Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Tuesday, July 3

WITO/NDOTO

Wito hutokana na sauti itokayo ndani kwa mtu..wito si shinikizo.Ni sauti ya pekee imuitaye mtu kutekeleza jambo fulani. kila mmoja wetu huitwa kutekeleza jukumu lake hapa duniani...na kila mmoja anaitwa kwa wakati wake...ni vema kila mmoja akatambua.lakini je,tunatambua kama tumeitwa,je tunaisikiaje sauti hii? kuna jambo ambalo moyo wako hukutuma mara nyingi kulifanya.....wakati mwingine unakuwa hulitilii maanani lakini hurudi na kukukumbusha....tofautisha na tamaa ya mwili ambayo mara nyingi huchagua vitu rahisi na vinavyotuletea umaarufu,wito hutuma kulifanya jambo hilo wakatio wote...na moyo husikia faraja kulitenda jambo hilo...japo wakati mwingine fikra hutuma mtu kutochukulia maanani,kwani wito ni kujitolea zaidi....wito ni kujitoa na kujitolea kuliko kupewa/kupokea. kama nlivyoeleza hapo awali,wito ni msukumo wa moyo,ni sauti ya Mungu inayotutuma kutenda kwa upendo,unyenyekevu na kujitolea vkuhakikisha nuru yako (Mungu aliye ndani mwako)inaonekana kwa wengine kwa vitendo...wito si nukuu tu ya maneno....wito ni kuishi maisha halisi,na kushirikisha kipawa/vipawa ulivyonavyo kwa wengine na kuhakikisha kuwa kila binadamu anafaidika na matunda ya kipawa chako......kama ni kuimba..imba kwa moyo wako wote na kuwafunza wengine.......kama ni kucheza,cheza kwa moyo wako wote......kama ni kufundisha...fundisha kwa moyo wako wote....kama ni kuandika...andika kwa moyo wako wote...kama ni kutibu.....tibu kwa moyo wako wote.......kama ni kulea lea kwa moyo wako wote. Unahitaji kujiuliza,wewe ni nani na je Kw A nini upo hapa duniani?...kisha tambua ya kuwa MUNGU ambaye wakatiwote tunamtafuta...yupo ndani mwako......kisha mpe ruhusa ya kuwa mueklekezi wako kwa kufungua moyo wako....na kusikiliza sauti yake....epuka kujichagulia jambo kwa sababu litskupstis tu fedha ama ukwasi....usichagua kuwa daktari ili upate ukwasi,usichaguia kuwa muhubiri ili upate ukwasi...usichagua kuwa injinia,mwanamuziki,muigizaji ili tu upate fedha....bali sikiliza sauti ya moyo wako ambayo daima hukutuma kuyatenda yote kwa upendo,unyenyekevu na huku ukijitoa kila ulichonacho kutimiza ndoto....naye Mungu aliye ndani mwako atakupa vyote..... furaha yangu si katika kupata umaarufu,ama utajiri...bali ni kuona kila mmoja anajitambua na kuifanya dunia kuwa sehemu bora

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 Comments:

Post a Comment

maoni yako hapa