Upo wakati ambao tunawalaumu wengine kwa matatizo yetu wenyewe ,lakini hakika,ukijitambua utajua ya kuwa wewe ni kiongozi wa maisha yako, utatambua kuwa wewe ni chemchem ya kila jambo,utaweza kuchanganua lipi la kushika,lipi la kuachia,utakwenda sambamba na mdundo wa maisha yako. utasimama na daima utakuwa na furaha maishani......
Wakati mwingi maishani,tunatengeneza maadui.tunawachukia wengine kwa kudhani kuwa wao ni sababu ya matatizo yetu,tunadhani ya kuwa wapo watu ambao ni wateule katika kutatua matatizo yetu wenyewe,na wakati mwingine tukiwaogopa na kuwafanya kuwa wakuu,ukweli ni kuwa fikra zetu ndiye adui mkuu,utambuzi tu humfanya adui huyo mkuu kuwa rafiki mkuu katika kutatua matatizo yetu,kusonga mbele na kuyatawala mazingira yetu,na ndipo tutavitazama vitui katika uhalisia wake..
Kila jambo lina kinyume chake,kuna upendo na chuki,kuna kishinda na kushindwa,kupanda na kuvuna.....utakapoanza kutazama kila jambo kwa mtazamo mpya,mtazamo chanya,utagundua kuwa kila jambo linapotokea huwa si mwisho,bali huwa ni mwanzo wa jambo lingine......kifo si mwisho wa maisha,ni mwanzo wa maisha mapya,kushindwa ni mwanzo wa ushindi.,dhihaka ni mwanzo wa heshima,chuki ni mwanzo wa upendo,udhalimu ni mwanzo wa ubinadamu......na hivi vyote hutoka ndani yetu wenyewe
Tunafikiri k uwa nafsi zetu na Muumba wetu ni utengano...kwamba Muumba wetu yupo mbali nasi,kumbe yupo ndani mwetu,ni mawazo yetu tu ndio yanayotutenganisha na asili yetu..
Shujaa si yule aliye na nguvu nyingi,wala hasira nyingi,wala simwenye umbo la kutisha,ama anayeweza kuwapiga watu kwa hesabu yake....shujaa wa kweli ni yule ambaye huamini katika ushindi,huamini kuwa anaweza,na akawa tayari kupita magumu yote hata anapofika pale anapopachagua kufika,shujaa wa kweli hutazama kila jambo kama nafasi yakwenda mbele.
Anayekata tamaa hana tofauti na yule ambaye anapoteleza ama kujikwaa na kuanguka hanyanyuki tena akiamini kuwa hawezi tena.
Kila jambo huwa na mwanzo,anayeanza vibaya na kumaliza vibaya ni yule tu anayeamini kuwa kuna nguvu nje yake ya kubadili kile alichokichagua na kukiishi,naye mwanzo wake na mwisho wake,vyote husababishwa na nguvu hiyo iliyo nje yake,lakini ,yule anayejitambua....husimama na kuanza upya pale anapotambua kuwa nguvu zote za ushindi zipo ndani mwake.
Aibu,hasira,woga,chuki,ubinafsi na kulipiza kisasi(visasi) ni sifa za mtu asiyejitambua,asiyetambua kuwa anapotenda yote hayo kwa wengine anajitendea mwenyewe....anayefikiri kuwa ana akili na uwezo kuliko wengine hushusha uwezo wake wa kutenda na kujenga mambo mapya,anapofika ukomo wa fikra zake....husema kuwa haitawezekana tena na hakuna atakayeweza tena
Anayelitambua jambo pasipo kulitekeleza ni sawa na chumvi ama sukari isiyofaa...kama unajua kuwa wengine wananyonywa,ukanyamaza,kama unafahamu hakuna linaloshindikana ,kisha ukaogopa kuchukua hatua,utajilaumu sana wakati wa kuiaga dunia hii,utajilaumu kwa kutokuwa chanzo cha mabadiliko,kuwa chanzo cha upendo,kuwa chanzo cha kuwaamsha wengine..lakini ukitenda lile unaloliamini,unapokuja muda wa wewe kuiaga dunia,utaiaga kwa furaha,nawe utakumbukwa kama ishara ya ushindi na nuru ya Mungu iliyo ndani mwako,,itang,aa daima,naamini,dunia itakulilia utakapoondoka
.
“Wewe hukusoma” na Madhara Yake Katika Ndoa
4 days ago
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa