Nuru Ndani Yako

Nuru Ndani Yako
Nuru Ndani Yako
Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.

KARIBU SANA

HONGERA KWA KUCHAGUA BLOG HII.MAISHA NI UCHAGUZI...NA KILA UCHAGUZI NI SAHIHI....KILA UCHAGUZI UNA MATOKEO YAKE.......KUCHAGUA KUSOMA YALIYO KATIKA BLOG HII KUTAKUFANYA UJITAMBUE,,UUJUE UWEZO MKUBWA ULIO NDANI MWAKO NA HIVYO KUFIKIA MAFANIKIO UNAYOYAKUSUDIA........WEWE NI ZAIDI YA UJIONAVYO,NI ZAIDI YA UJIPIMIAVYO.....UTATAMBUA YA KUWA MUNGU AMBAYE KILA UCHAO WATU WANAMTAFUTA...YU NDANI MWAKO.....UTATAMBUA KUWA U MWANGAZA.....NA UTATAMBUA JINSI YA KUUTUMIA KUWAMULIKA WENGINE...NA KUIFANYA NURU YA MUNGU ILIYO NDANI MWAKO IONEKANA KWA WENGINE-PONGU JOSEPH

Friday, July 27

UTAMBUE UHURU WA KUCHAGUA USIO NA MIPAKA


 BINADAMU TUMEPEWA UHURU WA KUCHAGUA NA UHURU WA MAWAZO USIO NA MIPAKA
                      Kama  unaishi maisha ambayo ni matokeo ya kuchaguliwa na mtu,basi wewe si huru.Kama unafanya jambo mfano biashara ama kazi yeyote kwa sababu tu wengine wanafanya basi haupo huru,unaishi maisha ya utumwa ,ni mtumwa wa maamuzi ya wengine.Je unaishi na kutenda mambo ambayo eitha mama ama baba yako anakusukuma utende?(Sizungumzii kuwa unapaswa kukataa ushauri wa wazazi ama marafiki,namaanisha ujifunze kuamua na kutenda kadiri moyo wako unavyokutuma na si kuishi maisha ambayo unachaguliwa).unapaswa kuwa halisi,kuchagua unachokipenda,unachokikusudia na kuishi maisha yenye sababu itokayo moyoni mwako.Je umeeza kuamua kuwa huru katika fikra zako na kuwa huru katika kuchagua maisha uliyoyakusudia?
          
                  Tumepewa uhuru mkubwa wa kuchagua kila kitu.Mungu aliyetuumba ametupa wa  kuchagua kila jambo pasipo mipaka.....ametupa pia uwezo wa kufikiri pasipo mipaka..na kutafuta suluhisho la matatizo yanayotukabili pasipo  mipaka.Ni fikra zetu wenyewe ndizo huweka mipaka katika uhuru huu wa kuchagua na kufikiri na hivyo tunafikiri kuwa Muumba wetu ametuwekea sheria na mipaka katika kuwaza na kufikiri.(Ni sawa na kusema fikra zetu ndio mpaka(ukomo) katika kuwaza na kuchagua).Tunafikiri kuwa kufikiri  pasipo mipaka ni dhambi,hivyo tunapofikia ugumu katika kutatua matatizo yetu wenyewe na kuchagua,huwa tunaogopa na kudai kuwa 'tunamwachia Mungu' ama' Mungu  ndo anayejua.'
   
                Unapofika hapa duniani unakuwa huru kabisa katika kuchagua.Fikiri kama tungekuwa tuna mipaka,ugunduzi unaofanya tuyatawale mazingira yetu ungepatikanaje?Uhuru wa kuchagua na kufikiri tuliopewa si sawa na uhuru tunaoutengeneza sisi katika maisha yetu ya kila siku wenye vigezo na masharti,uhuru usio kamili.Uhuru huu ni ule ambao wewe binafsi ni mwamuzi wa kila jambo.Nayo nchi hutekeleza yale unayoyaamuru. Muumba anakuwa mtazamaji tu katika kila uchaguzi unaoufanya (na si mwamuzi katika uchaguzi unaoufanya).Kwake kila jambo ni jema(simaanishi utende kinyume na jinsi sauti ya moyo wako inavyokutuma ambako huleta majuto).Hakusukumi wala kukuzuia kuchagua jambo lolote ama katika kuwaza pasipo mipaka.Anataka wewe uchague utakuwa  nani,anataka wewe uchague kile kilicho ndoto yako(chaguo la moyo wako),anataka uwe na uhuru katika kuwaza na kuchagua kutatua ugumu wowote wa kimazingira ili uweze kuitawala dunia na kuifanya kuwa sehemu bora kabisa.Anataka uchague jambo ambalo kila ukiamka  unakua namsukumo wa kulitenda kwa ajili ya utukufu wake  na  kwa ajili ya kila binadamu.Haingilii uchaguzi wowote,hata ule ambao unauchagua na unakuletea matokeo yasiyo mazuri.Huu tunauita kuwa ni uhuru usio na mipaka wa kuchagua na kuwaza.
                
