEZI KUPAA,USILALAMIKE,...KIMBIA,  KAMA HUWEZI KUKIMBIE USIKATE TAMAA,TEMBEA......KAMA HUWEZI KUTEMBEA USIBAKI TU UNALALAMA, TAMBAA,ILI MRADI TU KILA SIKU UNASONGA MBELE

Saturday, July 28

AMUA KUBADILIKA AMA KUBAKI ULIVYO


 ni wewe unaeweza kuamua juu ya kubadilikakuyaendea mafanikio AMA kutobadilika na kubaki ulivyo(picha kwa hisani ya mtandao)
           
          Ni wazi kuwa unatambua kwamba nazungumzia kuhusu kufanya mabadilko ili kuyafikia mafanikio uliyoyakusudia.Mafanikio kwangu nina maana ya kutimiza jambo lolote lile ambalo umepanga kulifanya maishani mwako,ambalo linakuletea furaha moyoni mwak Kila mara tumekua tukisubiri kuchukua hatua ya kubadilika,tumekuwa tukitarajia tutabadilika baadae,kesho,wiki ijayo,mwezi ujao ama mwakani,lakini hakuna wakati zaidi ya sasa,yaani wakati uliopo.Usisubiri kesho ama mwakani,kila jambo lipo mikononi mwako,ni wewe tu kuamua.Na pale tu utakapotambua sababu ya wewe kuishi,ndipo utakapoanza hatua kubwa kuelekea mafanikio.
            Tunao pia uwezo wa kuamua kutofanya chochote,kuamua kubaki tulivyo,kubaki na umasikini wetu,kubaki na malalamiko yetu,kubaki na huzuni zetu...tunao uwezo huu.Tunaweza pia kujifanya tumeamua kubadilika,hasa pale ambapo hatujitambui...tutajifanya tumebadilika ili kuwafurahisha watu fulani,kwa uoga wetu...Tunaweza kuamua hili.Tunaweza kuamua kukaa tu pasipo kazi,tunaweza kuamua kuchagua ujinga badala ya kuelimika, tunaweza kuchagua kuamini uzushi  dhidi ya ukweli,,kuchagua woga dhidi ya kujiamini,yoote haya ni uchaguzi wetu.......Tunaweza kujikumbusha toka kwa Shakespear,ambaye alisema(kwa tafsiri isiyo rasmi)kwamba 'suluhisho la matatizo ytu na maamuzi yetu halipatikani juu,kwenye nyota,bali ndani yetu wenyewe 
          Tunayo jukumu na maamuzi juu ya uchaguzi wa maisha yetu wenyewe,ili kuandaa maisha bora kwa ajili yetu kesho na kwa ajili ya wengine.....na maamuzi haya yanaanza sasa.Anayetafuta mafanikio hatafuta miujiza wala maneno mengi,bali ni msukumo wa maamuzi unaotoka moyoni,kutenda kwa ukweli na kwa bidii,Anayehitaji mafanikio hatazami nyuma na kukata ytamaa,bali hutazama mbele kwa matumaini,akijitolea nafsi yake yote kutenda.Anatambua kuwa hakuna muda wa kujadili afanye nini,wa kujadili mambo yaliyopita,bali kwake,hutazama kufanya tofauti na mawazo ya wasio liona tumaini jipya,wasiouona ushindi mbele...
                  Kwa yeyote anayehitaji mabadiliko katika maisha yake,kama unaona unachokifanya hakibadili maisha yako,badlika ukitazama malengo yako...wewe si jiwe,una akili na uwezo,amua kubadilika sasa.


 ni maamuzi yako kuchukua hatua ama kubaki ulivyo(picha kwa hisani ya the rhododendron  walk,George Mark)
     
     Kama utazidi kuzamisha kichwa chako ndani ya maji,ukiwa huna kifaa chochote,basi tambua kuwa huwezi kutambua upo sehemu gani,unakwenda wapi na umefika hatua gani,mpaka pale utakapoamua kunyanyua kichwa na kutazama,..tunafundishwa kuchukua hatua juu ya kubadili maisha yetu wenyewe.Tambua kuwa ili kubadili maisha yetu ,tambua unataka kuwa nani,weka maleno,chukua hatua kutekeleza malengo,amini uwezo wakop na kuutumia,vumilia mpaka mwisho,...wale wote waliofanikiwa walifanya maamuzi,wakachukua hatua kuyatekeleza.Ukiamua,zipo nafasi zisizo na ukomo..chukua hatua ........kila ukitakacho kitakuwa chako.siku njema

Friday, July 27

UTAMBUE UHURU WA KUCHAGUA USIO NA MIPAKA


 BINADAMU TUMEPEWA UHURU WA KUCHAGUA NA UHURU WA MAWAZO USIO NA MIPAKA
                      Kama  unaishi maisha ambayo ni matokeo ya kuchaguliwa na mtu,basi wewe si huru.Kama unafanya jambo mfano biashara ama kazi yeyote kwa sababu tu wengine wanafanya basi haupo huru,unaishi maisha ya utumwa ,ni mtumwa wa maamuzi ya wengine.Je unaishi na kutenda mambo ambayo eitha mama ama baba yako anakusukuma utende?(Sizungumzii kuwa unapaswa kukataa ushauri wa wazazi ama marafiki,namaanisha ujifunze kuamua na kutenda kadiri moyo wako unavyokutuma na si kuishi maisha ambayo unachaguliwa).unapaswa kuwa halisi,kuchagua unachokipenda,unachokikusudia na kuishi maisha yenye sababu itokayo moyoni mwako.Je umeeza kuamua kuwa huru katika fikra zako na kuwa huru katika kuchagua maisha uliyoyakusudia?
          
                  Tumepewa uhuru mkubwa wa kuchagua kila kitu.Mungu aliyetuumba ametupa wa  kuchagua kila jambo pasipo mipaka.....ametupa pia uwezo wa kufikiri pasipo mipaka..na kutafuta suluhisho la matatizo yanayotukabili pasipo  mipaka.Ni fikra zetu wenyewe ndizo huweka mipaka katika uhuru huu wa kuchagua na kufikiri na hivyo tunafikiri kuwa Muumba wetu ametuwekea sheria na mipaka katika kuwaza na kufikiri.(Ni sawa na kusema fikra zetu ndio mpaka(ukomo) katika kuwaza na kuchagua).Tunafikiri kuwa kufikiri  pasipo mipaka ni dhambi,hivyo tunapofikia ugumu katika kutatua matatizo yetu wenyewe na kuchagua,huwa tunaogopa na kudai kuwa 'tunamwachia Mungu' ama' Mungu  ndo anayejua.'
   
                Unapofika hapa duniani unakuwa huru kabisa katika kuchagua.Fikiri kama tungekuwa tuna mipaka,ugunduzi unaofanya tuyatawale mazingira yetu ungepatikanaje?Uhuru wa kuchagua na kufikiri tuliopewa si sawa na uhuru tunaoutengeneza sisi katika maisha yetu ya kila siku wenye vigezo na masharti,uhuru usio kamili.Uhuru huu ni ule ambao wewe binafsi ni mwamuzi wa kila jambo.Nayo nchi hutekeleza yale unayoyaamuru. Muumba anakuwa mtazamaji tu katika kila uchaguzi unaoufanya (na si mwamuzi katika uchaguzi unaoufanya).Kwake kila jambo ni jema(simaanishi utende kinyume na jinsi sauti ya moyo wako inavyokutuma ambako huleta majuto).Hakusukumi wala kukuzuia kuchagua jambo lolote ama katika kuwaza pasipo mipaka.Anataka wewe uchague utakuwa  nani,anataka wewe uchague kile kilicho ndoto yako(chaguo la moyo wako),anataka uwe na uhuru katika kuwaza na kuchagua kutatua ugumu wowote wa kimazingira ili uweze kuitawala dunia na kuifanya kuwa sehemu bora kabisa.Anataka uchague jambo ambalo kila ukiamka  unakua namsukumo wa kulitenda kwa ajili ya utukufu wake  na  kwa ajili ya kila binadamu.Haingilii uchaguzi wowote,hata ule ambao unauchagua na unakuletea matokeo yasiyo mazuri.Huu tunauita kuwa ni uhuru usio na mipaka wa kuchagua na kuwaza.
                
                     Kwa kutambua hili kuwa Muumba wetu katupatia uhuru,wa kuchagua na kuwaza,usio kuwa na mipaka yeyote,ni wazi kwamba mafanikio ama kutofanikiwa kupo ndani yako,furaha ama huzuni ni uchaguzi wako,usawa ama matabaka yanatoka kwako,upendo ama chuki unatoka kwako,kuanguka mna kusimama kunatoka kwako,kuishi  maisha ya furaha ama yasiyo na furaha ni uchaguzi wako,na tukumbuke kuwa kwa kuwa uchaguzi ni uhuru wa kila mmoja,hivyo anayehusika na uchaguzi wako ni wewe mwenyewe.
                   
                  Kama nilivyoeleza hapo awali,fikra zetu wenyewe ndizo zinazoleta mipaka katika kuchagua na kutafuta suluhisho la matatizo yetu wenyewe.Natoa mfano,majuzi nilikuwa nikijadiliana na rafiki yangu ambae tumekua pamoja na kusoma pamoja.Tulikuwa tukizungumza kuhusu suala la ajira,yeye aliniambia kuwa amekuwa akitafuta kazi kwa muda mrefu  sana,na hata kukata tamaa,katika kujadiliana nikamshauri ni vema akaanza sasa kufikiri kuhusu kujiajiri yeye na kuajiri wengine,badala ya kufikiri kuajiriwa tu.Hapa ndipo  palipokuwa na mjadala mkali,kwamba licha ya kusoma,lakini familia zetu hazina uwezo wa  kutupatia mitaji,mimi nikamueleza kuwa mtaji mkuu kwetu sisi si fedha tuliyonayo,bali ni mawazo tulionayo....wazo hili lilionekana kuwa haliwezekani'haiwezekani kujiajiri kabisa....haiwezekani nikafanya kazi mtaani saa na mtu ambaye hajasoma,na ni mpaka miaka mingapi ntafanikiwa'
             
                      Mawazo ya msomi huyu ndiyo adui mkubwa wa yeye kudhubutu kufanya na kuchagua kufanya kile anachokipenda,elimu aliyoipata ni elimu ambayo inamfanya wakati wote afikiri tu kuajiriwa(inamuwekea ukomo katika kufikiri na kutatua matatizo),elimu tunayoipata katika vyuo vyetu na shule zetu ni elimu ya kikoloni,inayolenga kuwafanya watu wawe wafanya kazi wa wengine(kutumika),wawe tegemezi na kwao kufikiri kujiajiri ni kosa kubwa,..elimu hii inafanya fikra zetu ziwe  na mipaka katika kufikiri na katika kuamua.Inatengeneza ukuta mkubwa kati ya fikra zetu na maamuzi.Tusipogundua hili na kubomoa ukuta huu,mafanikio na kutimiza ndoto (matarajio tuliyoyapangilia)

uhuru usio na mipaka,mafanikio yasiyo na mipaka




  uhuru wa kuwaza usio na mipaka,uhuru wa kuchagua usio na mipaka ndio unaoleta ugunduzi katika dunia hii,ndio unafanya binadamu ayatawale mazingira.

uhuru  wa kuwaza usio na mipaka,unaotoka ndani ya mtu mwenyewe umeondoa ule msamiati wa haiwezekani(imposible)
picha zote kwa hisani ya mtandao na fresh mind matter



                              Kumbuka kutumia uhuru huu usio na mipaka kuchagua maisha yako,sikiliza moyo wako,usisikilize sauti za watu ambazo si halisi kwako.U CHAGUZI WAKO BINAFSI NDIO UCHAGUZI WA MUNGU KWAKO (kila ambacho moyo wako hukusukuma kutenda kikuleteacho furaha na amani moyoni mwako,hutoka kwa Mungu,ndio sauti ya Mungu na uchaguzi wa Mungu kwako).Unaweza kuchagua kuamka na kuanza upya baada ya kuumizwa katika mahusiano,ama kuendelea kulala,unauhuru wa kuchagua kuishi maisha yako mwenyewe kwa kufanya unachokipenda,ama kufanya tu kwa kufuata mkumbo,una uhuru wa kuchagua upendo,ama chuki,una uwezo wa kuchagua  mtumwa ama kuwa huru

  mazingira na athari katika fikra na uhuru wa kuchagua
                     Tumezaliwa katika mazingira tofauti,lakini yote yakiwa na misukumo yenye athari katika fikra zetu.Tumezunguka na mazingira yenye umasikini wa fikra ,na umasikini katika uhuru wa kuchagua.Mazingira yetu yanatufanya tuamini kuwa kuna nguvu ambayo inayo maamuzi juu ya maisha yetu,na ni pale tu nguvu ile itakapoamua kutupa uhuru,wa mawazo na kuchagua basi ndipo  tunapata mafanikio,ama kama nguvu hiyo itachagua kinyume basi hutokea.Kumbe ukweli ni kwamba uhuru wa kuamua maisha yetu yaweje,tuishi vipi upo ndani yetu.
                     Tunaaminishwa kuwa pale fikra za moyo wako zinapokusukuma utende kuwa ni shetani,tunaogopa kutimiza kuishi vile mioyo inatutuma,matokeo yake tunaishi kadiri wazazi ama viongozi wetu wa kiimani wanavyotaka, tunaishi kwa hofu maisha yetu yote--(kiongozi bora si yule anayekufundisha utende anavyotaka yeye,bali anayekupa mwanga wa kutambua maisha yako halisi,kuyasikiliza na kuyaishi,ambaye furaha yake ni wewe kuishi kadiri nuru yako inavyokuongoza na si kadiri ya maamuzi yake)
                       Unaweza ukajiuliza maswali ,kwa nini sisi waafrika hasa,hatufanyi ugunduzi,na wala hatuamini katika mambo yetu tunayopanga kuyafanya,tunaamini katika kila jambo ambalo linasemwa na watu toka ulaya na amerika?Ni kwa nini  kila jambo linapotokea linalohusisha uzembe,uvivu na mapango mibaya tunalichukulia kuwa  ni kazi ya Mungu ama shetani/?
  

     ni fikra zako ndizo zinazokuwekea ukomo wa kuwaza na kutenda

                           Jibu umelipata,licha ya kutojiamini katika tutendacho,hatuamini katika uwezo wetu,na imani zetu zilitwazo na mazingira zimetujengea hofu na mipaka,tunajiogopa wenyewe,tunamuogopa Muumba wetu abaye ni rafiki aliye ndani mwetu,na kisha tunaamini kuwa wapo wengine waliobarikiwa kufanya kila jambo kwa ajili yetu,tukiwaabudu hao.(ukimuogopa Mungu  badala ya kumpenda na kumchukulia kama rafiki ambaye wakati wote upo nae,utaishi kwa woga na hofu maisha yako yote,na wala hutapata kujua dhamira yako kuwepo duniani).
ELIMU YAO WALIOTUJENGEA IMETUFANYA TUWE WATUMWA,tumekuwa wafungwa sio kwa kuwa tupo  jela,bali jela yetu ni fikra zetu wenyewe.Namaliza kwa kusema,Tunahitaji watu wanaoutambua uhuru wa kufikiri na kuchagua maisha ,usio na mipaka na hivyo wanaodhubutu kubadili msamiati wa haiwezekani kuwa inawezekana.Wanaoweza kutafuta mbinu mpya(sio zile tu ambazo tumekariri na kuamini hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo(hizo)),pasipo kujali kuwa ni mjini ama kijijini,pasipo kujali kuna vifaa ama hakuna,pasipo kujali tumewezeshwa ama hatujawezeshwa,bali katika kila hali ushindi utapatikana......kama wapo walioweza katika mazingira magumu,kwa nini tusiwe sisi,kwa nini tunaogopa kuchukua hatua..kwa nini tunauogopa uwezo wetu......TUSIMAME TUSEME TUTASHINDA




Tuachane Na Fikra Za Malalamiko, Upanuliwe Wigo Katika Ubunifu




Na: Meshack Maganga, Mjengwablog-Iringa.

Rais wa enzi hizo wa taifa la Marekani Theodore Roosevelt (Oktoba 27, 1858- Januari 6, 1919) alipata kusema, “What we need is more people who specialize in the impossible”, kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili ni kwamba, “Tunachohitaji ni watu wengi zaidi ambao wamebobea katika kufanya mambo yanayoonekana ama kudhaniwa kuwa hayawezekani, (specialists)”.

Kauli ya Roosevelt inanikumbusha habari ya vijana wawili waliohitimu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Vijana hawa walipokuwa chuoni muhula wa pili, mwaka wao wa kwanza wa masomo walibuni biashara ya usafiri wa bajaji. Walichanga shilingi laki nane kutoka fedha ya mkopo wanayopewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu, ndipo wakanunua gari hiyo ya miguu mitatu na kufanya biashara hiyo ambayo iliwasaidia sana kuwakwamua kiuchumi.

Kwa mujibu wa maelezo yao ni kuwa wakati wakitambulisha wazo lao kwa wenzao waliambiwa “hilo haliwezekani!”. Wanasema kuwa katika kauli ambayo hawataisahau ni ile waliyoambiwa hivi, “Hiki kitabu cha UDSM kitawapaje muda wa kusimamia hiyo biashara yenu? Labda kama mpo tayari kwa supp zisizokwisha zitakazofuatiwa na disco”. Maneno hayo hayakuwazuia, walianzisha biashara wakaendeleza na bado walifaulu masomo yao. Wakafanikisha kisichowezekana!

Miaka ya karibuni watanzania tumeshuhudia kuanzishwa kwa utaratibu wa kuchangia gharama katika elimu ya juu. Suala hili ndilo lililopelekea kuundwa kwa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Bodi hii hutoa mikopo kwa wanafunzi hao; katika viwango tofauti tofauti kutegemea na vigezo ambavyo imeweka kwa mujibu wa sheria na taratibu za uendeshaji wa bodi hiyo.

Mabadiliko ya mifumo ya gharama za elimu ya juu nchini Tanzania yanatupa somo muhimu sana kuhusu alama za nyakati. Ni suala la uhakika kuwa siku zijazo mchango wa moja kwa moja wa serikali katika kusomesha vijana wetu utafutika. Hapa naikumbuka kauli aliyopata kuisema Mkurugenzi wa shule ya Star International ya mjini Iringa, Madam Jessca, namnukuu, “Ninawekeza leo kwa kutoa sadaka na kuimarisha biashara zangu, ili siku Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, itakapokosekana, wanangu wasishindwe kupata elimu ya juu” mwisho wa kunukuu. Hakuna haja ya kupambana na nyakati kwa kuzililia zama za Mwalimu J.K Nyerere ambapo elimu ilitolewa bure, bali tukabili nyakati zilizopo na kujipanga kwa nyakati zijazo

Tangu kuundwa kwa bodi hii kumekuwepo na malalamiko mengi sana kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusiana na mfumo huu wa uchangiaji wa gharama pamoja na utaratibu na utendaji wa bodi hii katika kufanikisha lengo hili.

Kuna wadau ambao kwa asilimia mia moja wanapingana na utaratibu huu wa kuchangia elimu ya juu na kuna kundi ambalo linaunga mkono. Sehemu kubwa ya kundi la pili inakwazwa na namna bodi hii inavyotenda kazi zake na kupelekea, mikopo kuchelewa kuwafikia wanafunzi kwa wakati husika, kukosekana kwa mbinu sahihi katika kubaini wapi wanastahili madaraja gani, pamoja na upendeleo (ama uzembe?) katika kupanga madaraja haya ya mikopo.

Bodi hii hutoa mikopo kwa madaraja kwa upande wa ada, “tuition fees” pamoja na fedha ya mafunzo kwa vitendo. Kuhusu fedha za chakula na malazi wanafunzi hupewa kiwango kinacholingana bila kuzingatia madaraja waliyopata. Hadi wakati huu bodi hii inatoa shilingi, elfu tano kwa siku, ama laki moja na nusu kwa mwezi, kama gharama za chakula na malazi.


Kumekuwa na changamoto zinazobainishwa na wanafunzi hawa kwamba kiwango cha fedha wanazopewa hazitoshi katika kuwawezesha kusoma kwa uzuri. Ingawaje vyuo hivi vipo katika maeneo tofauti tofauti, changamoto zinazowakabili wanafunzi hawa nyingi zinashabihiana.

Wanafunzi wengi wanatoka katika familia za kimasikini ambazo pengine hata 70,000/= ya kulipia ada katika sekondari walizotoka zilikuwa zinawapiga chenga. Sasa chukulia kuwa huyu mwanafunzi anapewa mkopo wa asilimia themanini, na yupo katika chuo ambacho gharama ya shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo ni 1,800,000/= Hii ina maana kuwa bodi ya mikopo itamlipia ada shilingi milioni moja na laki mbili na itampa shilingi milioni moja na laki mbili ya malazi na chakula kwa mwaka.

Katika ada atakuwa anadaiwa shilingi laki sita, (600,000/=). Hizi laki sita anatakiwa azilipe kutoka katika ile fedha ya malazi na chakula. Akilipa hizo ina maana anabakiwa na shilingi laki sita tu kwa mwaka wa masomo. (Isisahaulike kuwa bodi ina ukomo wa viwango vya kuwalipia ada wanafunzi inaowadhamini, ukomo huo ni milioni moja na nusu kwa mwaka wa masomo.) Laki sita kwa miezi nane ya masomo, kulipia pango, kununua chakula na kujipatia mahitaji mengine ya msingi kiuhalisia haitoshi.

Tatizo la mikopo isiyotosha elimu ya juu ni la kimtambuka kwa maana kuwa linahusisha pembe nyingi. Kuna suala la ada kubwa katika baadhi ya vyuo, kiwango kisichotosheleza cha fedha inayotolewa na Bodi ya mikopo kwa siku kwa chakula na mavazi, mfumo wa utoaji wa elimu ya juu nchini pamoja na fikra zilizopo miongoni mwa wanafunzi wengi wanaosoma elimu za juu.

Mwanazuoni mmoja wa nchi za Magharibi, G.K Chesterton amewahi kuelezea shida inayowakumba watu kupata ufumbuzi kwa matatizo yanayowakabili, yeye anasema “It isn’t that they cant see the solution. It is that they can’t see the problem” (Sio kwamba hawaoni ufumbuzi wa tatizo, ila ni kuwa hawalioni tatizo). Kuwa na tatizo ni kitu kimoja na kulielewa tatizo (chanzo cha tatizo, lilipo na madhara yake ikiwa halitatatuliwa) ni kitu cha pili. Tuna tatizo la mikopo isiyotosheleza kwa wanafunzi wa elimu ya juu lakini ufumbuzi wake umeendelea kuwa suala la kufikirika na imebaki kulaumiana.

Wanafunzi wa elimu ya juu na baadhi ya wadau wanadhani kuwa suluhisho la tatizo hili ni kuongezwa kwa kiwango cha mikopo. Serikali inasikia lakini haitendi kwa mujibu wa matakwa haya. Tayari pande mbili husika hazijakubaliana na ufumbuzi wa tatizo hili; ina maana kuwa eidha upande mmoja haujalielewa tatizo vizuri ama pande zote hazijalielewa.

