MWANAMKE HUSIKIA MLIO WA UA HATA UPITAPO UPEPO |
Lengo langu katika makala hii si kufananisha(kulinganisha )kati ya mwanamke na mwanamme,hii ni kwa sababu hakuna kilicho bora kuliko kingine....kila kitu kipo vile kilivyo na ubora huja na kukamilika pale mtu anapotumia uhuru wake wa kuchagua,kuchagua anavyotaka awe,aishi....na kila achaguapo huwa.
Lengo langu ni kutaka kufunua yale yaliyofichika kuhusu mwanamke......ni baada ya kujifunza kupitia wanawake wengi......nikapata hisia za kuandika kuhusu kiumbe hiki kilicho bora,ishara ya upendo,uaminifu,huruma na chemchem ionekanayo ya ubinadamu na uwezo wa Mungu kwa mwanadamu....hisia zinanituma kumuona mwanamke kuwa ni ukamilifu aliouumba Mungu baada ya mwanaume kuwa na mapungufu mengi.(nieleweke kuwa simaanishi mwanaume si bora)(kwa Mungu kila kitu ni bora kadiri alivyokiumba)...
yapo mambo mengi ambayo mwanaume alikuwa ameyakosa kuitimiliza dunia.....hivyo mwanamke akaumbwa akikamilisha yale ambayo yalikuwa ni muhimu(alikamilika yeye kama mwanamke katika dunia timilifu na si kwamba anautimiliza ukamilifu wa mwanaume,mwanaume anabaki kuwa bora jinsi alivyoumbwa,na mwanamke anabaki na ubora wake, wote wakiuishi utimilifu wao kwa ushirika wao
.
Maisha yetu huwa yapo katika mzunguko...yanaanza na maisha fulani,yakimalizika,huanza mengine,mfano tupo hapa duniani,baada ya kumaliza maisha yetu hapa,huenda kuanza maisha mengine mapya,kadiri tunavyochagua.......anayefahamu hili anathawabika kwa ufahamu wake...lakini anayeliishi...ana hekima na hufanikiwa...
mwanamke huishi kwa kufuata mfumo huu....hata pasipo kutambua.,.mwanamke hukubali haraka maisha anayoyaishi..akiyaishi pasipo kuigiza...akitenda upendo...akiishi huruma,akiishi ubinadamu,akiishi kwa kila matarajio ya maisha ya baadae.....
Mwanamke huyaishi maisha yake kwa unyoofu wake...pale anapoamua kuishi kwa dhati,huishi kwa dhati..hulea kwa dhati,hukarimu kwa dhati,hufungua moyo wake kwa wengine kwa dhati....hushiriki na wengine katika kila jambo linalohitaji ushirikiano....huuguza kwa dhati,huvisha kwa dhati...na hii ni ishara ya kila mafanikio katika maisha...yaani kulichagua jambo na kulifanya kwa dhati...wanaume wachache huweza kuamua hivyo...wanaume hugusa hiki na kile,hufanya kwa muda tu,hutamani dunia bandia,huchelewa kukubali maisha yaliyo halisia.....
MWANAMKE ,UPENDO,UVUMILIVU ULIOTUKUKA....HATA PALE ANAPOONEKANA KUSHINDWA..HUSIMAMA-HUJITOLEA KWA DHATI HATA KATIKA NYAKATI AMBAZO YEYE HUHITAJI ZAID |
Mwanamke huuona upendo usioonekana,hutambua wakati wa kulia,wa
kucheka,anatambua wakati wa kulishika jambo (na kulishika kwa moyo wake
wote,) na anafahamu wakati wa kuachana na jambo linalomuumiza na kuanza
upya maisha.....huu ni mfano bora wa mafanikio katika
maisha..................yaani kulishika jambo kwa dhati....na kuyaacha
yale yanayoturudisha nyuma,kwani mara nyingi tunashindwa kwenda mbele
kwa sababu tunashikilia mambo ambayo yanatuumiza na kutufanya tuhindwe
kwenda mbele......mwanamke huweza kuyatambua mambo haya
vema..........hata akitelekezwa,husimama na kuanza upya maisha...ishara
ya uvumilivu na ishara ya kujikubali na kujiamini na kwenda mbele hata
pale ambapo wale wanaomzunguka hawaamini ya kuwa....ATASIMAMA TENA
kwa mwanamke majaribu kwake ni mtaji wa ushindi |
MWANAMKE HUFURAHIA MAISHA,NA KWENDA NA MDUNDO WA MAISHA |