                     Kwa kutambua hili kuwa Muumba wetu katupatia uhuru,wa kuchagua na kuwaza,usio kuwa na mipaka yeyote,ni wazi kwamba mafanikio ama kutofanikiwa kupo ndani yako,furaha ama huzuni ni uchaguzi wako,usawa ama matabaka yanatoka kwako,upendo ama chuki unatoka kwako,kuanguka mna kusimama kunatoka kwako,kuishi  maisha ya furaha ama yasiyo na furaha ni uchaguzi wako,na tukumbuke kuwa kwa kuwa uchaguzi ni uhuru wa kila mmoja,hivyo anayehusika na uchaguzi wako ni wewe mwenyewe.
                   
                  Kama nilivyoeleza hapo awali,fikra zetu wenyewe ndizo zinazoleta mipaka katika kuchagua na kutafuta suluhisho la matatizo yetu wenyewe.Natoa mfano,majuzi nilikuwa nikijadiliana na rafiki yangu ambae tumekua pamoja na kusoma pamoja.Tulikuwa tukizungumza kuhusu suala la ajira,yeye aliniambia kuwa amekuwa akitafuta kazi kwa muda mrefu  sana,na hata kukata tamaa,katika kujadiliana nikamshauri ni vema akaanza sasa kufikiri kuhusu kujiajiri yeye na kuajiri wengine,badala ya kufikiri kuajiriwa tu.Hapa ndipo  palipokuwa na mjadala mkali,kwamba licha ya kusoma,lakini familia zetu hazina uwezo wa  kutupatia mitaji,mimi nikamueleza kuwa mtaji mkuu kwetu sisi si fedha tuliyonayo,bali ni mawazo tulionayo....wazo hili lilionekana kuwa haliwezekani'haiwezekani kujiajiri kabisa....haiwezekani nikafanya kazi mtaani saa na mtu ambaye hajasoma,na ni mpaka miaka mingapi ntafanikiwa'
             
                      Mawazo ya msomi huyu ndiyo adui mkubwa wa yeye kudhubutu kufanya na kuchagua kufanya kile anachokipenda,elimu aliyoipata ni elimu ambayo inamfanya wakati wote afikiri tu kuajiriwa(inamuwekea ukomo katika kufikiri na kutatua matatizo),elimu tunayoipata katika vyuo vyetu na shule zetu ni elimu ya kikoloni,inayolenga kuwafanya watu wawe wafanya kazi wa wengine(kutumika),wawe tegemezi na kwao kufikiri kujiajiri ni kosa kubwa,..elimu hii inafanya fikra zetu ziwe  na mipaka katika kufikiri na katika kuamua.Inatengeneza ukuta mkubwa kati ya fikra zetu na maamuzi.Tusipogundua hili na kubomoa ukuta huu,mafanikio na kutimiza ndoto (matarajio tuliyoyapangilia)

uhuru usio na mipaka,mafanikio yasiyo na mipaka




  uhuru wa kuwaza usio na mipaka,uhuru wa kuchagua usio na mipaka ndio unaoleta ugunduzi katika dunia hii,ndio unafanya binadamu ayatawale mazingira.

uhuru  wa kuwaza usio na mipaka,unaotoka ndani ya mtu mwenyewe umeondoa ule msamiati wa haiwezekani(imposible)
picha zote kwa hisani ya mtandao na fresh mind matter