Hata hivyo mwathirika mkubwa ni huyu mwanafunzi anayesomeshwa na bodi ya mikopo katika taasisi hizi.Hakuna namna zaidi ya mwanafunzi huyu kupanua wigo wa fikra zake na kuona ni namna gani ataishinda changamoto hii kwa mbinu na njia zilizo halali. Daima ufahamu uliopanuliwa katika njia mpya za kupata majibu ya changamoto, haurudi kamwe katika mipaka yake ya mwanzo. Zikomeshwe fikra za malalamiko, wigo upanuliwe katika ubunifu, badala ya mawazo ya kuilaani Bodi ya mikopo na serikali kwa mikopo isiyotosheleza ni vema kupanua fikra katika kujitegemea

Huu ni wakati ambao vijana wetu wanatakiwa kushusha chini vidole vyao vilivyoielekea serikali na kutazama ni nini kinaweza kufanyika kujikwamua. Mwanaharakati wa kweli hupambana kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vyake vijavyo. Tujiulize, maswali yafuatayo. Je, vizazi vijavyo vitaishije pindi mchango wa serikali kwa elimu zao utakapofutika, ikiwa hatuweki misingi ya kujitegemea sasa? Vilio vyetu vimesikilizwa kwa kiasi gani? Je, tuendelee kulia ama tufute machozi, tujifunge mikanda tutazame tatizo kwa namna tofauti?

Hakuna maana ya kuweka nadhiri za chuki zitakazoliangamiza taifa kutokana na yale yanayopitiwa kwa sasa. Nafahamu wapo vijana wetu ambao kutokana na adha wanazozipata katika utaratibu huu wa mikopo, wananadhiri kuja kulipiza kisasi. Nao wanaweka nia za kuja kupukutisha rasilimali za taifa ili kunufaisha matumbo yao na ya ndugu zao. Vijana wetu wa vyuo vikuu lazima watambue jambo hili, ya kuwa uovu wa baadhi ya viongozi waliopo madarakani haupaswi kuhalalisha wengine kutenda maovu. Msomi ni lazima awe na ndoto za kuubadili ulimwengu wake kutoka hatua moja kwenda nyingine iliyobora zaidi.

Ipo haja kubwa sana kwa wanafunzi wa elimu ya juu kujijengea utamaduni wa kijasiriamali ili kwa fedha kidogo wanayokopeshwa waweze kuzalisha na kufidia upungufu unaojitokeza katika gharama za masomo yao. Nikigusia suala la ujasiriamali inawezekana kuwepo na vikwazo vingi, ikiwemo muda na mazingira ya kufanya huo ujasiriamali, ukosefu wa rasilimali (mitaji) na mengine mengi upendayo kuorodhesha. Anayevuka na kutatua vikwazo hivyo, huyo ndiye “specialist” wa yasiyowezekana!

Wanafunzi wengi waliopo katika taasisi zetu si wenye juhudi katika kufikiria, ubunifu na kufanya kazi kwa kujituma. Waangalie wanafunzi hawa jinsi wanavyoutumia muda wa likizo zao ndefu na fupi, mara nyingi hawafanyi kazi eidha za kulipwa ama za kujitolea. Mara nyingi hutoa sababu zinazosema na kuonesha kuwa hakuna kazi. Wananata, hawataki kukaa vijijini hata kama kuna fursa nyingi, wanataka kumalizia likizo zao Dar es Salaam.

Kuna wakati unaweza kudhani kuwa vyuo vya elimu ya juu hupendelea kufanya udahiri wa kimikoa, kwa sababu wengi wanataka kutambulika kama wakazi wa majiji hasa Dar es Salaam. Miezi mitatu ama mine ya likizo mtu yupo jijini kwa mjomba, binamu au kwa wa kutoka kijiji kimoja kule Songea, hana kazi zaidi ya kula, kulala, kuoga na kuangalia TV. Wakati mwingine analala sebuleni, na kulala kwake ni mpaka wote waende kulala! Kama mwanafunzi huyu angeenda hata kijijini kwenye kata ya nyumbani kwao akajitolea kufundisha shule ya kata kwa miezi minne angekuwa amezalisha angalau laki mbili!

Ninao mfano wa rafiki yangu mmoja ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe, ambaye amekuwa mbunifu na alishaupiga teke ulimbukeni wa kujiona kuwa eti “wa elimu ya juu” kuna kazi hatakiwi kuzifanya hata kama zinamwingizia kipato. Huyu kila likizo huwa anarudi kijijini kwao na huko huutumia muda wote katika kufanya biashara ya alizeti. Huzunguka vijiji mbalimbali akikusanya na kisha kusafirisha alizeti hizo kwenda mjini. Katika moja ya likizo yake ya miezi minne, aliingiza mtaji wa shilingi laki tatu (fedha za bodi ya mikopo) na kuzalisha jumla ya shilingi milioni moja na laki sita.

Hawa wanafunzi wa vyuo vya juu, imewapasa kuwa na macho ya ndani yenye uwezo wa kuvumbua na kuzitumia fursa. Kuna kuwekeza kwa aina nyingi ambako wakati mwingine mtu si lazima awepo muda wote katika kusimamia alivyowekeza. Inawezekana kumiliki hisa katika makampuni, kuingia ushirika wa kibiashara (partnership) ama kuitumia jamii ya wanafunzi wanaowazunguka, kubuni biashara ama miradi itakayowaingizia vipato.

Pale juu katika makala haya nilitaja pembe zinazochangia mtambuka wa tatizo hili. Ingawa niliacha pembe zingine tatu, ni dhahiri kuwa zinachangia sana katika kufanikisha ufunguzi wa hizi fikra  za hawa wanafunzi wa elimu ya juu. Nitachambua pembe hizi katika makala mengine, lakini itoshe tu kusema, ukiwa na tatizo ni lazima ujikague na kujirekebisha vizuri kabla hujamvaa anaechangia kukua kwa tatizo lako.

Leo hata kama wanafunzi hawa wakaongezewa fedha na kulipwa 20000/= kwa siku, bado watagundua kuwa fedha hiyo haiwatoshi. Suluhisho sio kuililia serikali pekee wakati tumekaa na kubweteka. Tutalala, tutaamka, tutaandamana na kujikuta bado tuko pale pale. Badala ya kuwaza ukahaba, wizi na ujanja ujanja wa kukopeshana na kudhulumiana hebu wasomi wetu waanze kutumia taalveuma zao kufanya ubunifu na kujikwamua. Hii inawezekana ila kwa wale watakaojitolea ku-specialize katika yasiyowezekana.
 Na kila mwanafunzi wa elimu ya juu anayeguswa na hili analazimika kuwa specialist wa yasiyowezekana!

Thursday, July 26

KUMBUKA YAFUATAYO UNAPOPATA HOFU NA KUVUNJIKA MOYO

 Upo wakati ambapo tumnapita katika magumu ,huwa tunafika wakati tunashindwa kujitambua,na wakati mwingine tunapatwa na msongo mkubwa wa mawazo hata tunakata tamaa.Kila wakati jitazame ndani mwako,usome uwezo wako ulio ndani mwako...utaondoa hofu,woga na kukata tamaa.Jikumbushe ya kuwa wewe u bora vile ulivyoumbwa.....wewe ni bora kwa sababu zifuatazo

   Wewe  ni wa pekee,unaipenda nafsi yako,hivyo unampenda Muumba wako na watu wote   pasipo kujali sura,rangi,kabila,dini , na hivyo upo katika uhuru na usalama pote ulipo

