NA hivi ndivyo ilivyo.....kila wakati tunapohisi ama kuwaza kwamba jambo fulani matokeo yake yanawezekana ama hayawezekani,ndivyo inavyokuwa...na tunajifunza kuwa binadamu ana uwanja mpana wa kuumba vipya(re create) usio na ukomo.......na pia tuna uchaguzi usio na ukomo wa kufanya jambo......na pale tunapoweka nguvu zetu zote,fikra na uwezo wetu basi jambo hilo hutokea kadiri tunavyolifikiria...... tafakari hili........... msimu wa kilimo umefika,kila mmoja ana uhuru wa kuchagua kwenda kulima na kupanda ,na vivyo hivyo kila mmoja ana uhuru wa kutofanya hivyo...... kila anayechagua kupanda,hupanda mbegu kadiri yA malengo yake na matarajio yake ni kuvuna anachopanda,yaani anayepanda karanga mategemeo yake ni kuvuna karanga....wa mahindi kuvuna mahindi.....mwisho wa msimu kila mmoja atavuna kadiri ya juhudi za palizi na kutunza mazao hayo hivi ndivyo tunavyojifunza,kuwa kila tunapowaza jambo kwa upeo tunao utengeneza,basi jambo hilo hutokea vile vile............ukiamini unaweza kutengeneza kitu kipya na kufanya juhudi,basi hutokea kadiri unavyopangilia.......... ukipanda chuki utavuna chuki,ukipanda upendo,vivyohivyo utavuna upendo picha kwa hisani ya fresh mind matters kwa yule anayechagua kutopanda kabisa,huyo ni yule asiyeamini uwezo juu yake na husingizia mara nyingi changamoto zinazojitokeza.....huyu anaamini kuwa wapo ambao wamepewa uwezo huo na si yeye hivyo,kugundua jambo jipya,ama kutengeneza mwelekeo wa maisha yako.haitokei kwa bahati kwma tunavyofikiri,na wala maisha yako hayakutengenezwa na mtu yeyote...bali wewe una jukumu la kutengeneza kwa fikra isyo kikomo ,na kwa kutumia uhuru mkubwa uliopewa picha kwa hisani ya fresh mind matter
“Wewe hukusoma” na Madhara Yake Katika Ndoa
4 days ago
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa