Umeumbwa ukiwa mshindi....wewe ni mshindi....tambua ya kuwa wewe ni mzaliwa wa ukoo wa ushindi toka hapo awali....lakini kushinda yote yapasa kwanza kujitolea kwa moyo wote na nguvu zote kutekeleza yale ambayo umedhamiria kuyafanya...tekeleza majukumu yote kwa uaminifu na bila shuruti..jiamini katika K ila ukifanyacho binafsi na katika maamuzi ya jumuia..kuwa na moyo wa imani kuwa unao uwezo wa kufanya kitu kipya chochote unachokidhamiria hata kama wapo wameamini ya kuwa haiwezekani...kwani tumezungukwa na wale ambao kwao vingi haviwezekani...kwao wao ,wapo wateule ambao wamepewa uwezo fulani(jambo ambalo si sahihi)kuwa na tumaini moyoni mwako hasa pale ambapo tumaini huwa ni hitaji(wakati wa changamoto ) na kuwa kioo kwa wote wanaokuzunguka..(kuwa kioo haimaanishi kutafuta umaarufu ama kutenda ili ujulikane na kujipatia chochote,bali ni kutenda kwa bidii yako yote...na mafanikio yako yanakuwa ni mfano kwa wengine)uwe na moyo wa kujitolea kila wakati...tena kujitolea pasipo tegemeo la kupewa chochote(unconditional giving)kupenda na kuwajali wote na kwa maana hiyo kuufundisha upendo kwa wengine...jiamini na kupigania imani yako hasa pale ambapo wengine wote huona ama hudhani kuwa hauko sahihi(mradi tu wewe unaongozwa na visheni yako)uwe tayari kutenda kwa wema kwa wengine,na kujifunza kutoa kwa wale wenye mahitaji...jitoe(jitolee) kwao pasipo fikira na malengo ya kujipatia ama sifa ama zawadi yeyote.jiamini na kutenda na kufikiri kwa mfano wako wa kipekee bila kufuata fikra na njia za watu(simaanishi usifuate ushauri wa wengine,bali kwa mwenye visheni yake..huongozwa na mwongozo wa visheni yake na sio mitazamo ya wengine),kwani naamini njia za wengine zitakupeleka ktk matokeo yao,bali isikilize sauti iliyo moyoni mwako ili maisha yako yawe ya mfano kwa watu wote,na kwa kufanya hivi utawafundisha wengine kujitambua na kuishi maisha yao yasiyo ya bandia...ukumbuke ya kuwa Ipo sauti inayokutuma kutenda jambo moyoni mwako...hii ni sauti iliyo moyoni mwako na mwisho...usikate tamaa.
“Wewe hukusoma” na Madhara Yake Katika Ndoa
4 days ago
great Mr Pongu
ReplyDeletethanks Uncle Tom
ReplyDelete