  • Unatambua kuwa furaha,amani havitoki nje yako na kwamba furaha ya kweli huanza ndani yako
  • Wakati wote katika maisha yako unaishi ukithamini wengine na kuhakikisha kuwa wewe ni sababu ya wengine kuamka na kufanikiwa,hivyo unapata marafiki na ndugu kwa maisha yako halisi,hivyo wote anaoutambua mchango wako,wanathamini maisha yako.
  • yote yaliyopita kwako,hayakufanyi uwe mnyonge bali yote hayo yalikuwa ni mwanzo wa wewe kuyaendea mafanikio,na hivyo daima utatazama sasa(wakati uliopo) na kuyaandaa maisha yako yajayo kwa kujali pia maisha ya wengine.
  • unatambua kuwa kuanguka(kushindwa) si mwisho wa maisha ,bali ni mwanzo wa kuuelekea ushindi na kadiri unavyoshindwa mara nyingi,ndivyo unavyokuwa mpya kupambana na huhesabu ni mara ngapi umeanguka,bali ni mara ngapi na namna gani umesimama na kushinda.
  • unatambua ya kuwa katika maisha hakuna jambo lililo baya kama kukata tamaa,hivyo magumu hayatakupoteza katika lengo uliloliweka,bali yatakupa mbinu mpya za kufika uendapo.
  • kwa kuwa kila jambo unalolitenda linasukumwa na upendo,na daima unafurahi kuona wengine wakifurahi,unajitolea,unatazama wengine kwa huruma,unawakumbuka wenye mahitaji,hivyo yote yaliyo mema unaowatendea wengine yatakuja kwako pasipo wewe kutegemea.
  • kwa sababu  unayo imani,unayo matumaini na upendo na daima unaepuka hasira,masengenyo,woga,choyo na visasi.
  • unatambua kuwa kutochukua hatua kwa kuogopa kufa ama kuumia ni usaliti wa nafsi yako mwenyewe.
  • moyo wako unawapenda wale ambao jamii imewasahau,unawatia moyo wale walioshuka moyo na wenye katika hali ya kukata tamaa,wwe ni rafiki wa waliotengwa,na  tumaini jipya kwa wasio na tumaini.
  • Daima upo tayari kusamehe,unatazama mbele kwa tumaini la maisha mapya,unaitika sauti ikuitayo kwa ajili ya yatima,wafungwa,wagonjwa,wajane na daima unasimama upya kuyafikia matazamio yako.
    • unapokuwa msaada kwa wanyonge,watima,wajane,wafungwa,matatizo yako yote hupata suluhisho(picha kwa msaada wa mtandao)
    • kwa kuwa unakiri na kutambua na kutumia nguvu na uwezo,akili na  uwezo usioonekana uliopewa na Muumba(Mungu)  kwa utukufu wa Muumba wako,na yote utayafanya kwa ajili ya binadamu wote,hivyo utaepuka kudhuru,kuumiza wengine.
    • kwa sababu unatambua tu kuwa,ili kuwa mkuu mbele ya wengine...ni lazima uwe mtumwa kwanza

Wednesday, July 25

HEKIMA.

Upo wakati ambao tunawalaumu wengine kwa matatizo yetu wenyewe ,lakini hakika,ukijitambua utajua ya kuwa wewe ni kiongozi wa maisha yako, utatambua kuwa wewe ni chemchem ya kila jambo,utaweza kuchanganua lipi la kushika,lipi la kuachia,utakwenda sambamba na mdundo wa maisha yako. utasimama na daima utakuwa na furaha maishani......

Wakati mwingi maishani,tunatengeneza maadui.tunawachukia wengine kwa kudhani kuwa wao ni sababu ya matatizo yetu,tunadhani ya kuwa wapo watu ambao ni wateule katika kutatua matatizo yetu wenyewe,na wakati mwingine tukiwaogopa na kuwafanya kuwa wakuu,ukweli ni kuwa  fikra zetu ndiye adui mkuu,utambuzi tu humfanya adui huyo mkuu kuwa rafiki mkuu katika kutatua matatizo yetu,kusonga mbele na kuyatawala mazingira yetu,na ndipo tutavitazama vitui katika uhalisia wake..

 Kila jambo lina kinyume chake,kuna upendo na chuki,kuna kishinda na kushindwa,kupanda na kuvuna.....utakapoanza kutazama kila jambo kwa mtazamo mpya,mtazamo chanya,utagundua kuwa kila jambo linapotokea huwa si mwisho,bali huwa ni mwanzo wa jambo lingine......kifo si mwisho wa maisha,ni mwanzo wa maisha mapya,kushindwa ni mwanzo wa ushindi.,dhihaka ni mwanzo wa heshima,chuki ni mwanzo wa upendo,udhalimu ni mwanzo wa ubinadamu......na hivi vyote hutoka ndani yetu wenyewe

 Tunafikiri k uwa nafsi zetu na Muumba wetu ni utengano...kwamba Muumba wetu yupo mbali nasi,kumbe yupo ndani mwetu,ni mawazo yetu tu ndio yanayotutenganisha na asili yetu..

  Shujaa si yule aliye na nguvu nyingi,wala hasira nyingi,wala simwenye umbo la kutisha,ama anayeweza  kuwapiga watu kwa hesabu yake....shujaa wa kweli ni yule ambaye huamini katika ushindi,huamini kuwa anaweza,na akawa tayari kupita magumu yote hata anapofika pale anapopachagua kufika,shujaa wa kweli hutazama kila jambo kama nafasi yakwenda mbele.
  
 Anayekata tamaa hana tofauti na yule ambaye anapoteleza ama kujikwaa na kuanguka hanyanyuki tena akiamini kuwa hawezi tena.
  Kila jambo huwa na mwanzo,anayeanza vibaya na kumaliza vibaya ni yule tu anayeamini kuwa kuna nguvu nje yake ya kubadili kile alichokichagua na kukiishi,naye mwanzo wake na mwisho wake,vyote husababishwa na nguvu hiyo iliyo nje yake,lakini ,yule anayejitambua....husimama na kuanza upya pale anapotambua kuwa nguvu zote za ushindi zipo ndani mwake.

Aibu,hasira,woga,chuki,ubinafsi na kulipiza kisasi(visasi) ni sifa za mtu asiyejitambua,asiyetambua kuwa anapotenda yote hayo kwa wengine anajitendea mwenyewe....anayefikiri kuwa ana akili na uwezo kuliko wengine hushusha uwezo wake wa kutenda na kujenga mambo mapya,anapofika ukomo wa fikra zake....husema kuwa haitawezekana tena na hakuna atakayeweza tena
  
  Anayelitambua jambo  pasipo kulitekeleza ni sawa na chumvi ama sukari isiyofaa...kama unajua kuwa wengine wananyonywa,ukanyamaza,kama unafahamu  hakuna linaloshindikana ,kisha ukaogopa kuchukua hatua,utajilaumu sana wakati wa kuiaga dunia hii,utajilaumu kwa kutokuwa chanzo cha mabadiliko,kuwa chanzo cha upendo,kuwa chanzo cha kuwaamsha wengine..lakini ukitenda lile unaloliamini,unapokuja muda wa wewe kuiaga dunia,utaiaga kwa furaha,nawe utakumbukwa kama ishara ya ushindi na nuru ya Mungu iliyo ndani mwako,,itang,aa daima,naamini,dunia itakulilia utakapoondoka
.

Monday, July 23

KWANGU MAFANIKIO NI.........

   UPENDO HUSHINDA YOTE

PICHA KWA HISANI YA MTANDAO

sihesabu  mafanikio katika maisha yangu kwa  kuhesabu idadi ya  namba za wale wanaonipigia simu,ama wale nliopata kuwa nao,nisiokuwa nao na nilio nao,sihesabu ni fedha kiasi gani nlichonacho,ama mimi ni wa daraja lipi,sihesabu nguo nlizonazo,ama ni vyuo gani na vingapi nimesoma....sihesabu ni marafiki wangapi ninao,ama kama nipo pekee,,,,,,,.nahesabu mimi ninawapenda wengine kiasi gani,na ni kiasi gani nawaumiza wengine,na mimi mwenyewe kwa chuki....nnahesabu,mimi ni nani na najitambua kiasi gani,,nahesabu heshima,usawa ,furaha,ubinadamu,amani..nahesabu ni namna gani nimeleta upendo palipo na chuki,,najifunza kutojisifu wala kutafuta sifa...nahesabu kutazama mbele na kuwa na imani na hakika ya ushindi,nahesabu ni maneno gani ninayasema na yana maana gani,yanawajenga vipi wengine.Kwangu maisha ya mafanikio ni kuwakubali wengine jinsi walivyo na si kwa kutazama mali wanazomiliki,Zaidi ya yote,kwangu maisha ni kuishi kwa kusikiliza moyo wangu,kwa dhati,na kuifanya nuru ya maisha yangu iwaguse wengine ,ili nao  wanapochagua  kuishi maisha yao kwa dhati-Pongu Joseph-0717903089

SIKILIZA SAUTI YA MOYO WAKO

Kabla ya kuanza kusoma makala hii,nakusihi uifanye huru fikra yako,fungua fikra zako,usifungwe na imani na mafundisho fulani ili usiathiri uelewa wa makala hii(your mind may become your great enemy,so empty it) ......Pili uwe huru kutafakari ndani ya moyo wako na kuuliza.