                              Kumbuka kutumia uhuru huu usio na mipaka kuchagua maisha yako,sikiliza moyo wako,usisikilize sauti za watu ambazo si halisi kwako.U CHAGUZI WAKO BINAFSI NDIO UCHAGUZI WA MUNGU KWAKO (kila ambacho moyo wako hukusukuma kutenda kikuleteacho furaha na amani moyoni mwako,hutoka kwa Mungu,ndio sauti ya Mungu na uchaguzi wa Mungu kwako).Unaweza kuchagua kuamka na kuanza upya baada ya kuumizwa katika mahusiano,ama kuendelea kulala,unauhuru wa kuchagua kuishi maisha yako mwenyewe kwa kufanya unachokipenda,ama kufanya tu kwa kufuata mkumbo,una uhuru wa kuchagua upendo,ama chuki,una uwezo wa kuchagua  mtumwa ama kuwa huru

  mazingira na athari katika fikra na uhuru wa kuchagua
                     Tumezaliwa katika mazingira tofauti,lakini yote yakiwa na misukumo yenye athari katika fikra zetu.Tumezunguka na mazingira yenye umasikini wa fikra ,na umasikini katika uhuru wa kuchagua.Mazingira yetu yanatufanya tuamini kuwa kuna nguvu ambayo inayo maamuzi juu ya maisha yetu,na ni pale tu nguvu ile itakapoamua kutupa uhuru,wa mawazo na kuchagua basi ndipo  tunapata mafanikio,ama kama nguvu hiyo itachagua kinyume basi hutokea.Kumbe ukweli ni kwamba uhuru wa kuamua maisha yetu yaweje,tuishi vipi upo ndani yetu.
                     Tunaaminishwa kuwa pale fikra za moyo wako zinapokusukuma utende kuwa ni shetani,tunaogopa kutimiza kuishi vile mioyo inatutuma,matokeo yake tunaishi kadiri wazazi ama viongozi wetu wa kiimani wanavyotaka, tunaishi kwa hofu maisha yetu yote--(kiongozi bora si yule anayekufundisha utende anavyotaka yeye,bali anayekupa mwanga wa kutambua maisha yako halisi,kuyasikiliza na kuyaishi,ambaye furaha yake ni wewe kuishi kadiri nuru yako inavyokuongoza na si kadiri ya maamuzi yake)
                       Unaweza ukajiuliza maswali ,kwa nini sisi waafrika hasa,hatufanyi ugunduzi,na wala hatuamini katika mambo yetu tunayopanga kuyafanya,tunaamini katika kila jambo ambalo linasemwa na watu toka ulaya na amerika?Ni kwa nini  kila jambo linapotokea linalohusisha uzembe,uvivu na mapango mibaya tunalichukulia kuwa  ni kazi ya Mungu ama shetani/?
  

     ni fikra zako ndizo zinazokuwekea ukomo wa kuwaza na kutenda

                           Jibu umelipata,licha ya kutojiamini katika tutendacho,hatuamini katika uwezo wetu,na imani zetu zilitwazo na mazingira zimetujengea hofu na mipaka,tunajiogopa wenyewe,tunamuogopa Muumba wetu abaye ni rafiki aliye ndani mwetu,na kisha tunaamini kuwa wapo wengine waliobarikiwa kufanya kila jambo kwa ajili yetu,tukiwaabudu hao.(ukimuogopa Mungu  badala ya kumpenda na kumchukulia kama rafiki ambaye wakati wote upo nae,utaishi kwa woga na hofu maisha yako yote,na wala hutapata kujua dhamira yako kuwepo duniani).
ELIMU YAO WALIOTUJENGEA IMETUFANYA TUWE WATUMWA,tumekuwa wafungwa sio kwa kuwa tupo  jela,bali jela yetu ni fikra zetu wenyewe.Namaliza kwa kusema,Tunahitaji watu wanaoutambua uhuru wa kufikiri na kuchagua maisha ,usio na mipaka na hivyo wanaodhubutu kubadili msamiati wa haiwezekani kuwa inawezekana.Wanaoweza kutafuta mbinu mpya(sio zile tu ambazo tumekariri na kuamini hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo(hizo)),pasipo kujali kuwa ni mjini ama kijijini,pasipo kujali kuna vifaa ama hakuna,pasipo kujali tumewezeshwa ama hatujawezeshwa,bali katika kila hali ushindi utapatikana......kama wapo walioweza katika mazingira magumu,kwa nini tusiwe sisi,kwa nini tunaogopa kuchukua hatua..kwa nini tunauogopa uwezo wetu......TUSIMAME TUSEME TUTASHINDA




Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com