Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Monday, July 9

SAMEHE,FUNGUA MILANGO YA FURAHA NA MAFANIKIO

Sote tu binadamu,sote hufanya uchaguzi ambao huweza kuwaumiza wengine na kutuumiza sisi pia. Tunaweza kufanya uchaguzi huo eitha kwa kusudi ama pasipo kusudio.Tunawaumiza wengine na kuumiza mioyo yetu...tufanyapo hivyo tunafunga nafasi ya urafiki,ushirikiano na maelewano....,tunajiwekea mipaka ya kupata nafasi za mshikamano. Tunafunga milango ya mafanikio...tunafunga milango na kuweka mstari mpya wa utengano...chuki,ubaguzi,masengenyo, na kikubwa tunajenga uadui mkubwa ambao hutuumiza mioyo yetu wenyewe....


Kutosamehe ni kukaribisha giza(chuki )mioyoni mwetu
Wengi hufikiri tu kwamba kutosamehe ni kuwakomoa wengine,ni kuwafungia milango..kumbe kutosamehe kunafunga milango yako mwenyewe.....Pia wengi hufikiri tu kuwa tunapaswa kusamehe wengine...pasipo kutibu majeraha ya kuumia katika mioyo yetu pale tunapoamua kufanya uchaguzi ambao hutubomoa...Tunafika wakati tunakuwa  na  aibu, na kukata tamaa kutokana na kutosamehe........

 Kutosamehe kunafunga milango yote ya mafanikio...Ni  kuonesha udhaifu mkubwa...kutosamehe ni kutoamini katika upendo...ni kukaribisha uadui wenye aibu mwishoni. Na zaidi ya hayo  ni kuwasha moto wa huzuni moyoni mwako,ni kufifisha uamsho wa mafanikio moyoni mwako

KUSAMEHE NI KUONDOA UCHUNGU,NA MAUMIVU YA MOYO {PICHA KWA HISANI YA MTANDAO)
 KUSAMEHE NI KUONDOA UCHUNGU,NA MAUMIVU YA MOYO...NI KUAMSHA UPYA NGUVU ZAKO ZA USHINDI JIFUNZE kusamehe..

Samehe nafsi yako kwa yote ambayo huwezi kujivunia ya kuwa yalikupa faida mbaya...fungua Moyo wako na kusahau yaliyopita.

1.Fungua mlango wa muujiza wa maisha yako....wote tunahitaji maisha yaliyo na nuru angavu,iletayo mafanikio kwa kuyaishi vyema maisha yetu, kwa kuchagua kutenda kwa upendo kwa wengine,kuwajali na kujali thamani ya kila mmoja...

 2.Kumbuka uwezo wetu mkubwa wa kuifanya dunia kuwa sehemu bora,upo katika kuyatazama maisha ya wengine hasa kwa kusamehe licha ya kuwa upo wakati ambao tuliumia sana

3.Tambua ya kuwa huruma,kupenda usawa,amani na kuyahubiri maisha yajayo na kuyahubiri maisha yetu yaifanyayo nuru ya Mungu ndani mwetu kung'aa ama kufifia, hupimwa na uwezo wa kusamehe...
si kwamba kuonesha udhaifu..bali ukomavu katika kutazama kwa ubinadamu na upendo uliotukuka,hasa kwa wale wanayoyaishi maisha ya ulimwengu usioonekana,lakini pale wengine wanapoweza kujifunza kwao ktk ulimwengu uonekanao..

KUSAMEHE NI KUFUNGUA MLANGO WAKO KWA MOYO WAKO,KUIFANYA SAUTI YAKO ISIYOSIKIKA,ISIKIKE HATA KWA WALE TUWAONAO KUWA NI MAADUI(PICHA NA unconditional love}
4.Kwa kutambua kuwa wenye hasira,jeuri,visasi,majivuno hawawezi kuijenga dunia,bali huibomoa...........twapaswa kujifunza kuijenga,kwani dunia bora huanza kujengwa ndani ya mioyo ya wale walio tayari kujitolea kwa wengine pasipo ghiliba wala majivuno...wala visasi...hivyo basi ni vema kusamehe na kuifanya dunia sehemu bora .

 KUSAMEHE NI KUFUNGUA MLANGO WAKO KWA MOYO WAKO,KUIFANYA SAUTI YAKO ISIYOSIKIKA,ISIKIKE HATA KWA WALE TUWAONAO KUWA NI MAADUI.

 Hili ni jambo kubwa sana kujifunza...pale unaposamehe,na kujisamehe mwenyewe...unafungua mlango wako kwa sauti iliyo ndani mwako,ambayo huanza kufanya kazi,kukufanya uwe wwe uliyo,ufungue mlango wa mawasiliano wewe ni Muumba wako...na ndipo hata sauti yako,ya upendo husikika na kusambaa,hata wale wakuonae adui,sasa huwa marafiki,wakikuthamini na kuutambua ukuu wa kiMungu ulio ndani mwako.........samehe...ufungue mlango wa furaha na mafanikio-

{picha zote kwa hisani ya unconditional love}

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com