 Simaanishi unachoamini wewe ni uongo nami nnaandika ukweli.Jambo haliwi kweli eti  tu kwa sababu limeandikwa ama limesemwa..ama kwa sababu wengi wanaliamini,bali ukweli kuhusu jambo hutoka kwa mtu mwenyewe,kwa kuliishi jambo na kulifahamu.Mfano,hakuna anayeujua ukweli kuhusu wewe,isipokuwa wewe,hakuna anayeweza kujua ukweli kuhusu upendo,isipokuwa ameuishi upendo na kuifahamu chuki.

  Moyoni mwako,pana siri kubwa......ambayo ukiitambua,utakuwa umefungua njia ya ushindi katika kila jambo unalolitaka.


moyo wako ni chemchem ya uwezo wa ki Mungu
moyo wako ni chemchem ya uwezo wa ki Mungu ,ni hekalu la mawasiliano kati yako na asili yako(Muumba wako,Mungu,Mwenye uwezo wote)

   Moyo wako ndipo chimbuko kuu la mawasiliano kati yako na ASILI YAKO(MUNGU).Mungu hawasilIani nawe kwa kutumia vitabu,ama kwa kutumia maneno,bali huwasiliana nawe kupitia moyo wako.

Yeye huweza kutumia njia zingine endapo tu mhusika hasikilizi sauti ya moyo wake.Kwake matumizi ya lugha si ya lazima kwa sababu lugha huweza kuchanganya na wakati mwingine tafsiri huchangia kudhoofisha ujumbe uliokusudiwa.Hivyo  basi,kumbe Mungu huweza kutumia njia mbalimbali kufikisha ujumbe kwa watu,lakini njia iliyo kuu isiyoweza kupotea ama kuchanganya ni kupitia moyo wa mtu husika..

  Kwa wale wakristo,watakumbuka ya kuwa,miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu....
   Pia ikumbukwe kuwa Yesu alipata kuwaambia wanafunzi wake ya kuwa,hawaisikilizi sauti ya Mungu kwa sababu wameifanya migumu mioyo yako.
  Kuna wakati ambapo mtume Mohamed (S.A.W) alipata kuwaambia wafuasi wake ya kuwa yeye alikuwa akisikia sauti ya Mungu ikimtuma kutenda......wakashangaa,wakataka kujua ni kwa nini wao hawakusikia,sababu ni moja....waliifanya migumu mioyo yao.

  Hivyo ni  wakati sasa wa kutambua kuwa ule uzima tunaoutafuta kila siku,ile chemchem ya ushindi katika maisha,haipo mbali nawe,usiitafute juu kwenye nyota,usiitafute ndani ya sinagogi,usiitafute tu msikitini,na wale haijajitenga nawe,bali ipo ndani mwako.
SAUTI KUU IKUONGOZAYE KWENYE USHINDI IPO NDANI MWAKO
SAUTI KUU IKUONGOZAYE KWENYE USHINDI IPO NDANI MWAKO
 
    UTAITAMBUAJE?
    Mungu hukutuma kutenda kupitia moyo wako...pale unapopata hisia  na msukumo wa kutenda uletao faraja na furaha,usio na chemchem ya tamaa ya kupata sifa,wala fedha wala utajiri wa aina yeyote,bali kila unapoisikiliza sauti hii na kutenda kadiri inavyokutuma,hufungua milango ya ushindi(UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU ,KISHA YOTE MTAZIDISHIWA)

    Sauti hii hutuongoza kutenda kwa upendo,na sauti hii humjuza muhusika mwisho wa jambo alitendalo,naye aisikiaye hutambua matokeo yake,na hivyo kila aisikiaye sauti hii,haklati tamaa,hasikilizi maneno yanayomvunja ari,bali huyafanya yote kwa bidii.
  KUMBUKA..
  Kwa kuwa moyo wako huwasiliana na asili yako(mungu),basi,kila aliye tayari kuisikiliza sauti ya moyo wake,huwasiliana moja kwa moja na asili yake(mungu),wakati wowote ule pasipo vikwazo.Wapo wanoamini kwamba kuna wateule tu ambao huweza kuzungumza na Mungu,jibu ni laah,kila mtu ana uhuru na usawa mbele za Muumba,naye Muumba huwasiliana na kila mtu pale mtu huyo anaposikiliza moyo wake...
  Kwa udadisi huu,ni wazi kuwa moja ya sababu kwa nini wakati fulani unaomba.,haupati majibu,ama haufanikiwi ni kwa sababu,wewe huchagua jambo kwa kutazama tu faida,na wala si lile ambalo moyo wako unakusukuma kutenda(litokalo kwa Muumba) ama  unaomba usichokipenda toka moyoni mwako(kwa tamaa eitha ya kuona toka kwa wengine,eengi tunatafuta kufanya jambo tuwe kama watu fulani,tupate pesa ama mali,ama umaarufu,-vijana wengi siku hizi wanatafuta kazi ambayo wanasikia wanalipwa vizuri,wengi wanasomea kozi mbalimbali kwa msukumo wa malipo,si kwa msukumo toka moyoni-mfano udaktari kwa sababu wanalipwa fedha nyingi,ama uhasibu,ama kompyuta nk,lakini wale wanaosoma kwa msukumo wa moyo,wanaosukumwa na kujitolea na kutoa huduma kwa kujali utu na ubinadamu,hao hufunguliwa milango ya mafanikio......nao hutenda kwa bidii)
 Jifunze kutambua hisia za moyo wako.....jifunze kuingia ndani ya moyo wako na kujitazama kwa kina,tazama muungano kati yako na asili yako.....sikiliza moyo wako,sikiliza sauti ya moyo wako
                       
     

SHUKRANI

    SHUKRANI KWA KUJALI NA KUTHAMINI


Kila binadamu huhitaji kutambulika na kila mmoja wet u hufurahi kuona ya kuwa wengine wanamjali na kuthamini mchango wake.....kile anachokifanya,ama kukisema.......kwa kutambua hili,nachukua  nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote ambao wamekuwa wakitembelea blog hii.
  Shukrani yangu ya kwanza iende kwa Muumba wa vyote,ambaye ndiye aliye asili na chemchem ya elimu yote,kwa kuniweka salama na kunifanya mimi nijitambue ni nani,kisha kushiks kalam na karatasi na kuandika.......yale ambayo yanawaamsha wengi,na kuwafanya si tu wajitambue...bali wasimame na kuchukua hatua ya kuishi maisha wanayoyakusudia,wakijitolea kwa ajili ya wengine.
  Pili kwenu ninyi mnaoingia katika blog hii na kushiriki katika kusoma,na hata kuwaeklimisha wengine.Mnapoonesha kujali na kutaka tufike mbali zaidi na kuwaamsha wengi.Shukrani yangu kwangu ni kuendelea kujitolea zaidi,kuandika kwa sababu najua kila wakati yatupasa kutazama ni jninsi gani tutashinda.Si kwamba mimi ni mwalimu,bali ninyi mnaoingia na kushiriki kutoa maoni...mmekuwa walimu wangu...najifunza mengi kupitia wote wanaotuma maoni na wengine wengi.Rai yangu kwenu ni kwamba waalikeni wengine wengi tujifunze.....kama unao uwezo print pasipo kuathiri umiliki,wape wengine wasioweza kufikia huduma hii .....kuwa nuru kwa vitendo...amsha walio wahitaji..jitolee kwa dhati.
                                        

