tupo hapa duniani kwa ajili ya wengine,si kwa ajili yetu tu.....tuwatazame wengine kwa upendo,kama tunavyojipenda sisi.....huwezi kusema una upendo kama hujafanya matendo yanayouonesha upendo,huwezi kusema una utu kama matendo yako si ya utu...wala huwezi kusema kuwa wewe ni wa thamani kwa wengine kama hutendi kwa thamani kwao wakati wote...ni vema upendo uwe ni mwongozo wetu ili nuru ya maisha yetu ing'ae.maisha ya yeyote anayejitambua ni kutenda kwa ajili ya wengine..ka anayetambua,katika macho ya ndani,basi vitu vidogo ni vikubwa na kila kimoja huhesabiwa na kurudisha kadiri utoavyo,kutambua ni kujielewa..unaweza kufanya chochote pale upatapo moyo wa kufanya hivyo.....nawe unapata moyo wa kuendelea mbele..ni ukweli kwamba huwa tunafanya uchaguzi usio na manufaa kwa wengine na kwetu wenyewe,na hivyo ndovyo tunavyojifunza....hizi ni changamoto....nuru tulionayo ...ni dawa tosha kwa wengine...hasa pale upendo unapokuwa ndio msukumo wa awali...tazama kila tunapohitaji kunyanyuka tuangukapo,twatazama ile nuru......na kumbe hiyo nuru ndiyo ile waitazamiayo wengine...kumbe tumeunganishwa.....kila mmoja wetu kwa upendo..binafsi ... mimi si wa tofauti,nawe huna tofauti nami...wote tu wamoja...kila mmoja akiitazamia nuru ...nuru iliyo ndani ya kila mmoja...kila mmoja wetu..na tazama kila nijitoleapo kwa wengine...moyo wangu hujazwa furaha isiyo kifani....na ndipo sauti iliyo juu ya upeo wangu inapozidi kuniamsha na kunifundisha mengi.....na kuzidi kunifanya nitambue ya kuwa nipo ka ajili ya wengine.nawe kumbka ya kuwa upo kwa ajili ya wengine.la sivyo maisha yako yasingekuwa katika dunia hii ya kutegemeana kwa vipawa vyetu
“Wewe hukusoma” na Madhara Yake Katika Ndoa
4 days ago
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa