KWA NINI UMEINGIA KWENYE MAHUSIANO?
JE ILI UPENDWE>?JE UMEINGIA KWENYE MAHUSIANO ILI KUJAZA PENGO AMBALO LI WAZI? UMEINGIA KWENYE MAHUSIANO ILI UFANANE NA WENGINE WALIO KWENYE MAHUSIANO? JE UMEINGIA KATIKA MAHUSIANO ILI KUUMALIZA UPWEKE ULIOKUA NAO?UMEINGIA ILI UWEZE KUWA NA MTU UNAYEWEZA KUMUITA MPENZI?
Je ili kumaliza mgandamizo wa kuachika ama mawazo yeyote?ILI kumkomoa yeyote uliyekuwa nae kwenye mahusiano?ili uolewe?...........................................................?
Kama hizi ni sababu za kuingia katika mahusiano,basi tambua kuwa mahusiano hayo yatakusumbua sana,na itafika wakati utatoa maana mbaya ya mahusiano.....na kumbe wewe ndiye muanzilishi mkuu wa kuteswa,kuumizwa,kupigwa,kudhalilishwa,kutothaminika...na wewe ndiye unayetoa ruhusa ya yote hayo...
Kila mmoja wetu ana uhuru wa kuchagua...usio na mipaka.Na kila unachokichagua ni chema.....ni chema kwako....lakini ukumbuke kila uchaguzi unaoufanya una madhara yake(yenye faida na yasiyo na faida kwako.........
Kabla ya kuingia kwenye mahusiano yeyote,hakikisha unaingia si tu ukitegemea kuwa mwenzi wako atakupa kitu fulani,furaha ama amani,atakufanyia nini,atakujali kiasi gani,atafuata taratibu unazoziweka wewe kwa kiasi gani,atakupenda kwa kiwango gani,atakufariji kwa kiwango gani............bali jiulize wewe utakuwaje chanzo cha upendo katika mahusiano yenu,wewe utakuwaje chanzo cha uhuru usio na mipaka kwa mwenzi wako,utakuwaje ni tunu ya mwenzi wako kukua na kufikia malengo aliyoyapanga,je,wewe utakuwa ni chanzo cha mwenzi wako? kuiona na kuiishi nuru ya Mungu iliyo kwa kila mmoja wenu.....na je ni kwa kiasi gani wewe hauchukui uhusiano kuwa kifungo cha kisheria kati yenu wawili,bali zaidi kuwa ni chachu ya uhuru na msukumo wa mwenzi wako kukua?
Upendo ni kutoa/kujitolea |
Jiulize upendo ni msukumo utokao moyoni kwenda kwa mwingine pasipo kujali chochote jiulize,je unaingia katika mahusiano ili tu utimize matamanio yako ama raha ya mapenzi....?
Upendo wa kweli ni ule ambao hutoka kwa anayejipenda yeye kwa dhati na kuwafikiri wengine juu ya upendo alio nao.....upendo huu huwa juu ya rangi,juu ya ukabila,juu ya dini ,juu ya itikadi, juu ya tofauti za kimtazamo na kifikra......na upendo huu hushinda yote!!!!!!!1
UPENDO NI KUMJALI MWENZAKO LICHA YA TOFAUTI ZENU |
Mahusiano ya kweli yenye afya kwa pande zote mbili huanza na upendo unaotoaka ndani mwa kila mmoja,kwenda kwa mwingine pasipo kuhesabu faida,rangi,kabila, ama tofauti yeyote,bali husaidia kila mmoja aliye ndani ya mahusiano hayo kukua,kutimiza ndoto za kila mmoja ...na kwao hao upendo hushinda yote....
Hivyo basi,ni vema ukajipenda na kutambua maana ya kupenda,ni vema ukasukumwa na upendo ambao ni kitu halisi na si vitu visivyo na mashiko katika mahusiano...ni vema ukatambua kuwa mahusiano ama ndoa,ikijengwa katika minajili ya kila mmoja kuhakikisha anaheshimu mawazo,uhuru wa mwenzi na kuhakikisha kuwa anamsaidia mwenzi wake kuendelea na kukua hata kutimiza malengo yake na hisia zake....upendo ukiwa msukumo mkuu....hushinda yote