   chagua kuwa chemchem ya wengine kuamka

    Haikuwa  rahisi kuanza kufanya kazi hii ya uandishi....auonae mwisho husukumwa na upendo ,kutenda pasipo kukata tamaa,kuna furaha katika kutoa kuliko kupokea,na ndio maana tunaendelea mbele........Zipo blog nyingi sana,zinazofahamika sana na zenye kutembelewa na maelfu wa watu.......sisi tumeanza ....tutafika huko.Kwa ushirikiano wetu tutafika,lengo likiwa kuwafanya wengi wajitambue,na kuamsha upya matumaini ya wengi......tutafika,kwani katika mapambano(ushindani),wapo wenye kasi,wapo walio nanguvu...lakini anayeshinda ni yule anayeamini katiaka ushindi.....Tutashinda kuwafanya watu wajitambue,tutashinda kuamsha matumaini,tutashinda na kufundisha upendo....
    Natambua ya kuwa  mimi na wewe tunayo sababu ya kuwepo hapa duniani,nikitambua hilo,nitaishi kwa upendo,nitafundisha upendo na kuufundisha  kwawengine si kwa kuusema tu bali kwa kuuishi.Nitajiamini na kutenda kwa upendo..nikijitolea kwa ajili ya wengine pasipo kujali malipo ,ama dharau na kejeli.,kwa sababu hivi havitabadili ukweli ya kuwa mimi ni nani ....nitajitolea na kushiriki kuwaamsha waale wote walio wahitaji..nimejifunza kuwa mimi si chochote pasipo wengine,hivyo matendo yangu na majitoleo yangu yatatazama furaha ya wengine,nikiwapenda na kuwajali kama ninavyoitendea nafsi yangu....nina imani ya kuwa nitakua na kufikia mafanikio hata pale panapoonekana kuwa hapawezekani...kwa pamoja tutaweza
    Shukrani ziende kwa familia yangu,kwa wote waliokuwa tayari kujitolea ili blog hii ifanikishe lengo lake..Ahsante Mtaki R Muyenjwa Gamba kwa ushauri wa kiufundi  nilipohitaji,Lazaro Mafie,Faith Kassano,na wote walioshiriki kwa kila namna.

Friday, July 20

MAADUI WAKUU KUFIKIA MAFANIKIO

Mafanikio ni kutimiza jambo lolote lile ambalo umelipangilia na kuamua kulitenda kwa dhati.Kuyafikia mafanikio kunahitaji kujitolea,kutenda kwa moyo wote na kwa nguvu zote...ukitilia mkazo lengo(malengo) uliyoyaweka.

Ikiwa umekuwa ukifuatilia makala hizi,utakuwa umeanza kujitambua wewe ni nani na hata kuanza kuchukua hatua stahili kuyainua maisha unayoyapenda,ukichagua na kusikiliza moyo wako.Unaweza kuwa unajaribu tu kutenda na wala si kuamua kuchukua hatua na kuamka,kuishi maisha unayoyahitaji,ukitenda kwa bidii kuyafikia mafanikio,mimi pia nimechagua kusimama,kuacha yaliyopita ambayo hayakuwa msaada kwangu,kusimama na kufurahia maisha,nikitenda kwa upendo na msukumo wa kuona kuwa kupitia mimi,wengine wataiona nuru ya Mungu iliyo ndani mwao kama ilivyo kwangu,wakiishi maisha waliyoyachagua,wakitumia vipawa vyao vyema,na kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi. Yapo mambo ambayo,ni chanzo kikubwa cha kutofikia mafanikio tunayoyakusudia...hayo ni kama ilivyo hapa chini....nakusihi usome kwa makini,ili uweze kuelewa vyema.

 1.KUTOCHUKUA HATUA

KUTOCHUKUA HATUA KUNACHELEWESHA MAENDELEO

USISUBIRI,KESHO AMA MWAKANI KUAMUA KUTENDA,WAKATI NI SASA USIUDHARAU AMA KUUSHUSHA UWEZO ULIO NDANI MWAKO....CHUKUA HATUA
USISUBIRI,KESHO AMA MWAKANI KUAMUA KUTENDA,WAKATI NI SASA .
 USIUDHARAU AMA KUUSHUSHA UWEZO ULIO NDANI MWAKO....CHUKUA HATUA

Wengi wetu tumekuwa tukifikiri kwamba upo wakati fulani wa kuamua kuchukua hatua na kuchagua kutenda kile ambacho sauti ya moyo wako inakutuma kufanya.Tumekuwa tunasubiri kesho,ama tukimaliza shule,ama mwanzoni mwa mwaka unaofuata,ama nikiruhusiwa....Tambua kuwa hakuna wakati mwingine wa kuweka mpango wako wa maisha yako yajayo zaidi ya sasa.

Wakati ni sasa,amua sasa kutenda,usiogope kushindwa,tazama kila jambo katika mtazamo chanya,kushindwa huleta mwanga utakaotuonesha ni njia ipi itakayotufanya kugundua njia mpya ya ushindi,mafanikio yahaji pasipo kukwama,kuangua na kunyanyuka,amini nakwambia kushindwa ndio njia pekee ya kuuendea ushindi.....kama unafanya jambo lisilo na changamoto,tambua kuwa njia hiyo si sahihi kwako...tambua pia kuwa hakuna aliye na jukumu la kuyaandaa maisha yako,Hakuna mwenye jukumu la kukuchagulia maisha,hakuna wa kukusukuma,bali fukuto la ushindi hutoka ndani mwako
HAKUNA WA KUCHUKUA HATUA JUU YA MAISHA YAKO,NI WEWE,HATUA MOJA TU YA MWANZO ITAKUPELEKA KWENYE HATUA NYINGINE YA MAFANIKIO
(REJEA MAKALA- USHINDI HUANZA NA FUKUTO NDANI YAKO Soma hapa)

 2.KUKATA TAMAA
Nikupe siri moja,kama unaamini kwenye dhambi.....hakuna dhambi iliyo kubwa kama kukata tamaa.Kama unaamini katika usaliti...hakuna usaliti ulio mkubwa kama kukata tamaa.
Kukata tamaa ni kutoamini katika uwezo ulio nao,kukata tamaa ni kutotambua uwezo ulio nao,kutoitambua nuru iliyo ndani mwako,kutomjua Mungu aliye ndani mwako.....kukata tamaa ni kwa wale wasio tambua nini wanachokifanya.....anayekata tamaa ni yule asiyeona kinachokuja mbele yake...ni kwa yule asiye na maono ya ndani ya moyo wake.....ni usaliti wa sauti iliyo ndani mwako
ANAYEKATA TAMAA NI YULE ASIYEUJUA MWISHO,ASIYE SIKILIZA SAUTI YA MOYO WAKE...ASIYE NA TUMAINI YA MAMBO YAJAYO
LICHA YA VIKWAZO,WEWE  ATENDAYE KWA UPENDO HAKATI TAMAA,ANAYESIKILIZA SAUTI ya moyo wake
Aujuaye mwisho hakati tamaa
 3.WOGA
 Woga ni matokeo ya kutojitambua, kuogopa kutenda jambo kwa sababu ya kushindwa ama sababu ambazo si halisi,zitokazo katika fikra ya mtu binafsi.
Katika maisha yetu kila mahali tumefundishwa kuogopa.Tumefundishwa kuogopa wazazi,kuogopa walimu,kuogopa viongozi,kuogopa vitu visivyoonekan,tumefundishwa kumuogopa Mungu.....na ndio maana kila wakati tunaogopa kutenda pale moyo unapotutaka kutenda kwa sababu ya woga...woga umetuletea aibu...hatutendi kwa kuogopa macho ya wengine.......(mfano mhitimu wa chuo kikuu anaogopa kupita nyumba hadi nyumba kuuza bidhaa yake..kwa woga wa kuonekana kwa wengine kuwa labda hajasoma...kwa kifupi anaogopa mafanikio yake mwenyewe).

