hakuna elimu iliyo bora kama elimu imfanyayo mtu kujitambua yeye ni nani,anatoka wapi na anakwenda wapi....tofauti na elimu zingine zinazofanya BINADAMU akariri mambo waliyoyafanya wengine,nakumfanya aishie pale walipoishia hao(kwa maneno mengine kupita katika njia ileile walopita hao waliotangulia),elimu hii humfanya mtu awe na uhuru wa kufikiri usio na kikomo....na kumfanya binadamu kufanya mambo makubwa na yasiyo na ukomo,ili nuru iliyo ndani mwake,ionekane kwa wengine,ili nao wajitambue......elimu hii ipo ndani mwa kila mmoja pale anapopiga hatua moja na kuamua kuishi maisha yake halisi..kutimiza yale ambayo moyo wake unamtuma...akipanda milima,mabonde,tambarare,katika nyakati za kuumia,kuanguka na kuamka.....na mwisho kujitambua ya kuwa hakuna uchawi wala ujanja.,..bali kila kitu ki ndani mwake.....kwa wale wanaomfahamu Yesu ama kusoma habari zake(yesu kristo wa nazareti),ambaye alichukua hatua...akaishi maisha yake ...pasipo ubandia...akaipanda milima,mabonde,magumu,akababa kila lawama....lakini alitaka kufundisha jinsi ya kufanya maamuzi ambayo hutufanya tujitambue....hii ndio elimu kubwa aliyotaka tuifahamu
“Wewe hukusoma” na Madhara Yake Katika Ndoa
4 days ago
0 Comments:
Post a Comment
maoni yako hapa