Kumbe woga unatokana na kutoamini uwezo wetu wenyewe...woga ni kukataa kufikia mafanikio yako mwenyewe..chagua kuondoa uoga,chagua umakini,chagua kuwa rafiki wa vyote unavyoviogopa,chagua kuwa rafiki wa Mungu wako

 4.KUTOAMINI KUWA TUNASTAHILI TUNACHOKITAKA
Hiki pia ni kikwazo kikubwa na adui mkubwa wa maendeleo.Wengi  hawaamini kuwa wanastahili kuishi maisha bora,hawastahili elimu bora,hawastahili hata kutenda mambo makubwa..
Mfano ni rafiki yangu mmoja,alipata kuniambia kuwa yeye eti kwa sababu aliishia darasa la saba,haoni kwamba anaweza na wala anastahili kuwa kiongozi,haoni kama anastahili kuishi maisha bora yenye furaha....anaona mbele yake kuwa kuna ukuta mkubwa kati yake na maisha bora ama mafanikio yeyote....anaona hastahili furaha,anajiona kuwa hastahili hata kuitwa katika kazi,hajiamini,haamini kama anastahili kila jambo analolipenda....kwa hivyo huyu hawezi kuijua sauti ya moyo wake. Wakati mwingi maishani tunakosa kufanikiwa kwa sababu tunaamini hatustahili.....rejea makala..(NI JINSI GANI TUNAPATA TUWAZACHO)

Ukiamini huwezi umeshindwa tayari...ukiamini unaweza lakini huchukui hatua,umeshindwa......ushindi ni kwa yule amabaye anaamini ya kuwa mwisho wa pambano atashinda.

 5.KUSHIKILIA MAMBO(JAMBO)AMBAYO YANARUDISHA NYUMA(CHELEWESHA)
Upo wakati tunashikilia mambo ambayo yanatuchelewesha ama yanatuzuia kusonga mbele...mfano kung'ang'ania kukaa katika mahusiano ambayo ni ya maumivu kila wakati....kufanya jambo ambalo (biashara)ama huduma yeyote ambayo moyo wako haupati furaha na wala haukusukumi kufanya....achia songa mbele...kumbuka kwisha kwa jambo moja hufungua milango kwa mambo mengine mengi.....tazama kila jambo kama nafasi ya wewe kwenda mbele......kuumizwa kwenye mahusiano,hakufungi milango ya wewe kwenda mbele....inapobidi,pima,anza upya...utaipata furaha

Wednesday, July 18

WEWE NI BORA JINSI ULIVYO,

i mwanariadha maarufu wa afrika ya kusini,Oscar Pistorius
WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO....ULEMAVU NI FIKRA ZAKO .

Ni wakati mwingine wa kujitambua,sisi ni akina nani na tunakwenda wapi,na tunawezaje kwenda tuendako.....,Leo hii tukijadili kwa undani,uwezo tulionao,tusioutambua..Na mwisho tutatambua ya kuwa,ulemavu unaotambulika wa viungo si kitu,bali ulemavu mkubwa ni wa kukosa kutumia uwezo wetu tulionao wa kufikiri na wa kuumba vitu vipya tukiifanya dunia kuwa sehemu bora na kuishia kuishi kwa uoga na kulalamika,tukitegemea wengine kufikiri na kutenda kwa ajili yetu,tukiwa na macho yasiyo upeo wa kuona,tukiwa na akili,na tusiitumie.......(huu ukiwa ni ulemavu mkubwa)
SINA MIKONO,LAKINI HAIMAANISHI YA KUWA SINA UWEZO WA KUFIKIRI WALA KUTENDA (picha kwa hisani ya mtandao)
  Wewe ni kiumbe wa kipekee,uwe na miguu yote ,uwe umekosa miguu, ama mikono ,ama kiungo chochote cha mwili,bado unabaki kuwa kiumbe wa pekee aliyeumbwa,ukifanana na Muumba (asili yako) kwa uwezo wa kutenda na kuumba(wapo watakaohisi ya kuwa nafananisha moja kwa moja na Mungu,

Ni vema tukatambua ya kuwa Mungu anabaki kuwa Muumba kwa asili yake,na sisi tunabaki na ubora aliouumba,tukifanana na yeye aliye asili ya yote.....). Hivyo uwezo wa binadamu kuyatawala mazingira yake haupo kwenye nguvu za mwili(misuli),haupo kwenye miguu,haupo kwenye mikono bali upo kwenye fikra zake.

 Kwa kifupi,wewe ni bora jinsi ulivyo...uwe na miguu,uwe huna miguu,unabaki kuwa binadamu,unabaki kuwa kiumbe bora wa Mungu,...wewe ni bora jinsi ulivyo.....

 Kila tunapojitazama sisi,tusiishie kutazama sura tu,tusiishie kutazama rangi tu,tusiishie kutazama mvuto wa viungo vyetu tu, bali tujitazame ndani yetu ambako hutufanya tutambulike kwa wengine, kwani ndiko kunakoumba na kutufanya tuchague tutakuwa akina nani,tutaishi maisha yapi,na kutambua matokeo ya uchaguzi wetu kwa wengine...

Yupo kijana mmoja,anayetambulika kwa jina la Nick Vujicic,aliyezaliwa akiwa hana mikono na akiwa na miguu mifupi sana,akizaliwa katika familia isiyo na uwezo mkubwa,alifika wakati akajitambua kuwa jinsi alivyo ni bora sana. Kautambua uwezo wake ulio ndani mwake,akasoma na hata kumaliza chuo kikuu,akitenda mambo makubwa katika michezo,na hadi sasa ni mwenye mafanikio aliyoyakusudia, Anatambua kuwa nuru ya maisha yake haionekani tu kwa sura yake bali kwa uwezo ulio ndani mwake...akitenda kwa ajili ya wengine....Huyu anatufunza ya kuwa ,sisis ni bora jinsi tulivyo...na tunastahili ushindi wowote kadiri ya uchaguzi wetu
NICK VUJICIC AKIWA KATIKA MOJA YA MICHEZO AIPENDAYO,WEWE NI BORA JINSI ULIVYO
NINATAMBUA YA KUWA MIMI NI BORA JINSI NILIVYO,NIKICHAGUA MAISHA YANGU,NA NJIA YA KUISHI,NI KIYATIMIZA YOTE PASIPO KUJALI VIKWAZO VILIVYOPO,HATA PANAPOONEKANA HAPAWEZEKANI,MIMI NITAWEZA
nayafurahia maisha kwa kuwa mimi ni bora jinsi nilivyo
. KWA KUWA NINAJUA NA KUTAMBUA KUWA MIMI NI BORA JINSI NILIVYO,NIKIWA NINA UWEZO MKUBWA NDANI MWANGU...NINAFURAHIA MAISHA YANGU,NIKIFURAHI,NIKICHAGUA MAISHA NA KUYAISHI...WEWE JE
NINAFURAHIA MAISHA YANGU,NIKIFURAHI,NIKICHAGUA MAISHA NA KUYAISHI...WEWE JE
Hivyo basi,ulemavu ni tatizo la kifikra kuliko ilivyo kwamba,ulemavu ni kukosa viungo fulani vya mwili.Hii ni tafsiri yangu ya kimtazamo....kama nlivyoandika katika makala iliyopita yenye kichwa cha habari..NI JINSI GANI TUNAPATA TUWAZACHO...Soma hapa.

NIKIJITAMBUA,NITATAMBUA UWEZO WANGU ,NITAWEZA KUCHAGUA MAISHA YANGU NA KUYAFIKIA MAFANIKIO AHSANTENI SANA
Ni wakati sasa kuamka na kuondoa fikra zote za vikwazo ambavyo vinatufanya tusifanikiwe Ni wakati sasa wa kutambua kuwa sisi ni zaidi ya vile wengine wanavyotutazama,ama kudhani,na ni zaidi ya tunavyofikiri....sisi ni bora jinsi tulivyo na kila wakati tunapojitambua tunapata nafasi ya kuchagua maisha ambayo tunayapenda,tukiyaishi kwa furaha,na kuanzia sasa, hutasikiliza maneno ya wengine kuwa u mbaya,u kituko,ama hauvutii.....haya kwako si kitu,kwani wewe ni bora ukiwa na uwezo wa kuchagua na kuyaishi maisha yenye furaha..na hayo ndiyo mafanikio. PONGU JOSEPH